• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Madaktari Mt. Meru Arusha wala njama kumuua mgonjwa

TENGEFU

TENGEFU

Member
Joined
Jan 25, 2017
Messages
53
Points
125
TENGEFU

TENGEFU

Member
Joined Jan 25, 2017
53 125
Hii imetokea baada ya kijana aitwaye Kennedy Mathias Shirima kugongwa akiwa akiendesha pikipiki na Mwanajeshi ambaye ni daktari akiwa amelewa chakari majira ya saa 5 asubuhi. Mwanajeshi huyu ni kutoka kambi ya jeshi Tanganyika Parkers Arusha. Ajali hii ilitokea tarehe 08/01/2020

Mwanajeshi huyu alikuwa amelewa chakari majira ya saa 5 asubuhi alipohama upande wake na kwenda kumgonga Kennedy akiwa upande wa pili wa barabara eneo la Kilimani karibu na kilipo kituo maarufu cha kona ya Kiseriani.

Kennedy aliumia kichwani licha ya kwamba alikuwa amevaa kofia ngumu na alipelekwa hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mt. Meru. Madaktari walisema akafanyiwe kipimo cha CT scan na kwa sababu hakipatikani katika hospital ya Mt. Meru. Ndugu na majirani walimpeleka hospital ya NSK na kufanyiwa kipimo hicho na ripoti pamoja na picha zikaletwa hospitali ya MT. Meru alipokuwa amelazwa chumba cha majeruhi na hapa ndipo mchezo wa kummaliza ukaanza. Dakatari wa jeshi aliyemgonga kwa kushirikiana na madaktari wa MT. Meru wakahakikisha kipimo hakisomwi wala kufanyiwa matibabu stahiki ili Kennedy apoteze Maisha na hivyo kupoteza Ushahidi wa kesi inayomkabili Daktari mwanajeshi. Taarifa za ajali hii ya kizembe lipo kituo kikuu cha polisi Arusha.

Madaktari walikataa kusoma kipimo kwa sababu za kitoto ambazo ni (i) hawawezi kusoma ripoti ya CT scan bila kuwa na picha na CD, (ii)wametoka kufanya upasuaji wamechoka, (iii) wanasikia njaa wanaenda kula. Mimi nilikwenda personally kumuuliza nurse na aliniambia madaktari wamemaliza operesheni ya mwisho sasa hivi wanasikia njaa na wamechoka hawawezi kusoma kipimo labda kesho yake. Wakati huo hali ya mgonjwa ilikuwa siyo nzuri kwani alikuwa analalamika maumivu makali ya kichwa na hakuwa anaweza kuongea vizuri.

Siku ya tatu ndipo Madaktari walikuja kusoma kipimo na kusema picha imepigwa upande mmoja na inabidi ikapigwe na ya upande wa pili ndipo waweze kusoma. Hawakuonyesha udharura wowote wala kujali chochote kuhusu hali ya Kennedy.

Siku ya jumanne tarehe 14/01/2020 Kennedy akiwa katika hali mbaya akapewa discharge kurudi nyumbani. Lengo lilikuwa akafie nyumbani. Hali yake ilizidi kuwa mbaya na tarehe 15/01/2020 ndugu zake tulimchukua na kumpeleka katika hospital nyingine na madaktari walimpokea kama mgonjwa wa emergency na walivipokea na kuvisoma vipimo vilevile vya CT scan na kusema anatakiwa afanyiwe upasuaji wa haraka within 12hours la sivyo tutampoteza. Vipimo hivi hivi madaktari wa Mt. Meru walikataa kuvisoma kwa sababu ambazo ni very unprofessional.

Ilionekana kuna damu inavuja taratibu kichwani na ingeachwa basi alikuwa siku si nyingi apoteze Maisha. Tunaomba Mungu operesheni hii ifanyike kwa mafanikio.

Madaktari wa Mt. meru walijua kila kitu kuhusu hali ya Kennedy lakini kwa sababu mhusika wa ajali ni Daktari mwenzao tena Mwanajeshi basi wakaamua kula njama ili atoweke kumnusuru mwenzao.

Naiomba serikali iwachukulie hatua Madaktari hawa ambao wamekula njama chafu ambazo ni kinyume na kiapo chao cha udaktari.

