Madaktari wa Muhimbili: This is unprofessional....!

Madaktari wa Muhimbili: This is unprofessional....!

Sitaki hata kusikia walimyanyapaa ndugu yangu mpaka akafa lol .tz hamna madactari ni wajinga tu.na waganga njaa
 
nimukuelewa moto2012...! lakini lakini stil nilicho kiandika kimeelewa maana nilikuwa kama najaribu mfafanulia mtambuzi kamavile ni mtu ambaye hajakutwa na tatizo hilo ..! kwahiyo nimemvua uhusika ili aweze kuliona tatizo hilo kwa ujumla...! napia nikasema kuwa tatizo ambalo mimi nimeliona nimoja tuu kuwa daktari aliongea kitu ambacho mgonjwa hakupaswa kukisikia ..! lakini kwaswala la mgonjwa wake kutumika kama ubao mimi sina tatito nalo..! nahata wewe siku ukienda hospital na ukiona umegeuzwa ubao hata usishangae tena ndiyo unatakiwa kuonyesha ushirikiano wa haliya juu ili huyo daktari aje kumtibu mjukuu wako miaka ya usoni:rockon:...!

Sidhani kama kuna anayekataa wagonjwa kutumiwa katika kufundishia. Kama yupo mtu wa aina hiyo basi atakuwa na matatizo makubwa sana. Sio tuu kwenye sekta ya afya bali sekta nyingine huwa zinatumia wateja wao kufundishia.

Hicho ni kitu cha kawaida kabisa. Hata kwenye baadhi ya makampuni, ukiwapigia simu, unaambiwa kwanza "This call may be recorded for training purposes" kama hutaki unapewa fursa ya kukataa au alternative communication.

Tatizo ni kwamba wagonjwa wanatumika kufundshia bila ridhaa yao. Baadhi ya watu wanadai kuwa kutafuta voluntary consent imekuwa ngumu kwa sababu wagonjwa wanakataa. Kwa hiyo, ndiyo maana wakaamua kuwa na automatic consent. Lakini kama umesoma post yangu huko nyuma tafiti zinaonyesha kuwa zaidi wa asilimia 90 ya wagonjwa wako tayari kutoa ridhaa ya kutumika kufundishia.

Personally, kati ya wateja waliokataa kutumiwa ili mimi kama trainee nifundishwe au mimi niwatumie kuwafundisha tranees wengine, so far ni mteja mmoja tuu. Na huyo mteja (mwanamke) alikataa kwa sababu trainee alikuwa mwanaume na kutokana na tatizo lake, she was right to kutotaka mwanaume mwingine kuwa pale.

Pia kuna watu wanadai kuwa automatic consent ina-apply kwenye university hospitals zote duniani. Lakini nimeshatibiwa kwenye university hospitals na walipokuwa wanataka kunitumia kwenye trainings zao walitaka ridhaa yangu, which, of course, I consented.

Kwenye suala la Mtambuzi, tatizo la daktari kutoomba ridhaa kutoka kwa mgonjwa wao linaonekana wazi kabisa. Lack of consent imesababisha beach of confidentiality, a fundamental legal and ethical duty for every medical doctor.
 
EMT nimekuelewa mkuu bila shakaa...! muheshimiwa mtambuzi alipo lileta swala hili katika jamvi ..! alikuwa anaseama kuwa kilicho muudhi siyo kwamba mgonjwa wake kutumiwa ila kuna kauli ambayo Dr. aliiongea mbele ya mgonjwa ambayo haikumridhisha..! lakini pia nadhani kinacho sababisha mpaka hali hii inatokea nikuwa kuwa na vyuo vingi sehemu yenye hiospital chache..! utakuta sehemu kama hospital ya mwananyamala wameenda wanafunzi wa IMTU, KAIRUKI,KAM MEDICAL COLLG..! SASA UNADHANI WOTE WAKIKUTANA HAPO NINI KITATOKEA MAANA WANAKUTANA THE SAME DAY KAKA...! YAANI TUNACHANGAMOTO NYINGI KWA KWELI
 
Of course, changamoto tunazo. Nilitoa mfano, jinsi inavyoweza kuwa ngumu kwa daktari ku-maintain confidentiality kwenye wodi kama Kibasila au Mwaisela ambayo kuna wakati inafurika wagonjwa mpaka wengine kulala chini.

Kwa mfano, haiwezekani wakati mgonjwa anapofanya contact ya mwanzo kabisa na hosipital husika kujulishwa kwamba anaweza kutumika katika kufundishia ili aweze kutoa ridhaa yake mapema kabisa hata kabla hajaanza matibabu yoyote?

Sometimes, mgonjwa anaweza kuathirika zaidi kwa "kuvamiwa" na kundi la watu anahisi ni madaktari kumbe ni trainees tuu. Anaweza kudhani anaumwa ugonjwa ambao ni serious zaidi na ndiyo maana amezungukwa na "madaktari" wote hao.

Kama unavyojua tena, mtu akionekana amevaa koti jeupe maeneo ya hospital automatically wengi wanadhani kuwa ni daktari.
 
nimejifunza mengi kwenye hii hii thread. Asante sana Mtambuzi, EMT na ZeMarcopolo kwa kuwataja kwa uchache tu baadhi waliochanagia kwa weledi mkubwa.

Ushauri mmoja nitoe kwa madaktari kwamba wakiguswa kwenye ishu yeyote wawe watulivu na wajibu hoja kwa hoja tena kwa busara bila jazba na kukurupuka

pole sana Mtambuzi kwa mgonjwa wako
 
Last edited by a moderator:
Pole zana kaka kwa yaliyokukuta, kiukweli co vzr na czan kama maadili ya kaz yanawafundisha ivo, ivi hawajui unapomkatisha tamaa mgojwa ya kuishi n tatizo kubwa? Hata kama mgonjwa anaweza kupona kutokana na maneno yao wanaweza sababisha mgonjwa akafariki hata kabla ya cku kwa sababu hata hizo dawa hazitokua zinafanya kaz kama inavyotakiwa bcoz hata kile kilichopo mwilin kinachopambana na ugonjwa kitashinda bcoz akili ya mgonjwa itakuwa haion kama kuna uzima tena. Ila vzr kwa kua umemuamisha mama.
 
nimukuelewa moto2012...! lakini lakini stil nilicho kiandika kimeelewa maana nilikuwa kama najaribu mfafanulia mtambuzi kamavile ni mtu ambaye hajakutwa na tatizo hilo ..! kwahiyo nimemvua uhusika ili aweze kuliona tatizo hilo kwa ujumla...! napia nikasema kuwa tatizo ambalo mimi nimeliona nimoja tuu kuwa daktari aliongea kitu ambacho mgonjwa hakupaswa kukisikia ..! lakini kwaswala la mgonjwa wake kutumika kama ubao mimi sina tatito nalo..! nahata wewe siku ukienda hospital na ukiona umegeuzwa ubao hata usishangae tena ndiyo unatakiwa kuonyesha ushirikiano wa haliya juu ili huyo daktari aje kumtibu mjukuu wako miaka ya usoni:rockon:...!
Sikupanga nikujibu, lakini nimelazimika kukujibu kwa sababu inaonekana hujasoma maelezo yangu vizuri, najua nji kutokana na jazba kwa sababu taaluma yako imeguswa......

Hebu soma hapa chini, maana sikukataa mgonjwa wetu kutumika kufundishia:

Sikatai mgonjwa kutumika kufundishia wanafunzi, hawa ni ndio madaktari wetu wa kesho wakajifunzie wapi. Lakini pale dakatari anapowaambia wanafunzi wake kwamba huyu mgonjwa aliyeko mbele yao yuko katika TERMINAL STAGE huku wanaomuuguza wakiwa karibu na hata mgonjwa mwenyewe akisikia, huu ni uuaji. Daktari huyo aliendelea kuwaonyesha wanafunzi wake dalili zinazothibitisha kuwa mgonjwa wetu yuko kwenye terminal stage.

Kisha soma hiki kisa ambacho niliwahi kukiandika hapa JF.......

https://www.jamiiforums.com/mahusia...jors-je-alikuwa-ni-malaika-wa-kifo%85%85.html

Ukisoma utaona ni jinsi gani wataalamu wetu wa tiba wanavyocheza na roho zetu, na hii si kwa Tanzania pekee hata katika nchi zilizoendelea kama nilivyosimulia katika kisa hicho cha kweli....

Labda nikushangaze kidogo, katika kipindi cha wiki nzima ambacho mkwe wangu alilazwa pale Muhimbili, nimeshuhudia vifo vya wagonjwa kwa wastani wa wagonjwa wanne mpaka watano kwa siku katika ward ya Mwaisela, wagonjwa hao walikuwa wanakufa huku wauguzi wakiwatazama na wakiitwa hawaendi wanasubiri tu kuwafunika, sikuona mgonjwa yeyote alionyesha kutapatapa katika kukata roho akifanyiwa CPR, sikuona. Na hata wale walioonekana kuzimia hakuna juhudi iliyofanyika kuwafanyia CPR.. Mkuu bado unaweza kusimama na kutetea uzembe huu wa Muhimbili....?
 
Sioni ni kwa sababu gani daktari alazimishe consent simply because a patient will make a decision you don't disagree with. Otherwise, hiyo itakuwa ni duress kama siyo undue influence.

Kwanza, unaposema university hospital unamaanisha university hospital zote duniani au ni zile za Tanzania tuu?

Pili, kama ni Tanzania, unaweza kutupa hiyo sheria au guideline inayohalalisha automatic consent kwenye university hospital kama Muhimbili? This will help a lot.

Tatu, kuna aina mbili za consent: explicit consent na implied consent. Explicit consent ni pale mgonjwa anapompa daktari specific permission to do something. Explicit consent inaweza kuwa ya mdomo au ya maandishi.

Implied consent ni pale mgonjwa anapoonyesha ridhaa yake indirectly, kwa mfano, kwa kuleta prescription ili umpe dawa. This is not a lesser form of consent but it is only valid if the patient knows and understands what they are consenting to.

Hii automatic consent inatoka wapi? Najua sometimes hasa wakati wa emergency treatment, kunaweza kuwa na automated informed consent kutokana na hali mbaya ya mgonjwa au kutokuwepo kwa mtu wa karibu kutoa explicit consent. Lakini mgonjwa ana capacity ya kutoa consent lakini analazimishwa kutoa consent automatically?

OK, let's assume pia kuna "automatic consent". Sheria inasema wazi kuwa ili consent iwe valid, lazima anayetoa awe na capacity ya kuitoa, lazima awe amefanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yoyote, lazima awe amepewa "sufficient, balanced information" ili kumwezesha kufanya an informed decision, na pia ni lazima awe na uwezo wa kujua na kupima maelezo aliyopewa kabla ya kutoa ridhaa yake.

Sasa nyie kama madaktari mna-ensure vipi kuwa mgonjwa anajua kuwa hosipitali anayoenda ni university hosipital na kwamba consent yake ya kutumika katika kufundishia itakuwa obtained automatically? Hivi mgonjwa wa kawaida atajuaje hii ni teaching hospital na ile siyo kama hatapewa maelezo kabla?

Wangejuaje kuwa hawakupaswa kuwepo pale wakati mwalimu anafundisha? Nani alikuwa na majukumu ya kuwaeleza kuwa hawakupaswa kuwa pale? Who led them to breach the ethics? Unaona jinsi tatizo moja linavyozaa tatizo lingine? Kutokuomba prior consent, kumesababisha breach of confidentiality.

Kama mgonjwa angekuwa ametaharifiwa kabla kuwa atatumika kufundishia basi angekuwa na fursa ya kuamua kama ndugu zake wawepo pale wakati anatumika kufindishia. In fact, daktari alikuwa na duty ya kumwuliza mgonjwa kama angetaka ndugu zake wandelee kuwepo wakati anatumika kufundishia.

Kwa hiyo hapo sidhani kama kuna "contributory negligence" kwa upande wa ndugu zake. Daktari alikuwa na duty ya ku-seek consent, hakufanya hivyo. Alikuwa na duty ya ku-maintain confidentiality, hakufanya hivyo. Hata kama kuna "automatic consent" sidhani kama ina dispense the duty of confidentiality automatically. Does it?
EMT ...am not a lawyer, what I shared was my experience kwanza kwa kusoma Muhimbili for 5yrs, pili Internship for 1yr, na tatu kwa kufanya hapo kazi for 3yrs. Kipindi chote nimekuwa Muhimbili, filosofia ndio hiyo...it is a University 'Teaching' Hospital, haiwezekani amekuja mgonjwa ana rare/very interesting condition..then wanafunzi wasijifunze kwa sababu tu mgonjwa au ndugu hawataki! Kama unataka maelezo kwa mrengo wa kiSheria, tafadhali wasiliana na mwanasheria wa Muhimbili National Hospital (au pia KCMC, Bugando, Mbeya) anaweza kukusaidia maswali yako.

Lakini hilo halisababishi maDaktari kutofuata maadili (ethics) yao za kikazi kutokana na kiapo, na pia haki za mgonjwa. Katika miaka hiyo 8 sikuwahi kusikia mgonjwa akilalamika amekosa/amenyimwa huduma kwa kukataa kutumika kwa ajili ya mafunzo. Na wapo ambao walilalamika kutotumika kwa mafunzo kwani kutumika kwa mafunzo kulikuwa na advantage ya ugonjwa kujadiliwa 'comprehensively' na Professor/Consultant...na hivyo matibabu yake kuwa bora zaidi!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Sikupanga nikujibu, lakini nimelazimika kukujibu kwa sababu inaonekana hujasoma maelezo yangu vizuri, najua nji kutokana na jazba kwa sababu taaluma yako imeguswa......

Hebu soma hapa chini, maana sikukataa mgonjwa wetu kutumika kufundishia:

Kisha soma hiki kisa ambacho niliwahi kukiandika hapa JF.......

https://www.jamiiforums.com/mahusia...jors-je-alikuwa-ni-malaika-wa-kifo%85%85.html

Ukisoma utaona ni jinsi gani wataalamu wetu wa tiba wanavyocheza na roho zetu, na hii si kwa Tanzania pekee hata katika nchi zilizoendelea kama nilivyosimulia katika kisa hicho cha kweli....

Labda nikushangaze kidogo, katika kipindi cha wiki nzima ambacho mkwe wangu alilazwa pale Muhimbili, nimeshuhudia vifo vya wagonjwa kwa wastani wa wagonjwa wanne mpaka watano kwa siku katika ward ya Mwaisela, wagonjwa hao walikuwa wanakufa huku wauguzi wakiwatazama na wakiitwa hawaendi wanasubiri tu kuwafunika, sikuona mgonjwa yeyote alionyesha kutapatapa katika kukata roho akifanyiwa CPR, sikuona. Na hata wale walioonekana kuzimia hakuna juhudi iliyofanyika kuwafanyia CPR.. Mkuu bado unaweza kusimama na kutetea uzembe huu wa Muhimbili....?

sasa kaka unajua muhimbili iko katika range gani katika mode of referral mbona hata hao wanne wachache coz most of the pt referred there are at end stage, coz of poor dx and Investigations. Sasa wakulaumu hapa si Dr ila serikali yako ya ccm. Labda unambie kati ya hao waliokufa unafikiri hawakupewa huduma zinazostahili.
 
muheshimiwa MTAMBUZI ...! naheshimu sana mawazo yako...! na pia huwa i use to keep my eyes open ninapoona comment yako...! nimekuelewa nawala sina nia ya kutetea uzembe ambao unatokea pale muhimbili lakini pia napenda kukuambia kuwa siyo kila tatizo linalo tokea ukalichukulia kama ni uzembe bali ni changa moto...! hakuna mtu anaye penda kucheza na roho za watu...! changa moto pia ni sababu kubwa..! nataka nikuulize kitu kimoja..! wewe binafsi najua unajua kuwa pale kuna changamoto nyingi sana kama hospital ya taifa na pia changamoto hizo zimedumu kwa muda mrefu sana... JE? KUNA HATUA ZOZOTE ZILIZO CHUKULIWA AWALI AU AMBAZO ZINAZO ENDELEA KUCHUKULIWA KWA SASA ILI KUWE KUKABILIANA NA CHANGA MOTO HIZO..! NA WEWE KAMA MTANZANIA UNAMCHANGO GANI KITIKA HATUA HIZO HATA KWA MAWAZO..!? TANZANIA NI YETU SOTE
 
Hatuna madaktari kabisa
hata wenye vvu huwa taarifa zao zinasambazwa na wananyooshewa vidole hata na wauguzi
 
Ukweli ni kwamba wkt wa round hakuruhusiwi relative yyte aingie wodini sasa nashangaa kusikia daktari alifundisha mbele ya relative kama aliingia alikiuka utaratibu
 
sasa kaka unajua muhimbili iko katika range gani katika mode of referral mbona hata hao wanne wachache coz most of the pt referred there are at end stage, coz of poor dx and Investigations. Sasa wakulaumu hapa si Dr ila serikali yako ya ccm. Labda unambie kati ya hao waliokufa unafikiri hawakupewa huduma zinazostahili.
Hiyo ni kwa ward namba 4 ya Mwaisela na hapo nimesema kwa wastani, sijataja ward nyingine mkuu........
 
Mtambuzi pole sana, wanaacha kumkomoa Kikwete na CCM yake, wanatukomoa sisi ambao hatuna uwezo hata wa kulipia hospitali kama ya Aga Khan.
Waganga wa kienyeji nao feki ile mbaya,
waombeaji nao wamekuwa magumashi ile mbaya.
Sijui tukimbilie wapi ili tupone.
Na wakati huohuo kila tunachokula na tunywacho tunaambiwa eti ni sumu.
Duhh

TATIZO ASKOFU kAKOBE AKIWAAMBIA UKWELI mnampinga na kusema hana nguvu za Mungu anatumia pepo na matusi kibao. nendeni huko utakutana na Mungu wa kweli wa Biblia, mie nimeenda nimeona ukweli wa haya
 
Back
Top Bottom