Memento
JF-Expert Member
- Jun 13, 2021
- 4,423
- 9,962
Madaktari wameishauri Serikali chanjo ya Corona iwe lazima. Si jambo baya na wapo sahihi kwa kuwa wao ni wataalamu.
Serikali haipaswi kukataa ushauri wowote wa wataalamu kwa maana mambo yakienda ndivyo sivyo watakuwa hawana wa kumwajibisha. Hivyo ushauri uzingatiwe pia.
Na mimi binafsi Sina shaka na huu ushauri wa hawa madaktari nguli kabisa, Hoja kubwa ni wataalamu wa afya kufariki wakiwa wanaendelea kupambana na ugonjwa wa corona, ila kuna mambo lazima waweke bayana.

- wataalamu wa afya wanaendelea kufa, Ina maana hawa wataalamu wa afya walikuwa hawajapata chanjo? Ikiwa hawajapata, kwanini? Na wao ndio sisi tunategemea wawe mfano kwenye kutumia sayansi kukabili huu ugonjwa, hapa pana wasiwasi.
- Ikiwa walipata chanjo, maswali yatabaki kwanini wanakufa kwa Corona ikiwa tayari walipata chanjo. Ina maana tutarudi kuwaambia watu kuwa chanjo haizuii kufa kwa corona?