Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Taarifa za awali zinaeleza kuwa ndege aina ya Let L-410 yenye namba za usajili 9S-GUC imepata ajali mjini Kenge, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), siku ya Ijumaa, Septemba 25, 2026, huku taarifa zikidai kuwa watu 13 wamepoteza maisha.

Kwa mujibu wa taarifa zinazozunguka kuhusu orodha ya abiria na wafanyakazi waliokuwa ndani ya ndege hiyo, jina la Luteni Jenerali Mutombo Katalay Tiende Joseph, ambaye ni Mkuu wa Kwanza wa Mahakama Kuu ya Kijeshi ya DRC, limetajwa miongoni mwa waliokuwemo katika ndege hiyo.

Taarifa rasmi za awali zinazopatikana pia zinamtaja Mutombo Katalay Tiende Joseph kama Mkuu wa Kwanza wa Mahakama Kuu ya Kijeshi.

Aidha, hati ya safari ya kikazi ya tarehe 19 Agosti 2026 inadaiwa kuonyesha kuwa ujumbe huo uliongozwa na Luteni Jenerali Mutombo Katalay Tiende Joseph.

Miongoni mwa maafisa wengine waliotajwa katika ujumbe huo ni Luteni Jenerali Likulia Bakiumi Lucien René, Meja Luntala Kibanzidi Albert na Kapteni Mbuku Pasipamba, pamoja na maafisa wengine.

Hata hivyo, utambulisho wa waathirika wa ajali hiyo bado haujathibitishwa rasmi na mamlaka husika. Hivyo, majina yaliyotajwa katika orodha hizo yanapaswa kuchukuliwa kama taarifa za awali hadi pale mamlaka za DRC zitakapotoa uthibitisho rasmi.
1790358273383.jpg
 
According to JC EXPLORER..... ndege za kisasa zina mfumo wa flaps. Ambazo zinavuta ndege nyuma ili kupunguza kasi ya mwendo na upepo... flaps zinapatikan kwenye mabawa. Kama dreamliner za air tanzania au BOEING 777-300ER.
 
Unapoitazama anga kutoka ardhini, linaweza kuonekana kuwa kubwa na lisilo na mipaka. Lakini nyuma ya safari ya kila ndege kuna mfumo maalum wa njia za angani zilizopangwa na kudhibitiwa kwa umakini mkubwa ili kuhakikisha ndege zinafika salama kutoka sehemu moja hadi nyingine.

Ndege haziruki tu katika mwelekeo wowote zinapotaka. Zinafuata njia maalum zinazojulikana kama 'Airways au Air Corridors, ambazo zimeainishwa na mamlaka za usafiri wa anga kwa ajili ya kupanga na kudhibiti mtiririko wa ndege.

Moja ya mambo muhimu katika mfumo huo ni urefu wa ndege angani. Njia za ndege hutenganishwa kwa viwango tofauti vya urefu vinavyojulikana kama Flight Levels.

Kwa mfano, ndege inaweza kuwa katika Flight Level 330, sawa na takribani futi 33,000, huku nyingine ikiwa Flight Level 370, takribani futi 37,000.

Hivyo, ndege zinaweza kupita katika eneo moja la anga bila kuwa katika kiwango kimoja cha urefu, jambo linalosaidia kupunguza hatari ya migongano.

Lakini si urefu pekee unaoongoza safari. Ndege pia hutumia Waypoints, ambazo ni sehemu maalum zilizowekwa kwenye mfumo wa urambazaji wa anga (Air Navigation).
Rubani na mifumo ya ndege hutumia taarifa hizi kufuata njia iliyopangwa kutoka wakati wa kuondoka hadi kufikia eneo la kutua.

Katika safari hiyo, waongiza ndege 'Air Traffic Control (ATC) huwa na jukumu muhimu la kufuatilia na kupanga mienendo ya ndege angani. Waongoza ndege huwapa marubani maelekezo kuhusu mwelekeo, urefu na mabadiliko ya njia pale inapohitajika, kulingana na hali ya anga na msongamano wa ndege.

Jambo jingine linalozingatiwa ni hali ya hewa na matumizi ya mafuta. Njia ya ndege inaweza kubadilishwa ili kuepuka maeneo yenye dhoruba, upepo mkali au hali nyingine hatarishi. Wakati mwingine, ndege pia hupanga njia zinazoweza kunufaika na upepo wa juu angani, ikiwemo jet streams, ili kupunguza muda wa safari na matumizi ya mafuta.

Kwa hiyo, kila unapouona ndege ukipita juu yako, ujue kuwa nyuma ya safari hiyo kuna mfumo mkubwa wa urambazaji, mawasiliano, teknolojia na udhibiti wa anga.

Anga linaweza kuonekana kuwa wazi na lisilo na mipaka, lakini kwa ndege, kuna “barabara” zisizoonekana ambazo zinahitaji kufuatwa kwa usahihi mkubwa ili kuhakikisha usalama wa safari.
1790419406329.jpg
 
1790457205376.jpg
 
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imesimamisha mara moja Cheti cha Uendeshaji Ndege (AOC) cha TRACEP Congo Aviation, kufuatia ajali ya ndege aina ya Let 410 UVP iliyotokea Ijumaa karibu na Kenge, mkoani Kwango.

Ajali hiyo, iliyohusisha ndege yenye usajili 9S-GUC, ilisababisha vifo vya watu 17, wakiwemo abiria 13 na wafanyakazi wanne, pamoja na maafisa wawili wa ngazi za juu wa kijeshi.

Kwa mujibu wa Wizara ya Uchukuzi ya DRC, shughuli zote za TRACEP Congo Aviation zimesimamishwa nchini kote hadi kukamilika kwa uchunguzi unaoendeshwa na BPEA, chombo kinachohusika na uchunguzi wa ajali za anga.
1790485588217.jpg
 
Kuanzia Oktoba 1, 2026, wasafiri wa kigeni wanaoingia Tanzania Bara kupitia viwanja vya ndege, bandari au mipaka ya nchi watahitajika kuwa na bima ya lazima ya safari (Inbound Travel Insurance) yenye gharama ya Dola 44 za Marekani kwa mtu mmoja.

Kwa mujibu wa Government Notice No. 256, iliyochapishwa katika Gazeti la Serikali tarehe Septemba 4, 2026, bima hiyo itatolewa kupitia National Insurance Corporation (NIC) na itakuwa na uhalali wa hadi siku 92.

Bima hiyo itagharamia huduma mbalimbali ikiwemo matibabu ya dharura, uokoaji wa kitabibu, kurejeshwa kwa mgonjwa au mwili wa marehemu, pamoja na upotevu wa mizigo.

Hata hivyo, raia wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wameondolewa kwenye sharti hilo.
1790489517976.jpg
 
Back
Top Bottom