Madam rita & master jay mnajichora

Mimi kuhusu Vincent sina uhakika sana, ila huyo mhindi pia kajitahidi this time jamani ingawa mimi nawafagilia Wababa, Nsami na Walter
 
jamani nimefall in love ghafla baada ya kumwona Meninyah Atick sijui ni Chotara yule mtoto,daah naumia,ningekuwa na Pesa ningemtafuta kwa udi na uvumba...
 
haters,nyie ni mchango gani mmetoa kuinua vipaj vichanga vya wasanii apa tanzania,na je uwa mnapiga kura kwa wasanii,mwisho wa siku kura zenu uwa zinaamua lakin watanzania wengi ni washabik kwenye midomo,kura awapigi mwisho wa siku wanalalamika tu,
ni vigumu kumrizisha kila mtu,na nyie mko free kuanzisha bobgo star search zenu kama mnaona ni kitu easy na mtaweza mlizisha kila mtu
 
mi nilishatupa kule kuchoma muda wangu kutazama vipindi vya mashindano ambavyo washindi wanafahamika tayari!season one sikuridhika kabisa na mshindi(si mwanamuziki mzuri na utabiri wngu kwa rafiki zangu kwamba hatauza sokoni ukatimia),nikawapa nafasi sseason two nikakereka kabisa,nikaacha hata kufuatilia kwakweli.pop idol walinizingua baadae,nikaangalia x factor nayo nikaona upuuzi mwingi,nikatupa kule,walau sasa The Voice ndo show inayonipa raha,judges wanajua kiukweli na contestants,hata yule wa mwisho kabisa unaona kiwango cha hatari!
 
Kuna kale kadogo kana punk na yule dada wa zenji,pale hamna kitu.
 
yaani BSS ya mwaka huu haina waimbaji wazuri. halafu Majaji wanashindwa kabisa kutoa Judgement ya Ukweli. Bora salama huwa anasema Ukweli japo unauma. Namkumbuka sana EDSON TERI wa ile Bss ya mwanzo ambaye naye wlimkataa. Madam Rita anawapa wasanii hawa sifa za UONGO.
 
Ulitakiwa kumpigia kura ili asiende nyumbani!

Hebu kuweni fair, yaani Vincent anarudishwa nyumbani na Salma (mpiga-gita)anabaki hata bila kuingizwa danger zone huku mama Rita anasema hakuna kama huyo na master J anakenua meno tu wakati taaluma inanyewa hivi hivi?

Sipendi kuamini kuwa kuna watu wameandalia ushindi siku nyingi lakini mkiendelea na upuuzi huu sisi wapiga kura tutaanza kuwapigia ninyi kura za kukosa imani nanyi. Angalia mlivyombeba yule Salma (mhindi) amewashinda kubeba mgongoni mwishoe mmeamua kumbwaga kwa uchungu sana. Huyo hakustahili hata kuingia BSS 21 bora, ni dada anaye temea mate tu kwenye kipanza sauti na sauti ya kuua ngoma za masikio ya watu.

As for Salama Jabir huwa hatumchukulii serious maana inategemea kaamkaje na nani kampa kaneno ka kumzuzua perfomer. Lakini kwa Master J (mtaalam wa muziki) na Madam Rita (Chief Judge) angalieni sana mnahatarisha biashara yenu, maana siku za usoni hakuna atakayetoa udhamini kwa kuwa na upendeleo wa wazi namna hii.

Sikilizeni, mimi simfahamu yeyote katika washiriki lakini nawashauri kuwa hivi nyote watatu kaeni mahala m-playback episode ya Jumapili 07/10 mumsimilize Vincent as compared to the others Wavulana kwa wasichana (mtaona Kijana ana sauti ya mvuto, kaimba vizuri, good choice of song with a lot of feelings, anatawala steji, anaimba mistari ya kutosha sio kama wengine wanaimba kidogo tu halafu kudance na kuchombeza viungo yaaa!! yeeee!! n.k. Yaani hata ingawa Wababa namkubali lakini kwa episode ya Jumapili alifunikwa na Vincent maana alikuwa na wimbo wa kubore na hakuna cha maana cha kumsifia kwa siku hiyo na ndivyo ilivyokuwa kwa wengine wachache ambao hakika walikuwa off tune na wamewekwa tu danger zote.

Msibweteke na jina la mtu au alifanya vipi mwanzoni, toeni comments za ukweli kufuatana na performance ya siku hiyo! dada mpiga gitaa anaweza kuwa musician kwa kuweza kuchalaza nyuzi lakini kwa sauti na hata kutamka maneno hawezi anaumauma maneno na anaimba sauti isiyo na mvuto tena yenye pitch ya chini sana kila siku na kujificha chini ya kivuli cha usanii. Naye mumsikilize yeye toka episode ya mwanzo mtaliona hili waziwazi na mtaona aibu kwa kumsimamia na kumsalute wakati ni mweupe.

