Madaktari wa Mwanza wanaipima Serikali?

Madaktari wa Mwanza wanaipima Serikali?

Hapana mkuu sipo kwa ajili ya kubishana bali kwa kujibu hoja. Hivi kweli ulitaka nikubali kuwa mazingira magumu ya kazi ndiyo sababu ya kupokea rushwa? Sikatai ni kweli mazingira ya kazi ni mabovu.
Mimi ningeomba kuuliza hivi unafikiri ni kwanini kumekuwa na sintofahamu kati ya Wananchi na watumishi wa afya?
ni mwuliza unajua sababu ya madaktari na watumishi wengine wa umma wanapokea rushwa,hilo la mazingira magumu umeunganisha mwenyewe japo lina husiana na hali halisi pia
 
nakwambia wewe kwa comment zako tu ni mjinga si kidogo,nimejaribu kufatilia comment zako kama tatu hap nakuona ujinga wako ulivyo mwingi uko kwa ajili ya kukwaza watu sio kuchangia
We jiangalie upya bhana

Nilitegemea utashauri vitanda viongezwe mahospitalini, madawa ila daaah nimekua dissapointed kusikia eti wafunge cctv wakati vitanda hamna daaaah
 
We jiangalie upya bhana

Nilitegemea utashauri vitanda viongezwe mahospitalini, madawa ila daaah nimekua dissapointed kusikia eti wafunge cctv wakati vitanda hamna daaaah
ukokimalumbano zaidi endelea kulumbana sibishani na mjinga mimi endelea kuwa diappointed na ujinga wako
 
ni mwuliza unajua sababu ya madaktari na watumishi wengine wa umma wanapokea rushwa,hilo la mazingira magumu umeunganisha mwenyewe japo lina husiana na hali halisi pia
Kuhusu kwa nini wanachukua rushwa nilijibu katika mtazamo wa watu kuwa more materialistic na kuhusu kuunganisha mazingira magumu, katika comment yako ya kwanza umesema majengo na mazingira kwa ujumla ni mabovu(mimi nafikiri hayo ndiyo mazingira magumu). Labda tu na mimi nirudishe hili swali kwako, kwanini watu wanachukuwa rushwa?
 
Kuna shida sana kwa wa Tanzania,hivi kuna MTU kati yetu amewahi kwenda klinik akakutana na mwanasiasa akimuuliza wapi panauma? Wanasiasa wanawabugudhi watenda kazi wa afya sisi tunashangilia wakati tatizo kuwa link kwa wanasiasa. Imagine nesi anashutumiwa kwa kuuza glove,kwa nini serikali isijaze gloves hospitali tuone hiyo nesi atamuuzia nani? Daktari anashutumiwa kwa kupokea rushwa wakati hajapewa mshahara wake kwa miaka 2 ?Kuna hospital I Mona naijua ya serikali hapa hapa nchini naijua ina madaktari bingwa watano hawajapewa mishahara yao ya ubingwa mwaka wa tati sasa,wanapigwa tarehe tu and then sis jamii badala ya kuna ubovu wa wanasiasa tunaona wa watalaamu wanaotusaidia kwenye mazingira magumu. Baba na mama wakigombana chumbani bora mtoto use upande wa mama anayeingia jikoni LA hivyo utalala njaa!

a
 
ni mwuliza unajua sababu ya madaktari na watumishi wengine wa umma wanapokea rushwa,hilo la mazingira magumu umeunganisha mwenyewe japo lina husiana na hali halisi pia
na rushwa ya ngono je?
 
Daktari anafanya kazi masaa mangap kwa siku? siku ngapi kwa week??
Daktari analipwa sh. Ngap? anakatwa sh. Ngap?
daktari anapaswa kuwa na familia au laaaah?? akiwa nayo mke wa daktari anakaa na mumewe au mkewe lini? watoto wake wanapataje wasaa wa kukaa na wazazi wao??
most of u guys mnalala jumamosi na jumapili. Weekdays mnatoka kazin sa. 11 Maximum.
Most of us tunakaa hospital mpaka sa 2, na usiku tunaamshwa kuja kuwahudumia nyie kama ndugu zetu. We work 7days a week, and our timetable always accomodate room ya kuitwa hata kama usiku sa. 10 Niko natengeneza mtoto... u think we get paid fo that? Well we dont. Our children wanakua with pride wazaz wao madr. But we are poorest parents ever, its not a choice is default kwenye system yetu.. sio kwamba nilichagua niwe daktari so as kutake every crap ambayo utakuja nayo kwakuwa we ni mgonjwa. And sisi ni watu pia, nina familia, nina ndugu... mshukuru mungu ukienda kazini unaenda kuhesabu hela au Kuandika kwenye makaratasi.. nataman siku moja ungejua inakuaje unaamkia kuwasikiliza watu ambao wengi wao sio waekewa na hawajali wenzao bali wao wenyewe..
Ofisi ya serikali ikifika sa. 7-8 Ni muda wa kula ila dr. Akiacha clinic muda huo kwenda kula utaambiwa tumekuja sa. 12 Bila hata kujua wewe upo pale tangu jana.. you dont ask, you never ask.. doctors are most non-selfish people out there but hamuwez kujua kwakua mnaangalia mambo mnayoyafanya kwenye 24 hours nakuzan tinalingna..
fine, ni vizuri kuwaza mnavyowaza kwakua scope ya what mmewitness haiwaruhusu kuwaza beyond that..
Anf no, drs. Hawana lugha mbaya but kama human akiwa na bad mood learn kuongea naye pia..
We work in most difficulty environments, tunajitoboa kuhudumia wagonjwa wa HIV, personally nishawah kumzalisha mtoto kwa mikono mitupu 5years ago wakati hamna gloves. I risked my life mom was positive, alafu leo mnakuja kuongea ujinga without hata kusikiliza mazingira yakoje..
Its shame nchi kama yetu inamadaktar wachache na tuko 45 mil.
mnazan madakatari wenye vyet wanafika hata elfu 20???
Fine, we bleed for ua relatives, we abandon our husbands, wives for you.. tunachoka pia, tutachoka one day.. its not fair, u may not see these but one day mtajua.. NIMEIKUTA MAHALI!!
Mbona mnajificha nyuma ya keyboard!?

NYUMBU TU NYIE
 
ndugu yangu hawa manesi na madaktari wanafanya kazi kama mbwa aikwambie mtu,unakuta nesi mmoja ila anawagonjwa zaidi ya mia wanamsubiri awape huduma,hapo kuna mama mjamzito kaja kupima uzito na kujua maendeleo ya mimba,kuna mwingine kaja kwa ajili ya chanjo,mwinge kaja kupa ushauri wa lishe na unyonyeshaji hivi unadhani ufanisi unapatikanaje hapa??alafu mtu kama mulugo ambae kazi yake kutukanana na wanasiasa na kuamrisha polisi anakuja kutoa amri za kitoto bila kuruhusu taratibu za kitaaluma kutumika ni upuuzi ulio pitiliza
Kweli serikali nayo isijotoe katika hili lazima inahusika katika kiwango kikubwa. Watu watu muda mwingine wanafanya kazi chini ya pressure kubwa.
Kuhusu upungufu wa watumishi wa afya umekuwa created na trend ya udahili wa wanafunzi katika kozi za afya. Kwa mfano MD hapo mwanzo zilikuwa zinachukuliwa div 1, baada ya kuongezeka vyuo kidogo wenye 2 nao wakaanza kupata nafasi. Sina uhakika kama sasa hivi wenye div 3 wanapata nafasi. Hivi mtu akiwa na div 3 hawezi kusoma MD? Kama ni mbovu hatoziweza kozi perfomance yake chuoni itamtoa!
 
Mbona mnajificha nyuma ya keyboard!?

NYUMBU TU NYIE
Haha, wewe wasema mkuu. Hayo mawazo ya mtu ambaye yuko emotional, pinga kwa hoja tafadhali. Mbona wanajamvi wanajadili kwa hoja humu?
 
Kuhusu kwa nini wanachukua rushwa nilijibu katika mtazamo wa watu kuwa more materialistic na kuhusu kuunganisha mazingira magumu, katika comment yako ya kwanza umesema majengo na mazingira kwa ujumla ni mabovu(mimi nafikiri hayo ndiyo mazingira magumu). Labda tu na mimi nirudishe hili swali kwako, kwanini watu wanachukuwa rushwa?
ndoma nikasema tukishajua tatizo hili tukalitengenezea mazingira ya kuepukika kwanamna moja au nyingine ndio tuje nimkazo ulio imara hata zaidi ya huu wa sasa,haiwezekani tuwe na mabaango kila ofisi rushwa ni adui wa haki lakini rushwa bado ni mtendaji katika mazingira ya ofisi za umma..!! wakati mwingine watendaji mnawaonea hawa hawa wateja kunawakati wanawatia ushawishi watoa huduma,siwatetei watoa huduma moja kwa moja nachotetea mimi ni uwajibishwaji wa hawa watumishi uko kishabiki zaidi kuliko kihalisia
 
Kweli serikali nayo isijotoe katika hili lazima inahusika katika kiwango kikubwa. Watu watu muda mwingine wanafanya kazi chini ya pressure kubwa.
Kuhusu upungufu wa watumishi wa afya umekuwa created na trend ya udahili wa wanafunzi katika kozi za afya. Kwa mfano MD hapo mwanzo zilikuwa zinachukuliwa div 1, baada ya kuongezeka vyuo kidogo wenye 2 nao wakaanza kupata nafasi. Sina uhakika kama sasa hivi wenye div 3 wanapata nafasi. Hivi mtu akiwa na div 3 hawezi kusoma MD? Kama ni mbovu hatoziweza kozi perfomance yake chuoni itamtoa!
yaahhwapo wenye dv3 wanachukuliwa niliona hata Bugando kwenye intake ya mwaka jana kama sikosei
 
mpuuzi sana wewe unatafuta sifa kama huyo unayeimwita

Upuuzi wake ni upi. Hivi unadiriki kweli kujificha kwenye JF na kumdhalilisha hata Rais wetu kwa maneno yako kwamba "MPUUZI SANA WEWE UNATAFUTA SIFA KAMA HUYO UNAYEMWITA (KWA MAANA YA RAIS WETU) ? Hivi unajiamini sana??!!! Unadhani mkono wa dola hauwezi kukufikia hapo ulipo?
 
Habari wana JF, hivi karibuni tumeona tukio moja likitokea huko Mtwara la Kusimamishwa Daktari mmoja aliyehusika katika kuomba rushwa kutoka kwa mgonjwa aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji.

Japo ushahidi ni mgumu wa mazingira ya hiyo rushwa, ni ukweli usio na kificho kuwa Wahudumu wa afya walio wengi wamekuwa si waaminifu tena wasiokuwa na chembe ya huruma kwa binadamu wenzao kiasi cha kutojali uhai wa wagonjwa wanaowahudumia.

Tukio la Mtwara limefuatana na matukio mawili ya kusikitisha yaliyotokea katika jiji la Mwanza, wilaya ya Nyamagana kwenye hospitali ya wilaya ya Nyamagana (Butimba) na hospitali ya mkoa ya Sekou Toure.

Likitangulia la hospitali ya Butimba, mama mmoja alijifungulia chooni watoto mapacha na wakafariki kwa kile kilichodaiwa ni uzembe wa manesi waliokuwa wakimtolea kauli chafu mjamzito huyo kuwa awaite Majaliwa na Magufuri waje wamhudumie.

Tukio jingine lililofuatia ni kufariki kwa mama na watoto wake mapacha katika hospitali ya mkoa (Sekou Toure) kwa kucheleweshwa kuongezwa damu.

Kutokana na matukio hayo, kuna manesi na madaktari wametiwa nguvuni kutokana na kasi iliyopo sasa ya kurejesha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma.

Sasa Madaktari wamefanya mgomo katika hospitali ya Butimba kwa madai wanaogopa usalama wa kazi yao kwa kuwa wao hawawezi kuzuia kifo kwa mgonjwa pale muda wake unapokuwa umefika.

Mheshimiwa Rais, sichelei kusema hawa madaktari wanataka kutunishiana misuli na serikali yako kwa kile kilichotokea Mtwara. Kwanini Wananchi wote wanaokumbwa na masahibu haya kutoka kwa wahudumu wa afya katika maelezo yao wanaambiwa wawaite Majaliwa na Magufuli wawahudumie?

Mheshimiwa watumie vijana wako wa TISS wakupe taarifa kamili ili ujue utapambana vipi na udhalimu wa baadhi ya watumishi wa afya ambao wanafikiri kuwa wao ni bora katika jamii kuliko watu wengine wakisahau kuwa wao pia ni product ya mwalimu, hivyo tunaishi kwa kutegemeana.

