Mrimi
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 1,691
- 640
Yaani ndugu yangu wewe ni mgumu kuelewa,hata Muhimbili kama utaki kufundishiwa toa taarifa kwa uongozi,sio kusumbua madaktari wodini,ili ni teaching hospital,ukikataa kufundishiwa hamia IPPM na matibabu yako hayataathirika na kitu chochote.Unasoma articl alafu huzielewi,lakini tatizo sio field yako but unakomaa tu,wewe kweli mkomavu inaeelekea sura yako imukunjana njoo tukufanyie plastic surgery
Mkuu naona huko tunakoelekea,tunaweza tusifike... Matusi tena?!
Unahisi madaktari wote(wa TZ) wana mtazamo kama wako,huh?
Mimi siamini kama mtu anaweza kujua kila jambo,ila naamini ni busara kujifunza kutoka kwa wengine. Mimi ninaamini ZeMarcopolo lazima atakuwa ni daktari kutokana na michango yake humu JF ingawa siamini kama yupo hapa nyumbani.Kwa hiyo kusema hiyo sio field yake,sidhani kama ni sahihi.Anyway,hayo niwaachie ninyi wawili..
Hapa kuna malalamiko yametolewa,fine.Ila ni ya upande mmoja.. Hatujapata kusikia upande wa pili unasemaje.Kwa hulka ya kawaida ya kibinadamu kila mtu anapojieleza ni kawaida kabisa kuvutia kwake.. Tutaamaini vipi kama kila alichosema kina ukweli kwa kiasi gani? Mimi sijui.
Sina hakika kama wewe ni daktari au medical student/intern/resident doctor,whatsoever.. Nataka nikuulize kitu,je wakati wa kuchukua maelezo ya mgonjwa au kumfanyia physical examination,unaomba concert yake? Na ikiwa ndivyo,what for? What if mgonjwa akikubali ukachukua history yake vizuri,ila akakataa kumfanyia physical examination?
Anyway mimi nadhani pande zote zinatakiwa kutimiza wajibu wake.Madaktari wafanye kazi kwa ethics na sisi ndugu wa wagonjwa tutimize wajibu wetu.Lakini pia tukubali kwamba mazingira ya hospitali zetu nayo yanachangia sana kukandamiza haki za wagonjwa.Kwenye mjadala huu sijaona hata mtu mmoja akicomplain kuhusu mgonjwa 'X' kusikiliza siri ya tatizo la mgonjwa 'Y'.. Hii pia sio ethical.
Siku zote tusi ni baya ikiwa umetukanwa mbele za watu! Ndivyo na hili jambo ninavyolichukulia.Hapa tatizo sio kwamba dr.ametoa kauli hiyo mbele za wanafunzi.. ni kwa sababu dr.amesema mbele ya wagonjwa,na relatives waliokuwepo pale.Vipi kwa mfano kama mgonjwa angekuwa kwenye chumba cha peke yake na huyu ndugu yetu naye asingekuwapo? Vyoyote tukakavyojadili hapa,pamoja na kwamba wahudumu wetu nao wana mapungufu yao,ila hata mazingira ya kufanyia kazi nayo ni kikwazo kikubwa ktk kumaintain siri za wagonjwa.
Mimi nadhani,ili tupate competent doctors tunahitaji wapate mafunzo ya kutosha..tunahitaji wagonjwa wengi wa kujifunzia..elimu itolewe kwa watu wetu ili waone umuhimu wa kutumika kujifunzia..kwenye mafunzo ya udaktari models ni binadamu..Ndio maana kuna maiti nyingi zilizohifadhiwa kwa ajili ya kujifunzia,sio midoli(ingawa kwa nchi nyingine wanatumia midoli,lakini ni kwa level za chini tu)..tunatakiwa kujifunza kujitolea kutumika kwa ajili ya vizazi vijavyo..Kwa nchi nyingine(walipoelimika),watu wanajitolea miili na viungo vyao kutumika ktk vituo vya utafiti na medical schools pindi wanapokuwa wamefariki. Kwa hapa kwetu ni tofauti sana ndio maana hata tuna upungufu wa damu ktk vituo vyetu,kwa kuwa watu hawako tayari kujitolea kuchangia damu..
Kuhusu kutimuliwa kwa mgonjwa anapokuwa amekataa kutumika kujifunzia,sina hakika sana maana sijawahi kutibiwa muhimbili..ila kwingine nilikopita hiyo sijaona kwa mfano KCMC hiyo haipo.
Last edited by a moderator: