#COVID19 Madaktari waishauri Serikali chanjo ya Corona kuwa ya lazima

Jana waganga wa vituo vya afya vyote waliitwa Dar kwenye kikao na viongozi wa wizara ya afya, viongozi wa serikali na wafadhili. Katika maazimio yao walipendekeza serikali itangaze chanjo iwe ni lazima kwa kila mtu atake asitake.

Sababu ya kutaka chanjo iwe lazima ni kwamba madaktari wengi wanafariki kwa covid kutokana na kuambukizwa na wagonjwa pale wanapowapa huduma.

Swali la kujiuliza, wafadhili waliitwa kwenye hicho kikao ili iweje?
View attachment 1941596
Sasa kama wao wamechanjwa na wanaambukizwa na kufa,sasa sisi tuchanje ili iweje tena??
 
Hao ni

Kama hawa madaktari ni wataalam kweli.Watuambue kwanini watu wengi wanakufa baada ya chanjo tu.Kuna mama mmoja alijanjwa hapa DSM,na kwa msisitizo hakapiga marufuku ndugu zake na marafiki wasiochanjwa kufika kwake.Lakini huyu mama ametangulia mbele ya haki baada ya kuchanjwa.Nina Daktari rafiki yangu amechanjwa na kufariki baada ya siku chache.Je, hawa madaktari wanataka tuchanjwe ili tufe?Au wanataka waongezewe mishahara tu ,kwa kuwa wamesikia pesa za uviko zipo?
Inasikitisha sanaaa. Watu wengi wamekufa na serikali haitaki kukiri. Hili suala la chanjo ya majaribio ni hatari sana. Linaua kuliko hata covid yenyewe.
 
Hasira za nini mkuu, ukisema tuanze kubaguana au kupiga kura nani kafiri na nani siyo kafiriri, mtapata rais hata maramoja kweli? Acha matusi kabisa, pia wewe ni kafri tuu maana hizi dini wote tumeletewa, soma historia kama babu yako hakuwa manamba basi alikuwa mtumwa.
Tena muache kabisa masuala ya Dini zenu kuyaingiza ktk siasa. Na mkome kabisa tunavumiliana na kupeana nafasi tu. Mkristo au Muislam wote tuanjenga Tanzania moja. Udini na Ukabila Ni Upumbavu na ujinga. Ndo maana Muislam anachinja Mkristo tunakula Mkristo akichinja Muislam hali, lakn Wakristo hawahoji, kwa nia yako mkuu unataka sasa tuwe na mabucha ya waislam na wakristo? Hatutaki kwenda huko.
twendeni polepole
 
Iko sheria mtu akitaka kujiua mfano kujinyonga kwa kamba/kanga/ sarawili kwa kujitundika mtini au darini na bahati mbaya mpango huo ukabuma na akagundulika hushitakiwa kwa kosa la kutaka kujiua kwa kukusudia.

Wako wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa yanayo tesa na kufikia mahali kukutaa dawa za kutibu au kuupoza ugonjwa na hatimaye kuhatarisha maisha yao. Sijawahi kusikia pahala wameshitakiwa au iko sheria inayo taka walazimishwe kutumia dawa au washitakiwe kwa kukusudia kujiua kwa kukataa matibabu. Wako wengi tu wanaotembea na ukimwi wakijua au hawajui na kuendekea kuambukizana HIV. Lakini serikali hailazimishi kila mtu kwenda kupima HIV na madaktari hawalalamiki kuambukizwa ukimwi kwa kujichoma/ kujikata kwa bahati mbaya wakiwahudumia. Tunachosikia ni kampeni za kutumia gloves, kondomo dume na jike. Corona watumie kondomu zake ambazo ni barakoa na satinaiza waachane na hizi hoja za kujivunjia heshima mbele ya jamii inayo waheshimu tena sana tu.

Serikali kama inavotoa takwimu za walio chanjwa ingetoa na takwimu za wanaokufa kwa sababu za kuchanjwa na walio ambukizwa na walio chanja. Hii ingesaidia kuwahamasisha wasio chanja kuchukua tahadhari za umakini zaidi ya hii ya kukataa chanjo. Hili la kulazimishia chanjo ni kutafuta kukwaza wananchi wake na kuifanya ichukiwe nao bila sababu ya msingi.

