Madaktari wenzangu: Only "Mass resignation" itawaamsha watawala!

Mkuu SANING'O LOSHILU, hebu niambie ni wapi DUNIANI, daktari anakuwa "cheap labour"??Hapa tunaongelea madaktari wenye MD na kuendelea sio Assistant medical oficcer(AMO), Huyo daktari unayemsema ana uwezo wa kufanya kazi popote pale duniani, Vyuo vingi vya Afya vimeanzishwa hivi karibuni, lakini chuo cha muhimbili(ambako ndio idadi kubwa ya madaktari wanatoka) kilikuwepo toka zamani ikiwa chini ya UDSM hadi mwaka 2007, ingekuwa vizuri ukafanya utafiti na kuangalia kinashika nafasi ya ngapi DUNIANI na nafasi ya ngapi katika vyuo vya afya ndipo utapojua kwanini madaktari wa kitanzania wanatafutwa sana nje, UKISHAFANYA HIVYO NJOO ULETE PROPAGANDA ZAKO HAPA..na shida ya watu wa uelewa kama wako na wasiofanya utafiti matatizo haya yanatokea na hivyo madaktari wanakomolewa!!
kwa idadi ya madaktari 1700(hii ni takwimu ya W/Afya kwani bado hutajishughulisha na kuhakikisha) wakiwemo na mawaziri, wastaafu..subiri mwisho wa mwaka uone wangapi watabaki hapa nchini kwa kile mnachokiita "kazi ya wito"
 
Hawataweza,hela ya kula wanayo??wafanya mchezo weyee!hawa ni mchecheto tu unaowasukuma na watapelekeshwa sana na hii serikali ya huyu mkwele,kesha jua udhaifu wao ndio maana wanaambiwa leo wanaitwa wizarani mmoja mmoja,mara uandike melezo mara wanashitakiwa yaani wamefanya kituko cha aina yake ukiamua kujenga hoja siku zote simamia hoja yako bila kuteteleka.Hivi waliona mgomo wa madaktari na nurses wa kenya mwaka huu ulikuwa mtiti si mchezo ninyi hapa hamna strategy ndio maana mnashindwa,mgomo wa kwanza mlishindwa na huu wa sasa ndio kabisaaaa ni wa aibu kwenu.
 
ABDULHALIM, Hapo ndipo unapokosea
-Unajua kuna aina ngapi za upasuaji(procedure)..i.e elective and emergency, etc??
-kwa siku unajua procedures zinazohitajika kufanywa ni ngapi??
-Unajua kuna aina ngapi za gloves au unaongea ili kufurahisha umma?
-Unajua ni gloves ngapi zinatumika kwa upasuaji(procedure) mmoja?? unajua ni nani na nani wanaotumia hizo
gloves??Tunaongelea Sterile gloves na si Clean gloves,
otherwise ukilazimisha kutumia gloves zozote tutakupatia
magonjwa kama ulishawahi kuwa chumba cha upasuaji au ndugu/rafiki/jamaa utakuwa unaelewa nachomaanisha, kama
bado fanya utafiti!!

Halafu kama ni kununua gloves unajua bei ya sterile gloves(maana ndio zinazotakiwa SI clean gloves)?? Mgonjwa anapokuja ndio uende ukanunue gloves?!!!
-Unajua kazi za Bohari ya vifaa na madawa(Medical Store Department)??
-Utanunuaje kila siku kama yule unayemnunulia(ILI KUMSAIDIA KWA KUTUMIA UTU WAKO) hathamini msaada wako na
kuwa na majibu ya daharau/kejeli na kashfa hasa pale unapomwambia Akanunue na yeye kwa sababu wewe umekuwa
ukinunua bila kuchoka "wito" ANAAMINI KUWA UNAMTENGENEZEA MAZINGIRA YA KUOMBA RUSHWA na maneno
lukuki kuwa madaktari hawajali!!!!!!

Hoja ya kwamba ninyi kwenda kikazi bila malipo ndiyo mnapaswa kuidai na sio kujustify madai ya wengine kwa aidha uzembe au uoga wenu wa kudai haki!!Mfano kama una uwezo wa kununua baiskeli ikusaidie katika mahitaji yako ya kila siku na jirani yako hana uwezo, huwezi kuacha kununua eti tu kwa sababu jirani yako atakufikiria vibaya, aukwasababu ile ya kwamba haitakuwa picha nzuri mimi kuwa na baiskeli na yeye kutembea kwa miguu!! What if hataki baiskeli? what if anapendelea kutembea?Siku akilala njaa utaamua kulala njaa ili tu mwe na usawa wakati unajua ANAO UWEZO wakujipatia chakula?
The bottomline here ni wewe kudai haki yako, na siyo kuzuia wengine wanapodai haki yao(atleast zuia kwa sababu za msingi) na si eti "mbona sisi tuna shida sana".."If you dont like how things are,change them..you are not a tree".
 
