Madaktari wa Muhimbili: This is unprofessional....!

Soma hii

Sasa kama wagonjwa katika teaching hospital watapewa huru wa kukataa au kukubali kufundishiwa, mwisho wa siku wagonjwa wote watakataa kufundishiwa na hao wanfunzi watafundishiwa wapi.

Then linganisha na hii

By the way teaching round mgonjwa anafaidika sana kuliko munavyofikiria, maana mgonjwa anajadiliwa kwa undania zaidi kuliko vile anavyopita daktari mmoja

Kama unajichanganya hivi, nahisi kama wewe ni daktari basi utakuwa unachanganya mpaka dozi za wagonjwa.

Unahoji "mwisho wa siku wagonjwa wote watakataa kufundishiwa na hao wanfunzi watafundishiwa wapi" lakini wakati huo una unasema "By the way teaching round mgonjwa anafaidika sana kuliko munavyofikiria,maana mgonjwa anajadiliwa kwa undania zaidi kuliko vile anavyopita daktari mmoja"?

Kama kuna hizo faida kwa nini then mgonjwa akatae kutumiwa katika kufundishia?

Ukiwa kama daktari kwa nini unashindwa hata kuwa-convince hao wagonjwa kuwa huwa kuna faida zake kama wakitumiwa katika kufundishia ili wakupe consent ya kutumika katika kufundishia?
 
Actually hata hiyo article ya Damascus niliyoiweka hapo juu inaonyesha kuwa waginjwa wako willing kutumika kufundishia as long as wamejulishwa manufaa yake.

Kama mawazo ya daktari huyu yanakuwa shared na madaktari wengi nchini basi tuna safari ndefu mno katika kuboresha sekta ya afya!!!

wewe kilaza ile ni reseach tu,ebu nenda huko damascus teaching hospital ukaone,unatoa mapovu tu
 
Tatizo mida hii madaktari kama nyinyi unaweza kukuta hauko sober!!! Sasa kama unaweza kukaa kwenye keyboard na kukataa chapisho la kisayansi bila kutoa alternative evidence, kitu gani kinachoweza kukupa utashi wa namna hiyo zaidi ya VIROBA?
 
Mama mkwe wangu alilazwa Muhimbili kwa wiki moja, lakini jana nililazimika kumtoa kutokana na kile nilichokishuhudia pale. Pamoja na vituko vingi tu tulivyoviona kutoka kwa manesi wa ward ya Mwaisela, lakini nisingependa kuzungumzia hayo kwa kuwa si mageni masikioni mwa wengi. Tulimpeleka mgonjwa wetu kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kuwa na complication nyingi nadhani ni kutokana na uzee (mkwe wangu ana miaka 70 hivi sasa)

Tulipofika pale alichukuliwa vipimo vyote ikiwapo x-ray, tatizo lilikuwa ni pale madaktari wanapopita round kuona wagonjwa. kwanza walikuwa wamemgeuza mama mkwe wangu kama vile ni darasa la kufundishia wanafunzi, kila daktari alikuwa anafika na wanafunzi wake na kufungua darasa. Cha kushangaza walikuwa wameyakalia majibu ya mgonjwa wetu huku wakiendelea kumuweka pale kama mtu wa kufundishia wanafunzi.

Sikatai mgonjwa kutumika kufundishia wanafunzi, hawa ni ndio madaktari wetu wa kesho wakajifunzie wapi. Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage.

Kitu ambacho madaktari wale walikuwa hawakijui ni kwamba mke wangu pamoja na dada yake ni wauguzi by professional na wanazijua hizo terminology vizuri sana. Sasa iweje waropoke hivyo bila kuangalia walioko karibu. kitendo hicho kilifanyika muda wa kuona wagonjwa na nadhani ndio walikuwa wanamalizia round.
Tumelazimika kumchukua mgonjwa wetu kwa ajili ya kuangalia ustaaarabu mwingine.

