Madaraka ya Rais wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba

Sikonge

JF-Expert Member
Jan 19, 2008
11,550
6,062
Wana JF,

Mie nimekuwa nafikiri kuwa Rais wetu anapata shida na mafisadi kwa sababu MADARAKA aliyonayo Rais wetu ni kidogo sana. Ninaombi kwa Wabunge na Mawaziri waliopo hapa JF kuwa huko BUNGENI ibadilishwe katiba ili UWEZO wake uwe Mkubwa zaidi. Hiyo itasaidia sana kupambana na mambo mengi ambayo kwa sasa hawezi kwani KATIBA hamruhusu. Ikibidi basi hata cheo cha PM kife na ibaki Rais na makamu wake. Mbona UK wana PM tu bila Rais?

Walau kila BAYA tutajua nani alaumiwe.
 
Quite the contrary,

Kama kuna tatizo la rais na madaraka ni kwamba rais ana madaraka makubwa sana, si kidogo.

Rais ana madaraka makubwa sana kiasi kwamba hata checks and balance haziwezi kufanya kazi, rais akiwa implicated kwenye rushwa tume iliyopewa kazi ya kupeleleza inaandika "mengine hatutayasema kwa kulinda heshima ya serikali"

Tatizo si madaraka, sema jingine.
 
Sioni kama rais hana madaraka ya kutosha, tatizo hajui nini cha kufanya au anawaonea haya wenzake ambao anajua akiwagusa watamuumbua.
 
Sikonge

Haya madaraka ya rais mtendaji (executive president) yamepunguzwa kidogo tu hivi majuzi ila bado ni makubwa sana. Huu ni urithi wa Mwalimu aliyeamua nchi hii iwe na 'imperial presidency', yaani urais wa kifalme na ndio maana Mwalimu aliwahi kuwaambia BBC kuwa Katiba ya Tanzania inamruhusu kuwa dikteta. Mfumo huu ni chachu ya ufisadi maana unaruhusu kulindana.

Dawa ya ufisadi ni kuwa na uhuru wa bunge, uhuru wa mahakama, uhuru wa kitengo cha uendeshaji mashtaka, uhuru wa taasisi ya kudhibiti na kuzuia rushwa, uhuru wa jeshi la polisi, uhuru wa tume ya uchaguzi, uhuru wa vyombo vya habari na zaidi ya yote, uhuru wa wananchi. Tunahitaji katiba huru.
 
Last edited by a moderator:
Sioni kama rais hana madaraka ya kutosha, tatizo hajui nini cha kufanya au anawaonea haya wenzake ambao anajua akiwagusa watamuumbua.

GM,
Kwa mawazo yako Rais ana madaraka ya kutosha au hana?. Mie sisemei Kiwekte peke yake ila nasemea RAIS kwa ujumla na wale wote watakaofuata hata mwaka 2050. Hiki ndicho ningelipenda watu tukijadili.
Ila mie narudia tena. Haya mambo ya kusema ohh, PM aliunda Richmonduli, sijui Yona alinunua Kiwira, AKA. Ijulikane ni nani MCHAWI na asije akasema Ohh, sikuwa na uwezo. Rais awe mtu wa kubeba sifa au kubebeshwa lawama zote za Uchafu wote na maovu ya serikali.
 
Haya madaraka ya rais mtendaji (executive president) yamepunguzwa kidogo tu hivi majuzi ila bado ni makubwa sana. Huu ni urithi wa Mwalimu aliyeamua nchi hii iwe na 'imperial presidency', yaani urais wa kifalme na ndio maana Mwalimu aliwahi kuwaambia BBC kuwa Katiba ya Tanzania inamruhusu kuwa dikteta.

Subiri Mwanakijiji aione hii......Lol
 
Madaraka aliyonayo JK akitaka kuwakamata MAFISADI wote ni suala la AMRI TU!

Anatudanganya watanzania kuwa anashirikiana na bunge na bunge lina nguvu kubwa sana kwasababu anajuwa wazi ni kina Chenge watakaoshinda huko Bungeni.

Hivyo kama ni madaraka Rais tayari anayo makubwa sana na tunaweza kuyafananisha na UDIKTETA!
 
Companero

Kumbe yamepunguzwa? Nilitegemea yaongezwe. Sasa kitu gani kapunguziwa? Isije ikawa kapunguziwa ili iwe rahisi kusema SINA UWEZO NAVYO hivyo kikatiba. Mie nasema au yapunguzwe hadi yawe nusu yake au yaongezwe na TUMJUWE MCHAWI wetu siku zote ni nani.
 
Last edited by a moderator:
Sikonge,

Katiba sasa hivi inasemaje?
Kuhani ehh,
Mie niko huku kijijini ntaijuwa wapi KATIBA? Nijuavyo mie kwa kuangalia ayafanyayo Rais wetu kila siku au kwa miaka mingi ni kuwa kuna vitu huwa anashidwa kufanya kikatiba. Pia kumekuwa na kutupiana mpira kati yake na PM na ndiyo maana nikasema PM aondolewe na yeye awe kama alivyo PM wa UK yaani Kiongozi wa serikali na kila kitu au walivyo Wajerman. Kikifanyika kibaya basi ni RAIS ajibu na asitupe mpira kwa mtu mwengine yeyote.
 
Tayari ana madaraka yanayotosha kuwakamata mafisadi bila hata ya bunge wala mtu yeyote yule!
Hilo la kujifanya hana madaraka ni janja ya kutoshughulikia UFISADI!
Jamaa ana nguvu sana Sikonge fwatilia utajuwa!
Cheki na katiba.
 
jmushi1

Kama ana madaraka namna hiyo sasa kuna haja gani ya kuwa na PM? Si aondolewe tu na kila kiti afanye yeye na Mawaziri wote wawe wanajibu kwake moja kwa moja. Kila kikiharibika basi ni Waziri Mhusika na RAis ndiyo wako Responsible. Makamu wake ndiyo awe kama PM. Kwani huyu jamaa huwa yupo tu kula kodi yetu? Mwache na yeye amenyeke.

Jamani haya ya kusema katiba inasemaje au sheria inasemaje kila mtu anajua kuwa HAWAFUATI hii katiba wala sheria. Sasa msiniulize mie huku shamba kuwa nisome katiba au ninayo au inasemaje. Mie kama Fundi Mchundo huwa ni mtu wa kuangalia NINA NINI nijenge nyumba na si WAMENIAHIDI nini au wamesema nina nini.
 
Last edited by a moderator:
1. Rais ana madaraka ya kubadilisha Waziri Mkuu (Mzee Ruksa alibadilisha mawaziri wakuu na enzi za zidumu fikra sahihi za Mwenyekiti wa Chama, Rais alikuwa na uwezo wa kutumia dhana ya chama kushika hatamu kumbana Makamu wa Rais ajiuzulu kikaoni kunapokuwa na kuchafuka kwa hali ya kisiasa)

2. Rais ana madaraka ya kutokukubali kupitisha muswada wowote wa Bunge, ikiwamo muswada wa Bajeti, na hivyo kuvunja Bunge na uchaguzi mpya kuitishwa (Hili ni vigumu sana kutokea katika nchi ambayo bado ina chembechembe za nasaba ya 'dola-chama' na yenye utamaduni wa kisiasa wa kulindana kunakotokana na vimelea vya urithi wa siasa ya chama kushika hatamu)

3. Rais ana madaraka ya kubadilisha wanasheria wakuu, wakuu wa taasisi za kupambana na kudhibiti rushwa, wakuu wa taasisi za usalama na ulinzi, makatibu wa wizara, magavana wa benki kuu, na kadhalika (Mwalimu alitumia sana madaraka haya kudhibiti viongozi wake japo ualimu wake ulimfanya aishie kuwahamisha na kuwapa nafasi nyingine ili wajaribu tena na kujisahihisha)

"Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, madaraka ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano yatatekelezwa ama na Rais mwenyewe moja kwa moja au kwa kukasimu madaraka hayo kwa watu wengine wenye madaraka katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano" - Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 (Toleo la 2005) Ibara ya 34 (4)
 
Wana JF,
Mie nimekuwa nafikiri kuwa Rais wetu anapata shida na mafisadi kwa sababu MADARAKA aliyonayo Rais wetu ni kidogo sana. Ninaombi kwa Wabunge na Mawaziri waliopo hapa JF kuwa huko BUNGENI ibadilishwe katiba ili UWEZO wake uwe Mkubwa zaidi. Hiyo itasaidia sana kupambana na mambo mengi ambayo kwa sasa hawezi kwani KATIBA hamruhusu.

Sikonge,

Katiba sasa hivi inasemaje?

Kuhani ehh,
Mie niko huku kijijini ntaijuwa wapi KATIBA?

Sina swali lingine.
 
Good observation Kuhani!!,

.....wee Sikonge....inabidi ufanye h/work yako sawa sawa kabla ya kubandika judgements zako humu.......kama una-claim Rais ana madaraka madogo...hebu tuwekee facts ulizonazo kuthibitisha claim yako
 
Kuhani ehh,
Mie niko huku kijijini ntaijuwa wapi KATIBA? Nijuavyo mie kwa kuangalia ayafanyayo Rais wetu kila siku au kwa miaka mingi ni kuwa kuna vitu huwa anashidwa kufanya kikatiba. Pia kumekuwa na kutupiana mpira kati yake na PM na ndiyo maana nikasema PM aondolewe na yeye awe kama alivyo PM wa UK yaani Kiongozi wa serikali na kila kitu au walivyo Wajerman. Kikifanyika kibaya basi ni RAIS ajibu na asitupe mpira kwa mtu mwengine yeyote.

Mkuu sasa kabla ya kuleta hii hoja, si unge-download hio katiba na upitie sehemu inayoonesha madaraka ya raisi?

Naona hili ndio tatizo lako. Easy budy, unafanya utafiti halafu unatoa mada.
 
Wana JF,
Mie nimekuwa nafikiri kuwa Rais wetu anapata shida na mafisadi kwa sababu MADARAKA aliyonayo Rais wetu ni kidogo sana. Ninaombi kwa Wabunge na Mawaziri waliopo hapa JF kuwa huko BUNGENI ibadilishwe katiba ili UWEZO wake uwe Mkubwa zaidi. Hiyo itasaidia sana kupambana na mambo mengi ambayo kwa sasa hawezi kwani KATIBA hamruhusu.

Sikonge,

Katiba sasa hivi inasemaje?

Kuhani ehh,
Mie niko huku kijijini ntaijuwa wapi KATIBA?

Sina swali lingine.

Gademu Kuhani....!!!! Hii tabia yako inaweza kufanya mtu akimbie mada yake mwenyewe.... LOL
 
Kuhani ehh,
Mie niko huku kijijini ntaijuwa wapi KATIBA? Nijuavyo mie kwa kuangalia ayafanyayo Rais wetu kila siku au kwa miaka mingi ni kuwa kuna vitu huwa anashidwa kufanya kikatiba. Pia kumekuwa na kutupiana mpira kati yake na PM na ndiyo maana nikasema PM aondolewe na yeye awe kama alivyo PM wa UK yaani Kiongozi wa serikali na kila kitu au walivyo Wajerman. Kikifanyika kibaya basi ni RAIS ajibu na asitupe mpira kwa mtu mwengine yeyote.

...kumbe hata madaraka ya raisi hujui then unatuletea hizi BS yako...nenda kasome katiba kwanza na hata humu unapoandika ukiitafuta inapatikana
 
Back
Top Bottom