ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,685
Pole mkuu kwa yote,lakini watanzinia inatupasa kutambua kwamba unapoingia teaching hospital umeshasign conset ya kuwa teaching model,hakuna conset zaidi ya ile kuwa teaching hospital.Kama hautaka mgonjwa wako afundishiwe wanafunzi please mpeleke hospitali isiyokuwa teaching hospital,tena ukikataa mgonjwa wako kufundishiwa inapaswa ufukuzwe kwenye teaching hospital.
Kwa muhimbili kama hutaki mgonjwa afundishiwe mpeleke first grade uone kama kuna mwanafunzi hatakuja huko kumgusa mgonjwa wako,hata intern doctor akija unamfukuza.
Hili la madaktari kufanya teaching round wakati relative wapo ndani ni uzushi wa mleta mada,hakuna daktari anayekubali kufanya round wakati relative wapo ndani,utapata usumbufu usio na mfano wake,utazingukwa na relative wewe mpaka ukome.
Ninachokiona mimi labda kwa kuwa mke wa mleta mada ni nesi pengine aliingia ndani kwa huo unesi wake baati mbaya akakuta watu wanpigwa shule,kulikuwa hakuna jinsi ispokuwa daktari kuwaonesha wanfunzi wake the real symptoms and signs za terminal stages,sasa nyinyi mulitaka wakazione wapi kwenye lecture room?
Kuhusiana na majibu,inawezekana utafiti ulikuwa bado unaendelea au kwa vile mgonjwa yupo kwenye terminal stage baada ya round doctor angemuambia nesi ili awashauri ndugu wa mgonjwa,mara nyingi manesi ndio wanaoongea na ndugu za wagonjwa isipokuwa pale nesi hasipoeleweka na ndugu wa mgonjwa ndio daktari uzungumza na ndugu wa mgonjwa.
Pamoja na maelezo yangu yote nakubaliana na wadau wengine ya kwamba system yetu ya afya inamatatizo,madaktari wamezidiwa na wagonjwa wengi mpaka wote wanakuwa na kisirani na hasira za karibu,plus maisha magumu kulinganisha na kazi wanayoifanya,so ukimvaa daktari kichwa kichwa na yeye atakutoa nduka kwa maneno makali,ni stress za kazi,we acha tunajuta kusomea hizi kazi hapa tz.
Chapisho lako linaonyesha wewe ni mdau wa sekta ya afya na kwamba unaifahamu vizui Muhimbili. Sasa nikuulize maswali mawili?
1. Hiyo mamlaka ya kuamua kuwa mgonjwa akilazwa Muhimbili ni lazima atumike kufundishia imepatikana vipi? Na iwaje wagonjwa wa gade 1 wasihusishwe? Kwahiyo masikini wasioweza kukaa grade 1 ndio wanalazimishwa kutumika bila kupewa fusa ya kuamua!!! Wakati unajibu hili, labda nikujulishe tu kuwa tafiti zinaonyesha kuwa hata mgonjwa akipewa fusa ya kuopt out majority ya wagonjwa watakubali kutumika kufundishia madaktari and that I fundamentally beleive it is wrong to deny a patient the right to opt out from medics lessons.
2.Huu utaratibu kuwa nesi ndio anayempa mgonjwa majibu ndio unaotumika Muhimbili au umeubuni tu? Kama ni utaratibu rasmi wa Muhimbili my friends we have a very very long way to go. Interpretation ya majibu ya mgonjwa ni very sensitive matter na jinsi majibu yanavyotolewa inachangia kumpa mgonjwa matumaini au kumkatisha tamaa. Muhimbili kuna interns, registrars, postgrads, specialists, consultants yaani hawa wote akosekane daktari wa kumpa mgonjwa majibu mpaka atumwe nesi. Hii si sahihi hata kidogo. Na katika hili tatizo sio system ya afya, hapo itakuwa ni kutafuta kisingizio tu...