Atakaye chukiwa zaidi ya wote hawa ni Mh Rais, sijui wenye huu mpango wa kulazimishana chanjo wanachuki gani na Rais mpaka kumchonganisha na anao waongoza. Mimi ni ulize inakuaje madaktari ambao mwanzoni walishauri chanjo iwe hiari leo wageuke kula matapishi yao eti chanjo iwe ni lazima? Tukisema hawana uhakika na utafiti wao tutakosea?
 
Kwani chanjo ya watanzania tu? mbona tunapenda kujitoa ufahamu utasema sisi USA kila mtu anatuonea wivu nchi yenyewe tunajaza wamachinga tu, Kuna watu hawaijui hata Tanzania iko wapi lakini ukisikia watu humu utadhani donors kumbe tunapigia hesabu pesa za misaada tu na tozo za miamala.
Umejichanganya...hebu soma tena kwa umakini ulichoandika.
 
Jana waganga wa vituo vya afya vyote waliitwa Dar kwenye kikao na viongozi wa wizara ya afya, viongozi wa serikali na wafadhili. Katika maazimio yao walipendekeza serikali itangaze chanjo iwe ni lazima kwa kila mtu atake asitake.

Sababu ya kutaka chanjo iwe lazima ni kwamba madaktari wengi wanafariki kwa covid kutokana na kuambukizwa na wagonjwa pale wanapowapa huduma.

Swali la kujiuliza, wafadhili waliitwa kwenye hicho kikao ili iweje?
View attachment 1941596
Na swali jingine lakuuliza ni kwanini madakatri wao wanakufa sana kwa corona na uku wameshachajwa?
 
Kwani chanjo ya watanzania tu? mbona tunapenda kujitoa ufahamu utasema sisi USA kila mtu anatuonea wivu nchi yenyewe tunajaza wamachinga tu, Kuna watu hawaijui hata Tanzania iko wapi lakini ukisikia watu humu utadhani donors kumbe tunapigia hesabu pesa za misaada tu na tozo za miamala.
Chanjo bado zipo nyingi nenda kachanjwe.
 
People have a right to their own body, hii ni moja ya kanuni kuu za haki za binadamu. Ndo maana hata wagonjwa wanakuwa na haki ya kukataa tiba.

Huwezi kulazimisha watu kuchanja, watumie akili kushawishi watu, na sio kwenda kinguvu nguvu.

Kama serikali haiwezi ikawalinda watumishi wa afya na kuwapa nyenzo muhimu za kujikinga na maambukizi, waibane serikali kwa kushindwa kuwajali.

Wametumwa hawa si bure.
Wametumwa si bure
 
Wakichanja wao kuna shida gani? hao watakuwa wanatumiwa na mabeberu kuweka kizuizi cha watu ambao hawajachanjwa kovid kunyimwa huduma za kiafya, tumeshashuhudia kule ufaransa kuna maandamano kwa sababu ya mambo kama haya, watu wananyimwa kuingia mahali kupata huduma kisa hawana cheti cha korona, Mwenyezi Mungu anawaona kwa kushiriki uovu......
 
Inasikitisha. Kuna watu wengi wamekufa kutokana na chanjo. Ushahidi upo mwingi mno, kila mtu anajua. Waache kujipendekeza, hakuna mtanzania atakaye jipeleka kwenye kifo.
Kwa hiyo upo kinyume na mwenyekiti wa ccm ambaye ni Rais wako? na kwa maana hiyo unaungana na Gwajima na polepole?
 
Kwa hiyo upo kinyume na mwenyekiti wa ccm ambaye ni Rais wako? na kwa maana hiyo unaungana na Gwajima na polepole?
Msimlishe Mwenyekiti wetu maneno. Yeye alishasema ni hiari. Kama kuna watu wamekufa kutokana na chanjo nani aendelee kuchanjwa???
 
Madaktari wameishauri Serikali chanjo ya Corona iwe lazima. Si jambo baya na wapo sahihi kwa kuwa wao ni wataalamu.

Serikali haipaswi kukataa ushauri wowote wa wataalamu kwa maana mambo yakienda ndivyo sivyo watakuwa hawana wa kumwajibisha. Hivyo ushauri uzingatiwe pia.

