Borat69
JF-Expert Member
- Jun 17, 2012
- 2,522
- 1,761
Watu Kama wewe inatakiwa uundwe Mkoa mpya(Lalaland)kwa ajili yenu.Pole sana mtambuzi,lakini tatizo letu wabongo tunapenda kudanganywa mgonjwa akiambiwa ukweli hatupendi.Pili muhimbili ni hospitali ya kufundishia,kwahiyo huwezi kwepa mgonjwa wako kutumika kama kitabu.
Suala la Work Ethics halina wabongo kupenda kudanganywa wala nini,kuna mambo ambayo unaweza kushabikia Kama mechi za mpira lakini sio suala la Afya na matibabu ya binadamu.
Hata Kama Muhimbili ni hospitali ya kufundishia,bado haiwapi uhuru wa kisheria au wa lazima kutoa hayo mafunzo mbele ya Mgonjwa bila ridhaa (Consent) yake. Ni rahisi Kwako kuona ni sawa kwa hayo ulioyoandika hapo juu kwa kuwa huyo Mgonjwa sio Mama yako wala hana uhusiano na wewe. Wewe inaelekea ni wale mnaoenda kutibiwa Apollo ukipata mafua,ndio maana shida na karaha za Mtanzania wa kawaida hazikugusi.