Madaktari wa Muhimbili: This is unprofessional....!

Madaktari wa Muhimbili: This is unprofessional....!

Pole sana Mtambuzi.. Ninaamini kabisa kuna makosa yalifanyika hata kama wakibisha wenye taaluma zao..

Hahahahahahahahahaha hii imenifurahisha sana.
Kwa hiyo kiujumla ni kwamba wote tuliohusika kwa namna moja au nyingine tumechemsha.
Katika hali kama hiyo kilichobaki ni kufuta ukurasa mzima na kuanza upya tu.

Ila jokes aside, daktari aliyesema hospitali ina haki ya kumfukuza mgonjwa aliyekataa kutumika kufundishia anatakiwa kurudi tena kwenye darasa la ethics...

Mkuu ZeMarcopolo nimefualitilia comments zako pamoja na evidences ulizozimwaga na jinsi ulivyo-present duuh.. Kichwa sana mkuu.. Umenipa darasa hapa kwa mengi ambayo nilikuwa siyafahamu..! Hii another side ya ZeMarcopolo sikuwahi kudhania kama ipo.. Big up Mkuu..
 
Last edited by a moderator:
Kama uliataka asifundishiwe ungeomba alazwe ippm yaani private ward ambako utaonwa na Dr wako tu, ukishakaa ward ya kawaida vumilia madaktari wote wa idara hiyo wanaruhusa ya kukuona. Na ninauhakika kuwa aliombwa concert lakini wewe ni mlalamishi. Mimi nimesoma pale hata kama ni muda wa kuona wagonjwa sehemu ambayo inatumika hufungwa na screen. Wewe jua hili ukienda Muhimbili lazima uwe tayari kutumika kama ubao either you like or not. Na kwa taaifa yako Muhimbili wagonjwa wote walio kwenye ward za kawaida wanatibiwa vizuri zaidi kuliko wa IPPM coz kwa huyu wa ward ya kawaida madaktari wengi wanajadiliana na kufanya vipimo mbali mbali kulingana ugonjwa wanaofikiri. Tofauti na ippm ambako only one Dr see you and when is absent no one will see you until he/she come back. Jua hilo ndugu tatizo wagonjwa nyinyi ni much know sana. Kamwulize ndugu yako je aliombwa concert siyo kulalamika tu wakati huna details

Hapo penye red nalo tatizo ndani ya madaktari wetu, Duniani kote ninavyojua Doctor hawezi hawezi fanya lolote kwa mgonjwa wake, narudia kwa mgonjwa wake bila kupata consent ya mgonjwa kwanza bila kujali ni Teaching Hospital au la, Huwezi huwezi kukurupuka tu na kumwambia mama eti..."panda kitandani nikupime" gosh... bila hata ya kupata ridhaa yake mgonjwa kwanza kisa wewe upo Teaching Hospital, kama ndivyo mnavyofanya basi hamuwezi kufanya kazi kwa wenzenu waliostaarabika

UKITAKA UWE DAKTARI MZURI BASI MGONJWA SIKU ZOTE NI SUPRIOR KWAKO WEWE DOCTOR
 
Pole sana mkuu.


Ukweli mgonjwa kutumika kufundishia si swala baya ila kuwepo na ruhusa ya mgonjwa. Na kwa uzoefu wangu mara nyingi mgonjwa huombwa kwa mdomo na hakuna form yoyote, na akikataa haitakiwi kumlazimisha. Na kama hakuombwa si sawa ila mgonjwa ana haki ya kusema No. Kingine ni kwamba taarifa za mgonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari/madaktari. Kwa hao wanafunzi kujua hilo si tatizo ila ni vema Daktari kuwa mwangalifu taarifa isiwafikie watu wengine isipokuwa kwa ridhaa ya mgonjwa. Ni vizuri daktari kujitahidi kulingana na mazingira.



Lakini katika hili hebu niambieni mnadhani wodi hizo kweli zipo standard? Kuna privacy pale Muhimbili kwa wodi za kawaida? Kwa hiyo ni kujitahidi kuwa makini.

