Madaktari wastaafu kutumika Muhimbili ni usaliti au uzalendo?

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,848
2,669
Katika gazeti la mwananchi la leo kuna picha ya daktari mstaafu ambaye serikali imemuajiri kwa mkataba maalum. Watakuwa wengi. Hawa wastaafu wanatumika kuziba pengo la madaktari waliogoma. Ni halali kwao kufanya hivyo? Haikuwa kwao sawa kuwaunga wenzao mkono katika kudai maslahi yao? Au kwa vile wao enzi zao zimepita na hawana cha kupoteza. Labda kwa wakati fulani walishiriki kuihujumu Muhimbili na hospitali zingine kwa kuiba wagonjwa na madawa na vifaa vingine wakahamishia kwenye zahanati zao. Nafikiri ilikuwa wakati muafaka kwao kuwaunga mkono wenzao. Serikali kitu ambacho ingeweza kufanya ni kwenda huko makambi ya jeshi na kuwachukua madaktari wanajeshi kuja kutumika kwenye hiki kipindi cha mputo
 
Huo si ufumbuzi wa tatizo, na watakaokubali wengi ni wale ambao wako choka mbaya. Wengine wako busy na mambo yao, hawatakubali kuwaste time. Unless wapewe mpunga wa kueleweka zaidi.
 
Walio kazini wanadai nyongeza ya maslahi na kujiudhuru kwa Blandina!...Sasa aliyestaafu ataungana na walio kazini kwa lipi?...kutetea fani tu au?
 
hivi kweli wananchi wanashindwa kuingilia kati swala hili na kuishinikiza serikal ili itatue tatizo walilonalo kati yao na madaktari, kwani nikiangalia hapa anaeumia ni mwananchi na wala si vinginevyo.
 
Walio kazini wanadai nyongeza ya maslahi na kujiudhuru kwa Blandina!...Sasa aliyestaafu ataungana na walio kazini kwa lipi?...kutetea fani tu au?

nadhani hiyo ni immediate measure kwa tatizo hili wakati wanatafuta suluhisho la kudumu.
Sidhani kama serikali itawacha wagonjwa wafe vivi hivi, hata kama madaktari wamegoma. Kama manesi nao wangegoma nadhani wangeomba hata watu wa kujitolea wa-attend kwa muda wagonjwa.
Ni maamuzi mazuri.
 
warudi kwa wingi ili kuokoa ndugu zetu wanaotaka kupoteza maisha kutokana na mgomo huu. Mi naona ni ubinadamu zaidi kuliko maslai.
 
binafsi niliona kama ingekuwa jambo la busara kwa hawa wastaafu kuendelea na mambo yao kuliko kutumika. Wao wanayafahamu madhila ya kwa daktari wa umma, na kwa kiasi kikubwa serikali imewaondolea moyo wa uzalendo.
 
nadhani hiyo ni immediate measure kwa tatizo hili wakati wanatafuta suluhisho la kudumu.
Sidhani kama serikali itawacha wagonjwa wafe vivi hivi, hata kama madaktari wamegoma. Kama manesi nao wangegoma nadhani wangeomba hata watu wa kujitolea wa-attend kwa muda wagonjwa.
Ni maamuzi mazuri.

hii immediate measure ingetumika kama kungekuwa na upungufu wa madaktari kwa sababu zingine zaidi ya migomo. Au kungetokea maradhi-epidemic kama flue na kipindupindu kiasi cha kusababisa madaktari kuonekana wachache. Hili tatizo la sasa ni la kupikwa na wapishi wanajulikana. Serikali inajua kuwa hata hawa wakigoma tuna wastaafu na wanajeshi wa kufidia upungufu. Hili ni tatizo
 
Tushukuru tu kwamba ni Tanzania. Ingekuwa ni nchi nyingine hao madaktari wastaafu wangekiona cha moto.
 
warudi kwa wingi ili kuokoa ndugu zetu wanaotaka kupoteza maisha kutokana na mgomo huu. Mi naona ni ubinadamu zaidi kuliko maslai.

ubinadamu si kitu. Utu zaidi. Utu ulitakiwa uanzie kwa watendaji wizarani na serikalini
 
yule daktar Tamimu bushiri aliwahi kupigwa na baba wa katoto kachanga kwa tuhuma za kussbabisha kifo cha kichanga hicho.
 
Kutibiwa na watu ambao miili na akili vilikwishachoka nayo ni shida nyingine!
 
Fani hailipi ndio unastaafu unabaki kula matembele nyama sikukuu lazima urudi kazini
 
acha watibu jamani watu wachini sisi tusiokuwa na uwezo tutakwisha wabaki matajiri tena wawaongeze kabisa na wanajeshi na hata polisi kama wapo
 
acha watibu jamani watu wachini sisi tusiokuwa na uwezo tutakwisha wabaki matajiri tena wawaongeze kabisa na wanajeshi na hata polisi kama wapo

yawezekana kipindi hiki wanajeshi wamewagomea maana kuna wakati walichukuliwa wakapelekwa Muhimbili, nadhani kulikuwa na mgomo tena kipindi hicho
 
Back
Top Bottom