Baadhi ya Madaktari Nchini ni Wanafki sana,

Ukisoma madai wanayoyalalamikia kipindi chote zaidi ya 70% ya madai yao kwa serikali ni maslahi yao binafsi, the rest ni kwa wagonjwa kwa maana ya vifaa tiba, madawa na mazingira bora ya hospitalini.

Kama kweli madkatari ni wazalendo na wanapigania kuboresha huduma za kiafya kwa ajili ya wagonjwa na Taifa kwa ujumla ikiwemo Vifaa Tiba, Madawa n.k kama ambavyo mleta mada na baadhi ya madaktari wanavyotaka kuuaminisha Umma sasahivi, Kwanini wasingekubali ku adjust/kushusha demands zao ikiwemo allowances za nyumba, usafiri, mazingira hatarishi, mishahara minono na mengine kama hayo ili sehemu ya pesa zote ambazo wangepewa ziende katika kuboresha mazingira bora ya hospitali zetu, kununua vifaa tiba, madawa n.k

Katika migomo/migogoro ya madaktari awamu zote mbili bado maslahi binafsi kwa madaktari illikua ni Priority no 1, baada ya hapo ndio ilikua suala la kuboresha mazingira ya utoaji huduma za kiafya pamoja na vifaa tiba na madawa mahospitalini.

Hapa naomba nieleweke vizuri sipingi maslahi ya madaktari lakini kwa kutazama maslahi ya wagonjwa na Taifa kwa ujumla kama ambavyo madakatri wengi sasa hivi na wadandia mada wanavotaka kujipambanua kwa watanzania, swala la nyongeza ktk mishahara na posho zao binafsi wangelipa Kipaumbele cha pili (Priority no 2) na hivyo kuwa flexible katika kupunguza uzito wa gharama ya madai yao serikalii kwa kuweza kupunguza mzigo mkubwa ambao serikali wangebeba kuwanufaisha/kuwalipa wao binafsi badala yake sehemu ya hizo pesa zingeenda kwenye (Priority no 1) ktk kuboresha huduma za kiafya mahospitalini, madawa pamoja na vifaa tiba.

Mleta mada anasisitiza Mass Resignation kwa ma Specialist, ukitazama kwa undani shabaha/lengo la Kuchukua hatua hiyo ni kuikomoa Serikali lakini tukumbuke mwisho wa siku wanaokuja ku athirika kwa maamuzi hayo, ama ni sisi wenyewe ama ndugu zetu, watoto wetu ama wazazi wetu na wala si serikali..

Nawasihi Madaktari wote nchini turudishe Uzalendo na Moyo wa kulijenga kwa pamoja Taifa letu la Tanzania.
Migomo/Migogoro ama Mass Resignation haitotupeleka mahala popote.

To me, Mass Resignation = Total Destruction

You better Think Twice
 
Kwani lazima umefanye kazi serikalini? Sometimes ni bora kuwa watu wachache dedicated ambao una uhakika wa huduma kuliko kuwepo wengi wenu ambao hatuna uhakika wa kupata huduma. Mwanzoni tutapata shida.
I advise you to ask UN to help you with your employment.
Other professions battle it out in the real world .

Ukiwaza ki-masaburimasaburi matokeo yake ndo haya!
 
Hii imewekwa vizuri, kiakili na ukiisoma inasikitisha. Inatoa wito kwa madaktari kuangalia wanachogombania ni nini hasa na kwa manufaa ya nani. Kama madaktari hawawezi kulazimisha serikali kukaa nao chini hakuna mfanyakazi wa kada nyingine yoyote atakayeweza kufanya hivyo. I support the doctors!

mambo yote jeshi bwana!
 
Mkuu Hippocratessocrates heshima yako mkuu.

Mimi mmoja wa wananchi ambae bado hata nikifika nyumbani kwetu Tanzania ntajivunia nikiona natibiwa na daktari mtanzania.

Maelezo yako ni mazuri na ingawa umeingia deep technically hilo ndilo eneo ambalo wawakilishi wa serikali na hata mawakala wake wanakuwa hawaelewi kwani wao wanachotaka mambo yaende kama yalivyo na kusiulizwe swali.

Mimi ntaendelea kuunga mkono mgomo mnaoufanya kwa kutambua wazi kabisa kwamba mnadai kuboreshwa kwa mishahara yenu, mazingira mnayofanyia kazi na marupurupu mengine kukidhi ugumu wa kazi yenyewe.

Lakini mgomo wenu unakabiliwa na matatizo ya aina mbili.

Kwanza, ni kwamba ninyi madaktari wenyewe mmegawanyika katika makundi mawili. Kundi la kwanza ni lile la madaktari ambao maisha yao tayari yamenyooshwa tokea wamemaliza kidato cha sita na pengine hata mikopo hawakugusa, kwahio wao hata katika mikutano yenu wanaweza kuhudhuria lakini wakiwa wasindikizaji. Pia humo wamo mapandikizi ambao wamewekwa ili kulinda maslahi ya serikali na mawakala wao na ndio mmeona yaliyomkuta mwenzenu Dr Ulimboka.

