pole sana ndugu wa mgonjwa, naomba tu upunguze jazba, hakuna m2 aliyezaliwa akijua kuongea wote wanajifunza na kufunzwa pia, katika hospitali kama muhimbili mgonjwa akishaingia wodini tayari ni kitabu kwa kuwa kuna madaktari wanofanya kazi kwa uangalizi wa wenzao na wapo wanaoongeza elimu na pasipo kutumia wagonjwa hatutaweza kutengeneza madaktari wengine.
kuna mida maalum yakuona wagonjwa na wakati madaktari wanakuwa na mgonjwa ni jambo la hekima kwa ndugu kutoa mwanya lakini kwa wa TZ wengi hawafuati utaratibu, hasa pale ndugu wa mgonjwa anapokuwa mtumishi wa afya au anavijisent na nafasi kidogo yakisiasa ndiyo wataomba vibali mpaka ikulu ili tu awe na mgonjwa wakati wote.
kuna magonjwa yanayoonekana kwa nadra na hivyo anapotokea mgonjwa mwenye tatizo kama hilo au mwenye dalili na alama kama kitabu hutumika sana kufundishia kwakuwa kusikia m2 husahau kwa asilimia nyingi, kuona huongeza kumbukumbu na kugusa huweka mihuri na uhakika katika jambo husika, fuatilia kisa cha tomaso.
matambue kuwa mgonjwa wa mgonjwa wapaswa kuwa siri kati yake na daktari/madaktari wake hivyo nawe ulipokuwa unataka majibu ya mgonjwa ulimuomba mgonjwa ruksa ya wewe kupokea majibu yake?
kama kawaida katika kila sekta huwezi kuwa na watu waaminifu katika mambo sensitive kama siri za wagonjwa hivyo kwa wale wanaotoa taarifa za wagonjwa wao wanapaswa kukemewa kwa nguvu zote kupitia katika masanduku ya maoni na kamati za afya za vijiji, kata........
uzi ni kwamba muda huo ulikuwa wa
jambo la msingi ni kushirikiana na kuheshimiana,