Katiba Mbovu Inambana Rais Kuwapata Wasaidizi Wabovu

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,566
41,086
Sote tumeshuhudia jinsi Rais anavyohangaika kuteua na kutengua kila mara. Hali hiyo inadhihirisha kuwa Mh. Rais anashindwa kuwapata watu sahihi wa kuweza kumsaidia. Hivyo anabakia kubahatisha, labda huyu, anapata matokeo tofauti kabisa, labda yule, hapati alichokitegemea.

Bahati mbaya uwigo wake wa uteuzi ni mdogo sana, na hivyo kubakia anazunguka humo humo, kumtafuta wa afadhali kutoka kwenye kundi wa wabovu.

Katiba yetu mbovu ndiyo chanzo cha haya yote. Katiba inamtaka Rais ateue mawaziri kutoka kwenye kundi la wabunge wa chama chenye wabunge wengi. Ukiwatazama wabunge wenyewe ndiyo hao majizi ya kura, na wengine ndiyo wale majizi ya mamlaka ya wananchi, mtu fulani tu akawatangaza kuwa ni wabunge, wakati hawana kura hata 1 ya mwananchi yeyote.

Mwizi wa soksi, hawezi kuacha kuiba kiatu, kama kitakuwa karibu. Majizi ya kura, majizi ya mamlaka ya wananchi kuwachagua watu wanaotaka wawaongoze, kamwe hayawezi kuwa na uadilifu katika kitu chochote. Tajiri aliyepata utajiri kupitia ujambazi, siku zote ataona ujambazi ndiyo njia sahihi ya kuufikia utajiri.

Hawa viongozi waliopitia njia chafu, siku zote wanaamini kupitia njia chafu kufanikisha jambo lolote. Kupitia hawa waovu, tusitegemee lolote jema. Rais atahangaika kuteua na kutengua, lakini hatakipata anachokitegemea kupitia wateule ambao wamefika hapo kwa kutegemea uovu.

Kama mh. Rais ana dhamira njema kwa Taifa hili, alistahili kukazania sana na kusukuma jitihada za kupata katiba mpya ambayo itafuta baadhi ya vifungu vinavyomlazimisha ateue mawaziri kutoka kwenye kundi la Wabunge. Watu wengi, wenye uwezo na wazalendo wa kweli siyo wabunge. Watu hawa kamwe hawawezi kujiingiza kwenye uchafu unaofanywa na hawa waliopo Bungeni.

Katiba ikimpa Rais mamlaka ya kumteua waziri mahali popote, bila ya kulazimika kuwa mbunge, akiwa makini, atawapata mawaziri wanaoweza kulitendea makubwa Taifa hili.
 
Back
Top Bottom