Madaktari waliomshambulia askari wajisalimishe - Kamanda Kova

Kova alisema Dkt. Ulimboka alikuwa na rafiki yake aitwaye Dkt. Deogratius Michael na watu wengine katika Klabu ya Leaders Kinondoni ambapo ghafla saa 5:30 usiku, walitokea watu watano wasiofahamika wakavamia klabu hiyo na kuwatishia na kuwataka walale chini.

Maelezo haya ya kamanda kova ni tofauti kabisa na maelezo yaliyotolewa na dr. ulimboka na kuripotiwa na vyombo vya habari mathalani television, ambapo amezungumza kwamba alikamatwa katika mazingira tofauti na anavyosema kova.
Hapa lazima kutakuwa kuna mchezo unataka kuchezwa na jeshi la polisi ili kuuficha ukweli halisi. Na ukilitazama kwa makini tukio la askari kushambuliwa na madaktari baada ya kusikika akipiga simu kwamba dr.ulimboka hajafa, hapo kuna dalili za wazi kwamba polisi walikuwa wanafahamu kinachoendelea.

Na hata hiyo tume aliyoiunda sitegemei kama itafanikisha kuufahamu ukweli, sana sana itawasaidia kuuficha ukweli. Sijawahi kuwa na imani na tume za polisi kujichunguza katika matukio ambayo wao wenyewe wanakuwa ni watuhumiwa.
 
Nikimwona Kamanda Kova namkumbuka alivyokuwa akitamba wakati wa sakata la Jerry Muro. Akatengeneza hadithi nzuri iliyotuchanganya wengi .... tukagawanyika .... lakini mwisho ikaonekana ilikuwa ni Movie! Jerry Muro leo anakula vyuku kwa mrija. Hongera Kamanda Selemani Kova.
 
Yote hii ni katika jitihada za kupoteza lengo. Hivi inakuwaje huyo mpelelezi anatoa taarifa kwa wenzie kuwa bado yupo hai angali walishafika Hospitalini. Angetoa taarifa hiyo akiwa Mabwepande ili serikali ilete usafiri wa haraka kumfikisha Hospitali tungemuelewa. Kama angekuwa mpelelezi wa kweli, angefatilia waliotenda uhalifu huo bila ya kujali kama Dr.Uli alikuwa hai ama amefariki.
Sawa kabisa na kwa kuongezea mbona Kova kwenye maelezo yake hamtaji yule mtu wa ikulu alie kuwa akimpigia sim mara kwa mara Dk Ulimboka kuwa waonane??? na je huyo jamaa wa ikulu yupo chini ya ulinzi kuisaidia police??? Kova angewataka waliomteka Dk Ulimboka wajisalimishe ningemwelewa!!!! ama kweli hii ni Tanzania ya leo!!!!!!!!!!!!
 
yeye analia na simu na radio wakati sisi tunataka watekaji wa Dr.Ull wapatikane haraka hajui alitendalo.!
 
Kova alisema Dkt. Ulimboka alikuwa na rafiki yake aitwaye Dkt. Deogratius Michael na watu wengine katika Klabu ya Leaders Kinondoni ambapo ghafla saa 5:30 usiku, walitokea watu watano wasiofahamika wakavamia klabu hiyo na kuwatishia na kuwataka walale chini.

"Dokta Ulimboka na wateja wengine walilala chini kwa kuhofia madhara kwa kuwa watu hao walikuwa na kitu wanachohisi ni silaha na hatimaye watu hao walimchukua Dkt. Ulimboka na kusema kwamba walikuwa wakimhitaji yeye na kumuingiza katika gari aina ya Suzuki Escudo nyeusi ambayo haikuwa na namba za usajili," alidai Kova.
Imethibitishwa kuwa Klabu ya Leaders ilivamiwa?
Hawa wateja wengine n akina nani? Amepatikana angalau mmoja kueleza kilichotokea hapo, kama kilitokea kama anavyosema Kova?

Msishangae kuwa ripoti ya uchunguzi ikamtaja Dr. Ulimboka kuwa ndiye aliyeongoza kundi la majambazi na wananchi wenye hasira wakamshambulia, majambazi wenzake wakamuokoa na kukimbie naye, lakini kwa kuogopa soo wakamtelekeza msituni. Tanzania kinaweza kutokea chochote, halmuradi tu walioko madarakani waendelee kubakia madarakani.
 
Eeh Mungu wa Ame angalia watu wako wanavyoteseka! Nilini maneno yako yata timia mbona watu wanazidi kukata tamaa? Mungu kama uishivyo na haki yako kuu simama sasa katika kiti chako cha enzi kuwalipa waovu sawa sawa na matendo yao!
 
Imethibitishwa kuwa Klabu ya Leaders ilivamiwa?
Hawa wateja wengine n akina nani? Amepatikana angalau mmoja kueleza kilichotokea hapo, kama kilitokea kama anavyosema Kova?

Msishangae kuwa ripoti ya uchunguzi ikamtaja Dr. Ulimboka kuwa ndiye aliyeongoza kundi la majambazi na wananchi wenye hasira wakamshambulia, majambazi wenzake wakamuokoa na kukimbie naye, lakini kwa kuogopa soo wakamtelekeza msituni. Tanzania kinaweza kutokea chochote, halmuradi tu walioko madarakani waendelee kubakia madarakani.

Yaani we acha tu...hawa jamaa wanafikiria wamejificha kumbe wanaonekana. Uzuri ni kuwa ukweli pekee ndio unaotuweka huru.
 
kova si muongo inawezekana anasema ukweli labda na yeye alishiriki nyie mnambishia shauli zenu
 
Yaani we acha tu...hawa jamaa wanafikiria wamejificha kumbe wanaonekana. Uzuri ni kuwa ukweli pekee ndio unaotuweka huru.
Kwa mtu muongo, ukweli wake ndio kweli wake. Huyu hufika pahali akaamini kuwa uongo anaosema ndio kweli na kama ni kiongozi basi ni ukweli usiopingika. Mungu ainusuru Tanzania, tunaelekea kubaya sana.
 
Hawa madaktari wetu sasa wameanza kuugua ugonjwa wa akili, yaani wamesikia tu askari ana report incident kwa kusema kwamba "Yupo hai" wakachukulia moja kwa moja kwamba askari ndiye aliyehusika. sasa wao walitaka wripoti vipi kwa wakubwa zake ?

No wonder mtu anaumwa mguu wanamfanyia operation ya kichwa halafu wanasema tatizo limeshashughulikiwa.
 
Kwani polisi na wao wakiugua wanapelekwa india? kama siyo, polisi akienda hosipitali yoyote achomwe sumu tuone kama hao watawala wanaowatii kama watawaokoa.
 
Huyu kova anajichanganya bwana. Siyo mkweli na anaonesha wazi kuwa anaijua mision yote.
Katika kundi la chui ati anajitokeza chui mmojawapo anasema yeye ni chui mpole sana na hana ugomvi na mbusi, kwa hiyo anadai wale mbusi waliojaribu kumvamia chui mmojwawao ajisalimishe. Hasemsemi chui mwenzake ajisalimishe kuomba radhi kwa mbusi, ati mkosefu sana ni mbusi, halafu anaahidi atawachunguza chui waliohusika kumrarua mbusi kwa utaalam na umakini. Anavyoongea hivyo yuko pamoja na yule chui mkorofi nambari moja ambaye anawajua wenzake aliokuwa nao kujeruhi mbusi. teh teh teeeeeeeh! Kova amesahau kwamba anaongelea walioenda shule miaka sio chini ya miaka 5 na wamefunzwa saikologia pia, te teh teh teeeeeeh! Anadhani anaongea na wanakijiji mabwepande ambako ndio msitu wanaoutumia mapolisi kuua raia (Viz yule mpora madini ya wafanya biashara maarufu)
 
MADAKTARI JANA WALIFANYA UHUNI
nakiri kuwa dokta ulimboka hakutendewa haki hata kidogo. ni kitendo cha kinyama ambacho kinafaa kulaaniwa na kila mpenda amani. hata hivyo, kitendo walichofanya madaktari hakiwezi kupita bila kulaaniwa.


kazi ya udaktari ina miiko yke na masharti. daktari lazima atangulize UTU ktk kila alifanyalo. laziwa atumie busara na AWE MTU MWENYE SUBIRA YA HALI YA JUU. daktari lazima atawaliwe na UPENDO na HURUMA. daktari akiingiza UANAHARAKATI katika shughuli yke, lazima atambulike kama daktari muovu. udaktari na uanaharakati na vitu viwili tofauti. TUNDU LISSU alikua mwanaharakati akaingia ktk siasa. siasa inamshinda na anazomewa kila siku bungeni kwa kuwa siasa na uanaharakati haviendani. ameshindwa kutupa uanaharakati. kwa mwanasiasa 1+1 inweza kuwa 2, 3 4 au hata 10 kutokana na mazingira. kwa mawnaharakati 1+1 = 2, thats all.


madaktari (na wale ni wanafunzi siyo madaktari bingwa) kupiga kelele hospitalini na kuimba huku wakimkimbiza polisi kwa kumrushia mawe ni wahalifu wakubwa. ITV ilionesha tukio lile. itabidi polisi watumie ule mkanda kuwatafuta na kuwaweka ndani. wazee wetu walipigania amani ya nchi hii ili tuishi kwa amani bila tupigwa by the so called medical professionals. professionals gani hawa!? KOMBA WATAFUTE MMOJA BAADA YA MWENGINE. WATIE NDANI
 
Back
Top Bottom