Madaktari wa Muhimbili: This is unprofessional....!

Madaktari wa Muhimbili: This is unprofessional....!

Mama mkwe wangu alilazwa Muhimbili kwa wiki moja, lakini jana nililazimika kumtoa kutokana na kile nilichokishuhudia pale. Pamoja na vituko vingi tu tulivyoviona kutoka kwa manesi wa ward ya Mwaisela, lakini nisingependa kuzungumzia hayo kwa kuwa si mageni masikioni mwa wengi. Tulimpeleka mgonjwa wetu kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kuwa na complication nyingi nadhani ni kutokana na uzee (mkwe wangu ana miaka 70 hivi sasa)

Tulipofika pale alichukuliwa vipimo vyote ikiwapo x-ray, tatizo lilikuwa ni pale madaktari wanapopita round kuona wagonjwa. kwanza walikuwa wamemgeuza mama mkwe wangu kama vile ni darasa la kufundishia wanafunzi, kila daktari alikuwa anafika na wanafunzi wake na kufungua darasa. Cha kushangaza walikuwa wameyakalia majibu ya mgonjwa wetu huku wakiendelea kumuweka pale kama mtu wa kufundishia wanafunzi.

Sikatai mgonjwa kutumika kufundishia wanafunzi, hawa ni ndio madaktari wetu wa kesho wakajifunzie wapi. Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage.

Kitu ambacho madaktari wale walikuwa hawakijui ni kwamba mke wangu pamoja na dada yake ni wauguzi by professional na wanazijua hizo terminology vizuri sana. Sasa iweje waropoke hivyo bila kuangalia walioko karibu. kitendo hicho kilifanyika muda wa kuona wagonjwa na nadhani ndio walikuwa wanamalizia round.
Tumelazimika kumchukua mgonjwa wetu kwa ajili ya kuangalia ustaaarabu mwingine.

The real meaning of hospitality is shunned or abandoned!!,.....I am not sure if the word "hospital" is well utilised after many years of being taught in colleges.
 
hiyo hospitali ndiyo yenye proffessional doctors wengi kuliko popote, ila kuna wakati huwa naona kama viini macho, yaani mambo ambayo hujayategemea kabisaaaaa, ndiyo yanatokea! pole Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Duuuh!! Pole sana Dina.
Wanamfanya mtoto au mgonjwa Kama "freak show". Halafu unakuta na Daktari mwingine casually anasema kwa pembeni "Huyu sidhani Kama atapona warudi nyumbani tu hawa" huku mgonjwa na ndugu zake wakisikia.
Kwa kweli kuwa Mtanzania kunahitaji uvumilivu wa hali ya juu.


BTW nimeikubali hiyo signature yako. Inaweza kuwa na maana nyingi katika maisha ya Mtanzania..that only it you think outside the box...tehe.

I know.....na nikajiapiza (potelea mbali if am the loser) kuwa sitarudi kwa daktari yule tena hata kama amebaki peke yake TZ. And the funny thing, siku nyingine nikaenda kumuona daktari mwingine, kwanza alivyonipokea, he pretended (nina hakika nilimsoma sahihi), kuwa that was like a millionth case he was seeing that day, yaani kawaida sanaaa....ambacho peke yake kilitosha kunirudisha kwenye mstari, na kujua how to deal with the situation, ilivyo na kuwa tayari kwa lolote litakalokuwa linaendelea kutokea....

Nakubaliana nawe, hiyo signature is more that what it seems to be, nina hakika if you give it to the 'right' author, atatoa kitabu kizuri tu....
 
.
Naona kwenye mada hii ya leo Madaktari wetu wa JF leo wapo kimya!
.
 
Me naomba kwanza nikupe pole kwa kuuguza na pia kwa yaliyotokea,labda niseme kwamba MNH imekuwa teaching hospital tangu enzi hizo,utaratibu unaotumika katika kuomba ridhaa ya mgonjwa ili aweze kutumika kufundishia wanafunzi ni VERBAL CONSENT na sio WRITTEN CONSENT ,Jambo lingine kipindi cha ward round relatives huwa wanatolewa nje na baada ya round kama kuna maelekezo yoyote hapo ndipo ndugu huitwa na kupewa hivyo naomba niwe mgumu kuamini kama ward round ilifanyika huku ndugu wakiwemo na pia haiwezekani Daktari akatoka tu from nowhere na kuanza kumtumia mgonjwa bila kuestablish rappot

Lakini mkuu, unapotumia verbal concent utathibitisha vipi kuwa mgonjwa alikubali itakapohitajika kufanya hivyo? Chukulia mfano Mtambuzi angeenda kushitaki, hospitali ingethibitisha vipi kuwa concent ilipatikana?

Kanuni za concent ni kwamba LAZIMA kuwepo na shahidi wakati concent inatolewa. Je, katika huo utaratibu nani huwa shahidi?

Halafu usiseme haiwezekani kama ulivyoandika hapo juu. Ingekuwa haiwezekani wasingekuwepo watu kama Mtambuzi na wengine wengi waliochangia kwenye thread hii wenye malalamiko.
 
waeleze baada, kwa Tz kwa sasa kila idara au professional ni janga la taifa
ETHICS! ETHICS! ETHICS! Hata
sie twaambiwa tu report with highest professionalism and Integrity ila
ndo kwanzaaa mpango wa Tax evasion, mambo ya dressing of FS na Ukwapuaji
wa kumzidi akili Auditor! We are who we are and we do what we
do!
 
Yaani wewe kuelezwa kuwa mgonjwa yuko katika Terminal care unakasirika kwa lip? je ulitaka udanganywe? Tembea UK ukirudi ndio uanze kulalamikia kitu usichokijua. Nenda dunia yeyote ile palipo na teaching hospital kama hutalikuta hilo ni jambo la kawaida kabisa.
Mama mkwe wangu alilazwa
Muhimbili kwa wiki moja, lakini jana nililazimika kumtoa kutokana na
kile nilichokishuhudia pale. Pamoja na vituko vingi tu tulivyoviona
kutoka kwa manesi wa ward ya Mwaisela, lakini nisingependa kuzungumzia
hayo kwa kuwa si mageni masikioni mwa wengi. Tulimpeleka mgonjwa wetu
kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kuwa na complication nyingi
nadhani ni kutokana na uzee (mkwe wangu ana miaka 70 hivi sasa)

Tulipofika pale alichukuliwa vipimo vyote ikiwapo x-ray, tatizo lilikuwa
ni pale madaktari wanapopita round kuona wagonjwa. kwanza walikuwa
wamemgeuza mama mkwe wangu kama vile ni darasa la kufundishia wanafunzi,
kila daktari alikuwa anafika na wanafunzi wake na kufungua darasa. Cha
kushangaza walikuwa wameyakalia majibu ya mgonjwa wetu huku wakiendelea
kumuweka pale kama mtu wa kufundishia wanafunzi.

Sikatai mgonjwa kutumika kufundishia wanafunzi, hawa ni ndio madaktari
wetu wa kesho wakajifunzie wapi. Lakini pale dakatari anapowaambia
wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika
TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa
mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha
wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye
terminal stage.

Kitu ambacho madaktari wale walikuwa hawakijui ni kwamba mke wangu
pamoja na dada yake ni wauguzi by professional na wanazijua hizo
terminology vizuri sana. Sasa iweje waropoke hivyo bila kuangalia
walioko karibu. kitendo hicho kilifanyika muda wa kuona wagonjwa na
nadhani ndio walikuwa wanamalizia round.
Tumelazimika kumchukua mgonjwa wetu kwa ajili ya kuangalia ustaaarabu
mwingine.
 
Pole. Nakubaliana na wewe kilichofanyika sio kitu kizuri. Kati ya system zilizo mbovu nchi hii ni hospitali na watz wengi ni wahanga wa matokeo. Kila mtu anafanya anavyojisikia. Wagonjwa wengi wanaondoka hospitalini bila kujua wanaugua nini.
 
Lakini mkuu, unapotumia verbal concent utathibitisha vipi kuwa mgonjwa alikubali itakapohitajika kufanya hivyo? Chukulia mfano Mtambuzi angeenda kushitaki, hospitali ingethibitisha vipi kuwa concent ilipatikana?

Kanuni za concent ni kwamba LAZIMA kuwepo na shahidi wakati concent inatolewa. Je, katika huo utaratibu nani huwa shahidi?

Halafu usiseme haiwezekani kama ulivyoandika hapo juu. Ingekuwa haiwezekani wasingekuwepo watu kama Mtambuzi na wengine wengi waliochangia kwenye thread hii wenye malalamiko.
Naomba niapologise kwa kusema haiwezekani,back to the topic labda niseme utaratibu unaotumika muhimbili ni verbal consent hata kama mgonjwa hawezi kuongea either awe mtoto,bubu,au kakata kauli na hawa wote ridhaa hutolewa na ndugu kama ni mzazi ama mlezi kama ni mtoto,na kama ni mtu mzima hutolewa na ndugu zake,kwa kuongezea mgonjwa aliye mahututi mara chache sana atatumiwa kwa ajili ya kufundishia labda iwe special case kwani kutakuwa ni kumsumbua na hakutakuwa na ushirikiano,pamoja na haya yote naomba nikupe like kwani written consent ni nzuri na inamlinda daktari vizuri hasa ndugu wakitaka kumgeuka daktari thanks.
 
Xidian nafikiri hujamuelewa Mtambuzi yeye anacholalamikia ni kwamba Dr. hajawahi hata siku moja kuwaambia kuhusu hali ya mgonjwa wao wamekuja kusikia tu kuwa ni wakufa wakati anawaeleza wanafunzi wake. Pia nafikiri kuhusu suala la kumtumia mgonjwa kama darasa ni lazima awaombe ndugu au mgonjwa mwenyewe.
 
Yaani wewe kuelezwa kuwa mgonjwa yuko katika Terminal care unakasirika kwa lip? je ulitaka udanganywe? Tembea UK ukirudi ndio uanze kulalamikia kitu usichokijua. Nenda dunia yeyote ile palipo na teaching hospital kama hutalikuta hilo ni jambo la kawaida kabisa.

Umeshasema Uingereza, na mimi ni Mmang'ati kutoka Dareda, sasa huoni tofauti hapo.......
Kumbuka kwamba, si lazima mgonjwa aliye katika hiyo Terminal Stage afe, wengi wanapona kabisa na kurudi katika ujenzi wa taifa, na hiyo inathibitisha kwamba Madaktari sio MIUNGU ni binadamu ambao hata wao watakufa siku moja........
 
Pole sana Mtambuzi na kadhia iliyokukuta na ya kuuguza pasipo na matumaini. Sala na subira hakika zitakupa faraja na mwelekeo. Sio kidato cha nne cha juzi pekee. Madudu yalianza kitambo, matunda ni kama ulivyoshuhudia. Pesa ndiyo mwanzo na mwisho kwao.
 
Nitasikitika sana kama uliamua kumchukua mgonjwa bila kumtaarifu dokta husika kwa uzembe huo walioufanya mbele ya ndugu wa mgonjwa na mgonjwa mwenyewe.
Nitakuona wa maana kama ulitoa dukuduku lako kwa dokta husika tena taratibu kwa upole ofisini kwa dokta husika ili kuepusha dhahama hii kwa waTZ wengine wala hupaswi kujiaminisha kuwa ushauri wako utapuuzi kwani pia utakuwa ume-play part yako.
Pole sana kwa yaliyomkuta mama mkwe.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Yaani wewe kuelezwa kuwa mgonjwa yuko katika Terminal care unakasirika kwa lip? je ulitaka udanganywe? Tembea UK ukirudi ndio uanze kulalamikia kitu usichokijua. Nenda dunia yeyote ile palipo na teaching hospital kama hutalikuta hilo ni jambo la kawaida kabisa.
Mkuu hapo utakuwa umedandia Fastjet tena kwenye tairi bila kujua tairi huwa linaingia ndani na kuweza kuhatarisha maisha yako. Sielewi Kama tatizo hapa ni kusoma au kumuelewa bwana Mtambuzi alikuwa anaongelea nini!?

Mtambuzi ametujuza yaliyomfika,ni kitu ambacho kinaweza kumtokea binadamu yoyote muda wowote. Nitamquote Bw. Mtambuzi ili iweze kukusaidia hapo mbeleni.
Mtambuzi aliandika "Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage".

Hakuna sehemu aliyoandika kulalamika au kukasirika kutokana na mgonjwa wao kuwa katika "TERMINAL CARE". Tatizo hapa lilikuwa ni kwa Ndugu wa mgonjwa kutojua au kupewa majibu kutoka kwa Madaktari.
Kutembea UK na kurudi sio tija siku hizi mkuu...wala hakumfanyi mtu awe mjuaji wa mambo.

Kwa taarifa yako katika hizo "Dunia" unazoongelea wewe Hilo Jambo lililotokea sio la kawaida. Kwa kuwa wenzetu wanajali sana na kuzingatia taarifa na hali ya mgonjwa. Isitoshe huko UK unakozungumzia hao jamaa wana kitu kinaitwa Code of conduct na accountability.

Sasa hapa sijui ni wewe uliyetembelea UK au Mtambuzi anayelalamika bila kujua!!???
 
Niliwahi kusema huko nyuma kuwa hapa tanzania hatuna madokta kuna wasoma biology wanagangia njaa mahospitalini. Na ndio maana viongozi wetu hawahangaiki na muhimbili wakiugua
 
pole sana ndugu wa mgonjwa, naomba tu upunguze jazba, hakuna m2 aliyezaliwa akijua kuongea wote wanajifunza na kufunzwa pia, katika hospitali kama muhimbili mgonjwa akishaingia wodini tayari ni kitabu kwa kuwa kuna madaktari wanofanya kazi kwa uangalizi wa wenzao na wapo wanaoongeza elimu na pasipo kutumia wagonjwa hatutaweza kutengeneza madaktari wengine.
kuna mida maalum yakuona wagonjwa na wakati madaktari wanakuwa na mgonjwa ni jambo la hekima kwa ndugu kutoa mwanya lakini kwa wa TZ wengi hawafuati utaratibu, hasa pale ndugu wa mgonjwa anapokuwa mtumishi wa afya au anavijisent na nafasi kidogo yakisiasa ndiyo wataomba vibali mpaka ikulu ili tu awe na mgonjwa wakati wote.

kuna magonjwa yanayoonekana kwa nadra na hivyo anapotokea mgonjwa mwenye tatizo kama hilo au mwenye dalili na alama kama kitabu hutumika sana kufundishia kwakuwa kusikia m2 husahau kwa asilimia nyingi, kuona huongeza kumbukumbu na kugusa huweka mihuri na uhakika katika jambo husika, fuatilia kisa cha tomaso.

matambue kuwa mgonjwa wa mgonjwa wapaswa kuwa siri kati yake na daktari/madaktari wake hivyo nawe ulipokuwa unataka majibu ya mgonjwa ulimuomba mgonjwa ruksa ya wewe kupokea majibu yake?

kama kawaida katika kila sekta huwezi kuwa na watu waaminifu katika mambo sensitive kama siri za wagonjwa hivyo kwa wale wanaotoa taarifa za wagonjwa wao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kupitia katika masanduku ya maoni na kamati za afya za vijiji, kata........

jambo la msingi ni kushirikiana na kuheshimiana,
 
Mtambuzi pole sana, wanaacha kumkomoa Kikwete na CCM yake, wanatukomoa sisi ambao hatuna uwezo hata wa kulipia hospitali kama ya Aga Khan.
Waganga wa kienyeji nao feki ile mbaya,
waombeaji nao wamekuwa magumashi ile mbaya.
Sijui tukimbilie wapi ili tupone.
Na wakati huohuo kila tunachokula na tunywacho tunaambiwa eti ni sumu.
Duhh

Halo jamani mnachosema ni sahìhi ila kwa habari ya hicho ieleweke kuwa madaktari huwa wanajifunza kwa vitabu na kwa vitendo pia. Unajua ikiwa mgonjwa mmoja kwenye vipimo ana findings ambazo zimeonekana, hivyo ni muhimu awashirikishe wanafunzi maana ndo maspecialists wa kesho. Hivyo ukimkatalia leo asijifunzie mgonjwa wako, jua kesho itatokea wewe au jamaa yako au mtu mwingine kaugua ugonjwa huohuo na wa kumhudumia ni huyo daktari ambae leo ni mwanafunzi. Mpaka huyo daktari kuwakusanya wanafunzi wa udaktari alikuwa sahihi kabisa ili wawe exposed kwa ajili ya msaada wa kesho. Hebu tufikirie kabisa kwa upande mwingine ile ni teaching hospital ingekuwa labda anasema hivyo kwa watu ambao wake nje ya profession hilo ni kosa na si maadili ila kuwafundisha wengine hiyo ni hazina ya kesho ni lazima kuwekeza for future.
 
Last edited by a moderator:
Kwakweli alichofanya ni unethical na unprofessional kabisa! Daktari ana kiapo kilichoelekeza yote yampasayo kuyatenda na huwa anakiapa siku ya ku graduate ili akafanye kazi yake kulingana na kiapo hicho, bahati mbaya nimekiacha nyumbani ningeki scan niki attach hapa ili kuonesha jinsi huyu ndugu alitakiwa kufukuzwa hata kwenye taaluma kwa kukiuka kazi na miiko ya taaluma.
Pole sana mkuu Mungu atamuafu mama mkwe.
 
Back
Top Bottom