Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
- Thread starter
- #21
...wee Sikonge....inabidi ufanye h/work yako sawa sawa kabla ya kubandika judgements zako humu.......kama una-claim Rais ana madaraka madogo...hebu tuwekee facts ulizonazo kuthibitisha claim yako
Kwa wote mliochangia,
Naona mnachanganya vitu vingi sana. Mie siyo mwana Siasa. Mie ninachosema ni kwa kuangalia mambo yanavyotendeka. Nchi nyingi huwa zinatabia za BOSS anagawa kazi kwa wadogo na kuwasukumia mambo machafu yote. Mambo yakikwama basi husema ni PM au Waziri ndiyo alifanya hivi. Tuangalie swala la RICHMOND au Kiwira. Kila mtu anaona kabisa kuwa ni Marais walishiriki kwa namna moja au nyingine. Lowassa alilivalia njuga hasa kwa kutoa AMRI kwa mdogo kwa wafanyaji wa chini. Sasa ukitaka ku-prove kuwa nani alifanya kosa utakuta kuwa SI RAIS wala SI PM. Ila ukweli kila mtu anauona wazi kabisa.
Mie ninachosema ni kuwa au PM awe kiongozi wa Mawaziri kwa kuwachagua yeye na SERIKALI yote kweli iwe chini yake. Au PM aondolewe na RAIS awe kiongozi wa SERIKALI yaani kwa maana nyingine RAIS AONGEZEWE MADARAKA. Hii sijui kama inahitaji kusoma KATIBA YOTE. Mie POINT yangu ni hiyo tu na hii ndiyo inayoendelea pale TANZANIA. Kuhani kama sivyo basi kweli mie HAZINITOSHI. Maana inaonekana huwa naona mambo KIVYANGU.
Kwa mawazo yangu ni kuwa kama RAIS au ATAONGEZEWA madaraka na yeye awe PM pia au KUPUNGUZIWA kama nilivyosema hapo juu, itaondoa utata wa NANI KAFANYA KOSA HILI kama la RICHMOND. Kila mtu anafahamu kuwa Helmet Cohl kwa kuchukua KICKBACK kutoka kampuni la mafuta la Kifaransa la ELF, aliubeba yeye mwenyewe MSALABA. Hakuweza kusema kuwa Ohh, ni mfanyakazi fulani kwani chama kilivyo, ni yeye tu anajibu mazuri na mabaya yote ya chama. Tanzania Kikwete anataka sifa zote ziende kwake na yakija mabaya hata kama ni yeye alitoa amri, ananawa mikono na kusema kuwa NI PM au Waziri au SERIKALI.
Sijui kama utakuwa umenielewa au bado utanituma zaidi kwenda kusoma katiba ambayo MILELE sintakujaisoma. Kama kuna mtu amenielewa na anaweza ielezea vizuri hii ISSUE basi ntashukuru.