Kwanini huu uwanja umejengwa huku maporini?
Huu ni Uwanja mpya wa michezo (sio football pekee) unaojengwa mkoani Arusha kwa ajili ya michuano ya AFCON. Ni uwanja wa kisasa. Kabla ya Ujenzi ilidaiwa utakuwa uwanja wa kisasa kuliko yote Afrika Mashariki, lakini kwa namna ulivyo sasa, sio rahisi kuamini ndio uwanja wa kisasa kuliko vyote; labda tusubiri tuone ubunifu wa kiteknolojia pindi utakapokamilika.
Turudi kwenye swali la msingi, kwanini huu uwanja ujengwe huku maporini?
Nimesoma maoni ya baadhi ya mashabiki wa soka kutoka nje ya Tanzania, wako na wasiwasi sana kuhusu mazingira na upatikanaji wa huduma za kijamii huku maporini.
Na kwa sasa, sidhani kama kuna muda wa kutosha kuhakikisha hiyo miundombinu itajengwa na kukamilika!
Vipi kuhusu miundombinu ya Starehe na buduma za vyakula! Mfano Baa, Migahawa na Vilabu vya starehe. Michezo huambatana na starehe na burudani. Kwa muda uliobakia, sioni uwezekano wa kujenga hiyo miundombinu. Labda kujengwe vibanda vya muda.
Pia, sioni mwekezaji wa kujenga miundombinu ya kudumu kwenye hili eneo kwa ajili ya mechi chache (pengine zisizofika kumi), tena kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja.
Nauona huu uwanja ukizungukwa na vibanda vya Mama ntilie, na machinga wakipanga jezi za timu barabarani kwenye mavumbi.
Kuna mpango gani baada ya AFCON?
Huu uwanja haujajengwa kwa ajili ya Football peke yake. Ni uwanja kwa ajili ya michezo mingi, ndio maana kuna runways na eneo kubwa la ardhi (ground) nje ya pitch ya football. Swali ni Je! hiyo michezo ipo? Na Je! Hiyo michezo itarudisha fedha zilizotumika? Au kuna shughuli yoyote itakayoingiza fedha kupitia huu uwanja kurudisha gharama zilizotumika?
Au sio lengo la mradi kurudisha gharama zilizotumika?
Ushauri wangu;
Katika mazingira ya sasa, na kwa kuzingatia hali za kiuchumi za wananchi na tabia zao, mradi kama huu ni WHITE ELEPHANT. Ni mradi ambao hauwezi kurudisha fedha zilizotumika. Na zaidi ni mradi ambao upo mbali nje ya mji kwahiyo unapunguza hamasa ya kuutumia.
Arusha kuna uwanja wa Sheikh Amri Abeid (unatajwa kuwa uwanja wa CCM, lkn ni uwanja wa umma kwa sbb ulijengwa kwa fedha za umma enzi za chama kimoja).
Hekima ingetumika kuuboresha Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, ufikie viwango vya CAF; kuweka majukwaa ya kisasa, miundombinu ya kisasa ndani ya uwanja, na ikibidi kuongeza capacity ya mashabiki (ubaki kuwa uwanja wa football pekee), kisha mazingira ya nje kama barabara yangeboreshwa na kuwa ya kisasa.
Kwanza ingetumika fedha kidogo, na pili ingevutia wawekezaji wakubwa kujenga mahoteli na/au appartments karibu na uwanja, kwa sababu ni eneo ka mjini na biashara ipo hata baada ya AFCON.
Sidhani kama uamuzi wa kujenga uwanja wa bilioni 300+ eneo la porini kama huku ulikuwa uwamuzi sahihi. Huu ni mradi mkubwa, umetumia fedha nyingi ambazo hazirarudi, na uwanja hautatumika ipasavyo. Hata kwa vilabu vya ligi kuu vitakavyotumia huu uwanja, vitapata shida kuingiza mashabiki wa kutosha!
Nawasilisha!
Dr. Chris Cyrilo.