Atolewa jiwe lenye uzito wa gram 800 kwenye kibofu cha mkojo kwa upasuaji

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,055
156,679
📍Mwanza

▪️MADAKTARI SEKOUTOURE WAFANIKISHA KUTOA JIWE LA GRAM 800 KWENYE KIBOFU CHA MKOJO

Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure wamefanikiwa kufanya upasuaji na kuondoa Jiwe ndani ya kibofu cha Mkojo kwa Mwanamke mwenye umri wa miaka 48.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hospitalini hapo jiwe hilo lenye uzito wa Gramu 800 lililomsumbua mhusuka kwa zaidi ya miaka mitatu.

Akizungumza leo Aprili 18, 2024 na Daktari Bingwa wa Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Dkt. Jackson Chiwaligo amesema hiyo ni mara ya kwanza kufanya upasuaji kama huo.

Dkt. Chiwaligo ameeleza kuwa mgonjwa huyo alifika Hospitali ya Sekoutoure akiwa na changamoto ya kupata maumivu makali sehemu ya chini ya tumbo kwa zaidi ya miaka mitatu.

“Baada ya vipimo aligundulika kuwa na uvimbe mkubwa sehemu ya kibofu cha mkojo ulisababisha kufanyiwa upasuaji na kuondoa lenye uzito wa Gramu 800”, amebainisha Dkt. Chiwaligo

Dkt. Chiwaligo ambaye aliwaongza madakatafi wenzake amesema uwepo wa jiwe kwenye kibofu ni mkusanyiko wa madini ya chumvi ambayo hukauka na kusababisha uvimbe kutokea katika kibofu cha mkojo.

Kuhusu dalili za awali za tatizo hilo Dkt. Chiwaligo amesema dalili mbalimbali zinazosababisha ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu, maumivu makali chini ya tumbo na kushindwa kuzuia mkojo.

“Namna ya kujikinga na ugonjwa huu ni kwenda haja ndogo kwa wakati pale unapoipata na kunywa maji ya kutosha kwa wakati ” , ameeleza Dkt. Chiwaligo

Dkt. Chiwaligo ametoa wito kwa jamii kuwa na utaratibu wa kufika hospitalini kupata huduma za vipimo na kuwa na mtindo bora wa maisha ili kuepuka changamoto ya magonjwa kama hayo.

MWISHO
 
Sio uchawi.

Majority of people especially watu wazima wana mawe kwenye kibofu cha mkono ambao ni mkusanyiko wa chembechembe ndogo zinazojigeuza kuwa mfano wa jiwe.

Kadri miaka inavyoongezeka ndivyo kijiwe kidogo huendelea kukua na kuwa jiwe kubwa.Dkt. Chiwaligo ambaye aliwaongza madakatafi wenzake amesema uwepo wa jiwe kwenye kibofu ni mkusanyiko wa madini ya chumvi ambayo hukauka na kusababisha uvimbe kutokea katika kibofu cha mkojo.

Kuhusu dalili za awali za tatizo hilo Dkt. Chiwaligo amesema dalili mbalimbali zinazosababisha ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu, maumivu makali chini ya tumbo na kushindwa kuzuia mkojo.

“Namna ya kujikinga na ugonjwa huu ni kwenda haja ndogo kwa wakati pale unapoipata na kunywa maji ya kutosha kwa wakati , ameeleza Dkt. Chiwaligo

Aidha ametoa wito kwa jamii kuwa na utaratibu wa kufika hospitalini kupata huduma za vipimo na kuwa na mtindo bora wa maisha ili kuepuka changamoto ya magonjwa kama hayo.
 
📍Mwanza

▪️MADAKTARI SEKOUTOURE WAFANIKISHA KUTOA JIWE LA GRAM 800 KWENYE KIBOFU CHA MKOJO

Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure wamefanikiwa kufanya upasuaji na kuondoa Jiwe ndani ya kibofu cha Mkojo kwa Mwanamke mwenye umri wa miaka 48.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hospitalini hapo jiwe hilo lenye uzito wa Gramu 800 lililomsumbua mhusuka kwa zaidi ya miaka mitatu.

Akizungumza leo Aprili 18, 2024 na Daktari Bingwa wa Upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekoutoure Dkt. Jackson Chiwaligo amesema hiyo ni mara ya kwanza kufanya upasuaji kama huo.

Dkt. Chiwaligo ameeleza kuwa mgonjwa huyo alifika Hospitali ya Sekoutoure akiwa na changamoto ya kupata maumivu makali sehemu ya chini ya tumbo kwa zaidi ya miaka mitatu.

“Baada ya vipimo aligundulika kuwa na uvimbe mkubwa sehemu ya kibofu cha mkojo ulisababisha kufanyiwa upasuaji na kuondoa lenye uzito wa Gramu 800”, amebainisha Dkt. Chiwaligo

Dkt. Chiwaligo ambaye aliwaongza madakatafi wenzake amesema uwepo wa jiwe kwenye kibofu ni mkusanyiko wa madini ya chumvi ambayo hukauka na kusababisha uvimbe kutokea katika kibofu cha mkojo.

Kuhusu dalili za awali za tatizo hilo Dkt. Chiwaligo amesema dalili mbalimbali zinazosababisha ugonjwa huo kuwa ni pamoja na kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu, maumivu makali chini ya tumbo na kushindwa kuzuia mkojo.

“Namna ya kujikinga na ugonjwa huu ni kwenda haja ndogo kwa wakati pale unapoipata na kunywa maji ya kutosha kwa wakati ” , ameeleza Dkt. Chiwaligo

Dkt. Chiwaligo ametoa wito kwa jamii kuwa na utaratibu wa kufika hospitalini kupata huduma za vipimo na kuwa na mtindo bora wa maisha ili kuepuka changamoto ya magonjwa kama hayo.

MWISHO

Mpaka sababu ya hilo jiwe umesema, sasa Mzee, issue ya uchawi imekujaje Mkuu? Kama sio kutuzalilisha wasukuma.
 
Dah! Kuwa msukuma kazi, tatizo likimpata mzungu tunaita cystolithiasis, likimpata msukuma tunaita uchawi sio
 
Karibu kila kitu chenye ubaya huko Usukumani sababu zake huwa ni uchawi!

Hata ukipata ajali ya gari au ajali yoyote ile, sababu ni uchawi.

Hata ukiugua halafu itokee umekufa, sababu ni uchawi tu.

Kwa akili za watu wengi wa Usukumani, kila kitu kilicho hasi sababu yake ni uchawi tu.

Yaani hata uking’atwa na mbu halafu uugue malaria, sababu yake itakuwa ni mtu kakuroga ili mbu wakung’ate upate malaria.
 
Back
Top Bottom