Sasa ukiwa na hali kama hii hakuna mgomo mtaofanya ukawa na mafanikio ila utaleta maafa mengi tu kwa kila mshiriki.

Pili ni kwamba hakuna independent trade union ambayo itawasimamia kule kwenye majadiliano na kuwa sauti kati yenu ninyi madaktari na serikali na ndio maana kwa kutumia watu ambao pengine hata hawafahamu vizuri sheria za kazi mnajikuta mkifanya migomo pila mpangilio na isijulikane ni nani hasa anawasaidia iwe MAT au association yenu.

Hizi takataka kama TUICO au nini sijui, hazina maana kwani jumuia hizi zinapewa ruzuku kutoka serikalini na zisiwe na watu ambao wanaitwa firebrand kwa kujenga na kutoa hoja na zikasikilizwa na kuheshimiwa. Sasa kama inaundwa jumuia ya watumishi wa sekta ya afya pekee na wakatoa michango yao kila mwezi, kunaweza kufanywa mgomo mzuri tu wenye mpangilio na ukazaa matunda kwa kila upande badala ya kuleta mapandikizi.

Kabla ya kufanya mgomo au industrial action ambayo itahusu hospitali zote nchini itabidi kama mpige kura na ipatikane asilimia fulani ambayo itajulisha kwamba hio industrial action is necessary na ni maeneo gani mtaacha kufanya kazi. Kwa mfano mtaacha kufanya routine checks kwa wagonjwa lakini mtaendeleza huduma za dharura na urgent cases.

Kwahio hapo serikali itafahamu kwamba madaktari wana shida na wanataka kusikilizwa shida yao na hata vyombo vya habari vinakuwa nyuma yenu lakini pia kwa kuzingatia kwamba huduma kwa wagonjwa zinaendelea kama kawaida.

Lakini inavyoonekana ni kwamba hapakuwepo mtiririko au plan ya namna mtakavyogoma na ikaonekana kwamba wagonjwa ndio waathirika na madaktari hawapo kazini na kuna mikanganyiko hata kufikia kuwachanganya watu hata kufikia kusema "liwalo na liwe".

Tatizo la hii industry yenu ni kwamba inaishi na serikali ambayo haijali kabisa mazingira yenu ya kazi wala kusema inawanunulia kila kifaa mnachohitaji na ushahidi ni bajeti wizara ya afya ambayo ni kichekesho.

Sasa tunapokuja kwenye mgomo, serikali inakuwa haiwaelewi na inajenga chuki kati yenu na wananchi na ni ninyi mnaonekana wabaya.

Ila kwa upande wenu madakari mnapogoma haimaanishi kwamba you will be picketing katika hospitali zenu au kuingia barabarani kufanya maandamano bali mtakuwa hospitali na kuhakikisha A&E, maternity deparments and units and also anyone needing an urgent diagnostic test or end-of-life care kutoka kwenu.

Hili tatizo la serikali kukataa kuwalipa 3.5 milions halitaisha leo na hii inatakiwa iwe mwangaza wa ukombozi kwa kujaribu kubadili serikali hii.

Ndio maana katika maoni yangu sehemu ingine nikasema inabidi kuanzishwe trusts ambazo zitakuwa independent na zenye kushughulikia mambo kama mishahara na trusts hizi zinakuwa ni za professionals sio wababaishaji.

Serikali inavuja pesa za walipa kodi, serikali ina viongozi wanatibiwa nje ya nchi kwa pesa za walipa kodi kwa kuogopa kutibiwa na madaktari iliowasomesha na kuwagharamia yenyewe, aibu sana hii.
 
Mimi nitakuwa upande wa madaktari hadi tone la mwisho la damu yangu.

Kumbukeni hayati Marley alivyowahi kutuhamasisha enzi hizo:

Last edited by a moderator:
Mkuu Hippocratessocrates heshima yako mkuu.

Mimi mmoja wa wananchi ambae bado hata nikifika nyumbani kwetu Tanzania ntajivunia nikiona natibiwa na daktari mtanzania.

.........

Mkuu Richard; umeweka bayana sana mambo ambayo hata mimi nayanona. Nina uchungu sana kuona fani ya tiba nchini inaporomoka sana nchini na kuwa tumejenga mradi wa kupeleka wagonjwa wetu India kila siku. Nina wasiwasi kuwa viongozi wetu wanaotibiwa nje ya nchi walishapandikizwa kitu fulani kwenye bongo zao kusudi wasiharibu biashara hiyo ya kwenda kutibiwa huko kwa kuhakikisha kuwa huduma za tiba nchini kwetu zinakufa kabisa.

I hope madakatri wote bila kujali nafasi zao watasimama kidete kwa pamoja na kusema enough is enough; profession ya medicine haiwezi kutukanwa na wanasiasa kimkato mkato hivi hivi tu. wote wawek manati chini tuone jinsi serikali itakavyoshughulikia swala lao. Kwa sasa hivi serikali inacheza mcehzo wa divide and conquer, na inoankena kama vile madaktari wanaelekea ku-surrender!.
 
Wengine bado wanaitaka kazi hivyo kuwahamasisha kuacha kazi ni kuto watendea haki. Kama kweli mazingila ni magumu mbona hayahitaji watu kuji organize ili yaonekane magumu, mi naona asiyetaka kazi aache kwa hiari yake na kama kweli ni suala lenye nguvu mtajikuta wote mmeshaachia ngazi. Halafu inaonekana mtoa maada jina lako lipo katika list ya walionyan'ganywa leseni.
 
Baadhi ya Madaktari Nchini ni Wanafki sana,

Ukisoma madai wanayoyalalamikia kipindi chote zaidi ya 70% ya madai yao kwa serikali ni maslahi yao binafsi, the rest ni kwa wagonjwa kwa maana ya vifaa tiba, madawa na mazingira bora ya hospitalini.

Kama kweli madkatari ni wazalendo na wanapigania kuboresha huduma za kiafya kwa ajili ya wagonjwa na Taifa kwa ujumla ikiwemo Vifaa Tiba, Madawa n.k kama ambavyo mleta mada na baadhi ya madaktari wanavyotaka kuuaminisha Umma sasahivi, Kwanini wasingekubali ku adjust/kushusha demands zao ikiwemo allowances za nyumba, usafiri, mazingira hatarishi, mishahara minono na mengine kama hayo ili sehemu ya pesa zote ambazo wangepewa ziende katika kuboresha mazingira bora ya hospitali zetu, kununua vifaa tiba, madawa n.k

Katika migomo/migogoro ya madaktari awamu zote mbili bado maslahi binafsi kwa madaktari illikua ni Priority no 1, baada ya hapo ndio ilikua suala la kuboresha mazingira ya utoaji huduma za kiafya pamoja na vifaa tiba na madawa mahospitalini.

Hapa naomba nieleweke vizuri sipingi maslahi ya madaktari lakini kwa kutazama maslahi ya wagonjwa na Taifa kwa ujumla kama ambavyo madakatri wengi sasa hivi na wadandia mada wanavotaka kujipambanua kwa watanzania, swala la nyongeza ktk mishahara na posho zao binafsi wangelipa Kipaumbele cha pili (Priority no 2) na hivyo kuwa flexible katika kupunguza uzito wa gharama ya madai yao serikalii kwa kuweza kupunguza mzigo mkubwa ambao serikali wangebeba kuwanufaisha/kuwalipa wao binafsi badala yake sehemu ya hizo pesa zingeenda kwenye (Priority no 1) ktk kuboresha huduma za kiafya mahospitalini, madawa pamoja na vifaa tiba.

Mleta mada anasisitiza Mass Resignation kwa ma Specialist, ukitazama kwa undani shabaha/lengo la Kuchukua hatua hiyo ni kuikomoa Serikali lakini tukumbuke mwisho wa siku wanaokuja ku athirika kwa maamuzi hayo, ama ni sisi wenyewe ama ndugu zetu, watoto wetu ama wazazi wetu na wala si serikali..

Nawasihi Madaktari wote nchini turudishe Uzalendo na Moyo wa kulijenga kwa pamoja Taifa letu la Tanzania.
Migomo/Migogoro ama Mass Resignation haitotupeleka mahala popote.

To me, Mass Resignation = Total Destruction

You better Think Twice
Engarenarok, u the man.
 
ABDULHALIM, Hapo ndipo unapokosea
-Unajua kuna aina ngapi za upasuaji(procedure)..i.e elective and emergency, etc??
-kwa siku unajua procedures zinazohitajika kufanywa ni ngapi??
-Unajua kuna aina ngapi za gloves au unaongea ili kufurahisha umma?
-Unajua ni gloves ngapi zinatumika kwa upasuaji(procedure) mmoja?? unajua ni nani na nani wanaotumia hizo
gloves??Tunaongelea Sterile gloves na si Clean gloves,
otherwise ukilazimisha kutumia gloves zozote tutakupatia
magonjwa kama ulishawahi kuwa chumba cha upasuaji au ndugu/rafiki/jamaa utakuwa unaelewa nachomaanisha, kama
bado fanya utafiti!!

Halafu kama ni kununua gloves unajua bei ya sterile gloves(maana ndio zinazotakiwa SI clean gloves)?? Mgonjwa anapokuja ndio uende ukanunue gloves?!!!
-Unajua kazi za Bohari ya vifaa na madawa(Medical Store Department)??
-Utanunuaje kila siku kama yule unayemnunulia(ILI KUMSAIDIA KWA KUTUMIA UTU WAKO) hathamini msaada wako na
kuwa na majibu ya daharau/kejeli na kashfa hasa pale unapomwambia Akanunue na yeye kwa sababu wewe umekuwa
ukinunua bila kuchoka "wito" ANAAMINI KUWA UNAMTENGENEZEA MAZINGIRA YA KUOMBA RUSHWA na maneno
lukuki kuwa madaktari hawajali!!!!!!

Hoja ya kwamba ninyi kwenda kikazi bila malipo ndiyo mnapaswa kuidai na sio kujustify madai ya wengine kwa aidha uzembe au uoga wenu wa kudai haki!!Mfano kama una uwezo wa kununua baiskeli ikusaidie katika mahitaji yako ya kila siku na jirani yako hana uwezo, huwezi kuacha kununua eti tu kwa sababu jirani yako atakufikiria vibaya, aukwasababu ile ya kwamba haitakuwa picha nzuri mimi kuwa na baiskeli na yeye kutembea kwa miguu!! What if hataki baiskeli? what if anapendelea kutembea?Siku akilala njaa utaamua kulala njaa ili tu mwe na usawa wakati unajua ANAO UWEZO wakujipatia chakula?
The bottomline here ni wewe kudai haki yako, na siyo kuzuia wengine wanapodai haki yao(atleast zuia kwa sababu za msingi) na si eti "mbona sisi tuna shida sana".."If you dont like how things are,change them..you are not a tree".
Kama alivosema genius mwenzako Christian Ibrahim, ni vugumu kwangu kuelewa kuhusu habari ya gloves na gharama zake, maana mimi ni kilaza, uamsho niliyeishia madrasat.

I am just curious, huko private mnakoenda kufanya huwa mnapata hizo gloves na vifaa vingine vyenye majina ya kutisha (kwamba sie vilaza tutashindwa hata kuyasoma? i guess).

IMHO, your timing kuja na haya mgomo / madai is equally impeccable. sjui una maoni gani? maana mie nilipokuja kukaa chini na kuona kununua karatasi kwa kazi za serikali hailipi, nilisepa kimyakimya bila kusubiri vijana wa field /interns wagome ili mimi nichomekee madai yangu.
 
Ningependa kutoa pole kwa yale yaliyotokea na yanayoendeleakutokea katika nchini na nje ya nchi kuhusu sisi(madaktari).Pole kwa kumuuguzamwenzetu Ulimboka Steven(Dkt), Kushtakiwa kwa MAT, Kuhojiwa kwa Rais wetu NamalaMkopi(Dkt), Kufukuzwa kwa madaktari walio mafunzoni (Intern doctors), vitisho kwa wakuu wa idara n.k.

Mwaka huu Vyuo vikuu na shirikishi vya afya na tibavinategemea kutoa wahitimu kama ifuatavyo:

-MUHAS (150), KCMC(80), WBUCHS(50), HKMU(55), IMTU(45) naUDOM(0).
Kati ya hawa wapo wageni(foreigners) watakaorudi ktk nchizao, wapo ambao watakwenda kufanya internship katika hospitali za binafsi, nawapo wataenda kufanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali(NGO)-kwaniinternship si lazima kufanya, ila hadi pale utakapoamua kufanya kazi katikahospitali. Kinachonishangaza serikali inasema inategemea madaktari 700 kutokavyuoni, inawatoa wapi?

MAONI:
Inawezekana katika kila jambo la nchi hii siasa(propaganda)imeingizwa, lakini si katika fani ya udaktari, hii ni fani(Profession) nainapaswa kuheshimiwa kama ilivyo. Si ajabu kiongozi kufika pale Hospitali yaTaifa na kukosa kipimo na kuambiwa kwenda Aga Khan au Regency, utamsikiaakisema "kwani havipo hapa" ukimweleza kuwa ni vibovu utasikia "wanapaswakuwakumbuka"..hii ni moja ya kauli ya kiongozi mmoja mkubwa serikalini!

-Si ajabu kumkutaSpecialist akifatilia damu kule Bloodbank,
-Si ajabu kumkuta Specialist analalamika hawezikuendelea na upasuaji kwani gloves zimembana sana(Sio saizi yake) nakushindwa kutumia vifaa vizuri,

Si ajabu kumkuta Specialist akisubiri hadi nguo za upasuajieti nguo hakuna!
Si ajabu kumkuta Specialist amejifunga shirt kichwani kamakofia, Si ajabu kumkuta specialist amevaa gauze kama mask!!
Si ajabu kumkuta Daktari amejihatarisha(being exposed) na damulakini hakuna Post Exposure Prophylaxis(PEP)

Hii ni katika hopitali ya Taifa, sasa jiulize kama hospitaliya Taifa hali ni hii, katika hospitali nyingine hali ikoje??

Kwa specialist, resident, registrar, interns wenye tabia ya kulalamika na kudaimabadiliko, ni mabadiliko yapi mnayoyadai ili hali muda wa mabadiliko hamsimamiimara katika kudai haki yenu??

Sitegemei madaktari wote kudai haki yao (kwani najua wasalitiwapo tu) lakini zaidi ya yote ni hawa wanaokuwa vuguvugu na wanafiki!!

KAMA WAZAZI/WALEZI
:

Mnawafundisha nini hawa wadogo wenu na watoto wenu, kuhusu kudai haki yako ya kikazI, "I know it is wisdom that takes courage to sit down and listen but it is the same wisdom which takes courage to stand for your right".

KAMA VIONGOZI/WALIMU:
Unapokuwa ukipita round na wanafunzi wako(medical students,interns, registrar, residents), unajisikia nini pale wagonjwa wanapokufiakatika round, kwa sababu tu ya kukosa huduma ambayo ungeweza kutoa kwa mgonjwana kuwa chahu kwa wanafunzi wako? Wanafunzi wanakuonaje wakati ukisema, "in other countries they could have done soand so" wakati muda wa kudai hivyo vifaa na dawa hizo ndio huu? Wanafunziwako wankuonaje wewe kama specialistwakati wenzako wako katika mgomo wewe unapita round, tena wanafunzi wako wakiwana vitambulisho tu bila makoti, wewe ukiwa na koti?

KAMA WASTAAFU NAMADAKTARI BINGWA WATARAJIWA:
Wakati wadogo/watoto wetu(intern doctors) waakiwa wameachiwamzigo huu, najiuliza kwa mfano tunapokuwa katika MWR, Discussion Panel huwatunapima uwiano wa wagonjwa na treatment options:
Leo hii tukipima Option ya MASS RESIGNATION inashindikana?

-Neurosurgeons(4),
-Orthopeadicsurgeons(15),
-Pediatricians(30),
-ObGynaecologists(45),
-Physicians(60)regardless of subspeciality ie Neurolgist, Gastroenterologist,etc.
-Psychiatrist(30)-notpsychologist,
-Surgeons (40)-regardlessof subspecialty like Cardiothoracic, Plastic surgeons etc,
-Otorhinolaryngologist(20),
- Anaesthiologist 25(notanaeshetist),
-Opthamologist 30(notoptician,optometrist)…HII NI IDADI KWATANZANIA NZIMA.

Hofu kwetu kama specialists na hawa residents ni kwamba mafao, lakini tujiulize leo kama Profesa anapewa mafao ya 50,000/=Tshs kwamwezi hii ndiyo inayokufanya usigome au kuamua kuresign? Kweli?

-Cha kushangaza kuna megabrains nyingi sana za kutegemewa lakini wanaact kama hawajui hili, naamini specialists, Residents, registrar nainterns pamoja na medical students tulikuwa na APGAR SCORE ya 10 – 10!! Sasa inakuwaje microbrains ifanye hivi kwa megabrains.

If I weigh the option of mass resignation I believe it fits the puzzle, because I believe it won't take even a month for the government to call us back to the discussion table (UNDER OUR TERMS THIS TIME) , and in the mean time(I dare to believe that none of us can perish because of financial crisis).

On the other side the Government cant import other doctors,look at WHO doctor-patient ratio, every country needs one, and for those whothink they will import, ask yourself these questions from which country? Will theybe able to pay them(THIS should be above their home salary), accommodation,transport?

This is a profession(medical terminologies) and not just mere English, I bet they might needtranslators, how many? Will they pay them? Will those doctors work in thisenvironment or they have to come with medical equipments, medicine? For howlong will they have to stay here? Will they gain trust to people(rapport etc)?

Hebu tusimame pamoja katika hili, mengi yanafanyika bila mpango hukumu kusomwa mahakamani wakati huo huo, interns kufukuzwa ..sasa unajiuliza kesi ya nini kama tayari wameshafukuzwa, na Rais kuingilia madaraka ya mahakama (kutoa hukumu wakati jambo hilo hilo kukataliwa bungeni), lakini kuumizwa sana kwa Dkt,UlimbokaSteven.

PLEAD/CALL: LET US STAND TOGETHER NOW MORE THAN EVER, THIS TIME NOT IN TOTAL TOOLS DOWN BUT IN MASSRESIGNATION.

Umejiunga tarehe 1 July 2012 ili kuleta hii makitu. Huna dhamira ya kweli wewe, na kama unahitaji hayo mambo yoote, si uende huko private? Ni kwa nini specialists, huwa hawaanzishi mgomo mpaka muwatoe chambo Interns? Hamla lolote. Hivi sasa vijana wametimuliwa na kufutiwa usajili wa muda, nyie mnakula tu. Drs. Hawana umoja, full matabaka, mara kikao cha Specialists, Mara kikao cha residents, mara kikao cha registrars. Mzee uwezi resign na wende unapopataka. Kwa taarifa yako, siyo Drs, wote wananjaa kama zako mzee!
 
Mambo vp wana JF?
Mimi naungana mkono kabisa na maDr. lakini siku nyingi tokea ule mgomo wa kwanza mimi nilikuwa nasema kama madai na kuboresha basi na sisi professional nyingine wangetushirikisha basi. Mimi nauhakika kabisa huu mgomo ungechukuwa wiki moja tu serikali ingekuwa imeshakaa sawa.

Wewe fikiria tu kusewe na maDr. ,nurses, wahudumu wote hadi motuary ,EMD's hadi kwa wakina mama wajawazito, nchi nzima mimi nakwambia ungechukua siku 2 hadi wiki tu. sisi wanasayansi hatuna maneno mengi sisi ni vitendo tu.