sasa kama ndugu zako ni manesi walikuwa wanajua hata status ya mgonjwa kwa nini walimpeleka coz i was expecting hawa ndo watusaidie counseling, na hakuna mgonjwa atakayefundishiwa bila ridhaa yake, pia kama ni wakati wa round hao ndugu zako walikuwa wanatafuta nini coz kwa Muhimbili hata muuguzaji haruhusiwi kulala wodin hata kama mgonjwa amezidiwa namna gani, pia wakati wa ward round hii ni routine lazima ipitwe na huku changanyikeni wanapita madaktari wengi hivyo lazima wajadiliane na hapa kwenye ward round hakuna consent hapa coz daily routine. Lakini kama Dr atakuja kufundisha apart from round time lazima aombe consent. Jua taratibu za hospital na pia kama uliona ndugu yako hajafanyiwa fair ungeenda pale kwenye dirisha la malalamiko ili utoe dukuduku yako na uelezwe utaratibu coz kulalamika hapa hakukusaidii hata kidogo zaidi unaoneka si mstaarabu, much know which u do not know.
 
Soma hii

Then linganisha na hii

Kama unajichanganya hivi, nahisi kama wewe ni daktari basi utakuwa unachanganya mpaka dozi za wagonjwa.

Unahoji "mwisho wa siku wagonjwa wote watakataa kufundishiwa na hao wanfunzi watafundishiwa wapi" lakini wakati huo una unasema "By the way teaching round mgonjwa anafaidika sana kuliko munavyofikiria,maana mgonjwa anajadiliwa kwa undania zaidi kuliko vile anavyopita daktari mmoja"?

Kama kuna hizo faida kwa nini then mgonjwa akatae kutumiwa katika kufundishia?

Ukiwa kama daktari kwa nini unashindwa hata kuwa-convince hao wagonjwa kuwa huwa kuna faida zake kama wakitumiwa katika kufundishia ili wakupe consent ya kutumika katika kufundishia?

wakati wa teaching round waginjwa wanatibiwa na maconsultant na maspecialists,na wanafunzi yaani medical studenta,interns na resedents wanafundishwa,mgonjwa akikaa mule wodini unajua faida ya teaching round,tatizo relative ndio wanalalamika kama huyu mleta mada.

Tatizo ni moja tu,kama watataka kumfanyia physical examination wanafunzi wengi watamshika mgonjwa so inakuwa usumbufu kwa mgonjwa,lakini kunakuwa na explanation kwa mgonjwa ili ajue nini anafanyiwa.

Cha kuzingitia ukiingia teaching hospital mambo haya lazima ukumbane nayo,kama hutaki nenda hospital nyingine kwani lazima kwenda teaching hospital!!!!!!!!!!!!
 
Hujui unachokisema, labda ungeudhuria teaching round(major ward round) moja baada ya hapo ungejua hiki unachokisema hakiwezekani,

Sikuwa na haja ya kuhudhuria "teaching round" kwa sababu mimi mwenyewe ndiye niliyekuwa mgonjwa.

Kwa hiyo, I was directly involved in the "teaching round" maana kama siyo mimi wala hiyo "teaching round" isingefanyika.

Pia kama ningekataa kutoa consent, hiyo "teaching round" isingefanyika na wala daktari asingekataa kunitibu. That is the fact.

kama unataka wanafunzi wafanye physical examination you have to ask verbal concert,na kama ni invasive procedure you have to ask written concert hata ukiwa dakatri bingwa,na mgonjwa akikataa sasa anakaa hospitali anafanya nini bora aende nyumbani kwake tu(discharge from hospital)

Patients are usually very happy to take part in teaching sessions but it is wise to obtain permission EXPLICITLY and RECORD that you have done so. Kuna ubaya au ugumu gani kufanya hivyo kwenye teaching rounds?

Tusitimie matatizo yaliyopo kwenye sekta ya afya ku-justify bad practice.
 
Cha kuzingitia ukiingia teaching hospital mambo haya lazima ukumbane nayo,kama hutaki nenda hospital nyingine kwani lazima kwenda teaching hospital!!!!!!!!!!!!

Tatizo unajaribu ku-generalise mambo. Kwa vile Muhimbili wanafanya hivyo, basi unadhani university hosipitals zote duniani wanafanya hivyo pia.

Pia kama vile unadhani kwenye university hosipitals zote duniani wagonjwa wanalundikwa kwenye wodi kama ilivyo Kibasila na Mwaisela.

