Leo tuwachane madaktari na manesi kujiona wadogo zake Mungu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,246
103,952
Hakuna shaka wanafanya kazi kubwa kuokoa maisha yetu. Mungu awabariki sana kwenye hilo. Lakini kama binadamu wengine nao wana mapungufu. Wengine mapungufu makubwa zaidi mpaka unajiuliza huyu mtu anatumia kiungo gani kufikiri. Ninayo machache ya kushangaza kwa hawa ndugu wakiwa anga zao;

1. Baadhi hawataki kusikiliza ushauri wowote toka kwa mgonjwa kama yeye ni mungu mdogo.
Wapo madaktari wamewaletea madhara makubwa wagongwa kutokana na kutowasikiliza. Mgonjwa mmoja alimwambia daktari asimchome hiyo sindano humletea madhara. Dr akakaza shingo, leo hii mgonjwa kavimba mwili mzima.

2. Kulazimisha ndugu asisogee wakati wa round wodini. Kwangu huu ni utoto. Mimi ndiyo ndugu nina haki ya kusikiliza maelekezo na hali ya mgonjwa wangu. Nina haki ya kusema juu ya maendeleo yake na hata kutoa ushauri. Kwanza mgonjwa mwingine unakuta hajiwezi, hana uwezo wa kujieleza. Daktari anakwambia toka nje.
Kuna siku nikamgomea kutoka akawa mpole.

3. Ubishi wa kijinga
Yupo daktari aliwahi kuacha kitambaa tumboni wakati wa operesheni. Mama yule akamweleza daktari baada ya maumivu kuzidi. Daktari hakufanya uchunguzi wowote. Mama akaenda hospitali ya rufaa wakakuta kitambaa. Akamrudia daktari mkuu basi wamrudishie gharama, wakakataa. Mama akasikiwa na wakili kesi ikaenda mahakamani wanadai 100m.
Vuta nikuvute ikaamuliwa walipe 50m.

4. Muda wa kuona wagonjwa
Wakati huu wa masika unakuta mvua inanyesha huwezi kuleta msosi kwa wakati. Unakutana na nesi anakaza hakuna kupita. Sasa mgonjwa afe njaa kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu.

Ongeza na zako....itaendelea

Ushauri
Usimuone daktari kama mdogo wake Mungu ukamuamini kwenye kila kitu, hasa hawa dot.com. Hakikisha unachanganya na zako au unakuwa na mtu wako pembeni wa kupima mwenendo wa matibabu
 
Ni kawaida ya binadam kujiona muhimu pindi anapogundua unamuhitaji, siyo wao tu ni popote unapoenda hali iko hivyo, ukiwa na shida na mwenyekiti wa mtaa utaona mbwembwe zake, ukiishi vijiji vyenye uasifiri wa shida na abiria ni wengi utaona mbwembwe za makondakta na madereva yaani ni tabia ya kibinadam

Ukiwa hauumwi nesi au doctor hana ubavu wa kukuletea mbwembwe anasubiri ile siku ukimuhitaji akunyooshe
 
Hao maroboti wanaoitwa madokta na manesi ni tatizo katika nchi.

Hawa ndio mabingwa wa kushabikia watu kudungwa machanjo ya corona.

Hawana clinical due diligence, hawana utafiti, hawana ujuzii, hawana utambuzi, wao ni kukariri tu VITINI VYA MEDICAL SCHOOL na kubugia maagizo ya kisiasa kama dodoki na MAKASUKU.

I wish i could be Rais wa Tanganyika nianze na hawa vibushuti.
 
Ni kawaida ya binadam kujiona muhimu pindi anapogundua unamuhitaji, siyo wao tu ni popote unapoenda hali iko hivyo, ukiwa na shida na mwenyekiti wa mtaa utaona mbwembwe zake, ukiishi vijiji vyenye uasifiri wa shida na abiria ni wengi utaona mbwembwe za makondakta na madereva yaani ni tabia ya kibinadam

Ukiwa hauumwi nesi au doctor hana ubavu wa kukuletea mbwembwe anasubiri ile siku ukimuhitaji akunyooshe
Wafany biashara vp
 
Umemaliza yote mkuu
Kila mtu anaringia cha kwake ukifika muda anahitajika sana
Hadi madereva daladala wanajiona miungu ikifika wakat wao, madereva wa mwendokasi ndio usiseme
 
Kwenye heading ingependeza kama ungetumia neno "Baadhi ya Madaktari na Manesi"

Ulivyofanya generalization tu, uzi umekuwa na kinazi
 
Back
Top Bottom