Tatu inavyopaswa kuwa (ideal kwa hapa kwetu) mgonjwa huyo alihitaji kujua hilo (yaani yupo kwenye terminal stage) na kufanyiwa death preparation. Hiyo ni kwa mujibu wa standard/ideal. Kwa jamii yetu hii huwa siioni, hatuna utaratibu wa kufanya hivyo na hata jamii zetu hazipokei vizuri, mi niliwahi jaribu; badala yake mgonjwa anakuona wewe mbaya, japo ni kitu kizuri tu. Mimi nina observation nyingine, Hivi kumbe Wauguzi wa Tanzania hawajui dalili za terminal stage? Sikutegemea kushtuka kiasi hicho kwa wife na sister. Tusaidiane, tuwekane sawa tunapokosea...


Privacy bado ni tatizo lakini pia wakati mwingine hata lugha... Hebu nisaidieni Terminal stage kwa kiswahili inakuwaje na itapokelewaje?
Mkuu narudia tena kukanusha, MGONJWA WETU HAKUWA KATIKA TERMINAL STAGE, mbona tumemtoa na kumhudumia nyumbani na sasa ameonyesha nafuu kubwa....
Wale walitaka kukamilisha somo lao kupitia mgonjwa wetu, hatukatai kufa, lakini hata wanaye waliona kwamba mgojwa wetu hajafikia hatua hiyo................
 
Kwa kweli hali inatisha na kusikitisha sana kutokana na kauli za hawa Madaktari na jinsi wanavyochangia hii mada humu kwenye Jamvi. Lakini hii ndio hali halisi baadhi yetu tunayojaribu kuijadili hapa jamvini.
Hakuna kitu kizuri na cha busara Kama kujadili Jambo kwa kutumia akili na fikra sahihi kuliko kutumia jazba na utemi kana kwamba wewe ni Mbingu na ardhi. Huku ukisahau kuna siku na wewe utatengenezewa Jeneza na kuchimbiwa kaburi.

Ukweli ni kwamba baadhi ya Madaktari hapa Tanzania wameenda shule ya utabibu either kwa msukumo wa familia au kwa kutaka kuwa Mungu mtu chini ya Mbingu. Bila kuelewa kwamba udaktari ni wito. Na hili linajidhihirisha kutokana na comments hawa baadhi ya Madaktari walizoandika humu. Daktari anapotumia lugha na kusema "Mgonjwa ukija ukaniletea zenye na mimi nakuzingua" huyu sijui nimuweke kwenye kundi gani???? Maana hata ndugu zetu wabaeba zege huwa wana adabu wakiwa kazini kwao na kuheshimu Karai,Cement na kokoto kwa sababu wanategemea ushirikiano wa vitendea kazi ili mkono uende kinywani.

Ni hatari sana Daktari unapodharau watu wa fani nyingine na kusahau kuwa Wewe pia unahitaji huduma za msingi za kibinadamu,kwa mfano kujengewa nyumba,kutengenezewa jeneza,kuchimbiwa kaburi na huduma nyingine nyingi ambazo naweza kujaza thread hapa.
Inashangaza na kusikitisha ya kwamba kuna Madaktari wachache Kama hawa tunaowaona humu wako tayari kusema na kuandika lolote ili mradi wao wanajua kila kitu na wako sawa na upotofu wao wa maadili na utovu wa Nidhamu.
Udaktari ni fani tu Kama fani nyingine. Na katika maisha ya binadamu ya kila siku hapa chini ya jua kila fani inategemea fani nyingine ili kusukuma gurudumu la Maendeleo.

Kutokana na statement za hawa Madaktari waliokuja kutoa utetezi wa shurti na kejeli humu jamvini,inanifanya na kunipa mwanga wa kuelewa kwa nini Serikali yetu Tukufu huwa inadeal na Madaktari kwa aina yake. Na sababu kubwa ni baadhi ya Madaktari Kama hawa tunaowaona hapa. Inatakiwa pia mtambue ya kwamba MISHAHARA YENU INATOKANA NA KODI ZETU SISI WATANZANIA. Hilo tu linatosha kuwakumbusha wajibu wenu kwetu WATANZANIA.

PS: Kwa nyinyi Madaktari uchwara mliokuja na kejeli na dharau kutoa majibu ya kipu.uzi nataka mfahamu ya kwamba hapa
JF kuna watu wa fani heshimika tofauti. Kwa hiyo mnapoamua kuja kuwadhalilisha MADAKTARI wenzenu mjipange
Na kutambua kila utakaloliandika linaakisi wewe ni mtu wa aina gani na uerevu wako ukoje.

pole sana ndugu yangu, daktari huyo huyo anatarajia baada ya kazi ale nyama choma, bia, aishi sehemu yenye usalama, aendeshe gari au apite kwenye bara bara nzuri yenye lami, mtoto wake afundishwe na mwalimu mwenye weledi, na huduma nyingine nyingi ambazo hana utaalamu nazo. Ndio maana waalimu walianza mgomo wa kimya kimya kama malipizi!
 
Maana ya Terminal Stage ni nini?

Close to death ...(but still can benefit on Palliative treatment), Bwana Mtambuzi unapokataa kuwa mgonjwa hakuwa kwenye terminal stage basi mimi inanikumbusha Doctor mmoja alikuwa mzee wa kizungu pale KCMC - Urology Dept alipomwambia mgonjwa wake wa Cancer kuwa ugonjwa umesambaa kila mahali na hana muda mwingi wa kuishi duniani then akampa discharge na tarehe ya kurudi, baada ya hapo Doctor akaenda kwao likizo na hukohuko akapata heart attack akafa, mgonjwa aliporudi kuja kuonwa alipanga foleni kwenye mlango wa Doctor marehemu akiwa hajui nini kinaendelea, Dr ....(mswahili) alipotaka kujua mbona haingii ofisini kwake amtibu? mgonjwa akasisitiza anapenda aonwe na Doctor wake mzungu, Doctor ikabidi amweleze kuwa yule Doctor alishakufa, baada ya hapo yule mzee alilia sana tu, manesi wakamuuliza kisa cha kulia sana? akawajibu kuwa "siku ananitoa wadini alisema mimi sina maisha marefu na nitakufa karibuni kumbe yeye ndio hakuwa na maisha marefu"
 
Mkuu inaonekana huijui Muhimbili na pia hujasoma maelezo yangu ukaelewa, bali umekurupuka..
Hii Muhimbili unayoijua ndiyo inayoongoza kwa wagonjwa kufa vifo vinavyoweza kuzuilika. Hili nitalizungumzia siku nyingine lakini kwa sasa hebu kwanza pitia hiki nilichoandika, halafu nitaendelea kujibu hoja zako nyingine...



Kwanza nakanusha mgonjwa au ndugu wa karibu kushirikishwa kabla ya mgonjwa wetu kutumika kufundishia, hilo halikufanyika. Pili si kweli kwamba mgonjwa wetu alikuwa yuko kwenye Terminal Stage kama yule daktari alivyotaka kuwaaminisha wanafunzi wake na kama hii ndiyo aina ya ufundishaji wa matatibu wetu, haiyumkini ndio sababu ya kuongezeka kwa vifo vingi vinavyoweza kuzuilika katika hospitali zetu.... ninavyoandika hapa mgonjwa wetu yuko nyumbani na ana afya njema kuliko alivyokuwa amelazwa pale Muhimbili. Tulimpeleka akiwa anatembea tukamrudisha akiwa hawezi hata kunyanyua mguu, lakini kutokana na juhudi za wanaye tumeendelea kumhudumia akiwa nyumbani na sasa anaweza kutoka nje na kuzungumza na wajukuu zake... Tatizo hapa sio kukataa kukubali ukweli kwamba mgonjwa wetu yuko kwenye Terminal Stage, Mimi ninapinga namna ujumbe ulivyofikishwa na hili lilifanyika muda wa kuangalia wagonjwa, nadhani walichelewa kumaliza darasa na hivyo mke wangu na shemeji yangu wakawakuta wakiendelea na darasa bila kung'amua uwepo wao yule daktari aliropoka hayo maneno.... Napinga kabisa mgonjwa wetu hakuwa kwenye hiyo stage bali walitaka kum-maliza ili somo likamilike........

kumbe walichelewa kumaliza round its ok, na kumbe walikuwa wanamwona ok. Sasa kaka wao walikuwa wanazungumza yanayowahusu, na huyu mkeo aliingiliaje mazungumzo yasiyomhusu. Nafikiri kwa hulka na tabia za kitanzania unapokuta watu wanazungumza mazungumzo yasiyokuhusu you stay aside wamalize ndo na wewe uendelee na shughuli zako sasa iweje umhukumu wakati yeye alikuwa anawambia wanafunzi wake. Kwa hiyo naweza sema huyo ndugu yako ni mmbea. Huyu ndo wale akikuta watu wanazungumza story pengine wakataja tu jina lako anakuja kusema ooooh walikuwa wanakusema. Naomba ufute kauli yako kuwa ANAROPOKA coz walikuwa wao tu na mgonjwa huyu mwingine hawamfahamu. Hivyo with this clarification you gave naona Dr hana hatia hata kidogo coz wao walikuwa wanazungumza. Mimi niseme wewe ni much know hata sasa unabisha na kulalamika kitu ambacho hujui. Coz wakati wa round wapo madaktari ambao hawamjui mgonjwa ambao watapenda kujua history ya mgonjwa sasa tushindwe kushirikishana coz tunaogopa vimeo kama wewe. By the way round siyo teaching coz wagonjwa wote waliokwenye ward tajwa waliptiwa vivyo hivyo kama ndugu yako. Yule ambaye tunamtumia kwa teaching kwanza huzungushiwa screen kusudi shughuli zingine ziende. Kama ulikuwa unataka aonwe na Dr mmoja tu basi pale Muhimbili ungeomba kuwa Dr nani akuone na wala hakuna Dr hata mmoja mwingine angeingiliwa na Dr mwingine na huo ndo utaratibu. Kama unafikiri hukufanyiwa fare basi nenda mahakamani uwashitaki muhimbili nao watakuja kujibu. Unatupotezea wakati. Na kwa taarifa yako mimi nimesoma pale, na ndugu zangu wakiwa referred pale huwa naprefer watibiwe ward za kawaida coz vipimo hata wiki haiishi nishavipata afu pia madaktari wengi watamwona na watatoa mchango wao at the end of the day pt anabenefit kuliko akiwa Private ambako Dr kumwona si lazima kila siku, na vipimo vya weza chukua hata 2wks afu kumbuka hapa unadepend single opinion ambayo most of the case has more mistakes.
 
Mkuu ligi inakushinda unaanza kutukana, toa evidence, kama huna si useme tu. Naanza kuamini wanywa viroba ni wengi hapo MNH. Tukienda APOLO mnalalamika tunawadharau......! Guys you need to accept/take constructive criticism.

Yaani ndugu yangu wewe ni mgumu kuelewa,hata Muhimbili kama utaki kufundishiwa toa taarifa kwa uongozi,sio kusumbua madaktari wodini,ili ni teaching hospital,ukikataa kufundishiwa hamia IPPM na matibabu yako hayataathirika na kitu chochote.Unasoma articl alafu huzielewi,lakini tatizo sio field yako but unakomaa tu,wewe kweli mkomavu inaeelekea sura yako imukunjana njoo tukufanyie plastic surgery
 
watu wanaoongea tu kwakuwa hawajauguliwa kwa mimi mgonjwa wangu atumike darasa au mimi mwenyewe nitumike darasa sijali chochote zaidi ya kupona. Hivi kuna mtu alishawahi kuishi China akahudhuria hospitali za wachina? especially opd? then kama yupo atupe experience ya aliyoyaona then hii thread ifungwe. sijaona kosa lolote hapa lilofanyika sana as far as ndugu yako alikuwa anapatiwa matibabu

Kwa hiyo kwako wewe China ndiyo point of reference?
 
watu wanaoongea tu kwakuwa hawajauguliwa kwa mimi mgonjwa wangu atumike darasa au mimi mwenyewe nitumike darasa sijali chochote zaidi ya kupona. Hivi kuna mtu alishawahi kuishi China akahudhuria hospitali za wachina? especially opd? then kama yupo atupe experience ya aliyoyaona then hii thread ifungwe. sijaona kosa lolote hapa lilofanyika sana as far as ndugu yako alikuwa anapatiwa matibabu

Kwa hiyo kwako wewe China ndiyo point of reference?

Na ugriti thinka wako wooote umeishia China tuu.
 
wewe mtambizi usiongee au usishabikie kitu ambacho hukijui...! umeshaambiwa kuwa huyo dactari alikuwa na wanafunzi anawandisha kupitia huyo mama mkwe wake ..! kisheria hilo siyo kosa kabisa maana ndiyo utaratibu duniani kote..! lakini kosa lakiufundi ambalo lilikuwa limefaniya hapo nikwamba kusema hali ambayo mgonjwa anayo na yeye akasikia..! ..! wewe unavyo waona madaktari unaona wanakaa tuu darasani ndiyo inatosha ..! lazima wafanye practical kwa wagonjwa kwama ilivyo tokea kwa huyo mgonjwa aliye elezewa hapo..! na hiyo ni dunia nzima..! kama hujui kitu kiundani usikurupuke kuongea na pia usiwe mvivu wa kufikiria..!:A S 39:
 
Pole sana mkuu wangu Mtambuzi. Yaani katika medical ethics hiyo kitu haitakiwi kabisa. Ingekuwa ni nchi za wenzetu yaani ni kufungua mashtaka kabisa dhidi ya madaktari hao. Huo ni udhalilishaji wa nafsi ya mgonjwa na unamwathiri kisaikolojia na ndugu pia. Aise wangelipa fidia ya kufa mtu. Yaani kweli sijui ni bangi au kitu gani hiki. Ila sasa Mtambuzi si bora wewe uliweza kumhamisha? Wengine ndiyo wamateseka na kejeli na manesi na madaktari na dawa wala hakuna. Dah kweli sijui tufanyeje Tanzania hii.
 
Lakini mkuu, unapotumia verbal concent utathibitisha vipi kuwa mgonjwa alikubali itakapohitajika kufanya hivyo? Chukulia mfano Mtambuzi angeenda kushitaki, hospitali ingethibitisha vipi kuwa concent ilipatikana?

Kanuni za concent ni kwamba LAZIMA kuwepo na shahidi wakati concent inatolewa. Je, katika huo utaratibu nani huwa shahidi?

Halafu usiseme haiwezekani kama ulivyoandika hapo juu. Ingekuwa haiwezekani wasingekuwepo watu kama Mtambuzi na wengine wengi waliochangia kwenye thread hii wenye malalamiko.

Haya mambo yapo jamani. Pengine na sisi wagonjwa hatuelewi haki zetu. Mi nilishuhudia wodi ya wazazi, intern wako na supervisor wao. Basi mtoto akikaribia kutoka wanaitwa wote ukiona wanavyochungulia anapotoka utaogopa.
 
Zamani ilikuwa mpaka mgonjwa atoe ridhaa, ikaonekana wagonjwa wengi wanakataa

Sioni ni kwa sababu gani daktari alazimishe consent simply because a patient will make a decision you don't disagree with. Otherwise, hiyo itakuwa ni duress kama siyo undue influence.

...baadae ikawa kila mgonjwa anayelazwa kwenye teaching hospital, automatically unakuwa umetoa ridhaa ya kutumika kufundishia..

Kwanza, unaposema university hospital unamaanisha university hospital zote duniani au ni zile za Tanzania tuu?

Pili, kama ni Tanzania, unaweza kutupa hiyo sheria au guideline inayohalalisha automatic consent kwenye university hospital kama Muhimbili? This will help a lot.

Tatu, kuna aina mbili za consent: explicit consent na implied consent. Explicit consent ni pale mgonjwa anapompa daktari specific permission to do something. Explicit consent inaweza kuwa ya mdomo au ya maandishi.

Implied consent ni pale mgonjwa anapoonyesha ridhaa yake indirectly, kwa mfano, kwa kuleta prescription ili umpe dawa. This is not a lesser form of consent but it is only valid if the patient knows and understands what they are consenting to.

Hii automatic consent inatoka wapi? Najua sometimes hasa wakati wa emergency treatment, kunaweza kuwa na automated informed consent kutokana na hali mbaya ya mgonjwa au kutokuwepo kwa mtu wa karibu kutoa explicit consent. Lakini mgonjwa ana capacity ya kutoa consent lakini analazimishwa kutoa consent automatically?

OK, let's assume pia kuna "automatic consent". Sheria inasema wazi kuwa ili consent iwe valid, lazima anayetoa awe na capacity ya kuitoa, lazima awe amefanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yoyote, lazima awe amepewa "sufficient, balanced information" ili kumwezesha kufanya an informed decision, na pia ni lazima awe na uwezo wa kujua na kupima maelezo aliyopewa kabla ya kutoa ridhaa yake.

Sasa nyie kama madaktari mna-ensure vipi kuwa mgonjwa anajua kuwa hosipitali anayoenda ni university hosipital na kwamba consent yake ya kutumika katika kufundishia itakuwa obtained automatically? Hivi mgonjwa wa kawaida atajuaje hii ni teaching hospital na ile siyo kama hatapewa maelezo kabla?

Cha tatu, haikupaswa ninyi kuwepo wakati mwalimu anafundisha wanafunzi wake kwa mgonjwa wenu...kwa sababu atawaonyesha technic mbali mbali za kuexamine na kufukia conclusion na wanafunzi watajaribu..hili linahitaji 'privacy', kwa hiyo hata ninyi hamkuwa na heshima kwa mgonjwa wenu kwa kuwepo hapo karibu hivyo mkiangalia na kusikiliza wakati mgonjwa yuko na madaktari wake. Mimi naona ethical breach kwa pande zote mbili.

Wangejuaje kuwa hawakupaswa kuwepo pale wakati mwalimu anafundisha? Nani alikuwa na majukumu ya kuwaeleza kuwa hawakupaswa kuwa pale? Who led them to breach the ethics? Unaona jinsi tatizo moja linavyozaa tatizo lingine? Kutokuomba prior consent, kumesababisha breach of confidentiality.

Kama mgonjwa angekuwa ametaharifiwa kabla kuwa atatumika kufundishia basi angekuwa na fursa ya kuamua kama ndugu zake wawepo pale wakati anatumika kufindishia. In fact, daktari alikuwa na duty ya kumwuliza mgonjwa kama angetaka ndugu zake wandelee kuwepo wakati anatumika kufundishia.

Kwa hiyo hapo sidhani kama kuna "contributory negligence" kwa upande wa ndugu zake. Daktari alikuwa na duty ya ku-seek consent, hakufanya hivyo. Alikuwa na duty ya ku-maintain confidentiality, hakufanya hivyo. Hata kama kuna "automatic consent" sidhani kama ina dispense the duty of confidentiality automatically. Does it?
 
Mkuu hakuna form yoyote tuliyojaza mgonjwa wetu kutumika kwa ajili ya kufundishia, lakini pia hakuwahi kumbiwa kwamba yuko kwenye terminal stage, kwa hiyo yeye na wanaye wamesikia taarifa hizo wakati daktari akiwafundisha wanafunzi wake... nilipofika niliwakuta nje wakilia na baada ya kuwadadisi wakaniambia kwamba daktari alikuwa anawaambia wanafunzi wake kwamba mama yuko kwenye terminal stage wakati anawafundisha na haikuwa ni taarifa kwao bali ilikuwa ni sehemu ya darasa huku akiwaonyesha dalili zinazothibitisha kwamba mgonjwa wetu yuko kwenye hali hiyo, kitu ambacho kiliwashtua sana.

Hata hivyo tumemrudisha mama nyumbani na hali yake inaonyesha kuimarika tangu jana jioni na leo asubihi amefanyiwa mazoezi ya kunyanyuka na kutembea na amemudu........

Pole kaka Mtambuzi, ni tatizo ambalo linapaswa kuwa addressed! Kuna mtazamo uliopitwa na wakati kwa baadhi ya makoligi wangu kudhani once mgonjwa amekuja hospitali wanaouhuru na haki ya kutenda na kusema lolote! Apart from being unprofessional it is also inhuman! Mungu awape nguvu ya kumuuguza mgonjwa, najua kupitia hapa Jf ujumbe utakuwa umewafikia
 
Last edited by a moderator:
wewe mtambizi usiongee au usishabikie kitu ambacho hukijui...! umeshaambiwa kuwa huyo dactari alikuwa na wanafunzi anawandisha kupitia huyo mama mkwe wake ..! kisheria hilo siyo kosa kabisa maana ndiyo utaratibu duniani kote..! lakini kosa lakiufundi ambalo lilikuwa limefaniya hapo nikwamba kusema hali ambayo mgonjwa anayo na yeye akasikia..! ..! wewe unavyo waona madaktari unaona wanakaa tuu darasani ndiyo inatosha ..! lazima wafanye practical kwa wagonjwa kwama ilivyo tokea kwa huyo mgonjwa aliye elezewa hapo..! na hiyo ni dunia nzima..! kama hujui kitu kiundani usikurupuke kuongea na pia usiwe mvivu wa kufikiria..!:A S 39:

Mhhh!! Soma in between lines ya comment yako, halafu vaa nafasi ya Mtambuzi, nadhan utapata jibu! Tena naona kama unamponda mleta maada! Jibu hoja kama Professional ondoa jazba, kwenye kosa kubali na iwe chalenge kuirekebisa. Nimependa mchango wa EMT
 
Last edited by a moderator:
Mkuu narudia tena kukanusha, MGONJWA WETU HAKUWA KATIKA TERMINAL STAGE, mbona tumemtoa na kumhudumia nyumbani na sasa ameonyesha nafuu kubwa....
Wale walitaka kukamilisha somo lao kupitia mgonjwa wetu, hatukatai kufa, lakini hata wanaye waliona kwamba mgojwa wetu hajafikia hatua hiyo................

Mkuu kuwa katika teminal stage haimaanishi mgonjwa anakufa on the spot! Bado tukubali daktari ni mwandamu anaweza ku-overlook kitu flan akaconclude vibaya! Jaman Mungu anayo nafasi na makusudi yake!!
 
nimukuelewa moto2012...! lakini lakini stil nilicho kiandika kimeelewa maana nilikuwa kama najaribu mfafanulia mtambuzi kamavile ni mtu ambaye hajakutwa na tatizo hilo ..! kwahiyo nimemvua uhusika ili aweze kuliona tatizo hilo kwa ujumla...! napia nikasema kuwa tatizo ambalo mimi nimeliona nimoja tuu kuwa daktari aliongea kitu ambacho mgonjwa hakupaswa kukisikia ..! lakini kwaswala la mgonjwa wake kutumika kama ubao mimi sina tatito nalo..! nahata wewe siku ukienda hospital na ukiona umegeuzwa ubao hata usishangae tena ndiyo unatakiwa kuonyesha ushirikiano wa haliya juu ili huyo daktari aje kumtibu mjukuu wako miaka ya usoni:rockon:...!
 
Hapo penye red nalo tatizo ndani ya madaktari wetu, Duniani kote ninavyojua Doctor hawezi hawezi fanya lolote kwa mgonjwa wake, narudia kwa mgonjwa wake bila kupata consent ya mgonjwa kwanza bila kujali ni Teaching Hospital au la, Huwezi huwezi kukurupuka tu na kumwambia mama eti..."panda kitandani nikupime" gosh... bila hata ya kupata ridhaa yake mgonjwa kwanza kisa wewe upo Teaching Hospital, kama ndivyo mnavyofanya basi hamuwezi kufanya kazi kwa wenzenu waliostaarabika

UKITAKA UWE DAKTARI MZURI BASI MGONJWA SIKU ZOTE NI SUPRIOR KWAKO WEWE DOCTOR
Mupirocin amesema amesoma Muhimbili, na wala hakusema kama ni daktari, naomba uelewe hili!!

My patients is and will always be my priority
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom