Madai: Aliyemuweka Mbongo rehani akamatwa!

Madai: Aliyemuweka Mbongo rehani akamatwa!

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2010
Posts
27,650
Reaction score
16,731

Mtanzania aitwaye Juma (jina lake la pili tunalihifadhi kwa sababu maalum) anayedaiwa kumuweka rehani ughaibuni Mbongo mwenzake Adam Akida Mwinyimkuu, mkazi wa Magomeni Mapipa jijini Dar es Salaam ambaye ametekwa na kushikiliwa na watu wanaoaminika kuwa ni ‘Wazungu wa Unga’ , amekamatwa na polisi jijini Dar.

Uchunguzi wa kina uliofanywa na waandishi wetu wiki iliyopita umebaini kuwa, Juma alikamatwa na polisi mwishoni mwa wiki iliyopita Tegeta na anahojiwa kuhusiana na kutuhumiwa kumuweka dhamana kijana Adam kisha kumtelekeza ughaibuni huku ikidaiwa kuwa yeye alikuja na shehena ya unga.

Habari zinasema ili Adamu awe huru, Juma anatakiwa kupeleka fedha shilingi trilioni moja ambazo ni gharama ya unga aliopewa, huku akimfanya mwenzake huyo kuwa ‘bond’ ya mzigo huo haramu.

“Fedha anazodaiwa Juma ni nyingi ni shilingi trilioni moja. Ni kwamba mzigo wenyewe (unga) hakufanikiwa kuuza kwani alikamatwa na askari wakamnyang’anya na sasa sijui atafanya nini ili kumuokoa mwenzake aliye ughaibuni,” kilisema chanzo chetu.

Habari zaidi zinasema kuwa licha ya Juma kuwa korokoroni, baba wa Adamu mzee Akida Mwinyimkuu naye alishikiliwa kwa muda na polisi katikati ya wiki iliyopita lakini hakuwa na msaada wowote kwa vyombo vya dola.

“Mzee Akida alikamatwa na polisi lakini badala ya kusaidia akawa anapotosha ukweli. Yeye aliwaambia polisi kuwa mtoto wake Adam hakwenda Pakistani bali alikwenda Afrika Kusini na ndivyo anavyojua. Alipooneshwa video ya mwanaye akiwa chini ya ulinzi, alishangaa na hakuwa na la kusema,” kilisema chanzo chetu.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, SACP Mihayo Msikhela (pichani) alipoulizwa na gazeti hili kuhusu kukamatwa kwa mzee Akida na Juma hakukiri wala kukataa.

“Unajua hili jambo bado lipo kwenye uchunguzi, hatuwezi kusema chochote hadi tumalize uchunguzi wetu lakini wote wanaotuhumiwa tunawasaka na tukiwakamata tutawahoji. Tukimaliza upelelezi wetu tutatoa taarifa kwa umma,” alisema kamanda huyo.
 
ndo hivyo ukikubali upunda inakula kwako bora ulime kijijini kwenu upate hela za halali
pia inaweza kuwa ni story ya kutungwa na hao jamaa zenu wa kitengo to create deterrence kwa vijana kuachana na biashara hii haramu, yote mawili yanawezekana pia. trillion moja is the hell of money, ni pesa nyingi sana sana
 
yep unaweza kujifunza tu kuwa hii bisashara ya ngada siyo nzuri unatengeneza akili yako sio lazima kila kilichoadikwa kwenye hiyo story ni 100% sure..............
 
huh kazi ipo trilion moja
Kama naona maruweruwe na siamini kinachoendelea. Trillioni moja zilipwe kwa wauza unga ili mateka aachiwe!!? Hii biashara itakuwa ya aina yake, yaani polisi itasimamia jinsi ya kuzifikisha hizo pesa au watamtuma mtu azipeleke ili mateka wetu aachiwe na wauza unga!!?
 
hahaha tr=ilon moja ngoja nimgoogle huyu mdaiwa nipate hata picha yake anafananaje kuwa na deni la trl 1 ......
 
Maajabu mtuhumiwa wa madawa ya kulevya tena aliyekamatwa na askari yupo mtaani anakula maisha, napata shida kuamini taarifa hii, ina maana askari wakikukamata na madawa ya kulevya hupelekwi Jela tena kutumikia kifungo au mahabusu zimejaa??
 
Ngoja leo nipitee kwA wanangu mtaa wa dosi,migomigo
 
kumbe unga unalipa eeeh
Unga una pesa kaka...
Nikupe mfano hai wa dada mmoja ambae ni mtu wa karibu san kwangu.
Alikua ananunua G mbili kwa siku G-ni kipimo cha kununulia hayo madawa, kila G ilikua ni 45,000/= alaf yeye anafunga kete za sh elfu mbili mbili, so kwa G moja ikua anaingiza kama 78000/= hivyo ukitoa bei ya manunuzi anapiga 35000/= kama faida ya jumla , hivyo kwa G mbili alikua anaingiza kwa siku 70000/= pimia kwa mwezi anaingiza bei gan. Tena huyo ni muuzaji wa hali ya chini sana...
Sasa hao wanaouza kwa kila cjui wanapata faida kiasi gan kwa maana hio G yenyewe ni kama viji-iliki viwili tu...
 
pia inaweza kuwa ni story ya kutungwa na hao jamaa zenu wa kitengo to create deterrence kwa vijana kuachana na biashara hii haramu, yote mawili yanawezekana pia. trillion moja is the hell of money, ni pesa nyingi sana sana
Kiukwel huyo jamaa wa pakistan kuzuiwa ni ukweli na juzkati polisi walivamia nyumba ya juma kigambon lakini hawakumpata ...
KUHUSU HIZO TRILION MOJA, BINAFSI NAONA NI JAHU TU, HIV WATU WANACHUKULIA POA TRILION MOJA EEENH, UKITAKA KUZIONA NYINGI SEMA NI BILIONI ELFU MOJA
 
Back
Top Bottom