Sasa unashangaa maDr bado hawataki kuwahusisha hata manurse tu ndio maana mgomo unakuwa mgumu coz wagonjwa wardini wanachopewa kule ni care tu. Kwahiyo hospitali sio madokta tu jamani.

Nawasilisha hoja.
 
ningependa kutoa pole kwa yale yaliyotokea na yanayoendeleakutokea katika nchini na nje ya nchi kuhusu sisi(madaktari).pole kwa kumuuguzamwenzetu ulimboka steven(dkt), kushtakiwa kwa mat, kuhojiwa kwa rais wetu namalamkopi(dkt), kufukuzwa kwa madaktari walio mafunzoni (intern doctors), vitisho kwa wakuu wa idara n.k.

mwaka huu vyuo vikuu na shirikishi vya afya na tibavinategemea kutoa wahitimu kama ifuatavyo:

-muhas (150), kcmc(80), wbuchs(50), hkmu(55), imtu(45) naudom(0).
kati ya hawa wapo wageni(foreigners) watakaorudi ktk nchizao, wapo ambao watakwenda kufanya internship katika hospitali za binafsi, nawapo wataenda kufanya kazi katika asasi zisizo za kiserikali(ngo)-kwaniinternship si lazima kufanya, ila hadi pale utakapoamua kufanya kazi katikahospitali. Kinachonishangaza serikali inasema inategemea madaktari 700 kutokavyuoni, inawatoa wapi?

maoni:
inawezekana katika kila jambo la nchi hii siasa(propaganda)imeingizwa, lakini si katika fani ya udaktari, hii ni fani(profession) nainapaswa kuheshimiwa kama ilivyo. Si ajabu kiongozi kufika pale hospitali yataifa na kukosa kipimo na kuambiwa kwenda aga khan au regency, utamsikiaakisema "kwani havipo hapa" ukimweleza kuwa ni vibovu utasikia "wanapaswakuwakumbuka"..hii ni moja ya kauli ya kiongozi mmoja mkubwa serikalini!

-si ajabu kumkutaspecialist akifatilia damu kule bloodbank,
-si ajabu kumkuta specialist analalamika hawezikuendelea na upasuaji kwani gloves zimembana sana(sio saizi yake) nakushindwa kutumia vifaa vizuri,

si ajabu kumkuta specialist akisubiri hadi nguo za upasuajieti nguo hakuna!
si ajabu kumkuta specialist amejifunga shirt kichwani kamakofia, si ajabu kumkuta specialist amevaa gauze kama mask!!
si ajabu kumkuta daktari amejihatarisha(being exposed) na damulakini hakuna post exposure prophylaxis(pep)

hii ni katika hopitali ya taifa, sasa jiulize kama hospitaliya taifa hali ni hii, katika hospitali nyingine hali ikoje??

kwa specialist, resident, registrar, interns wenye tabia ya kulalamika na kudaimabadiliko, ni mabadiliko yapi mnayoyadai ili hali muda wa mabadiliko hamsimamiimara katika kudai haki yenu??

sitegemei madaktari wote kudai haki yao (kwani najua wasalitiwapo tu) lakini zaidi ya yote ni hawa wanaokuwa vuguvugu na wanafiki!!

kama wazazi/walezi
:

mnawafundisha nini hawa wadogo wenu na watoto wenu, kuhusu kudai haki yako ya kikazi, "i know it is wisdom that takes courage to sit down and listen but it is the same wisdom which takes courage to stand for your right".

kama viongozi/walimu:
unapokuwa ukipita round na wanafunzi wako(medical students,interns, registrar, residents), unajisikia nini pale wagonjwa wanapokufiakatika round, kwa sababu tu ya kukosa huduma ambayo ungeweza kutoa kwa mgonjwana kuwa chahu kwa wanafunzi wako? Wanafunzi wanakuonaje wakati ukisema, "in other countries they could have done soand so" wakati muda wa kudai hivyo vifaa na dawa hizo ndio huu? Wanafunziwako wankuonaje wewe kama specialistwakati wenzako wako katika mgomo wewe unapita round, tena wanafunzi wako wakiwana vitambulisho tu bila makoti, wewe ukiwa na koti?

kama wastaafu namadaktari bingwa watarajiwa:
wakati wadogo/watoto wetu(intern doctors) waakiwa wameachiwamzigo huu, najiuliza kwa mfano tunapokuwa katika mwr, discussion panel huwatunapima uwiano wa wagonjwa na treatment options:
leo hii tukipima option ya mass resignation inashindikana?

