Angel Msoffe
JF-Expert Member
- Jun 21, 2011
- 6,781
- 1,639
Kova na pinda wajisalimishe kwanza kwa wananch mana wao ndo watuhumiwa wakuu
Kova alisema Dkt. Ulimboka alikuwa na rafiki yake aitwaye Dkt. Deogratius Michael na watu wengine katika Klabu ya Leaders Kinondoni ambapo ghafla saa 5:30 usiku, walitokea watu watano wasiofahamika wakavamia klabu hiyo na kuwatishia na kuwataka walale chini.
Sawa kabisa na kwa kuongezea mbona Kova kwenye maelezo yake hamtaji yule mtu wa ikulu alie kuwa akimpigia sim mara kwa mara Dk Ulimboka kuwa waonane??? na je huyo jamaa wa ikulu yupo chini ya ulinzi kuisaidia police??? Kova angewataka waliomteka Dk Ulimboka wajisalimishe ningemwelewa!!!! ama kweli hii ni Tanzania ya leo!!!!!!!!!!!!Yote hii ni katika jitihada za kupoteza lengo. Hivi inakuwaje huyo mpelelezi anatoa taarifa kwa wenzie kuwa bado yupo hai angali walishafika Hospitalini. Angetoa taarifa hiyo akiwa Mabwepande ili serikali ilete usafiri wa haraka kumfikisha Hospitali tungemuelewa. Kama angekuwa mpelelezi wa kweli, angefatilia waliotenda uhalifu huo bila ya kujali kama Dr.Uli alikuwa hai ama amefariki.
Kova huyu huyu au mwingine? Hvi ni kova wa intelejensia ya al-shabaab au mwingine? Hiv ni kova huyu wa cctv za posta kwa ajili ya jerry mulo au mwingine?
cova = zombekova huyu huyu au mwingine? Hvi ni kova wa intelejensia ya al-shabaab au mwingine? Hiv ni kova huyu wa cctv za posta kwa ajili ya jerry mulo au mwingine?
Imethibitishwa kuwa Klabu ya Leaders ilivamiwa?Kova alisema Dkt. Ulimboka alikuwa na rafiki yake aitwaye Dkt. Deogratius Michael na watu wengine katika Klabu ya Leaders Kinondoni ambapo ghafla saa 5:30 usiku, walitokea watu watano wasiofahamika wakavamia klabu hiyo na kuwatishia na kuwataka walale chini.
"Dokta Ulimboka na wateja wengine walilala chini kwa kuhofia madhara kwa kuwa watu hao walikuwa na kitu wanachohisi ni silaha na hatimaye watu hao walimchukua Dkt. Ulimboka na kusema kwamba walikuwa wakimhitaji yeye na kumuingiza katika gari aina ya Suzuki Escudo nyeusi ambayo haikuwa na namba za usajili," alidai Kova.
Imethibitishwa kuwa Klabu ya Leaders ilivamiwa?
Hawa wateja wengine n akina nani? Amepatikana angalau mmoja kueleza kilichotokea hapo, kama kilitokea kama anavyosema Kova?
Msishangae kuwa ripoti ya uchunguzi ikamtaja Dr. Ulimboka kuwa ndiye aliyeongoza kundi la majambazi na wananchi wenye hasira wakamshambulia, majambazi wenzake wakamuokoa na kukimbie naye, lakini kwa kuogopa soo wakamtelekeza msituni. Tanzania kinaweza kutokea chochote, halmuradi tu walioko madarakani waendelee kubakia madarakani.
Kwa mtu muongo, ukweli wake ndio kweli wake. Huyu hufika pahali akaamini kuwa uongo anaosema ndio kweli na kama ni kiongozi basi ni ukweli usiopingika. Mungu ainusuru Tanzania, tunaelekea kubaya sana.Yaani we acha tu...hawa jamaa wanafikiria wamejificha kumbe wanaonekana. Uzuri ni kuwa ukweli pekee ndio unaotuweka huru.
Katika kundi la chui ati anajitokeza chui mmojawapo anasema yeye ni chui mpole sana na hana ugomvi na mbusi, kwa hiyo anadai wale mbusi waliojaribu kumvamia chui mmojwawao ajisalimishe. Hasemsemi chui mwenzake ajisalimishe kuomba radhi kwa mbusi, ati mkosefu sana ni mbusi, halafu anaahidi atawachunguza chui waliohusika kumrarua mbusi kwa utaalam na umakini. Anavyoongea hivyo yuko pamoja na yule chui mkorofi nambari moja ambaye anawajua wenzake aliokuwa nao kujeruhi mbusi. teh teh teeeeeeeh! Kova amesahau kwamba anaongelea walioenda shule miaka sio chini ya miaka 5 na wamefunzwa saikologia pia, te teh teh teeeeeeh! Anadhani anaongea na wanakijiji mabwepande ambako ndio msitu wanaoutumia mapolisi kuua raia (Viz yule mpora madini ya wafanya biashara maarufu)Huyu kova anajichanganya bwana. Siyo mkweli na anaonesha wazi kuwa anaijua mision yote.