Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Zanzibar (ZAA) imetoa ufafanuzi kuhusu madai ya wizi wa mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume (AAKIA), katika taarifa yake iliyotolewa mnamo tarehe 11 Februari 2026.

Mkurugenzi Mkuu wa ZAA, Ndugu Seif Abdalla Juma, amekanusha madai hayo na kusisitiza kuwa si sahihi.

Uchunguzi wa kina uliofanyika na kamati maalumu iliyoundwa na ZAA, haikupata ushahidi wa moja kwa moja unaothibitisha kuwepo kwa vitendo vya wizi wa mizigo ndani ya uwanja huo ambapo mizigo mingi iliyokuwa imefunguliwa au kuharibika ilibainika kuwa ilifanyika kabla ya kuwasili Zanzibar.

ZAA imechukua hatua za ziada za usalama, ikiwemo kumtaka mtoa huduma ardhini (ground handler) kuweka kamera maalum ndani ya ndege na kuwapatia wapakuzi wa mizigo kamera maalum za kuvaa mwilini (Body Cam).

Mamlaka inawahimiza wananchi na wasafiri kuzingatia taratibu za kiusalama na kuepuka kusambaza taarifa ambazo hazijathibitishwa.
1770922540038.jpg
 
Mnamo Tarehe 11 Februari 2026, wafanyakazi watatu wa shirika la ndege la British Airways walilazwa hospitalini mjini Los Angeles baada ya kula peremende zenye madawa ya kulevya aina ya bangi zilizotolewa na abiria mmoja katikq safari ya kutoka London Heathrow kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles.

Taarifa inasema, Peremende hizo zilikuwa na 300mg ya THC na kusababisha mmoja wa wahudumu hao wa ndege kueleza kuwa alihisi "kuwa nje ya mwili wake".

Wafanyakazi hao walitangazwa kuwa hawafai kuendelea na kazi kwa wakati huo, na hivyo kusababisha shirika la ndege kutuma timu nyingine kuchukua nafasi yao kwa safari ya kurudi.
Wahudumu hao watatu walirudi London kama abiria.

British Airways imeanzisha uchunguzi wa ndani ili kubaini jinsi peremende hizo zilifikaje kwa wafanyakazi hao.

Shirika la ndege limethibitisha kuwa hakukuwa na athari kwa abiria na limesisitiza kuwa sera zake za dawa na pombe ni kali.
1771112353677.jpg
 
Thomas Salme, raia wa Sweden, alifanya kazi kama rubani wa ndege za abiria za kibiashara kwa zaidi ya miaka 10 kwa kutumia hati za kughushi za urubani.

Salme alianza kazi yake mwaka 1997 na kampuni ya ndege ya Italia Air One kama rubani msaidizi, na baadaye akawa nahodha wa ndege za Boeing 737 akikusanya zaidi ya saa za ndege 10,000 na kusafirisha maelfu ya abiria bila kusababisha tukio au ajali.

Hata hivyo, mpango wake uligunduliwa Machi 2010 wakati mamlaka za Uholanzi zilipopokea taarifa kuhusu hitilafu katika rekodi zake za leseni.

Salma alikamatwa akijiandaa kurusha katika ndege ya Corendon Airlines na baadaye kukiri kosa lake.

Mahakama ya Uholanzi ilimpa adhabu ya faini na kifungo jela kwa kosa la udanganyifu na kurusha ndege bila leseni halali.

Katika Kisa kingine....

William Chandler, rubani mkuu wa ndege wa shirika la ndege la Afrika Kusini (SAA), aliruka kwa zaidi ya miaka 20 kabla ya udanganyifu wake kugunduliwa mwishoni mwa 2018.

Chandler alikuwa na leseni halali ya urubani wa kibiashara (CPL), ambayo ilimruhusu kuruka, lakini alighushi leseni kubwa ya urubani wa usafiri wa anga (ATPL) - Leseni yaa kiwango cha juu kinachohitajika kwa safari za kimataifa za masafa marefu.

Inatajwa kuwa, Chandler alikataa kupandishwa cheo kuwa nahodha kwa miaka mingi kwa sababu jukumu hilo lingemhitaji kuwasilisha cheti chake cha ATPL (kilichoghushiwa) kwa uthibitishaji.

Hata hivyo udanganyifu huo uligunduliwa kufuatia "tukio la kuripotiwa" wakati wa safari kutoka Johannesburg kwenda Frankfurt mnamo Novemba 2018, ambapo ndege ilifanya "kona za ajabu" baada ya kukutana na misukosuko juu ya Milima ya Alps ya Uswisi.

Chandler alijiuzulu mapema 2019 mara tu uchunguzi ulipoanza.

SAA iliwasilisha mashtaka ya uhalifu kwa kosa la udanganyifu na kujaribu kupata milioni za mshahara na posho zilizolipwa kwake kwa njia ya udanganyifu.
1771168266678.jpg
 
Dario Costa, Rubani wa Red Bull, amefanya historia katika usafiri wa anga kwa kutua ndege yake kwenye treni linalosonga kwa kasi ya kilomita 120 kwa saa, na kisha kupaa tena kutoka kwenye treni hilo.

Hii ni mara ya kwanza kwa ndege kutua na kupaa kutoka kwenye treni linalosonga kwa kasi hiyo.

Costa alitumia ndege yake aina ya Zivko Edge 540, na alitumia muda wa sekunde 50 tu, wakati ambapo alilazimika kupambana na upepo mkali.

Kwa mujibu wa taarifa, Costa alifanya mazoezi ya kutua kwenye treni linalosonga kwa muda wa siku tatu huko Pula Airport, Croatia, kwa kutumia gari la Rimac Nevera R kama jukwaa la kumbukumbu ya uhalisia wa tukio hilo.

Picha;
Redbull
 
"Vibe la Chaka"

Tukio la kuvutia likionesha Simba wakiwa wamelala katika hali ya amani na utulivu
chini ya kivuli cha ndege ya kampuni ya Auric Air Services katika Uwanja wa ndege wa Kikoboga Airstrip katika Hifadhi ya mbuga Mikumi.
1771681193585.jpg
 
Dario Costa, Rubani wa Red Bull, amefanya historia katika usafiri wa anga kwa kutua ndege yake kwenye treni linalosonga kwa kasi ya kilomita 120 kwa saa, na kisha kupaa tena kutoka kwenye treni hilo.

Hii ni mara ya kwanza kwa ndege kutua na kupaa kutoka kwenye treni linalosonga kwa kasi hiyo.

Costa alitumia ndege yake aina ya Zivko Edge 540, na alitumia muda wa sekunde 50 tu, wakati ambapo alilazimika kupambana na upepo mkali.

Kwa mujibu wa taarifa, Costa alifanya mazoezi ya kutua kwenye treni linalosonga kwa muda wa siku tatu huko Pula Airport, Croatia, kwa kutumia gari la Rimac Nevera R kama jukwaa la kumbukumbu ya uhalisia wa tukio hilo.

Picha;
Redbull
Hiyo ndege inapaa between 110-130 km/h kawaida, so kama treni ilikuwa inakwenda 120km/h, maana ni kwamba ilishafikisha take off speed ikiwa juu ya treni.
 
Helikopta ya UH-60 Black Hawk ya Walinzi wa Kitaifa wa Mexico ilipigwa risasi na wahusika wa genge la wauza biashara wa dawa za kulevya (Cartels) huko Jalisco wakati wa operesheni iliyolenga kiongozi wa kundi hilo, El Mencho.

Ndege hiyo ilipata uharibifu mkubwa, ikiwa na mashimo ya risasi kwenye bodi (Fuselage) na matairi, lakini iliweza kutua salama bila kusababisha majanga kwa wafanyakazi.

Operesheni hiyo ilikuwa ni pamoja na vikosi vya usalama vya Mexico na vya upelelezi wa Marekani, na ilisababisha kifo cha El Mencho, kiongozi wa kundi la CJNG.

Hata hivyo, makundi hayo yameanzisha mashambulizi ya kulipiza kifo hicho, yakichoma magari na kushambulia walinzi wa kitaifa, na kusababisha vifo vya walinzi 25 na watu wengine kadhaa.
1772255304541.jpg
 
Ndege ya kijeshi ya Bolivia, Hercules C-130, imepata ajali jioni ya Ijumaa ya tarehe 27 Februari katika jiji la El Alto, na kusababisha vifo vya watu angalau 15 na kuibua ghasia kubwa baada ya pesa zilizokuwa ndani ya ndege hiyo kutawanyika eneo la ajali.

Ajali hiyo ilitokea karibu na Uwanja wa Kimataifa wa El Alto, ambapo ndege hiyo ilipoteza mwelekeo au kushindwa kupaa wakati wa kuondoka, na kuanguka kwenye barabara ya Costanera, eneo lenye shughuli nyingi za magari.

Ndege hiyo ilikuwa inasafirisha pesa mpya za Benki Kuu ya Bolivia (BCB) ndani ya nchi, na baada ya ajali, pesa hizo zilitawanyika kila mahali, na kusababisha vurugu kubwa.

Watu walikimbilia kukusanya pesa hizo, na kufanya kazi za uokoaji kuwa ngumu

Serikali ya Bolivia imesema kuwa uchunguzi wa ajali hiyo unaendelea, na sababu za ajali hiyo hazijulikani bado.

Uwanja wa Kimataifa wa El Alto ulifungwa kwa muda baada ya ajali hiyo, na kusababisha usumbufu wa shughuli za ndege
1772258047629.jpg
 
Uwanja wa Kimataifa wa Kuwait umeshambuliwa na 'drone' ya kujitoa muhanga ya Iran, na kusababisha majeruhi madogo kwa wafanyakazi kadhaa na uharibifu mdogo wa miundombinu ya uwanja wa ndege.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Kuwait ilianzisha taratibu za dharura na kuthibitisha kuwa hali imetulia.

Baadhi ya ripoti zilizotolewa zinaonyesha kuwa shughuli za uendeshaji ndege zimesimamishwa kwa muda na abiria wametakiwa kuondoka uwanjani.

Serikali ya Kuwait imemwita balozi wa Iran kuelezea malalamiko yake dhidi ya shambulizi hilo.

Shambulizi hilo linajumuisha sehemu ya mzozo mkubwa zaidi katika Mashariki ya Kati, ambapo Marekani na Israel zimefanya mashambulizi dhidi ya Iran, na kusababisha mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa njia ya 'drone' dhidi ya kambi za Marekani katika nchi za Ghuba.
1772333996369.jpg
 
Ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-15E Strike Eagle imeanguka magharibi mwa Kuwait asubuhi ya Jumatatu ya leo, Machi 2, 2026.

Video hiyo iliyosambaa mtandaoni inaonesha ndege hiyo ikiwaka moto injini huku ikianguka kwa mzunguko usiodhibitika (Flat Spin)

Rubani wa ndege hiyo na afisa wa mifumo ya silaha (Weapons system officer) walifaulu kujifyatua nje (Ejected) kwa usalama kabla ya ndege hiyo kuanguka.

Video zilizosambazwa mtandaoni zinaonyesha rubani akiwa salama chini akisafirishwa kwenye gari baada ya kujifyatua nje ya ndege na mwamvuli.

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijathibitishwa rasmi, lakini kuna uvumi kuwa inaweza kuwa kutokana na hitilafu ya kiufundi, injini kushika moto au hata kushambuliwa kwa bahati mbaya na mfumo wa anga wa Patriot (friendly fire)

Ajali hii inatokea wakati mvutano wa kijeshi katika eneo la Ghuba ya Persia umeongezeka, huku taarifa za mashambulizi ya kombora na ndege zisizo na rubani zikizidi

 
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, amekagua mradi wa ujenzi wa Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) jijini Dar es Salaam na kusisitiza umuhimu wake katika kuimarisha sekta ya usafiri wa anga nchini.
Mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 78 uko katika hatua ya awali, umefikia asilimia 10.3 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu.

Prof. Mbarawa alisema Serikali imefanya maendeleo makubwa katika sekta ya anga, ikiwemo ujenzi wa viwanja vya ndege na ununuzi wa ndege, na sasa inaendelea kuimarisha miundombinu ya mafunzo ya sekta ya anga ili kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), Bw. Salim Msangi, alisema mradi huo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha uwezo wa ndani katika mafunzo ya Usafiri wa anga, sambamba na miongozo na matakwa ya ICAO.
1772645832361.jpg
 
Back
Top Bottom