Ninataka niamini kuna watu wengi wamepoteza Maisha si kwa sababu Mungu alipenda ila kwa sababu ya Madaktari wachache wala rushwa na wasio na chembe ya utu. Hata kama serikali na hususani wizara ya afya itashindwa kuwashughulikia nina imani Mungu hatawaacha salama labda watubu warudishe fahamu za utu na waache kutanguliza mbele maslahi yao
 
Horseshoe Arch

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2009
Messages
12,697
Points
2,000
Horseshoe Arch

Horseshoe Arch

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2009
12,697 2,000
Huna details zaidi za kuweza kutoa mwanga juu ya hili? Haya yote una hakika nayo ama umezungumza emotionally kwa kuwa victim ni ndugu yako? Kama una ushahidi usioacha shaka kwanini usiuwasilishe kwenye mamlaka zinazohusika badala ya kuharibu ushahidi kwa kuleta hapa wakati jambo husika lipo kwenye vyombo vinine!
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
69,558
Points
2,000
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
69,558 2,000
Kama hii ni kweli sheria ichukue mkondo wake, Hakuna aliye juu ya sheria. Alafu mbona hawa madaktari wanakiuka proffesional ethics zao?

Sent using Jamii Forums mobile app
Tanzania haiwezi kuchukua hatua kwenye jambo linalomhusu mwanajeshi
 
Gerad2008

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2009
Messages
543
Points
250
Gerad2008

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2009
543 250
Kama hii ni kweli sheria ichukue mkondo wake, Hakuna aliye juu ya sheria. Alafu mbona hawa madaktari wanakiuka proffesional ethics zao?

Sent using Jamii Forums mobile app
MT Meru Arusha kuna tatizo kubwa sana hata ukifuatilia stori za mama wajawazito watakueleza vifo vingi vya watoto wanaozaliwa vinasababishwa na roho mbaya za manesi na madaktari kutokujali maisha ya watu
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
69,558
Points
2,000
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
69,558 2,000
Huna details zaidi za kuweza kutoa mwanga juu ya hili? Haya yote una hakika nayo ama umezungumza emotionally kwa kuwa victim ni ndugu yako? Kama una ushahidi usioacha shaka kwanini usiuwasilishe kwenye mamlaka zinazohusika badala ya kuharibu ushahidi kwa kuleta hapa wakati jambo husika lipo kwenye vyombo vinine!
unataka atekwe ?
 
Gerad2008

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2009
Messages
543
Points
250
Gerad2008

Gerad2008

JF-Expert Member
Joined Jun 9, 2009
543 250
Huna details zaidi za kuweza kutoa mwanga juu ya hili? Haya yote una hakika nayo ama umezungumza emotionally kwa kuwa victim ni ndugu yako? Kama una ushahidi usioacha shaka kwanini usiuwasilishe kwenye mamlaka zinazohusika badala ya kuharibu ushahidi kwa kuleta hapa wakati jambo husika lipo kwenye vyombo vinine!
Aliyeandika inaonyesha yuko well informed sidhani kama kakurupuka. Mi nafikiri ametoa taarifa baada ya kuona channel nyingine zinamzungusha (that is my assumption) hili ni jukwaa huru naona yuka sahihi kabisa
 
Crocodiletooth

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Messages
10,846
Points
2,000
Crocodiletooth

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2012
10,846 2,000
Serekali yako tukufu imekusikia "litafanyiwa kazi haraka"
Tumechoka na uzembe na makusudi ya wachache katika kuumiza watanzania.
HILI HALIKUBALIKI,NA UPEPELELEZI NA DHANI UTAANZA MAPEMA IWEZEKANAVYO.
Ndg.#Gambo alichukue hili,maana Rais akilijua Atachukia kweli kweli.
 
TENGEFU

TENGEFU

Member
Joined
Jan 25, 2017
Messages
53
Points
125
TENGEFU

TENGEFU

Member
Joined Jan 25, 2017
53 125
Huna details zaidi za kuweza kutoa mwanga juu ya hili? Haya yote una hakika nayo ama umezungumza emotionally kwa kuwa victim ni ndugu yako? Kama una ushahidi usioacha shaka kwanini usiuwasilishe kwenye mamlaka zinazohusika badala ya kuharibu ushahidi kwa kuleta hapa wakati jambo husika lipo kwenye vyombo vinine!
Details zipo hospitali na polisi. Mchakato mzima nilikuwa nina u monitor na kama ni uongo kacheki hizo tarehe nilizozitaja na ripoti ya polisi halafu dakatari waulizwe wali discharge vipi mgonjwa aliyekuwa hoi na kwa nini hawaku act kwenye CT scan accordingly. Hii ni fact hakuna emotion
 

Forum statistics

Threads 1,402,687
Members 530,969
Posts 34,402,285
Top