Madaktari wa Mwanza wanaipima Serikali?

Madaktari wa Mwanza wanaipima Serikali?

Hebu dadavua hoja yako in detail, kwamba what exactly happenned. Umekuwa biased zaidi kuwalaumu hao watumishi wote wa afya wa Mwanza bila kusema ni kitu gani hasa kimewafanya kuchukua maamuzi ya kufanya kitu kama mgomo hivi.

Mimi nimesikia kupitia vyombo vya habari haya kuhusu baadhi ya madaktari, manesi na wauguzi wa Mwanza;

1. Kwamba RC Mwanza alisikia malalamiko ya baadhi ya wagonjwa kutohudumiwa vizuri ikiwemo huyo mjamzito kujifungulia (sina hakika ni ktk mazingira gani na kwa nini, lakini inasemekana alijifungua mtoto/watoto ambao walifariki). Kwa incident hii wananchi walikasirika na kuona kuwa kuna uzembe flani ulitokea ndiyo maana hilo likatokea. Kelele hizi zikasikika na RC akafika ktk hospitali hiyo na kuamuru baadhi ya madkatari na manesi kusimamishwa kazi kwa malalamiko tu ya wananchi kupitia camera za TV!

2. Jana juma4 au juzi juma3 nikasikia tena kupitia vyombo vya habari kuwa madaktari, manesi na wahudumu wa afya wa hospitali nadhani ya Butimba ambayo ni DDH ya manispaa ya Nyamagana "wanatishia" = "kugoma" kutukuendelea na majukumu yao kwa sbb ya usalama wao kazini kutolindwa na pia kutotendewa haki especially kuadhibiwa pasipo kufuata taratibu na kusikilizwa.

Nadhani hoja ya msingi iko hapa yaani KUADHIBIWA PASIPO KUFUATA TARATIBU ZA KIUTUMISHI NA KUSIKILIZWA.

Aidha, watumishi wa afya kwa ujumla wao wanalalamikia mazingira duni ya utoleaji huduma kwa wagonjwa ikiwemo ukosefu kabisa wa vitendea kazi kwa maana ya vifaa tiba, upungufu wa madaktari, manesi na wahudumu wengine wa afya to the extent kwamba mtumishi mmoja analazimika kufanya kazi masaa mengi kuliko kawaida kuhudumia
wagonjwa, malipo duni nk

Swali ni je, tunafikiria haya kabla ya kuchukua hatua ya kuwalaumu hawa?

Kingine mimi nadhani matatizo mengine yapo kwa wagonjwa wenyewe na watu wao wanaowauguza.

Mfano kwa mama mjazito, alibeba mimba akakaa tu nyumbani na hata siku moja hakuwahi kuhudhuria kliniki ili kuwezesha daktari kufanyia monitoring ya ujauzito huo,muda wa kujifungua ukafika ikashindikana kujifungulia nyumbani na sasa uamuzi ukafika wa kupelekwa hospitali, ni lazima mama huyu na ujauzito wake atakuwa kwenye risk kubwa ya kupoteza maisha au mtoto wake.

Swali langu ni hili, kuwa was this considered kabla ya kufikia maamuzi yoyote? Je, ni kwa sbb tu wananchi wamepiga kelele, then na sisi viongozi kwa sbb tunatekeleza majukumu yetu kwa "mzuka" tu pasipo kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zilizopo? Wananchi hawa wana elimu ya kutosha juu ya wajibu na haki zao au ni kwa sbb tu wamelishwa kasumba na kuaminishwa kuwa watumishi wa umma madaktari na manesi wakiwemo ni wala rushwa na kwa hiyo popote mlipo pigeni kelele na serikali itachukua hatua? Tutakwenda na kufika salama kweli kwa mtindo huu wa ufanyaji kazi?

Hakuna anayebisha kuwa kuna baadhi ya watumishi wa umma kweli walikuwa wamejisahau na walikuwa hawatekelezi wajibu wao ipasavyo.

Mimi ninachojaribu kusisitiza hapa ni kuwa, katika kurudisha maadili na nidhamu katika utumishi wa umma ni lazima kufanyike kwa uangalifu mkubwa ili tusije kuwatia hofu hata wasio na matatizo na kushindwa kutekeleza majukumu yao na wakati huohuo taratibu, kanuni na sheria za utumishi wa umma zikizingatiwa ipasavyo.

Haiwezekani RC au DC au Waziri yeye ndiye awe mtoa amri tu ya fukuza huyu, simamisha kazi huyu au hamisha huyu na peleka kule. Itakuwa ni chaos

Aidha serikali nayo itende na itekeleze majukumu yake na isiwe ni chanzo cha watumishi hawa kuonekana hawafanyi kazi zao ipasavyo.

Mfano ipeleke vitendea kazi na pesa ktk hospitali zake kwa wakati ili hawa watumishi wasiwe na visingizio.

Mimi niko Shinyanga. Juzi kati mwanangu alikuwa anaumwa na nikampeleka ktk kituo cha afya cha serikali kilipo jirani nami. Akapimwa na kukutwa anasumbuliwa na minyoo na U.T.I.

Daktari akamwandikia dawa hizi kentrax, erythromicine na panadol. Amini usiamini, nilipata panadol pekee hapo na zingine zote nilikwenda kununua ktk maduka ya madawa mitaani licha ya kuwa natumia NHIF card na kila mwezi nakatwa ktk mshahara wangu takribani Tshs 60,000/= kuchangia bima ya afya!

Sasa ktk mazingira haya, who is to blame? Serikali au wauguzi naadaktari?

Haiwezekani focus iwe ktk hospitali za Muhimbili tu na kuzisahau zahanati na vituo vya afya vijijini ambako huko pia ndiko kuliko matatizo makubwa!!
Mkuu unaposema malipo kidogo sidhani kwa hali halisi ilivyo kwa watumishi wa umma hapa nchini upande wa mishahara ni sahihi kusema hivyo. Nadhani ukitoa wanasiasa na ma-CEO na ma-DG watu wakada hii wana unafuu kuliko wenzao. Hizi hospitali mbili za Mwanza, yaani ya Butimba(DDH) na hiyo ya Sekou Toure kumekuwa na matatizo ya rushwa iliyokithiri ambayo imejenga chuki kubwa kati ya watumishi na wananchi.
Mkuu chuki huwa haizuki ghafla tu, lazima inakuwa na chanzo. Hivi kweli mwananchi atakuwa na chuki dhidi ya daktari au nesi aliyemhudumia vizuri ili iweje? Kwa hali ya rushwa ilivyofikia hapa nchini, sasa hawa viongozi ambao wametaka kurejesha imani kwa wananchi dhidi ya serikali iliyochukiwa kwa kiwango cha hali ya juu wamelazimika kutumia nguvu kubwa sana ambayo sasa imelipua hasira za wananchi.
Mimi nadhani kuna haja ya kila mmoja wetu kujitathmini na kuanza upya lakini hali ya kutunishiana misuli haitotufikisha popote zaidi ya kuangamia.
 
UJUMBE KWA MADAKTARI WOTE TANZANIA
1. Fika kazini mapema kama taratibu za kazi zinavyoelekeza na tekeleza majukumu yako yote kwa ufanisi wa hali ya juu
2. Hudumia wagonjwa wako kwa upendo na upole hata hivyo upendo wako usivuke mipaka
3. Sio kila tatizo la mgonjwa wako ni jukumu lako shughulikia linalokuhusu tu
4. Wapi mgonjwa atapata dawa au vifaa tiba vyengine ambavyo havipatikani katika hospitali yako na ni bei gani sio jukumu lako, mwandikie vyote anavyohitajika kua navyo na mpe maelezo kwa nini vinahitajika. jukuma la kuvitafuta sio juu yako.
5. Usitoe vitendea kazi vyako au vifaa vyako mwenyewe ukampatia msaada mgonjwa. Utaingia matatizoni kwa tuhuma za kuiba vifaa vya hospitali au kufanya biashara eneo la hospitali
6. Hakikisha umetoka kazini muda tu unapohitajika. Kuendelea kuwepo kazini baada ya muda kwisha ni vizuri lakini kumbuka utawajibika kwa lolote litakalotokezea baadae sababu muda wako ulishakwisha
7. Usiingilie mgonjwa asiekuhusu. Utawajibika kwa yatakayotokezea
8. Kumbuka familia yako ingependa kukaa na kufurahi na wewe. kumbuka familia yako ni sehemu muhimu sana kwako. Ipatie muda inayostahiki
9. Wakati unapohudumia mteja usihangaishwe na foleni iliokuepo hospitali. Muhudumie kila mgonjwa anavyostahiki, mpatie maelezo ya kutosha na muache afanye maamuzi mwenyewe. heshimu maamuzi yake na hakikisha umeandika maamuzi yote na ameweka sahihi yake na yako au maamuzi hayo yameshuhudiwa na mashahidi stahiki
10. Usiombe rushwa, usiombe malipo yoyote yasiokua sahihi. Usitoe jumla ya gharama za matibabu sio kazi yako. kua muangalifu iwapo mgonjwa au jamaa yake amekupatia takrima inaweza kukugeuka.
11. Usiwe na tamaa ya haraka ya kutaka kua na maisha ya juu. ishi kwa uwezo uliokua nao, mshukuru mungu kwa yale aliyokupa
12. Hata daktari anayo haki ya kukataa mgonjwa. mueleze mgonjwa au jamaa wa karibu kwa nini huwezi kumhudumia na toa maelezo sehemu husika ya sababu zinazokufanya kumkataa mgonjwa huyo.
13. Kua muangalifu unaporifaa mgonjwa au pale unapompa maelezo ya kufuatwa huduma aliyoikosa katika hospitali nyengine. kua muangalifu unapomtaka mgonjwa ahudhurie hospitali ya binafsi. Wengi wao huamini hizo hospitali ni za madaktari husika.
14. Hudumia mgonjwa aliefuata taratibu husika tu isipokua kama ni dharura. hata hivyo hakikisha hospitali yako ina sera stahiki juu ya malipo ya dharura.
15. Huduma yoyote unayompatia mgonjwa mukiwa mbalimbali mfano kwa njia ya simu ni huduma yako. utawajibika kwa yatakayotokezea kwa huduma hiyo. Hakikisha huduma hiyo inafuata taratibu ikiwemo kufanya malipo stahiki.
16. Kumbuka mgonjwa na jamaa zake sio rafiki zako. watakustahi ikiwa mambo yanakwenda vizuri tu na watakugeuka kama mambo yataharibika
TUWAPATIE UJUMBE HUU MADAKTARI WOTE NA TUJITAHIDI KUBADILIKA. KUMBUKA LIKIKIFIKA NI LAKO NA FAMILIA YAKO.

NIMEIKUTA MAHALI
Hii umeikuta wapi? kwa haraka haraka inaonekana kama ni ushauri mzuri kwa madaktari, kama uchonganishi pembe tatu yaani mgonjwa, daktari na serikali, kama kebehi kwa serikali na kwa upande mwingine ni kama uchochezi wenye hila dhidi ya serikali.

Mimi nafikiri andiko hili hujaliona mahali popote ila umetunga na kuamua kuusambaza ujumbe wako kijanja.
 
Acheni kuingiza siasa kwenye taaluma zenye akili, madaktari wamekua Mungu kuzuia vifo..!!?
Hivi kuna taaluma zenye akili na zisizo na akili?! Mbona hata mkulima kijijini taaluma yake ina akili kwa sababu bila yeye hatuna uhakika wa kuiona kesho(Tutakufa kwa njaa). Kama madaktari hawawezi kuzuia kifo kwani hospitali wanafanya nini?
Mimi nadhani unataka kuchanganya mitazamo, ule wa spiritual world na real world.
 
Mkuu unaposema malipo kidogo sidhani kwa hali halisi ilivyo kwa watumishi wa umma hapa nchini upande wa mishahara ni sahihi kusema hivyo. Nadhani ukitoa wanasiasa na ma-CEO na ma-DG watu wakada hii wana unafuu kuliko wenzao. Hizi hospitali mbili za Mwanza, yaani ya Butimba(DDH) na hiyo ya Sekou Toure kumekuwa na matatizo ya rushwa iliyokithiri ambayo imejenga chuki kubwa kati ya watumishi na wananchi.
Mkuu chuki huwa haizuki ghafla tu, lazima inakuwa na chanzo. Hivi kweli mwananchi atakuwa na chuki dhidi ya daktari au nesi aliyemhudumia vizuri ili iweje? Kwa hali ya rushwa ilivyofikia hapa nchini, sasa hawa viongozi ambao wametaka kurejesha imani kwa wananchi dhidi ya serikali iliyochukiwa kwa kiwango cha hali ya juu wamelazimika kutumia nguvu kubwa sana ambayo sasa imelipua hasira za wananchi.
Mimi nadhani kuna haja ya kila mmoja wetu kujitathmini na kuanza upya lakini hali ya kutunishiana misuli haitotufikisha popote zaidi ya kuangamia.

Shebbydo

...Rushwa iko kila sekta ktk utumishi wa umma na ile ya binafsi na sio huko tu Sekou Toure na Butimba hospital

...Tena rushwa kubwa ziko kwa viongozi wa kisiasa kuanzia ktk michakato yao ya kuzipata hizo nafasi na sasa eti hao ndiyo wanataka kukomesha tatizo. Unaamini wataweza hawa mkuu?

...Nisome vizuri. Nimesema tunapaswa kurudi ktk misingi ya kikanuni, taratibu na sheria ktk kushughulikia haya. Tusiende kwa mizuka au kwa kuiga ili tuonekane tunafanya kumbe malengo yetu ni kulinda nafasi zetu tu kwa gharama ya baadhi ya watumishi wa umma

...Hiyo ishu ya Mwanza ni tatizo na imesababishwa na namna lilivyoshughulikiwa tu, basi.
 
Ukifuatilia uhusiano kuwa mbovu kati ya watumishi wa afya na jamii Mwanza, chanzo ni hao watumishi wa afya kutokana na rushwa iliyokithiri. Waulize watu wa Mwanza wakuambie hali rushwa ilivyo mahospitalini.
ulishawahi kujiuliza rushwa hii kwa watumishi wa afya chanzo nini,serikali yako imetengeneza mazingira rafiki ya kazi kwa watumishi wa afya,nyie wenyewe hamuwezi kukaa maeneo haya hata nusu saa kwa hali ilivyo mbaya ya majengo na mazingira kwa ujumla,serikali must play their part kwabla ya kuanza kufukuzana hovyo
 
Shebbydo

...Rushwa iko kila sekta ktk utumishi wa umma na ile ya binafsi na sio huko tu Sekou Toure na Butimba hospital

...Tena rushwa kubwa ziko kwa viongozi wa kisiasa kuanzia ktk michakato yao ya kuzipata hizo nafasi na sasa eti hao ndiyo wanataka kukomesha tatizo. Unaamini wataweza hawa mkuu?

...Nisome vizuri. Nimesoma tunapaswa kurudi ktk misingi ya kikanuni, taratibu na sheria ktk kushughulikia haya. Tusiende kwa mizuka au kwa kuiga ili tuonekane tunafanya kumbe malengo ni kulinda nafasi zetu tu!

...Hiyo ishu ya Mwanza ni tatizo na imesababishwa na namna lilivyoshughulikiwa tu, basi.
Ni kweli issue hiyo imekuwa hivyo kutokana na ilivyoshughulikiwa ila chuki ilianza kujengeka muda mrefu.
Kuhusu kanuni, taratibu na sheria ni kweli lazima utafutwe utaratibu mzuri ila mimi nadhani ile katiba ya Warioba ilikuwa ni dawa. Magufuli atakuwa ni kiongozi ambaye hatosahaulika vichwani mwa Watanzania endapo atairudisha ile ya Warioba.
Hawa wanasiasa hata mimi sijaamini 100% kama kweli wana nia ya dhati kuturudishia Tanzania yetu ambayo imepotea muda mrefu.
 
Daktari anafanya kazi masaa mangap kwa siku? siku ngapi kwa week??
Daktari analipwa sh. Ngap? anakatwa sh. Ngap?
daktari anapaswa kuwa na familia au laaaah?? akiwa nayo mke wa daktari anakaa na mumewe au mkewe lini? watoto wake wanapataje wasaa wa kukaa na wazazi wao??
most of u guys mnalala jumamosi na jumapili. Weekdays mnatoka kazin sa. 11 Maximum.
Most of us tunakaa hospital mpaka sa 2, na usiku tunaamshwa kuja kuwahudumia nyie kama ndugu zetu. We work 7days a week, and our timetable always accomodate room ya kuitwa hata kama usiku sa. 10 Niko natengeneza mtoto... u think we get paid fo that? Well we dont. Our children wanakua with pride wazaz wao madr. But we are poorest parents ever, its not a choice is default kwenye system yetu.. sio kwamba nilichagua niwe daktari so as kutake every crap ambayo utakuja nayo kwakuwa we ni mgonjwa. And sisi ni watu pia, nina familia, nina ndugu... mshukuru mungu ukienda kazini unaenda kuhesabu hela au Kuandika kwenye makaratasi.. nataman siku moja ungejua inakuaje unaamkia kuwasikiliza watu ambao wengi wao sio waekewa na hawajali wenzao bali wao wenyewe..
Ofisi ya serikali ikifika sa. 7-8 Ni muda wa kula ila dr. Akiacha clinic muda huo kwenda kula utaambiwa tumekuja sa. 12 Bila hata kujua wewe upo pale tangu jana.. you dont ask, you never ask.. doctors are most non-selfish people out there but hamuwez kujua kwakua mnaangalia mambo mnayoyafanya kwenye 24 hours nakuzan tinalingna..
fine, ni vizuri kuwaza mnavyowaza kwakua scope ya what mmewitness haiwaruhusu kuwaza beyond that..
Anf no, drs. Hawana lugha mbaya but kama human akiwa na bad mood learn kuongea naye pia..
We work in most difficulty environments, tunajitoboa kuhudumia wagonjwa wa HIV, personally nishawah kumzalisha mtoto kwa mikono mitupu 5years ago wakati hamna gloves. I risked my life mom was positive, alafu leo mnakuja kuongea ujinga without hata kusikiliza mazingira yakoje..
Its shame nchi kama yetu inamadaktar wachache na tuko 45 mil.
mnazan madakatari wenye vyet wanafika hata elfu 20???
Fine, we bleed for ua relatives, we abandon our husbands, wives for you.. tunachoka pia, tutachoka one day.. its not fair, u may not see these but one day mtajua.. NIMEIKUTA MAHALI!!
We bhana we kila mtu akianza kutaja changamoto za kazini kwake nani atakua na nafuu, mwalim akianza zake police akianza zake tutafikaaa? Point ni kwamba hiyo kazi ni ya wito na uliipenda mwenyewe ndo maana ulichukua miaka mitano kuisomea and najua yote hayo uliyajua so chakufanya wewe piga kazi acha kulia lia.
Najiuliza ivi ukiitwa jpili au jmosi si unalipwa overtime au?
 
Mama mmoja alikuwa anapigwa mara kwa mara na mumewe, naye alipochoka akabuni jinsi ya kumuadhibu mumewe ili aache tabia ya kumchapa, mumewe akiwa amelewa kalala ndani yeye akaondoka na mtoto mchanga kwenda Polisi na akiwa njiani mama akampiga ukucha mtoto sehemu ya siri na kuripoti kuwa mumewe kambaka mtoto, kesi iliendelea na mwisho hakimu akamtia hatiani mzee wa watu na kumfunga jela miaka 7 wakati huo, baada ya tamko hilo palepale mama mlalamikaji akatoa kilio kikubwa sana na kuelezea mpango mzima na kuwa hakutegemea adhabu kubwa kihivyo, watumishi wa serikali awamu hii kuweni waangalifu kwa kila mteja kwani wanaweza kufikiri kuwa wanatumbua jipu kumbe wanapasua Aneursm na wakakuua kwa uzembe wa wrong diagnosis
 
ulishawahi kujiuliza rushwa hii kwa watumishi wa afya chanzo nini,serikali yako imetengeneza mazingira rafiki ya kazi kwa watumishi wa afya,nyie wenyewe hamuwezi kukaa maeneo haya hata nusu saa kwa hali ilivyo mbaya ya majengo na mazingira kwa ujumla,serikali must play their part kwabla ya kuanza kufukuzana hovyo
Hivi kweli mazingira magumu ya kazi rushwa ndiyo suluhisho? Mimi nadhani chanzo cha rushwa katika sekta zote iwe ile kubwa ya wanasiasa ni watu tumekuwa materialistic sana. Vitu vimekuwa bora kuliko watu. Hii imetokana na heshima ya mtu katika jamii kuwa determined na vitu alivyonavyo.
 
Haya mambo yamepitwa na wakati kutegemea huruma ya daktari kuhudumia mgonjwa au panga la wanasiasa kutishia madaktari ndio wafanye kazi.

Dunia nzima sasa hivi hospitali zimefungwa systems ambapo mgonjwa akisajiliwa hospitalini tu inajulikana ni saa ngapi na kuonyesha amepangiwa daktari nani. Akihudumiwa na daktari kwenye system inasoma, akipangiwa kwenda maabara inaonyesha na kapima vipimo gani na majibu ni yepi hadi siku mgonjwa anatoka hospital na inabaki kwenye medical records. Kufanya kazi kisisiemu sisiemu kwa kutegemea huruma na kutishiana imebakia Tanzania tu na hata hao akina Majaliwa na Magufuli hawataweza kufika hospitali zote Tanzania, lakini MIS zinaweza kufungwa kila hospitali na kituo cha afya. Dunia imebadilika nyie maccm, wekeni MIS kwenye mahospitali, wekeni CCTV mabarabarani maisha yawe mazuri. Mbona kodi mnatukamua sana
We're developing country brother
 
Hebu dadavua hoja yako in detail, kwamba what exactly happenned. Umekuwa biased zaidi kuwalaumu hao watumishi wote wa afya wa Mwanza bila kusema ni kitu gani hasa kimewafanya kuchukua maamuzi ya kufanya kitu kama mgomo hivi.

Mimi nimesikia kupitia vyombo vya habari haya kuhusu baadhi ya madaktari, manesi na wauguzi wa Mwanza;

1. Kwamba RC Mwanza alisikia malalamiko ya baadhi ya wagonjwa kutohudumiwa vizuri ikiwemo huyo mjamzito kujifungulia (sina hakika ni ktk mazingira gani na kwa nini, lakini inasemekana alijifungua mtoto/watoto ambao walifariki). Kwa incident hii wananchi walikasirika na kuona kuwa kuna uzembe flani ulitokea ndiyo maana hilo likatokea. Kelele hizi zikasikika na RC akafika ktk hospitali hiyo na kuamuru baadhi ya madkatari na manesi kusimamishwa kazi kwa malalamiko tu ya wananchi kupitia camera za TV!

2. Jana juma4 au juzi juma3 nikasikia tena kupitia vyombo vya habari kuwa madaktari, manesi na wahudumu wa afya wa hospitali nadhani ya Butimba ambayo ni DDH ya manispaa ya Nyamagana "wanatishia" = "kugoma" kutukuendelea na majukumu yao kwa sbb ya usalama wao kazini kutolindwa na pia kutotendewa haki especially kuadhibiwa pasipo kufuata taratibu na kusikilizwa.

Nadhani hoja ya msingi iko hapo yaani KUADHIBIWA PASIPO KUFUATA TARATIBU ZA KIUTUMISHI NA KUSIKILIZWA. Hii inadhalilisha, kuogepesha na kukatisha tamaa sana!

Aidha, watumishi wa afya kwa ujumla wao wanalalamikia mazingira duni ya utoleaji huduma kwa wagonjwa ikiwemo ukosefu kabisa wa vitendea kazi kwa maana ya vifaa tiba, upungufu wa madaktari, manesi na wahudumu wengine wa afya to the extent kwamba mtumishi mmoja analazimika kufanya kazi masaa mengi kuliko kawaida kuhudumia
wagonjwa, malipo duni nk

Swali ni je, tunafikiria haya kabla ya kuchukua hatua ya kuwalaumu?

Kingine mimi nadhani matatizo mengine yapo kwa wagonjwa wenyewe na watu wao wanaowauguza kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya haki na wajibu wao.

Mfano kwa mama mjazito, amebeba mimba akakaa tu nyumbani na hata siku moja hakuwahi kuhudhuria kliniki ili kuwezesha daktari kufanyia monitoring ya ujauzito huo.

Muda wa kujifungua ukafika ikashindikana kujifungulia nyumbani kama walivyotarajia na sasa uamuzi ukafikiwa wa kupeleka hospitali. Ni lazima mama huyu na ujauzito wake atakuwa kwenye risk kubwa ya kupoteza maisha au mtoto wake.

Maswali yangu ni haya, kuwa was this considered kabla ya kufikia maamuzi yoyote?

Au ni kwa sbb tu wananchi wamepiga kelele, then na sisi viongozi kwa sbb tunatekeleza majukumu yetu kwa "mzuka" tu pasipo kuzingatia taratibu, kanuni na sheria zilizopo?

Je, wananchi hawa wana elimu ya kutosha juu ya wajibu na haki zao au ni kwa sbb tu wamelishwa kasumba na kuaminishwa kuwa watumishi wa umma madaktari na manesi wakiwemo ni wala rushwa na kwa hiyo popote mlipo pigeni kelele na serikali itachukua hatua? Na je, tutakwenda na kufika salama kweli kwa mtindo huu wa ufanyaji kazi?

Hakuna anayebisha kuwa kuna baadhi ya watumishi wa umma kweli walikuwa wamejisahau na walikuwa hawatekelezi wajibu wao ipasavyo.

Mimi ninachojaribu kusisitiza hapa ni kuwa, katika kurudisha maadili na nidhamu katika utumishi wa umma ni lazima kufanyike kwa uangalifu mkubwa ili tusije kuwatia hofu hata wasio na matatizo na kushindwa kutekeleza majukumu yao na wakati huohuo taratibu, kanuni na sheria za utumishi wa umma zikizingatiwa ipasavyo.

Haiwezekani RC au DC au Waziri yeye ndiye awe mtoa amri tu ya fukuza huyu, simamisha kazi huyu au hamisha huyu na peleka kule. Itakuwa ni chaos

Aidha serikali nayo itende na itekeleze majukumu yake na isiwe ni chanzo cha watumishi hawa kuonekana hawafanyi kazi zao ipasavyo wakati haijawajengea mazingira bora ya kuhudumia watu.

Mfano ipeleke vitendea kazi na pesa ktk hospitali zake kwa wakati ili hawa watumishi wasiwe na visingizio vya kutotenda yawapasayo kutenda.

Mimi niko Shinyanga. Juzi kati mwanangu alikuwa ana kohoa na homa, nikampeleka ktk kituo cha afya cha serikali kilicho jirani nami. Akapimwa na kukutwa anasumbuliwa na minyoo na U.T.I.

Daktari akamwandikia dawa hizi kentrax, erythromicine na panadol. Amini usiamini, nilipata panadol pekee hapo na zingine zote nilikwenda kununua ktk maduka ya madawa mitaani licha ya kuwa natumia NHIF card na kila mwezi nakatwa ktk mshahara wangu takribani Tshs 60,000/= kuchangia bima ya afya!

Sasa ktk mazingira haya, who is to blame? Serikali au wauguzi naadaktari?

Haiwezekani focus iwe ktk hospitali za Muhimbili tu na kuzisahau zahanati na vituo vya afya vijijini ambako huko pia ndiko kuliko matatizo makubwa!!
ndugu yangu hawa manesi na madaktari wanafanya kazi kama mbwa aikwambie mtu,unakuta nesi mmoja ila anawagonjwa zaidi ya mia wanamsubiri awape huduma,hapo kuna mama mjamzito kaja kupima uzito na kujua maendeleo ya mimba,kuna mwingine kaja kwa ajili ya chanjo,mwinge kaja kupa ushauri wa lishe na unyonyeshaji hivi unadhani ufanisi unapatikanaje hapa??alafu mtu kama mulugo ambae kazi yake kutukanana na wanasiasa na kuamrisha polisi anakuja kutoa amri za kitoto bila kuruhusu taratibu za kitaaluma kutumika ni upuuzi ulio pitiliza
 
Hivi kweli mazingira magumu ya kazi rushwa ndiyo suluhisho? Mimi nadhani chanzo cha rushwa katika sekta zote iwe ile kubwa ya wanasiasa ni watu tumekuwa materialistic sana. Vitu vimekuwa bora kuliko watu. Hii imetokana na heshima ya mtu katika jamii kuwa determined na vitu alivyonavyo.
wewe uko kimabishano zaidi so kulizungumzia hili swala kwa upana zaidi,kama ukoserious hauko kisiasa utataka muafaka katika jambo hili..tatizo la JF ni fake ID linatufanya tuna act wakati mwingine
 
Habari wana JF, hivi karibuni tumeona tukio moja likitokea huko Mtwara la Kusimamishwa Daktari mmoja aliyehusika katika kuomba rushwa kutoka kwa mgonjwa aliyetakiwa kufanyiwa upasuaji.

Japo ushahidi ni mgumu wa mazingira ya hiyo rushwa, ni ukweli usio na kificho kuwa Wahudumu wa afya walio wengi wamekuwa si waaminifu tena wasiokuwa na chembe ya huruma kwa binadamu wenzao kiasi cha kutojali uhai wa wagonjwa wanaowahudumia.

Tukio la Mtwara limefuatana na matukio mawili ya kusikitisha yaliyotokea katika jiji la Mwanza, wilaya ya Nyamagana kwenye hospitali ya wilaya ya Nyamagana (Butimba) na hospitali ya mkoa ya Sekou Toure.

Likitangulia la hospitali ya Butimba, mama mmoja alijifungulia chooni watoto mapacha na wakafariki kwa kile kilichodaiwa ni uzembe wa manesi waliokuwa wakimtolea kauli chafu mjamzito huyo kuwa awaite Majaliwa na Magufuri waje wamhudumie.

Tukio jingine lililofuatia ni kufariki kwa mama na watoto wake mapacha katika hospitali ya mkoa (Sekou Toure) kwa kucheleweshwa kuongezwa damu.

Kutokana na matukio hayo, kuna manesi na madaktari wametiwa nguvuni kutokana na kasi iliyopo sasa ya kurejesha nidhamu na uwajibikaji katika utumishi wa umma.

Sasa Madaktari wamefanya mgomo katika hospitali ya Butimba kwa madai wanaogopa usalama wa kazi yao kwa kuwa wao hawawezi kuzuia kifo kwa mgonjwa pale muda wake unapokuwa umefika.

Mheshimiwa Rais, sichelei kusema hawa madaktari wanataka kutunishiana misuli na serikali yako kwa kile kilichotokea Mtwara. Kwanini Wananchi wote wanaokumbwa na masahibu haya kutoka kwa wahudumu wa afya katika maelezo yao wanaambiwa wawaite Majaliwa na Magufuli wawahudumie?

Mheshimiwa watumie vijana wako wa TISS wakupe taarifa kamili ili ujue utapambana vipi na udhalimu wa baadhi ya watumishi wa afya ambao wanafikiri kuwa wao ni bora katika jamii kuliko watu wengine wakisahau kuwa wao pia ni product ya mwalimu, hivyo tunaishi kwa kutegemeana.
Kwa hali hii ya kujenga chuki dhidi ya madaktar itakuja kuleta maafa, siasa inachanganywa na kazi hawa watendaji wa mh rais hawajaelewa maana ya kasi cha zaid wanachofanya ni udhalilishaji. Kwenye huo mgomo dr mmoja kasema sasa hivi wagonjwa hawafati taratibu, hata ukimwambia apange mstari hataki. Pia kuna vifo vingine kwel daktr analeta uzembe na vingine ni nje ya uwezo wa dktari, sasa kifo kama hicho nacho ataambiwa ni uzembe. Lets wait mwisho wake
 
ulishawahi kujiuliza rushwa hii kwa watumishi wa afya chanzo nini,serikali yako imetengeneza mazingira rafiki ya kazi kwa watumishi wa afya,nyie wenyewe hamuwezi kukaa maeneo haya hata nusu saa kwa hali ilivyo mbaya ya majengo na mazingira kwa ujumla,serikali must play their part kwabla ya kuanza kufukuzana hovyo
Kumbe majengo mabaya ndo yanawafanya mchukue rushwa? Nilikua sijui hata, waalim na police wasemeje sasa?
 
Kumbe majengo mabaya ndo yanawafanya mchukue rushwa? Nilikua sijui hata, waalim na police wasemeje sasa?
tatizo ubongo wako haunauwezo wakung'amua nilichokiandika umekimbilia mstari mmoja na kuucommentia..ukikua utajua haya
 
wewe uko kimabishano zaidi so kulizungumzia hili swala kwa upana zaidi,kama ukoserious hauko kisiasa utataka muafaka katika jambo hili..tatizo la JF ni fake ID linatufanya tuna act wakati mwingine
Hapana mkuu sipo kwa ajili ya kubishana bali kwa kujibu hoja. Hivi kweli ulitaka nikubali kuwa mazingira magumu ya kazi ndiyo sababu ya kupokea rushwa? Sikatai ni kweli mazingira ya kazi ni mabovu.
Mimi ningeomba kuuliza hivi unafikiri ni kwanini kumekuwa na sintofahamu kati ya Wananchi na watumishi wa afya?
 
sikujua kama wewe ni mjinga kiasi hiki
We ndo mjinga bro Tanzania na umasikini huu ambao hospital hamna dawa hamnva vitendea kazi kama vifaa vya oparations, vitanda hamna badala ya kuangalia vitu kama hivyo unasema hospital kufungwe cctv camers wakati hata vitanda hamna

Ukapimwe akili wewe akyamungu sio mzima wewe
 
nakwambia wewe kwa comment zako tu ni mjinga si kidogo,nimejaribu kufatilia comment zako kama tatu hap nakuona ujinga wako ulivyo mwingi uko kwa ajili ya kukwaza watu sio kuchangia
 
Back
Top Bottom