-neurosurgeons(4),
-orthopeadicsurgeons(15),
-pediatricians(30),
-obgynaecologists(45),
-physicians(60)regardless of subspeciality ie neurolgist, gastroenterologist,etc.
-psychiatrist(30)-notpsychologist,
-surgeons (40)-regardlessof subspecialty like cardiothoracic, plastic surgeons etc,
-otorhinolaryngologist(20),
- anaesthiologist 25(notanaeshetist),
-opthamologist 30(notoptician,optometrist)…hii ni idadi kwatanzania nzima.

hofu kwetu kama specialists na hawa residents ni kwamba mafao, lakini tujiulize leo kama profesa anapewa mafao ya 50,000/=tshs kwamwezi hii ndiyo inayokufanya usigome au kuamua kuresign? Kweli?

-cha kushangaza kuna megabrains nyingi sana za kutegemewa lakini wanaact kama hawajui hili, naamini specialists, residents, registrar nainterns pamoja na medical students tulikuwa na apgar score ya 10 – 10!! Sasa inakuwaje microbrains ifanye hivi kwa megabrains.

if i weigh the option of mass resignation i believe it fits the puzzle, because i believe it won't take even a month for the government to call us back to the discussion table (under our terms this time) , and in the mean time(i dare to believe that none of us can perish because of financial crisis).

on the other side the government cant import other doctors,look at who doctor-patient ratio, every country needs one, and for those whothink they will import, ask yourself these questions from which country? Will theybe able to pay them(this should be above their home salary), accommodation,transport?

This is a profession(medical terminologies) and not just mere english, i bet they might needtranslators, how many? Will they pay them? Will those doctors work in thisenvironment or they have to come with medical equipments, medicine? For howlong will they have to stay here? Will they gain trust to people(rapport etc)?

hebu tusimame pamoja katika hili, mengi yanafanyika bila mpango hukumu kusomwa mahakamani wakati huo huo, interns kufukuzwa ..sasa unajiuliza kesi ya nini kama tayari wameshafukuzwa, na rais kuingilia madaraka ya mahakama (kutoa hukumu wakati jambo hilo hilo kukataliwa bungeni), lakini kuumizwa sana kwa dkt,ulimbokasteven.

plead/call: Let us stand together now more than ever, this time not in total tools down but in massresignation.

hapo kwenye red, nafikiri wewe una matatizo. Siyo kila daktari alikiwa na score ya 10-10! Wewe unaonesha bado ni kilaza sana!
 
Tuko pamoja madaktari lakini wazo langu ni moja tu, acheni ubaguzi hospitali sio maDr tu, washirikisheni na manesi tu sisi wengine tuwe nyuma yenu ndio mafanikio yataonekana.

Kama kweli mnadai kuboreshewa mazingira ya kazi basi wauguzi nao wapo kwenye mazingira hayohayo lakini kwenye madai yenu sijaona kama mligusia. Mkiunganisha nguvu mimi naamini kabisa hamtachukua muda serikali itakaa sawa.
 
Umeongea vizuri sana, ila hiyo haiwezekani kwa mind set and courage ya Mtanzania.

Ninachowashangaa nyie madr ni kimoja tu, kwanini unaanzisha kitu huwezi kukimaliza! hebu ona sasa ulimboka sijui Olimboka wa watu kaumizwa bure na rais wa mat ana kesi alafu wengine wamefukuzwa wengine wanarudi!!!!!!!

C'com guys DONT HUNT WHAT YOU CANT KILL.

YAANI MMENIBOA SAAAANA MADR, MMEGOMA MMESABABISHA UNREST ALAFU MNARUDI BILA HATA DAI MOJA KUTIMIZWA!!! SERIOUSLY!!! :redface:

ndo hapo sasa
 
Mambo vp wana JF?
Mimi naungana mkono kabisa na maDr. lakini siku nyingi tokea ule mgomo wa kwanza mimi nilikuwa nasema kama madai na kuboresha basi na sisi professional nyingine wangetushirikisha basi. Mimi nauhakika kabisa huu mgomo ungechukuwa wiki moja tu serikali ingekuwa imeshakaa sawa.

Wewe fikiria tu kusewe na maDr. ,nurses, wahudumu wote hadi motuary ,EMD's hadi kwa wakina mama wajawazito, nchi nzima mimi nakwambia ungechukua siku 2 hadi wiki tu. sisi wanasayansi hatuna maneno mengi sisi ni vitendo tu.

Sasa unashangaa maDr bado hawataki kuwahusisha hata manurse tu ndio maana mgomo unakuwa mgumu coz wagonjwa wardini wanachopewa kule ni care tu. Kwahiyo hospitali sio madokta tu jamani.

Nawasilisha hoja.

I tend to agree with you. It is increasingly clear that they seem to suffer from some kind of superiority complex which is a destructive malady just like inferiorty complex is.
 
Madaktari nguvu yao ilikuwa inategemea msimamo wa Dr Ulimboka,wanasambaratika kirahisi mpaka inashangaza! Hakuna mbinu ya ajabu serikali iliyotumia,hakuna tena watu wa kusimama mbele ili kuwatia ujasiri uliopotea! Imefikia mahali hamueleweki tena! Kazi ipo! Tuendelee kusubiri marekebisho ya sekta ya umma kwa ahadi za milele!
 
Back
Top Bottom