Madaktari Mt. Meru Arusha wala njama kumuua mgonjwa

Pole ndugu kwa kupoteza...is how corrupt system operate.. Maisha ya walalahoi yamegeuka makaratasi ya kubetia so far kwa kuwa rushwa ipo na tumekataa kuikemea basi natumai bwana Shirima ataenda kupata haki yake akifika juu maana hata unaotaraji wawe wachunguzi wa jalada lako hawatakuwa malaika hivyo ni kukaa tu chini kumuombea ndugu huyu apate pumziko la haki aendako wakati akisubiri taratibu nyingine kulingana na alivyoishi enzi za uhai wake!
Shirima hajafa..anapata matibabu hosipitali nyingine.

Acha uchuro!
 
Kama hizi taarifa zina ukweli basi acha watu waendelee kufungua nyuzi za kutafuta njia za kuikimbia hii nchi, huu ni zaidi ya unyama ambao Tz ndio nchi pekee ambapo jambo kama hili linatokea na hakuna hatua zozote zitachukuliwa, My poor Country.
 
Ukitaja hiyo Hospital naumia sana.
Nikikumbuka siku nilompeleka mama angu(APUMZIKE KWA AMANI)
Tulilokuwa tumetoka hospital nyingine baada ya kupimwa na kuonekana damu iko chini wakatuandikia mount meru Tukaenda na ndugu zaidi ya nne ili kuchangia dam. Tunafika mapokezi ni sifuri Bado twaingia kwa madaktar tunakuta ni wa field yaan tunaeleza tatizo anaanza ku google kuwa itakuwa shida ni ipi. Tunamueleza shida ni dam kama tulipotoka maana alipimwa kabisa anakwepa . Hakufanyiwa hata vipimo anatoa tuu maelekezo mkachukue dawa flan basi. Nilifika sa 3 ila huduma tulipata sa 10 tena sio huduma yaani kuskilizwa.

NISEME TUU TUTAFUTE HELA IKIWEZEKANA , MAANA VIFO VINGI VYA NDUGUZETU AU SISI NI KUTONA NA UMASKINI WALA SIO MUNGU KAPANGA.
Pole sana mkuu kwa kumpoteza mama inauma sana kuondokewa naye
 
Kama ni kweli hizi tuhuma basi hao madr wamepoteza Ethics ya kazi zao,japo kubalance stori ilikua vizuri kusikiliza upande wa pili pia,...Nurses na Doctors ni miongoni mwa kada zinazoongoza kurushiwa lawama kuliko pongezi pamoja na kazi kubwa wanayofanya kuokoa uhai,na lawama nyingi ukifuatilia hazina ukweli....nimekuwepo Hospitali moja hapa Dar inashutuma nyingi sana na inafahamika karibia nchi nzima kwa skendo, lakini kiuhalisia 96% ya hizo shutuma hazina ukweli, lkn kwa sababu raia wamekariri hivyo basi taswira yake ni mbaya tu....hatufurahii hawa watu wa Afya wanapo kwenda kinyume na maadiri ya kazi yao na wanaofanya hivyo ni wachache ambao kwenye kila kada wapo....lkn pia tujifunze kuwapongeza na kuwatia moyo wanapofanya vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Poleni sana mkuu nadhani lengo lao ni afariki ili apate unafuu wa kesi. Ila vijana wa bodaboda nao huwa barabarani wanasumbua sana hawapo makini kabisa ndiyo maana hupata ajali nyingi ingawa sitaki kusema kuwa rafiki yetu Kennedy naye ni mmoja wao kwa uendeshaji mbovu maana hatujapata taarifa za upande wa pili zaidi ya sababu uliyoitoa ya ulevi. Tunamuombea tu atoke salama chumba cha operation ili apate haki yake kwa case iliyopo
Hii imetokea baada ya kijana aitwaye Kennedy Mathias Shirima kugongwa akiwa akiendesha pikipiki na Mwanajeshi ambaye ni daktari akiwa amelewa chakari majira ya saa 5 asubuhi. Mwanajeshi huyu ni kutoka kambi ya jeshi Tanganyika Parkers Arusha. Ajali hii ilitokea tarehe 08/01/2020

Mwanajeshi huyu alikuwa amelewa chakari majira ya saa 5 asubuhi alipohama upande wake na kwenda kumgonga Kennedy akiwa upande wa pili wa barabara eneo la Kilimani karibu na kilipo kituo maarufu cha kona ya Kiseriani.

Kennedy aliumia kichwani licha ya kwamba alikuwa amevaa kofia ngumu na alipelekwa hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mt. Meru. Madaktari walisema akafanyiwe kipimo cha CT scan na kwa sababu hakipatikani katika hospital ya Mt. Meru. Ndugu na majirani walimpeleka hospital ya NSK na kufanyiwa kipimo hicho na ripoti pamoja na picha zikaletwa hospitali ya MT. Meru alipokuwa amelazwa chumba cha majeruhi na hapa ndipo mchezo wa kummaliza ukaanza. Dakatari wa jeshi aliyemgonga kwa kushirikiana na madaktari wa MT. Meru wakahakikisha kipimo hakisomwi wala kufanyiwa matibabu stahiki ili Kennedy apoteze Maisha na hivyo kupoteza Ushahidi wa kesi inayomkabili Daktari mwanajeshi. Taarifa za ajali hii ya kizembe lipo kituo kikuu cha polisi Arusha.

Madaktari walikataa kusoma kipimo kwa sababu za kitoto ambazo ni (i) hawawezi kusoma ripoti ya CT scan bila kuwa na picha na CD, (ii)wametoka kufanya upasuaji wamechoka, (iii) wanasikia njaa wanaenda kula. Mimi nilikwenda personally kumuuliza nurse na aliniambia madaktari wamemaliza operesheni ya mwisho sasa hivi wanasikia njaa na wamechoka hawawezi kusoma kipimo labda kesho yake. Wakati huo hali ya mgonjwa ilikuwa siyo nzuri kwani alikuwa analalamika maumivu makali ya kichwa na hakuwa anaweza kuongea vizuri.

Siku ya tatu ndipo Madaktari walikuja kusoma kipimo na kusema picha imepigwa upande mmoja na inabidi ikapigwe na ya upande wa pili ndipo waweze kusoma. Hawakuonyesha udharura wowote wala kujali chochote kuhusu hali ya Kennedy.

Siku ya jumanne tarehe 14/01/2020 Kennedy akiwa katika hali mbaya akapewa discharge kurudi nyumbani. Lengo lilikuwa akafie nyumbani. Hali yake ilizidi kuwa mbaya na tarehe 15/01/2020 ndugu zake tulimchukua na kumpeleka katika hospital nyingine na madaktari walimpokea kama mgonjwa wa emergency na walivipokea na kuvisoma vipimo vilevile vya CT scan na kusema anatakiwa afanyiwe upasuaji wa haraka within 12hours la sivyo tutampoteza. Vipimo hivi hivi madaktari wa Mt. Meru walikataa kuvisoma kwa sababu ambazo ni very unprofessional.

Ilionekana kuna damu inavuja taratibu kichwani na ingeachwa basi alikuwa siku si nyingi apoteze Maisha. Tunaomba Mungu operesheni hii ifanyike kwa mafanikio.

Madaktari wa Mt. meru walijua kila kitu kuhusu hali ya Kennedy lakini kwa sababu mhusika wa ajali ni Daktari mwenzao tena Mwanajeshi basi wakaamua kula njama ili atoweke kumnusuru mwenzao.

Naiomba serikali iwachukulie hatua Madaktari hawa ambao wamekula njama chafu ambazo ni kinyume na kiapo chao cha udaktari.

Ninataka niamini kuna watu wengi wamepoteza Maisha si kwa sababu Mungu alipenda ila kwa sababu ya Madaktari wachache wala rushwa na wasio na chembe ya utu. Hata kama serikali na hususani wizara ya afya itashindwa kuwashughulikia nina imani Mungu hatawaacha salama labda watubu warudishe fahamu za utu na waache kutanguliza mbele maslahi yao
 
Mkuu usilalamikie ulipoa anguka Ila ulipojikwaa umewahi kujiuliza kwanini wanalaumiwa sana
Kama ni kweli hizi tuhuma basi hao madr wamepoteza Ethics ya kazi zao,japo kubalance stori ilikua vizuri kusikiliza upande wa pili pia,...Nurses na Doctors ni miongoni mwa kada zinazoongoza kurushiwa lawama kuliko pongezi pamoja na kazi kubwa wanayofanya kuokoa uhai,na lawama nyingi ukifuatilia hazina ukweli....nimekuwepo Hospitali moja hapa Dar inashutuma nyingi sana na inafahamika karibia nchi nzima kwa skendo, lakini kiuhalisia 96% ya hizo shutuma hazina ukweli, lkn kwa sababu raia wamekariri hivyo basi taswira yake ni mbaya tu....hatufurahii hawa watu wa Afya wanapo kwenda kinyume na maadiri ya kazi yao na wanaofanya hivyo ni wachache ambao kwenye kila kada wapo....lkn pia tujifunze kuwapongeza na kuwatia moyo wanapofanya vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitendo cha madaktari kujivuta vuta kusoma ripoti ya CT scan kwa siku tatu kwa visingizo visivyo na mashiko lakini pia ku discharge mgonjwa ambaye hali yake ni mbaya kunatia shaka kubwa sana. Kwa kawaida Mgonjwa anakuwa discharged akiwa ame recover. Inakuwaje unam discharge mgonjwa halafu anakwenda kufanyiwa operation hospitali nyingine tena kwa dharura
 
Back
Top Bottom