Madagascar wapata dawa ya asili ya Corona

Madagascar wapata dawa ya asili ya Corona

RAIS WA MADAGASCAR ATANGAZA KUWA MADAGASCAR IMEGUNDUA TIBA YA CORONA: WHO YAPINGA VIKALI DAWA HIYO

Wakati wanasayansi duniani wakihangaika kupata chanjo na tiba ya virusi vya corona, Rais wa Madagascar Andry Rajoelina amezindua dawa ya mitishamba inayotibu' COVID-19.

Hata hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) na Marekani wamepinga vikali tiba hiyo ya COVID-19 baada ya Rais Rajoelina kutangaza dawa hiyo. WHO na Marekani imeitaka Madagascar kukoma kuendelea na matumizi ya dawa hiyo mara moja na endapo itakaidi kuacha matumizi ya dawa hiyo huenda Shirika hilo la Afya Duniani na Marekani zikalazimika kutoipatia msaada zaidi wa kupambana na janga la Corona.

Taasisi ya taifa ya tiba nchini Madagascar (Anamem) pia imepinga matumizi ya dawa hiyo inayoelezewa na Rais Andry Rajoelina kama yenye uwezo wa kuzuia na kuponyesha corona.

Taasisi hiyo imesema kuwa mitishamba inaweza kudhuru afya ya mtu kwani "hakuna ushahidi wa ufanisi wake kisayansi".

Mmea huo unatarajiwa kutolewa bure kwa watu wenye uwezekano mkubwa wa kuathiriwa na na virusi vya corona.

Ikizinduliwa kwa jina Covid-Organics, dawa hiyo imetengenezwa kutoka kwa mmea artemisia (pakanga) ambao ni mojawapo ya miti ambayo huchanganywa pamoja na mimea mingine ya Madagascar kama tiba ya ugonjwa wa Malaria. Mmea huo ni tiba maarufu ya malaria nchini Madagascar na kwa muda mrefu umetumika kutibu malaria kwa mafanikio makubwa.

Dawa hiyo imepakiwa kwenye chupa na kutangazwa kama chai ya miti shamba baada ya kujaribiwa kwa watu 20 kwa kipindi cha wiki tatu, katibu wa Rais Lova Hasinirina Ranoromaro ameiambia BBC.

Baada ya janga la Corona kutangazwa duniani, Rais aliwataka watafiti kuja na tiba ambayo kwa bahati nzuri 'waliipata kwamuda muafaka'.

"Vipimo vimefanyika na tayari wagonjwa wawili wa COVID-19 wamekwishapona kutokana na tiba hii," Bwana Rajoelina alisema katika uzinduzi wa Covid-Organics uliofanyika katika taasisi ya utafiti ya Madagascar- Malagasy Institute of Applied Research (Imra), ambayo ndiyo iliyotengeneza dawa hiyo ya mitishamba.

"Kinywaji cha dawa hii ya mitishamba huonesha matokeo katika kipindi siku saba," alisema Rais huyo mwenye umri wa miaka 45, ambaye aliwataka watu kuitumia kama hatua ya kujikinga na kujitibu ugonjwa wa corona.

Dkt Charles Andrianjara, Mkurugenzi mkuu wa taasisi ya utafiti ya Imra, anaafiki kuwa Covid-Organics inapaswa kutumiwa kama kinga.
Lakini alijihadhari zaidi kuzungumzia zaidi juu ya matumizi ya dawa hiyo kama tiba, lakini akasema kwamba uchunguzi wa kimatibabu umeonyesha "dalili ya ufanisi wake kama tiba", shirika la habari la AFP lilimnukuu akisema.

Kisiwa hicho cha Bahari ya Hindi kimekwisharekodi hadi sasa wagonjwa 121 wa virusi vya corona, na hakuna vifo kutokana na ugonjwa huo hadi sasa.

WHO YAPINGA DAWA HIYO, YASEMA 'HAKUNA NJIA ZA MKATO'

Ikizungungumzia uzinduzi wa Covid-Organics, WHO imeambia BBC kwamba shirika hilo la dunia halishauri "matibabu ya kibinafsi ya dawa zozote... kama njia ya kinga au tiba ya Covid-19."

Lilirejelea kauli za mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ambaye ni raia wa Ethiopia kwamba "hakuna njia za mkato" za kutafuta dawa ya kupambana na virusi vya corona. Majaribio ya kimataifa yanaendelea kupata tiba yenye ufanisi , WHO iliongeza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IKWETA KONZO M, Usikurupuke wakati wa kutoa taarifa kichwa cha habari umesema CHANJO nani umesema DAWA kiuhalisia hiyo SI chanjo ila ni dawa kama taarifa yak ilivyoeleza inaelekea hukuisoma hata wewe mwenyewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pumbavu WHO....Sasa wanategemea WHO ikubali kua kapata Tiba wakati wao wako na shetani bill gates anaforce chanjo kupitia huu ugonjwa..eti kisayansi...nyooooo.....kooo...apa Kama dawa inatibu hatuhitaji approve ya WHO..and for sure they don't need anyone to have vaccine or cure of this shit for this time untill population reduced to maximum..
 
Waafrica Kwa waafrica hatuaminiani, cheki tu post za wadau wanavyoponda uvumbuzi wa dawa wa nchi ya waafrica wenzetu, waje watuamini Wazungu na WHO? Waafrica sjui mnakula maharage ya wapi nyie?

Ukiwa maskini sio kigezo cha kukosa kila kitu, Pumbavu Sana wanaoshabikia na kuwatukuza wazungu! Ndiyo Maana watoto wetu wanaletewa michanjo mashuleni isiyoeleweka, akiri itakapokuja kuturudia, Wachina walishatuletea na dawa za kuongeza akiri!!

Mnaletewa midawa ya kuongeza matako dada zenu, wake zenu eti mnaona ni akiri njema za wazungu?
Pumbavu!!

Penda vya kwenu, wapende wa kwenu, wazungu sio Alfa na omega bhana
 
Kama inatibu wanataka scientific proof zipi si ndo proof hiyo kuwa watu wanapona
 
Marais wa Afrika ni nani aliyewaroga?
Kuwaloga katika lipi mkuu?

Kwa sababu nchi zao hazitakiwi kufanya utafiti wa chanjo wala tiba za magonjwa siyo?

Mkuu au na wewe ni wale wale WHO wabaguzi na hawaziamini nchi zetu za Africa Kwa kila kitu, Kama wewe sio wao, Anza kupenda vya kwenu sio kutukuza Wazungu, wanaotuona nusu watu, nusu Nyani, myeusi mingine bhana
 
Back
Top Bottom