Pendael laizer
JF-Expert Member
- Jan 14, 2012
- 958
- 101
serikali inatakiwa itafute suluhu haraka
acha watibu jamani watu wachini sisi tusiokuwa na uwezo tutakwisha wabaki matajiri tena wawaongeze kabisa na wanajeshi na hata polisi kama wapo
warudi kwa wingi ili kuokoa ndugu zetu wanaotaka kupoteza maisha kutokana na mgomo huu. Mi naona ni ubinadamu zaidi kuliko maslai.
nadhani hiyo ni immediate measure kwa tatizo hili wakati wanatafuta suluhisho la kudumu.
Sidhani kama serikali itawacha wagonjwa wafe vivi hivi, hata kama madaktari wamegoma. Kama manesi nao wangegoma nadhani wangeomba hata watu wa kujitolea wa-attend kwa muda wagonjwa.
Ni maamuzi mazuri.
Katika gazeti la mwananchi la leo kuna picha ya daktari mstaafu ambaye serikali imemuajiri kwa mkataba maalum. Watakuwa wengi. Hawa wastaafu wanatumika kuziba pengo la madaktari waliogoma. Ni halali kwao kufanya hivyo? Haikuwa kwao sawa kuwaunga wenzao mkono katika kudai maslahi yao? Au kwa vile wao enzi zao zimepita na hawana cha kupoteza. Labda kwa wakati fulani walishiriki kuihujumu Muhimbili na hospitali zingine kwa kuiba wagonjwa na madawa na vifaa vingine wakahamishia kwenye zahanati zao. Nafikiri ilikuwa wakati muafaka kwao kuwaunga mkono wenzao. Serikali kitu ambacho ingeweza kufanya ni kwenda huko makambi ya jeshi na kuwachukua madaktari wanajeshi kuja kutumika kwenye hiki kipindi cha mputo
RAT RACE IYO MKUU; wakati wa ujana wao wali spend kila shilingi waliyo make and more, walikopa kila kona wanayoweza kukopa; fainali uzeeni imewadia pensheni imeisha; sasa ni mizinga tu kwa vijana wao. Unategemea akipata dili la kuingiza mshiko aliache (heri lawama kaka kuliko....)
Nna imani asilimia kubwa ya wastaafu wakiambiwa warudi maofisini watachekelea mpaka pengo la mwisho.
na wameshachemsha leo wanaitisha kikao na uongozi wa mnh kuwaambia workload ni kubwa mno wapunguziwe wasiingie kwenye operation...serikali yetu na viongozi wenye ufinyu wa akili ndio wanaowaua wagonjwa
Walio kazini wanadai nyongeza ya maslahi na kujiudhuru kwa Blandina!...Sasa aliyestaafu ataungana na walio kazini kwa lipi?...kutetea fani tu au?
hakuna ambaye anapenda kulipwa kidogo. Tatizo ni hao wenye dhamana wanagawa kidogoMnaounga mkono madaktari kugoma kwa madai kuwa kazi yao ngumu so wanastahili malipo makubwa nielezeni ni professional gani inatakiwa kulipwa kidogo?
Mnaounga mkono madaktari kugoma kwa madai kuwa kazi yao ngumu so wanastahili malipo makubwa nielezeni ni professional gani inatakiwa kulipwa kidogo?
> Ni kweli serikali yatakiwa si tu kutafuta ufumbuzi, ila suluhu na uzalendo kwa upade wa madaktari ni bora zaidi.serikali inatakiwa itafute suluhu haraka
. Asiye njaa ni nani? Si vyema kuwatuhumu na kuwahukumu, na je kama wanasukumwa na dhamira ya huruma na uzalendo, ni vyema tukawa na maelezo ya kisayansi zaidi kuliko kuwa nafikra chafu na mbaya. Saikolojia inaeleza bayana juu ya huruma na uzalendo umri unapokuwa mkubwa lakini pia kwa maelezo ya Freud ttutumiayo yanaweza kueleza tabia zetu na hulka. rejea psychoanalysisNjaa inawasambua,TZ watu wakistaafu asilimia kubwa huomba wafanye kazi kwa mkataba.Hawa ma Dr wastaafu hapo wanaomba mgomo usiishe!kufa kufaana