The more you stand for professionalism, truth & fairness, the more we shall support this Epiq BSS-programme & Benchmark production Ltd.:A S embarassed:
 
Ni kweli kabisa mkuu mimi toka walipomtoa rossemerry mpangala nikaona hapo kwenye ujaji kuna walakini na wala sioni kigezo cha kumpa ujaji huyo salama muziki wenyewe haujui kazi kutusi watu na kuongea upuzi tu hana hata aibu na huyo rita angewapisha watu wenye taaluma ya muziki akabaki kuwa mmiliki tu wa bss kweni lazima nae awe jaji au ndio mambo ya uuza sura hana uweledi kabisa huyo ni mlevi tu salama mabangi
Siku walipomtoa huyu binti na mimi nikafunga milango ya kuangalia hicho kipindi chao. Kwa kweli ingekuwa enzi zile za "Klabu Raha leo Shoo!" sidhani hawa wakina Salama wangepewa hata mic wazungumze. Ndiyo maana mpaka leo nakumbuka enzi zile za "Misakato" na lile gita la solo lililopigwa kwenye sebene la Msondo Namba 5.
 
Katika nchi corrupt kama hii, ukichanganya na ignorance plus illiteracy yetu uwezekano wa akili dogo kutawala akili kubwa ni dhahiri, we have empty seats from the president seat to the lowest seat in every discipline. change or die.

kuna watu kwenye mchujo walikuwa wanatemwa mpaka unshangaa, kuna dada mmoja wa tanga simkumbuki jina anauwezo mkubwa sana alitoswa nikabaki nashangaa, baadae akili ikanirudia nikakumbuka hapa ndo bongo wajinga ndo wameshika hatamu.
 
hii kitu naona wamewaiga x factor maana na kwenyewe kule mambo sio mambo last time yule ma favorite alikuwa astro & chris rene naona wakawababia wakamchukua yule dada aliyekuwa kwenye audition ya florida

hata mimi nilishanga huyo dada wa florida alitemwa na paula abdul kwenye audition laklin simon cowell alimbeba tena fumba fumbua akaingia fainali na josh kreatick mwisho wa siku akachukua $5 record deal
 
Unaona jinsi majaji walivyobadilishwa kwenye X Factory mwaka huu Nicole katupwa nje kwa sababu ya kumfanyia yule binti wa 12 yrs Recho crow kitendo kilicho waliza watu wote sababu ya ukabila akampa Drew kura Paula Abdul nae mkataba kaukosa sababu aliwabeba Lakoda rhyne alimtosa Melanie Amaro Ila Walipopitia playback show wakagundua Demu ni mkali LA Reid na Simon cowell wakamwita tena akaja kwenye audition Miami ila...naamini makosa yao ndio yalimwibua Amaro kuwa Mshindi wa mkataba mnono wa $5 Mil. Record deal na sony otherwise wasingechunguza walikuwa wameshamuacha sasa nawashauri hawa EBBS Wasicheze vipaji vya hii tasnia hasa ya Ujaji(Judge)wawe wanabadilisha watoe hawa walevi na wasagaji huyu leo analeta mambo ya Yanga anaijuwa Yanga huyu? Watamtafuna Ndogo akome kufungua Domo hovyo na Mibhangi yake Lesbian la kipemba.
 
Hii BSS imejaa upendeleo wa aina fulani. Wale wadada wawili wa kisukuma wenye sauti nzuri hawakupaswa kuwepo kwenye BSS maana tayari wanasoma bagamoyo. wanafundishwa kila kinachohusiana na music ndio maana wanafanya vizuri. kama idea ya BSS ni kuinua vipaji vya wanyonge, basi wasiwepo, maana ikiwa wana uwezo wa kwenda kusomea music bagamoyo, ina maana sio wanyonge. Nakumbuka dada yao hawa, misoji, aliwahi kua mshindi wa kwanza BSS ya mwaka juzi kama sikosei. Alipata upendeleo kwa sababu kaka yake alikua mmoja wa wadhamini wakubwa wa kipindi kile. Alitoa computer 10 kwa ajili ya kuwapa washindi. Hivyo inawezekana hawa pia wapo for a reason.
Mhindi yule hata sijui alifikia vipi pale alipofika? sitaki kuongelea kutokua kwake na kupaji, ila kama hii ni kusaidia wanyonge, yule mhindi ana unyonge gani wakati anasoma laureate international school?
kuna jambo nyuma ya pazi ambalo nadhani wanaliangalia zaidi, kujuana na upendeleo ikiwa mojawapo. Kuna wasanii wazuri tu wametolewa mapema kabisa, sijui ni vigezo gani vilitumika, na hawa waliobaki sijui wamebaki kwa vigezo gani?
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom