Madaktari waliomshambulia askari wajisalimishe - Kamanda Kova | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari waliomshambulia askari wajisalimishe - Kamanda Kova

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fred Katulanda, Jun 28, 2012.

 1. Fred Katulanda

  Fred Katulanda Verified User

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 1, 2011
  Messages: 229
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Wakati Dkt. Ulimboka alipofikishwa nje ya Kitengo cha Mifupa (MOI), Madaktari wenzake ambao wamesusa kuhudumia wagonjwa, walifurika hospitalini hapo na kuanza kusukuma gari hilo huku wakiimba nyimbo za mshikamano na wengine wakilia.

  Hata hivyo, katika kile kilichoonekana ni kulipiza kisasi, Madaktari hao ghafla walimgeukia mmoja wa askari Polisi aliyekuwa amevalia kiraia na kumshambulia kwa kipigo kwa madai kuwa aliwasiliana na wenzake na kuwataarifu kuwa Dkt. Ulimboka bado yuko hai.

  Askari huyo pia alinyang'anywa simu na redio ya mawasiliano ambavyo vyote viliharibiwa vibaya na alionekana akiwa ameumizwa na kuvimba mwilini huku akiwa hajapatiwa huduma yoyote.

  Kutokana na majeraha hayo, askari wenziwe walimuondoa eneo hilo; na mara moja Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewataka waliomshambulia askari huyo kujisalimisha.

  Kova aliyezungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo, alikemea tabia ya wananchi kujichukulia hatua mkononi kwa kumshambulia askari huyo na kuongeza kuwa alikuwa kazini akichunguza tukio hilo.

  Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Namala Mkopi, alidai Dkt. Ulimboka alitekwa juzi usiku na watu wasiojulikana na kupigwa na kung'olewa kucha na meno na hali yake ni mahututi.

  Alidai Dkt. Ulimboka alizungumza kwa taabu alipofikishwa hospitalini ambapo alidai juzi jioni alipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kama Abduel anayedaiwa kutoka Ikulu na alitaka kuzungumza naye kuhusu maendeleo ya madai ya madaktari.

  "Alikubali kuonana na mtu huyo ambaye pia alikuwa akizungumza naye mara kwa mara na alikubaliana na wenzake asiende kuonana naye mwenyewe, aliongozana na rafiki yake Dk Deo hadi eneo walilopatana ambalo ni Kinondoni barabara ya Tunisia," alisimulia Dkt. Mkopi.


  Alidai Dkt. Ulimboka alisimulia kuwa akiwa katika eneo hilo pamoja na Abduel na Dkt. Deo, walitokea watu watatu; wawili wakiwa na silaha aina ya bastola na mmoja bunduki.

  Kwa mujibu wa madai ya Dkt. Ulimboka, watu hao walianzisha vurugu na kuwataka wengine waondoke na kumchukua peke yake na kumuingiza kwenye gari nyeusi yenye namba zisizosajiliwa na kutokomea naye.

  Kwa mujibu wa madai hayo, Dkt. Deo aliamua kuwasiliana na wenzake ambao walimtafuta kwenye vituo vyote vya Polisi bila mafanikio na kuishia kuandika maelezo ya tukio hilo katika Kituo Kikuu cha Polisi.

  Baada ya hapo, Dkt. Deo pia aliwasiliana na wanaharakati akiwamo Mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC) Hellen Kijo-Bisimba. Anadai alipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kuwa ni msamaria kwamba amemuokota Dk Ulimboka akiwa hoi eneo la Mabwepande.

  Inadaiwa Dkt. Deo aliwachukua wanaharakati hao hadi Kituo cha Polisi Bunju alikopelekwa Dk Ulimboka na kumchukua na kumkimbiza Muhimbili.

  Kova alisema Dkt. Ulimboka alikuwa na rafiki yake aitwaye Dkt. Deogratius Michael na watu wengine katika Klabu ya Leaders Kinondoni ambapo ghafla saa 5:30 usiku, walitokea watu watano wasiofahamika wakavamia klabu hiyo na kuwatishia na kuwataka walale chini.

  "Dokta Ulimboka na wateja wengine walilala chini kwa kuhofia madhara kwa kuwa watu hao walikuwa na kitu wanachohisi ni silaha na hatimaye watu hao walimchukua Dkt. Ulimboka na kusema kwamba walikuwa wakimhitaji yeye na kumuingiza katika gari aina ya Suzuki Escudo nyeusi ambayo haikuwa na namba za usajili," alidai Kova.

  Alidai wakati wakiwa njiani, watu hao walianza kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake na bila kusema wanataka nini kutoka kwake na walipofika maeneo ya Mwenge, walimvisha fulana nyeusi usoni na hakujua tena wanaelekea wapi huku wakiendelea kumpiga na mmoja wa watu hao akasema watamuua.

  Kamanda Kova alidai ilipofika asubuhi, Dkt. Ulimboka alijikuta yupo msitu wa Mambwepande na alijivuta hadi barabarani na alikutwa na msamaria akiwa amefungwa kamba miguuni na mikononi.

  Kwa mujibu wa Kamanda Kova, Dkt. Ulimboka alieleza kuwa gari yake aliiacha maeneo ya Leaders Club na watu hao waliuchukua ufunguo wake, nyaraka zake pamoja na fedha ambazo hakumbuki ni kiasi gani.

  Kamanda Kova alisema ameunda jopo la wapelelezi wa fani mbalimbali chini ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa kushirikiana na mlalamikaji mwenyewe na mashahidi walioona tukio hilo, ili uchunguzi wa shauri hilo ufanyike na kuwaomba raia wema kutoa ushirikiano ili matukio ya aina hiyo yasijirudie.

  "Naamini kwamba watu wengi watakuwa wameguswa na tukio hili ila nawasihi watuache polisi tufanye upelelezi na waachane na minong'ono kwa kuwa sisi hatukuwa na ugomvi wowote na Dk Ulimboka wala madaktari… upelelezi utafanyika kwa makini na taarifa rasmi zitatolewa baadaye." alisema.

  ---
  Taarifa via blogu ya Zito&Tina  Source: Madaktari waliomshambulia askari wajisalimishe - Kova - wavuti
   
 2. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Mwache kova awapeleke ffu na mabunduki yao na madaktari watumie vifaa vyao kujibu mapigo, piga sindano za ganz polis wote wafreeze..
   
 3. j

  jigoku JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Kova ni muongo kama tu ilivyoutamaduni wa jeshi la polisi kupindisha maneno,na kama hali iko hivyo haoni ni kutaka kusogeza ukweli kwa wananchi kwa kuwa askari huyo alisikika akipiga simu huku akiwaeleza wenzake ya kuwa yuko hai,hapo tunapata picha ya kuwa kulikuwa na mpango maalumu ambao hata huyu askari aliepigwa ma madaktari na wananchi wengine alihusika na utekaji wa Dr ulimboka.na kama watatumia maguvu kitaeleweka mbele ya safari
   
 4. F

  FJM JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Maelezo ya Kova yanaanza kwenda kushoto. Hapo kwenye red, ni tofauti na maelezo aliyotoa Dr Ulimboka mwenyewe ambapo alisema watu walikuja na kumuita pembeni. Sasa hizi taariza za wateja kulala chini Kova katoa wapi?
   
 5. H

  Hodarism Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Usalama wa nchi uko mashakani, haiwezekani Mtu achukuliwe kutoka leaders mpk Mabwepande na taarifa kusambazwa na mtu kupatikana asubuhi.Hakuna wa kutulinda.Tuwe makini na ulinzi na usalama wetu sisi wenyewe. Na Leaders club ile sifa yake ya Leaders Club haina maana.
   
 6. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  stupid wajisalimishe kwanza wapumbavu wa usalama wa taifa waliomteka kamanda wetu....mmelitibua,liwalo na liwe.....aluta continua
   
 7. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  teh teh teh yaani kuna vitu vinachekesha sana jamani.
  badala ya kuamrisha wajisalimishe waliompiga daktari ulimboka yeye kova
  anasema wajisalimishe waliompiga askari!!!!
  something is very much wrong somewhere.......!
   
 8. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Majasusi waliomjeruhi Mlimboka wajisalimishe, Exchange of PoW itafuata. Hii ni vita.
   
 9. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #9
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Kova huyu huyu au mwingine? Hvi ni kova wa intelejensia ya al-shabaab au mwingine? Hiv ni kova huyu wa cctv za posta kwa ajili ya jerry mulo au mwingine?
   
 10. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #10
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Tatizo kubwa ni kwamba, tulishapoteza imani nanyi kitambo.
   
 11. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #11
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  maelezo ya kova ni ya uongo mkubwa na yapingana na maelezo aliyotoa ulimboka mwenyewe na dr deo..
   
 12. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #12
  Jun 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Yote hii ni katika jitihada za kupoteza lengo. Hivi inakuwaje huyo mpelelezi anatoa taarifa kwa wenzie kuwa bado yupo hai angali walishafika Hospitalini. Angetoa taarifa hiyo akiwa Mabwepande ili serikali ilete usafiri wa haraka kumfikisha Hospitali tungemuelewa. Kama angekuwa mpelelezi wa kweli, angefatilia waliotenda uhalifu huo bila ya kujali kama Dr.Uli alikuwa hai ama amefariki.
   
 13. meeku

  meeku JF-Expert Member

  #13
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 571
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyu kova anajichanganya bwana. Siyo mkweli na anaonesha wazi kuwa anaijua mision yote.
   
 14. m

  mamajack JF-Expert Member

  #14
  Jun 28, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  hivi mbona taarifa a watu hawa zinakinzana.jamani acheni ubabaishaji bwana,dr ulimboka alichokieleza tumesikia na ndiyo tumemwamini.
  kova:waliambiwa watu walale chini.
  nchimbi:alipigwa kibao akaanguka.
  tumeshaiona nia ya serikali ni kuwaua watanzania wasio na hatia ili watu waogope kudai haki zao.nawapongeza sana madaktari,mmeonesha ushirikiani wa juu sana,na MUNGU atamponya dr.
  uzushi mwingine huu wa wauaji kutaka kupotossha ukweli hauna maana.
   
 15. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #15
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  hawana jipwa hao polisi wapuuzi tu kazi yao kutumikia mabwana wakubwa
   
 16. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #16
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Kova ni Muongo, Msanii na Mbabaishaji ambaye hujawahi kukutana naye!

  Hadi sasa sijawahi kukutana na askari anayempenda huyu jamaa......
   
 17. s

  sawabho JF-Expert Member

  #17
  Jun 28, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Tangu lini wananchi wenye hasira a.k.a Mob justice wakajisalimisha !!!
   
 18. Rohombaya

  Rohombaya JF-Expert Member

  #18
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 8,259
  Likes Received: 3,092
  Trophy Points: 280
  Wangejisalimisha ili kuhakakisha upelelezi. Wabongo tuna hamu kujua ukweli
   
 19. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #19
  Jun 28, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  huyu kova anaarisha kwa kutumia mdomo,
  anadhani tumesahau msitu wa mabwepande ndo uko uko kamanda mwenzake zombe alipowaua wale jamaa wa madini wa ulanga??
  Uyu kova msaaulifu sana, watu wamekuwa wakiuwawa uko na askari hawahawa wa policcm...
  Hatudanganyiki namuomba mungu izi picha za dr ziwe zimeonwa na watoto wa shule primary/ sekondari ili wazidi kuichukia hii serikali ya wauwaji
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Jun 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kova angekuwa na akili timamu na kama angekuwa anasikiliza nafsi yake asingesema hayo maneno. Anaonekana wazi anaegemea upande mmoja. Na ikifika leo jioni bila ya polisi kutangaza kuwa wamekamata watu waliomfanyia unyama Dr Ulimboka bas watanzania wana haki ya kuamini kuwa serikali ya CCM ndio mhusika mkuu.
   
Loading...