1. Rais ana madaraka ya kubadilisha Waziri Mkuu (Mzee Ruksa alibadilisha mawaziri wakuu na enzi za zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa Chama, Rais alikuwa na uwezo wa kutumia dhana ya chama kushika hatamu kumbana Makamu wa Rais ajiuzulu kikaoni kunapokuwa na kuchafuka kwa hali ya kisiasa)
2. Rais ana madaraka ya kutokukubali kupitisha muswada wowote wa Bunge, ikiwamo muswada wa Bajeti, na hivyo kuvunja Bunge na uchaguzi mpya kuitishwa (Hili ni vigumu sana kutokea katika nchi ambayo bado ina chembechembe za nasaba ya 'dola-chama' na yenye utamaduni wa kisiasa wa kulindana kunakotokana na vimelea vya urithi wa siasa ya chama kushika hatamu)
3. Rais ana madaraka ya kubadilisha wanasheria wakuu, wakuu wa taasisi za kupambana na kudhibiti rushwa, wakuu wa taasisi za usalama na ulinzi, makatibu wa wizara, magavana wa benki kuu, na kadhalika (Mwalimu alitumia sana madaraka haya kudhibiti viongozi wake japo ualimu wake ulimfanya aishie kuwahamisha na kuwapa nafasi nyingine ili wajaribu tena na kujisahihisha)
"Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano" - Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (Toleo la 2005) Ibara ya 34 (4)