Huu ni uchochezi katika ubora wake, sasa kama damu katika benki hakuna ulitaka wajikamue wao? Watu mkiambiwe mkajitolee damu mnaanza kuweweseka kwa vile hamjiamini kutokana na tabia zenu za kuchepuka.
 
ndoma nikasema tukishajua tatizo hili tukalitengenezea mazingira ya kuepukika kwanamna moja au nyingine ndio tuje nimkazo ulio imara hata zaidi ya huu wa sasa,haiwezekani tuwe na mabaango kila ofisi rushwa ni adui wa haki lakini rushwa bado ni mtendaji katika mazingira ya ofisi za umma..!! wakati mwingine watendaji mnawaonea hawa hawa wateja kunawakati wanawatia ushawishi watoa huduma,siwatetei watoa huduma moja kwa moja nachotetea mimi ni uwajibishwaji wa hawa watumishi uko kishabiki zaidi kuliko kihalisia
Upo sahihi mkuu! Sasa hivi kuna ombwe katika uongozi, kila mtu anataka aonekane ni mchapa kazi. Inabidi turudi katika kufanya kazi kwa uzalendo, wanasiasa wasijitazame wao tu kuwa ndiyo wanastahili maslahi bora. Watumishi walipwe vizuri katika kada zote ili wawe na moyo wa kuitumikia jamii.
Ndugu yangu kwa kiasi kikubwa wanasiasa wameiharibu nchi hii. Uharibifu huu umeanza katika awamu ya pili.
Katika awamu ya kwanza karibia watu wote tulikuwa sawa. Awamu ya pili ikaanza kutengeneza matabaka ambayo yamesababisha struggle kwa kila mmoja kivyake anavyojua mwenyewe.
 
Pana siku Dr Maua alipata ajali akiwa na rafiki yake wa wakati huo (sio sasa) na kupelekwa Hospitali akiwa na majeraha ya usoni, Daktari aliwagomea ma nurse kumshona na ile minyuzi isiyotakiwa na akaomba nyuzi stahiki zitolewe Theatre ziletwe na aendelee na kazi, Yule rafiki yake Dr Maua akaona Daktari ni jeuri hivyo akaenda kumwamusha Daktari Mkuu na kumpa uongo mwingi tu, pia Daktari mkuu wa zamu, KATIBU wa Tughe wa Hosptali ili wamvamie Dr aliyesemekana amegoma kazi pia amelala, walipofika wakamkuta Dr akiwa amekaa pembeni na aliwaelezea kwa nini hajaanza kushona, bahati mzuri Dr Maua aliingilia maongezi na kusema kuwa anakubaliana na Dr aliyeomba vifaa stahiki kwa ajili ya kushonea usoni, basi huyo Dr alipona tu kwa ajili ya utetezi wa Dr Maua na ingekuwa mgonjwa si Dr kwa fani angeeleza tofauti na yule Dr kwa leo angekuwa jipu, Drs naomba kila kitu unachoamua FANYA KU DOCUMENT IN BLACK AND WHITE
 
Lakini mkuu matatizo ya rushwa na kauli mbovu kutoka kwa wahudumu wa afya zimeanza muda mrefu. Hakuna utafiti ambao umefanywa kuhusu rushwa ukaiweka pembeni sekta ya afya.
 
Huu ni uchochezi katika ubora wake, sasa kama damu katika benki hakuna ulitaka wajikamue wao? Watu mkiambiwe mkajitolee damu mnaanza kuweweseka kwa vile hamjiamini kutokana na tabia zenu za kuchepuka.
Sijui hilo sakata unalifahamu kwa kiasi gani! Nikuulize tu, hiyo damu ilipatikana wapi baada ya hali ya mgonjwa imekuwa mbaya zaidi akatundikiwa?
 
Hata Serikali inauhusiano mbaya na watumishi wake: Serikali inajua kuwa citizens wake wanawachukuia watumishi wake, Serikali inashiriki kwenye mob justice ya kumsurubu daktari kwa mere allegations za mtummoja, Serikali inaamua ku create scarcity ya madsktar ili ijisafishe kwa wananchi, Serikali haioni kuwa sasa imeawaumiza wote- mzigo mzito kwa waliobaki na kuchelewesha huduma kwa wananchi wake, poor we.
Jana kuna mgonjwa kamchapa makofi Nurse huko Katavi ila hajachukuliwa hatua yoyote ile, ile chuki ya wananchi kwa serikali imehamia kwa madaktari
Hospitali haina vifaa wala dawa bado huyu daktari analaumiwa serikali nayo inamuangukia
 
na bado.
 
Back
Top Bottom