Na mimi binafsi Sina shaka na huu ushauri wa hawa madaktari nguli kabisa, Hoja kubwa ni wataalamu wa afya kufariki wakiwa wanaendelea kupambana na ugonjwa wa corona, ila kuna mambo lazima waweke bayana.
  • wataalamu wa afya wanaendelea kufa, Ina maana hawa wataalamu wa afya walikuwa hawajapata chanjo? Ikiwa hawajapata, kwanini? Na wao ndio sisi tunategemea wawe mfano kwenye kutumia sayansi kukabili huu ugonjwa, hapa pana wasiwasi.
  • Ikiwa walipata chanjo, maswali yatabaki kwanini wanakufa kwa Corona ikiwa tayari walipata chanjo. Ina maana tutarudi kuwaambia watu kuwa chanjo haizuii kufa kwa corona?
Nimejaribu kujiuliza hivyo pia si kwa ubaya, ila vyovyote vile bado Kuna nafasi ya kupambana na huu ugonjwa na kuutokomeza.
Za kuambiwa changanya na za kwako

Mtumishi alihoji
Ukichanjwa unapona? Unaweza kupona au usipone
Ukichanjwa huambikizwi virusi? Unaambukizwa
Ukichanjwa Huambukizi wengine virusi? Unaambukiza
 
Jana waganga wa vituo vya afya vyote waliitwa Dar kwenye kikao na viongozi wa wizara ya afya, viongozi wa serikali na wafadhili. Katika maazimio yao walipendekeza serikali itangaze chanjo iwe ni lazima kwa kila mtu atake asitake.

Sababu ya kutaka chanjo iwe lazima ni kwamba madaktari wengi wanafariki kwa covid kutokana na kuambukizwa na wagonjwa pale wanapowapa huduma.

Swali la kujiuliza, wafadhili waliitwa kwenye hicho kikao ili iweje?
View attachment 1941596
Sasa mtu anachanjwa kinga, halafu mgonjwa akija hiyo kinga haifanyi kazi mwilini, then anachoma ili imlinde na nini?!

Ni sawa na kulala kwenye chandarua chenye matundu makubwa yanayopitisha mbu, sasa unalala kwenye hicho chandarua kwa ajiri ya kupata ulinzi gani au kwa ajiri ya kutimiza wajibu wa kulala katika chandarua?!

COVID-19 ni ufala wa karne...ha ha ha ha ha. Sichanji Mimi.
 
Inasikitisha. Kuna watu wengi wamekufa kutokana na chanjo. Ushahidi upo mwingi mno, kila mtu anajua. Waache kujipendekeza, hakuna mtanzania atakaye jipeleka kwenye kifo.
Na mmoja ndugu yangu anahangaika na hali yake baada ya chanjo
 
Swali la kujiuliza, madaktari wao wamechanjwa, sasa kama wamechanjwa wanakufaje wakati wamechanjwa na tuliambiwa ukichwanjwa haufi hata ukiugua na wala haulazwi?

Mbona hatulazimishani kwenda kutibiwa tukiugua, chanjo bure na bado tulazimishane, mbona matibabu mengine hatulazimishani?
Kwa watu wanaotumia akili zao za kuzaliwa , tayari wameshastuka kuwa hii ni miradi ya watu.
 
Sasa mtu anachanjwa kinga, halafu mgonjwa akija hiyo kinga haifanyi kazi mwilini, then anachoma ili imlinde na nini?!

Ni sawa na kulala kwenye chandarua chenye matundu makubwa yanayopitisha mbu, sasa unalala kwenye hicho chandarua kwa ajiri ya kupata ulinzi gani au kwa ajiri ya kutimiza wajibu wa kulala katika chandarua?!

COVID-19 ni ufala wa karne...ha ha ha ha ha. Sichanji Mimi.
Mkuu hapo unakuwa unampoteza mbu maboya aanze kujiuliza mara mbili mbili, hivi hiki ni chandaruaaaa au nyavu ya kuvulia samaki.......wakati anabung'aa bung'aa kujiuliza anapigwa mweleka.
 
Madaktari wameishauri Serikali chanjo ya Corona iwe lazima.
===
Madaktari gani, wa wapi, waliishauri serikali lini, wakiwa wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom