Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Habari wana JF, hivi karibuni tumeona tukio moja likitokea huko Mtwara la Kusimamishwa Daktari mmoja aliyehusika katika kuomba rushwa kutoka kwa mgonjwa aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji.
Japo ushahidi ni mgumu wa mazingira ya hiyo rushwa, ni ukweli usio na kificho kuwa Wahudumu wa afya walio wengi wamekuwa si waaminifu tena wasiokuwa na chembe ya huruma kwa binadamu wenzao kiasi cha kutojali uhai wa wagonjwa wanaowahudumia.
Tukio la Mtwara limefuatana na matukio mawili ya kusikitisha yaliyotokea katika jiji la Mwanza, wilaya ya Nyamagana kwenye hospitali ya wilaya ya Nyamagana (Butimba) na hospitali ya mkoa ya Sekou Toure.
Likitangulia la hospitali ya Butimba, mama mmoja alijifungulia chooni watoto mapacha na wakafariki kwa kile kilichodaiwa ni uzembe wa manesi waliokuwa wakimtolea kauli chafu mjamzito huyo kuwa awaite Majaliwa na Magufuri waje wamhudumie.
Tukio jingine lililofuatia ni kufariki kwa mama na watoto wake mapacha katika hospitali ya mkoa (Sekou Toure) kwa kucheleweshwa kuongezwa damu.
Kutokana na matukio hayo, kuna manesi na madaktari wametiwa nguvuni kutokana na kasi iliyopo sasa ya kurejesha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma.
Sasa Madaktari wamefanya mgomo katika hospitali ya Butimba kwa madai wanaogopa usalama wa kazi yao kwa kuwa wao hawawezi kuzuia kifo kwa mgonjwa pale muda wake unapokuwa umefika.
Mheshimiwa Rais, sichelei kusema hawa madaktari wanataka kutunishiana misuli na serikali yako kwa kile kilichotokea Mtwara. Kwanini Wananchi wote wanaokumbwa na masahibu haya kutoka kwa wahudumu wa afya katika maelezo yao wanaambiwa wawaite Majaliwa na Magufuli wawahudumie?
Mheshimiwa watumie vijana wako wa TISS wakupe taarifa kamili ili ujue utapambana vipi na udhalimu wa baadhi ya watumishi wa afya ambao wanafikiri kuwa wao ni bora katika jamii kuliko watu wengine wakisahau kuwa wao pia ni product ya mwalimu, hivyo tunaishi kwa kutegemeana.