Inawezekana kabisa kuwa kutokana na matatizo kwenye sekta yetu ya afya ndiyo maana inakuwa ngumu kupata ridhaa ya wagonjwa wakati daktari anapofanya training rounds kwenye wodi kama Kibasila.

Personally, naona ni vigumu daktari iliyeko kwenye training round kuingia kwenye wodi iliyofurika wagonjwa mpaka wengine wamelala kwenye sakafu na kuanza kutafuta ridhaa ya kila mgonjwa.

Hapo inaweza kuwa ngumu na sidhani kama kutakuwa na confidentiality kwa sababu hata wagonjwa wengine watasikia kila kitu ambacho daktari anamweleza mwanafunzi. Hapo kwa kweli lazima nim-feel daktari.

Lakini bado siamini wakati unasomea udaktari, ulifundishwa kuwa kama unafanya training rounds kwenye university hospitals basi hakuna haja ya ku-seek consent kutoka kwa mgonjwa.

Kama ulifundishwa kuna hiyo exception, basi itakuwa ilitokana na mazingira ya hosipitali zetu and such exception is not universally applicable.

Ndiyo maana nimekwambia mwanzo kuwa mimi mwenyewe nimeshatibiwa kwenye hizo university hospitals na mara zote including training sessions aka training rounds, nilikuwa naombwa consent kabla ya session kuanza.

Nafikiri suala la kuomba consent ni good practice kwa sababu kama mgonjwa amezoea kutembelewa na daktari mmoja halafu ghafla anatembelewa na lundo la "madaktari" anaweza kudhani kiama kimefika.
 
Kwa kweli hali inatisha na kusikitisha sana kutokana na kauli za hawa Madaktari na jinsi wanavyochangia hii mada humu kwenye Jamvi. Lakini hii ndio hali halisi baadhi yetu tunayojaribu kuijadili hapa jamvini.
Hakuna kitu kizuri na cha busara Kama kujadili Jambo kwa kutumia akili na fikra sahihi kuliko kutumia jazba na utemi kana kwamba wewe ni Mbingu na ardhi. Huku ukisahau kuna siku na wewe utatengenezewa Jeneza na kuchimbiwa kaburi.

Ukweli ni kwamba baadhi ya Madaktari hapa Tanzania wameenda shule ya utabibu either kwa msukumo wa familia au kwa kutaka kuwa Mungu mtu chini ya Mbingu. Bila kuelewa kwamba udaktari ni wito. Na hili linajidhihirisha kutokana na comments hawa baadhi ya Madaktari walizoandika humu. Daktari anapotumia lugha na kusema "Mgonjwa ukija ukaniletea zenye na mimi nakuzingua" huyu sijui nimuweke kwenye kundi gani???? Maana hata ndugu zetu wabaeba zege huwa wana adabu wakiwa kazini kwao na kuheshimu Karai,Cement na kokoto kwa sababu wanategemea ushirikiano wa vitendea kazi ili mkono uende kinywani.

Ni hatari sana Daktari unapodharau watu wa fani nyingine na kusahau kuwa Wewe pia unahitaji huduma za msingi za kibinadamu,kwa mfano kujengewa nyumba,kutengenezewa jeneza,kuchimbiwa kaburi na huduma nyingine nyingi ambazo naweza kujaza thread hapa.
Inashangaza na kusikitisha ya kwamba kuna Madaktari wachache Kama hawa tunaowaona humu wako tayari kusema na kuandika lolote ili mradi wao wanajua kila kitu na wako sawa na upotofu wao wa maadili na utovu wa Nidhamu.
Udaktari ni fani tu Kama fani nyingine. Na katika maisha ya binadamu ya kila siku hapa chini ya jua kila fani inategemea fani nyingine ili kusukuma gurudumu la Maendeleo.

Kutokana na statement za hawa Madaktari waliokuja kutoa utetezi wa shurti na kejeli humu jamvini,inanifanya na kunipa mwanga wa kuelewa kwa nini Serikali yetu Tukufu huwa inadeal na Madaktari kwa aina yake. Na sababu kubwa ni baadhi ya Madaktari Kama hawa tunaowaona hapa. Inatakiwa pia mtambue ya kwamba MISHAHARA YENU INATOKANA NA KODI ZETU SISI WATANZANIA. Hilo tu linatosha kuwakumbusha wajibu wenu kwetu WATANZANIA.

PS: Kwa nyinyi Madaktari uchwara mliokuja na kejeli na dharau kutoa majibu ya kipu.uzi nataka mfahamu ya kwamba hapa
JF kuna watu wa fani heshimika tofauti. Kwa hiyo mnapoamua kuja kuwadhalilisha MADAKTARI wenzenu mjipange
Na kutambua kila utakaloliandika linaakisi wewe ni mtu wa aina gani na uerevu wako ukoje.
 
Principles of Medical Ethics

Preamble

The medical profession has long subscribed to a body of ethical statements developed primarily for the benefit of the patient. As a member of this profession, a physician must recognize responsibility to patients first and foremost, as well as to society, to other health professionals, and to self. The following Principles adopted by the American Medical Association are not laws, but standards of conduct which define the essentials of honorable behavior for the physician.
Principles of medical ethics

I. A physician shall be dedicated to providing competent medical care, with compassion and respect for human dignity and rights.

II. A physician shall uphold the standards of professionalism, be honest in all professional interactions, and strive to report physicians deficient in character or competence, or engaging in fraud or deception, to appropriate entities.

III. A physician shall respect the law and also recognize a responsibility to seek changes in those requirements which are contrary to the best interests of the patient.

IV. A physician shall respect the rights of patients, colleagues, and other health professionals, and shall safeguard patient confidences and privacy within the constraints of the law.

V. A physician shall continue to study, apply, and advance scientific knowledge, maintain a commitment to medical education, make relevant information available to patients, colleagues, and the public, obtain consultation, and use the talents of other health professionals when indicated.

VI. A physician shall, in the provision of appropriate patient care, except in emergencies, be free to choose whom to serve, with whom to associate, and the environment in which to provide medical care.

VII. A physician shall recognize a responsibility to participate in activities contributing to the improvement of the community and the betterment of public health.

VIII. A physician shall, while caring for a patient, regard responsibility to the patient as paramount.

IX. A physician shall support access to medical care for all people.

Source of Info : American Medical Association (AMA).

Hizo ni Principles of Medical ethics. Sasa Daktari anapokuja humu na kuleta dharau na kejeli kwa statement za kilevi Kama "Huo ndio utaratibu Dunia nzima,Kama hautaki mgonjwa unafukuzwa" , kwanza sijui yeye anazungumzia Dunia gani!? Na pili inapoteza heshima kwa Madaktari wengine kwa kuna wanywa Valeur Kama hawa tunawaamini na maisha yetu na ya familia zetu.
 
Google inakupa kiburi ambacho hakitakusaidia kitu chochote. Kwa mtu makini hawezi kufanya mlinganyo baina ya Tanzania na America kwa hali yeyote ile.

Huyu daktari anayeongea hapa anaongea huku akielewa fika mazingira ya pale Muhimbili na ndiyo maana imefikia wakati hata mambo ya kihuni yanayofanyika pale yeye anajua yanafanyika dunia nzima. Yeye anaongea huku akiRefer to MNH wewe huku kichwani mwako akili zako zipo kwenye hizo principles of medical ethics za AMA.

Tatizo umezoea kudanganywa ila ukweli ni kwamba ukilazwa kwenye wards za changanyikeni halafu ukajifanya mjuaji utakufa/utafiwa huku unaangalia kwa macho yako.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
watu wanaoongea tu kwakuwa hawajauguliwa kwa mimi mgonjwa wangu atumike darasa au mimi mwenyewe nitumike darasa sijali chochote zaidi ya kupona. Hivi kuna mtu alishawahi kuishi China akahudhuria hospitali za wachina? especially opd? then kama yupo atupe experience ya aliyoyaona then hii thread ifungwe. sijaona kosa lolote hapa lilofanyika sana as far as ndugu yako alikuwa anapatiwa matibabu
 
Kwa kweli hali inatisha na kusikitisha sana kutokana na kauli za hawa Madaktari na jinsi wanavyochangia hii mada humu kwenye Jamvi. Lakini hii ndio hali halisi baadhi yetu tunayojaribu kuijadili hapa jamvini.
Hakuna kitu kizuri na cha busara Kama kujadili Jambo kwa kutumia akili na fikra sahihi kuliko kutumia jazba na utemi kana kwamba wewe ni Mbingu na ardhi. Huku ukisahau kuna siku na wewe utatengenezewa Jeneza na kuchimbiwa kaburi.

Ukweli ni kwamba baadhi ya Madaktari hapa Tanzania wameenda shule ya utabibu either kwa msukumo wa familia au kwa kutaka kuwa Mungu mtu chini ya Mbingu. Bila kuelewa kwamba udaktari ni wito. Na hili linajidhihirisha kutokana na comments hawa baadhi ya Madaktari walizoandika humu. Daktari anapotumia lugha na kusema "Mgonjwa ukija ukaniletea zenye na mimi nakuzingua" huyu sijui nimuweke kwenye kundi gani???? Maana hata ndugu zetu wabaeba zege huwa wana adabu wakiwa kazini kwao na kuheshimu Karai,Cement na kokoto kwa sababu wanategemea ushirikiano wa vitendea kazi ili mkono uende kinywani.

Ni hatari sana Daktari unapodharau watu wa fani nyingine na kusahau kuwa Wewe pia unahitaji huduma za msingi za kibinadamu,kwa mfano kujengewa nyumba,kutengenezewa jeneza,kuchimbiwa kaburi na huduma nyingine nyingi ambazo naweza kujaza thread hapa.
Inashangaza na kusikitisha ya kwamba kuna Madaktari wachache Kama hawa tunaowaona humu wako tayari kusema na kuandika lolote ili mradi wao wanajua kila kitu na wako sawa na upotofu wao wa maadili na utovu wa Nidhamu.
Udaktari ni fani tu Kama fani nyingine. Na katika maisha ya binadamu ya kila siku hapa chini ya jua kila fani inategemea fani nyingine ili kusukuma gurudumu la Maendeleo.

Kutokana na statement za hawa Madaktari waliokuja kutoa utetezi wa shurti na kejeli humu jamvini,inanifanya na kunipa mwanga wa kuelewa kwa nini Serikali yetu Tukufu huwa inadeal na Madaktari kwa aina yake. Na sababu kubwa ni baadhi ya Madaktari Kama hawa tunaowaona hapa. Inatakiwa pia mtambue ya kwamba MISHAHARA YENU INATOKANA NA KODI ZETU SISI WATANZANIA. Hilo tu linatosha kuwakumbusha wajibu wenu kwetu WATANZANIA.

PS: Kwa nyinyi Madaktari uchwara mliokuja na kejeli na dharau kutoa majibu ya kipu.uzi nataka mfahamu ya kwamba hapa
JF kuna watu wa fani heshimika tofauti. Kwa hiyo mnapoamua kuja kuwadhalilisha MADAKTARI wenzenu mjipange
Na kutambua kila utakaloliandika linaakisi wewe ni mtu wa aina gani na uerevu wako ukoje.

yaani mie nilikuwa napitia huu uzi halafu nasikitika tu....hawa ndo madaktari?????? Wasomi? Waliotumia miaka kadhaa shule? Inasikitisha sana......

kwa sababu tu umelazwa changanyikeni basi madaktari ni Miungu watu hata kukueleza wanachotaka kufanya si lazima? Kweli umasikini ni shida sana........

Google inakupa kiburi ambacho hakitakusaidia kitu chochote. Kwa mtu makini hawezi kufanya mlinganyo baina ya Tanzania na America kwa hali yeyote ile.

Huyu daktari anayeongea hapa anaongea huku akielewa fika mazingira ya pale Muhimbili na ndiyo maana imefikia wakati hata mambo ya kihuni yanayofanyika pale yeye anajua yanafanyika dunia nzima. Yeye anaongea huku akiRefer to MNH wewe huku kichwani mwako akili zako zipo kwenye hizo principles of medical ethics za AMA.

Tatizo umezoea kudanganywa ila ukweli ni kwamba ukilazwa kwenye wards za changanyikeni halafu ukajifanya mjuaji utakufa/utafiwa huku unaangalia kwa macho yako.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

mkuu kwa hiyo ni sahihi kufa ukiwa umelazwa changanyikeni? Napata picha.....kuna mgonjwa aliletwa alikuwa amepata ajali kipindi nauguza pale tmk siku ya pili yake nikakuta kafariki baada ya kuuliza wagonjwa wakasema hakuna daktari aliyemgusa yule mgonjwa mpaka amefariki........ sasa naanza kuelewa ...............
 
Google inakupa kiburi ambacho hakitakusaidia kitu chochote. Kwa mtu makini hawezi kufanya mlinganyo baina ya Tanzania na America kwa hali yeyote ile.

Huyu daktari anayeongea hapa anaongea huku akielewa fika mazingira ya pale Muhimbili na ndiyo maana imefikia wakati hata mambo ya kihuni yanayofanyika pale yeye anajua yanafanyika dunia nzima. Yeye anaongea huku akiRefer to MNH wewe huku kichwani mwako akili zako zipo kwenye hizo principles of medical ethics za AMA.

Tatizo umezoea kudanganywa ila ukweli ni kwamba ukilazwa kwenye wards za changanyikeni halafu ukajifanya mjuaji utakufa/utafiwa huku unaangalia kwa macho yako.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Acha kufikiria kwa kutumia nanilii wewe. Google ni sehemu ambayo inasaidia kuwaweka sawa vilaza Kama nyinyi na Huyo anayejiita Daktari uchwara.
Nimemjibu kwa kuweka reference ya AMA kutokana na maneno yake alivyoandika mwenyewe kwenye Ukurasa wa 5 ( thread no.82)...nanukuu "Teaching hospital worldwide inajulika ukilazwa upo uje utatumika kufundishia,na kam hutaki basi muhamishe mgonjwa wako katika hospitali isiyokuwa teaching hospital". Tatizo lako wewe ni kati ya wale watu ambaye unamfukunyuko wa tabia na huna akili timamu ya kuelewa Bwana Mtambuzi alimaanisha nini alipoanzisha huu Uzi.

Ni hatari kuwa na watu Kama wewe kwenye jamii ya Watanzania ambaye unaamini mtu ukihoji njia zinazotumika kupata huduma ya matibabu eti unaweza kufa huku unaangalia macho!?
Tatizo la MTANZANIA kama wewe na Mwenye akili(Akili mtindi) na upeo wako ukimkosoa na kujaribu kumuelimisha anafikiri unamdhalilisha na kumshambulia. Acha kutoa au kuchangia maoni kwa hisia(Feelings) jitahidi Uwe unatumia hekima na Akili ulipendelewa na Mungu. Kama uwezo wako ni mdogo kwenye suala husika Kama hili hauna haja ya kuleta maneno yako ya kejeli hapa.

Kama wewe unajua nimezoea kudanganywa Hongera. Lakini kwenye hili suala la AFYA linalonihusu mimi,familia yangu na Watanzania wenzangu siwezi kudanganywa. Na tutawanyoosha tu Madaktari jeuri na watu wenye tabia Kama zako...mark my words. Maana mmezoea kufanya kazi na kuishi kwa mazoea. Change is coming, huwezi kupata matokeo tofauti kwa kufanya kitu kile kile muda wote. Shika Jembe rudi kijijini ukalime.
 
yaani mie nilikuwa napitia huu uzi halafu nasikitika tu....hawa ndo madaktari?????? Wasomi? Waliotumia miaka kadhaa shule? Inasikitisha sana......

kwa sababu tu umelazwa changanyikeni basi madaktari ni Miungu watu hata kukueleza wanachotaka kufanya si lazima? Kweli umasikini ni shida sana........

Kwa kweli inasikitisha na kushangaza. Hao ndio Madaktari tunaowaamini na kuweka maisha yetu na familia zetu mikononi kwao!!! Halafu cha kushangaza hizo Hospitali wanazoletea kiburi na ujeuri zinaendeshwa na hela ya Walipa Kodi. Ni Kama wanatufanyia favor kutenda wajibu wao. Wakati wamesoma kwa Kodi zetu na bado tunawalipa mishahara na Kodi zetu.
 
Acha kufikiria kwa kutumia nanilii wewe. Google ni sehemu ambayo inasaidia kuwaweka sawa vilaza Kama nyinyi na Huyo anayejiita Daktari uchwara.
Nimemjibu kwa kuweka reference ya AMA kutokana na maneno yake alivyoandika mwenyewe kwenye Ukurasa wa 5 ( thread no.82)...nanukuu "Teaching hospital worldwide inajulika ukilazwa upo uje utatumika kufundishia,na kam hutaki basi muhamishe mgonjwa wako katika hospitali isiyokuwa teaching hospital". Tatizo lako wewe ni kati ya wale watu ambaye unamfukunyuko wa tabia na huna akili timamu ya kuelewa Bwana Mtambuzi alimaanisha nini alipoanzisha huu Uzi.

Ni hatari kuwa na watu Kama wewe kwenye jamii ya Watanzania ambaye unaamini mtu ukihoji njia zinazotumika kupata huduma ya matibabu eti unaweza kufa huku unaangalia macho!?
Tatizo la MTANZANIA kama wewe na Mwenye akili(Akili mtindi) na upeo wako ukimkosoa na kujaribu kumuelimisha anafikiri unamdhalilisha na kumshambulia. Acha kutoa au kuchangia maoni kwa hisia(Feelings) jitahidi Uwe unatumia hekima na Akili ulipendelewa na Mungu. Kama uwezo wako ni mdogo kwenye suala husika Kama hili hauna haja ya kuleta maneno yako ya kejeli hapa.

Kama wewe unajua nimezoea kudanganywa Hongera. Lakini kwenye hili suala la AFYA linalonihusu mimi,familia yangu na Watanzania wenzangu siwezi kudanganywa. Na tutawanyoosha tu Madaktari jeuri na watu wenye tabia Kama zako...mark my words. Maana mmezoea kufanya kazi na kuishi kwa mazoea. Change is coming, huwezi kupata matokeo tofauti kwa kufanya kitu kile kile muda wote. Shika Jembe rudi kijijini ukalime.

Mleta mada anazungumzia mambo yanayotokea kwenye dunia ya tatu wewe unakimbilia kuGoogle unatuletea mambo ya kwenye dunia ya kwanza.

Akili zako zipo sawa kweli wewe?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mama mkwe wangu alilazwa Muhimbili kwa wiki moja, lakini jana nililazimika kumtoa kutokana na kile nilichokishuhudia pale. Pamoja na vituko vingi tu tulivyoviona kutoka kwa manesi wa ward ya Mwaisela, lakini nisingependa kuzungumzia hayo kwa kuwa si mageni masikioni mwa wengi. Tulimpeleka mgonjwa wetu kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kuwa na complication nyingi nadhani ni kutokana na uzee (mkwe wangu ana miaka 70 hivi sasa)

Tulipofika pale alichukuliwa vipimo vyote ikiwapo x-ray, tatizo lilikuwa ni pale madaktari wanapopita round kuona wagonjwa. kwanza walikuwa wamemgeuza mama mkwe wangu kama vile ni darasa la kufundishia wanafunzi, kila daktari alikuwa anafika na wanafunzi wake na kufungua darasa. Cha kushangaza walikuwa wameyakalia majibu ya mgonjwa wetu huku wakiendelea kumuweka pale kama mtu wa kufundishia wanafunzi.

Sikatai mgonjwa kutumika kufundishia wanafunzi, hawa ni ndio madaktari wetu wa kesho wakajifunzie wapi. Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage.

Kitu ambacho madaktari wale walikuwa hawakijui ni kwamba mke wangu pamoja na dada yake ni wauguzi by professional na wanazijua hizo terminology vizuri sana. Sasa iweje waropoke hivyo bila kuangalia walioko karibu. kitendo hicho kilifanyika muda wa kuona wagonjwa na nadhani ndio walikuwa wanamalizia round.
Tumelazimika kumchukua mgonjwa wetu kwa ajili ya kuangalia ustaaarabu mwingine.
Mtambuzi nani amhukumu mwenzake kwa suala la ethics Tanzania? Kokote utakakoangukia hakuna ethics. Iwe hospitalini, polisi, TRA, magazeti, ofisini kwako, yaani popote. Tutoe boriti kwenye jicho la kila mmoja kwanza kabla hajuwaangalia wenzetu.
 
Mama mkwe wangu alilazwa Muhimbili kwa wiki moja, lakini jana nililazimika kumtoa kutokana na kile nilichokishuhudia pale. Pamoja na vituko vingi tu tulivyoviona kutoka kwa manesi wa ward ya Mwaisela, lakini nisingependa kuzungumzia hayo kwa kuwa si mageni masikioni mwa wengi. Tulimpeleka mgonjwa wetu kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na kuwa na complication nyingi nadhani ni kutokana na uzee (mkwe wangu ana miaka 70 hivi sasa)

Tulipofika pale alichukuliwa vipimo vyote ikiwapo x-ray, tatizo lilikuwa ni pale madaktari wanapopita round kuona wagonjwa. kwanza walikuwa wamemgeuza mama mkwe wangu kama vile ni darasa la kufundishia wanafunzi, kila daktari alikuwa anafika na wanafunzi wake na kufungua darasa. Cha kushangaza walikuwa wameyakalia majibu ya mgonjwa wetu huku wakiendelea kumuweka pale kama mtu wa kufundishia wanafunzi.

Sikatai mgonjwa kutumika kufundishia wanafunzi, hawa ni ndio madaktari wetu wa kesho wakajifunzie wapi. Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage.

Kitu ambacho madaktari wale walikuwa hawakijui ni kwamba mke wangu pamoja na dada yake ni wauguzi by professional na wanazijua hizo terminology vizuri sana. Sasa iweje waropoke hivyo bila kuangalia walioko karibu. kitendo hicho kilifanyika muda wa kuona wagonjwa na nadhani ndio walikuwa wanamalizia round.
Tumelazimika kumchukua mgonjwa wetu kwa ajili ya kuangalia ustaaarabu mwingine.

Pole sana kaka Mtambuzi...sikatai hali ya kimaadili pale Muhimbili na hospitali nyingi za umma si nzuri. Na pia 'teaching hospitals' nyingi zimekuwa zikilaumiwa kwa jinsi wanavyotreat wagonjwa wakati wakifundisha. Zamani ilikuwa mpaka mgonjwa atoe ridhaa, ikaonekana wagonjwa wengi wanakataa...baadae ikawa kila mgonjwa anayelazwa kwenye teaching hospital, automatically unakuwa umetoa ridhaa ya kutumika kufundishia..ili mradi tu uwe unajua kuwa ulipoenda kutafuta tiba ni teaching hospital! Na unapoona wanafunzi wengi wanakuja kujifunza kwa mgonjwa wako tu, basi ujue mgonjwa wako ana interesting au rare condition/presentation ambazo ni nadra kupata mgonjwa wa hivyo..so inabidi tu wanafunzi wote waje jifunza hapo, hakuna jinsi..lakini haina maana kuwa haikeri!

Naomba kupingana nawe hapo kwenye 'terminal stage'...sijui ni kwa kiasi gani uko close na mama mkwe wako, lakini ili mgonjwa awe declared 'terminal stage', lazima awe amechunguzwa kwa daktari kumuexamine na n pia vipimo mbali mbali kuonyesha ni kwa kiasi gani ugonjwa umeadvance...so vipimo hawakuvikalia, ndio vilivyowafanya wadhani kuwa mgonjwa wako yuko terminally ill.

Cha pili, baada ya kugundua mgonjwa ni terminally ill, kama hayuko kwenye 'coma' na ana ufahamu wa kuweza kuelewa, lazima daktari wake aongee naye kumuelezea wanachodhani kisayansi..yaani kumcounsel mgonjwa kwanza ajue extend ya tatizo lake, options alizo nazo na nini ultimate outcome ya options hizo. I hope by the time mwalimu anafundisha wanafunzi wake na kusema hivyo..basi mgonjwa alishakuwa counselled...kama bado, haikuwa sawa!

Cha tatu, haikupaswa ninyi kuwepo wakati mwalimu anafundisha wanafunzi wake kwa mgonjwa wenu...kwa sababu atawaonyesha technic mbali mbali za kuexamine na kufukia conclusion na wanafunzi watajaribu..hili linahitaji 'privacy', kwa hiyo hata ninyi hamkuwa na heshima kwa mgonjwa wenu kwa kuwepo hapo karibu hivyo mkiangalia na kusikiliza wakati mgonjwa yuko na madaktari wake.

Mimi naona ethical breach kwa pande zote mbili. Pole sana kaka.
 
Back
Top Bottom