Mada maalum ya ndege toka FB

Mada maalum ya ndege toka FB

Mach Loop au Machynlleth Loop ni eneo maarufu nchini Wales linalotumiwa na ndege za kijeshi kufanya mazoezi ya kuruka chini na kwa kasi kubwa.

Eneo hili lilipo kati ya Dolgellau na Machynlleth, linajulikana kwa changamoto za ndege kuruka kati ya milima na mabonde.

Ndege kama Eurofighter Typhoons, F-15, F-35 na nyinginezo mara nyingi hufanya mazoezi hapa, na kuifanya kuwa sehemu maarufu kwa wapenzi wa usafiri wa anga kwenda kuketi kwenye milima na kunasa picha za ndege za kuvutia.
1773654069505.jpg
 
B-21 Raider ni ndege mpya ya kivita ya siri ya Marekani yenye uwezo wa kuruka bila kugunduliwa kirahisi na mifumo ya ulinzi (Radar)
Ndege hiyo ya kizazi cha sita imeundwa kiasili kwa ajili ya kuingia katika maeneo yenye ulinzi mkali na kufanya mashambulizi ya karibu.

Tofauti na mtangulizi wake, B-2 Spirit, B-21 Raider ni ndogo na gharama nafuu, ikitajwa kugharimu dola milioni 550 hadi 690 kwa kila ndege, ikilinganishwa na dola bilioni 2 kwa B-2 Spirit.

B-21 ina uwezo wa kubeba silaha za kawaida na za nyuklia, na inaweza kusafiri kwa umbali mrefu.

Teknolojia yake ya siri inajumuisha matumizi ya vifaa vya kufyonza mawimbi ya rada (Radar absorbing material & Equipments) na muundo wake wa programu ya wazi (open architect software) unaruhusu maboresho ya haraka na ya gharama nafuu.

Tofauti nyingine kati ya B-21 na B-2:

Ukubwa:
B-21 ni ndogo, na urefu wa mita 140, ikilinganishwa na mita 172 za B-2.

Gharama:
B-21 ni ya gharama nafuu, ikigharimu dola milioni 550, ikilinganishwa na dola bilioni 2 kwa B-2.

Injini:
B-21 ina injini mbili, ikilinganishwa na injini nne za B-2.

Uwezo wa Kubeba Silaha:
B-21 inaweza kubeba hadi tani 13 za silaha, ikilinganishwa na tani 27 za B-2

B-2 na B-21 ni ndege zinalindwa na usiri mkubwa wa teknolojia inayotumika malighafi, muundo na programu zinazoendesha hivyo kupatikana taarifa chache kuhusu uwezo wake kamili.
1773748829676.jpg
 
Helikopta ya Air Dynasty yenye nambari ya usajili 9N-AFQ ilipata ajali wakati wa kutua katika eneo la Khotang, huko Nepal.

Helikopta hiyo ilikuwa imebeba watu sita, ambapo watu wawili walijeruhiwa.

Ajali hiyo ilitokea saa 5 asubuhi Machi 18, wakati helikopta hiyo ikitua na kupoteza udhibiti ghafla ikionekana kuzolewa na upepo.
Watu wote walio ndani ya helikopta walipata msaada, na mmoja wa majeruhi alipelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ajali hiyo inaweza kusababishwa na upepo mkubwa na vumbi lililotanda wakati wa kutua.
1773907439648.jpg
 
Ndege ya China Southern Airlines, aina yaAirbus A330-300 yenye usajili B-1062, ilipata ajali ya kugongana na ndege hai mara baada ya kupaa kutoka Uwanja wa Kimataifa wa Shanghai Hongqiao.

Ajali hiyo ilitokea tarehe 21 Machi 2026 wakati ikisafiri kuelekea Shenzhen katika usawa wa futi 4,600.

Athari ya mgongano huo ilisababisha kupasuka kwa mfuniko wa rada (radome) mbele ya ndege.
Rubani alitangaza dharura mara moja na kurudi kutua salama kwenye uwanja wa Hongqiao baada ya dakika 20.

Hakukuwa na majeruhi yaliyoripotiwa miongoni mwa abiria au wafanyakazi.

Shirika hilo la China Southern lilipanga safari na ndege nyingine ya Boeing 777-300 ili kukamilisha safari hiyo ya kwenda Shenzhen, lakini ilichelewa kwa takika saa nne.

Ndege iliyoharibiwa ilibaki chini kwa ukaguzi na matengenezo.
1774110761641.jpg
 
Hapa kuna aina mbili za mafuta ambayo ndege nyingi hutumia.
Je, unaweza kutqlambua mafuta hayo kwa mujibu wa mtambo huu (Oil refinery plant)
1774191641344.jpg
 
Helikopta ya kijeshi ya Qatar imetajwa kupata ajali baharini kwenye pwani ya nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu sita.

Helikopta hiyo ilikiwa imebeba watu saba ilipata hitilafu ya kiufundi wakati wa misheni ya kawaida.

Tukio hilo limetokea siku ya jumapili Machi 22, 2026 katika eneo la bahari ya Qatar katika Ghuba ya Uajemi.
Wizara ya Mambo ya Ndani imethibitisha vifo sita, na mtu mmoja bado anatafutwa.

Wizara ya Ulinzi imesema kuwa helikopta hiyo ilipata hitilafu ya kiufundi wakati wa misheni ya kawaida.

Timu maalumu zimeanza operesheni ya utafutaji na uokoaji ili kumtafuta mtu aliyekosekana.

Hakuna ushahidi wa kuunganisha ajali hiyo na mgogoro wowote unaendelea katika eneo hilo.
1774198242957.jpg
 
Kuna taarifa zilizoenea kuhusu ndege a kijeshi a Israel aina ya F-16i kudunguliwa nchini Irani.

Vikosi vya Ulinzi vya Mapinduzi vya Kiislamu (IRGC) vilichapisha asubuhi ya Jumamosi, Machi 21, 2026, kwamba mifumo yao ya ulinzi ya anga ililenga na kuangusha F-16 ya Israel kwnye anga ya Irani.

IRGC ilisema ndege hiyo ilipigwa saa 3:45 asubuhi na inakuwa ndge ya tatu ya kivita ya adui kudungua tangu waliyoipiga tangu kuanza kwa mgongano huo.

Jeshi la Israel halijathibitisha kupoteza F-16, lakini nyingine zilisema kuwa moja ya ndege zao ilishambuliwa na ulinzi wa anga wa Irani lakini zinasisitiza kuwa ndege hiyo haikuangushwa na ilirudi salama nyumbani.

Madai haya yanafuatia taarifa nyingine juu za mapigano ya anga katika eneo hilo ambapo ndege ya kijeshi ya kizazi cha tano ya Marekani aina ya F-35 ilipata hitilafu inayotokana na moto mnamo Machi 20, 2026.

Marekani ilithibitisha kuwa F-35 ilitua kwa dharura kwenye kituo cha kijeshi cha kikanda baada ya kupata uharibifu unaotokana na moto unaoshukiwa kuwa kombora la Irani.
1774199176949.jpg
 
Uzembe mkubwa sanq

Ndege ya Air India (AI185) kutoka Delhi kuelekea Vancouver ililazimika kurudi katikati ya safari baada ya kugundua kuwa ndege iliyotumika, Boeing 777-200LR, haikuwa na kibali cha kuingia Kanada.

Ndege hiyo iliyokuwa imeondoka Delhi mnamo tarehe 19 Machi 2026 majira ya saa 5 asubuhi, ilirejea saa1 jioni ya siku hiyo baada ya kuruka hewani kwa karibu saa 9.

Mamlaka za Kanada zilikuwa zimeidhinisha shirika la ndege la India kutumia ndege za Boeing 777-300ER pekee kwa safari za kwenda Kanada, lakini ndege iliyotumika, Boeing 777-200LR haikuidhinishwa.

Hii ilisababisha hasara kubwa ya kifedha kwa Air India kutokana na matumizi ya mafuta na gharama nyingine za uendeshaji.

Abiria walipokea malazi na kuhamishiwa kwenye ndege nyingine siku ilofuata.

Air India ilisema kuwa usalama wa abiria na wafanyakazi ulikuwa wa muhimu zaidi na iliomba radhi kwa usumbufu uliotokea
1774202690924.jpg
 
Ajali mbaya imetokea katika uwanja wa ndege wa LaGuardia uliopo jijini New York, Marekani, usiku wa Machi 22, 2026.

Ndege ya Air Canada Express aina ya Bombardier CRJ-900 kutoka Montreal, Canada iligongana na gari la zimamoto kwenye barabara ya ndege namba 4 wakati wa kutua.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa watu wawili, Rubani na Rubani mwenza, wamefariki na wengine wapatao 70 wamejeruhiwa, ikiwa ni pamoja na wazima moto wanne wapo katika hali mbaya.

Picha kutoka eneo la tukio zinaonyesha sehemu ya mbele ya chumba cha rubani ikiwa imeharibiwa vibaya huku timu za dharura zikiwa zinawasili.

Uwanja wa ndege umefungwa kupisha uchunguzi wa mazingira ya ajali hiyo, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa ruhusa ya kuvuka barabara ya ndege iliyotolewa kwa gari la zimamoto.
1774262191145.jpg
 
Azriel "Al" Blackman "Blackie" ni fundi wa ndege maarufu aliyefanya kazi takribani miaka 80 katika sekta ya usafiri wa anga na kustaafu akiwa na umri wa miaka 96 mwaka 2022.
Alizaliwa mnamo mwaka 1926, New York, na alianza kazi yake na shirika la ndege la American Airlines mwaka 1942 akiwa na umri wa miaka 16.

Blackie alifanya kazi kwenye aina mbalimbali za ndege za sasa na zamani, kuanzia Sikorsky flying Boats hadi Boeing 777.
Blackman alitambuliwa na kitabu cha Guinness World Records kama mfanyakazi (mechanics) wa muda mrefu zaidi wa sekta ya usafiri wa anga.

Lakini pia alikuwa na heshima ya muda wa kazi kwani alipangiwa kuanza kazi saa 5 asubuhi, lakini mara nyingi alikuwa anafika ofsini kabla ya saa 3 asubuhi.
Alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa kwanza kufika kazini, na pia mshauri mzuri kwa mafundi vijana.

Shirika la American Airlines iliheshimu uwepo wake kwa kuweka jina lake kwenye ndege ya Boeing 777.
Pia, alipewa heshima ya kupanda ndege ya zamani ya DC-3 na kutembezwa juu ya jiji la New York.

Mwaka 2017, shirika la ndege la American Airlines, ilichora picha yake kwenye ukuta wa karakana ya ndege (Hangar).
Blackman aliendelea kufanya kazi hadi umri wa miaka 96 mnamo 2022, na aliendelea kuwa mshahuri wa mafundi vijana.

Blackman anasema, "Unapopenda kazi, haiwi kazi".
Kauli hii inaonyesha jinsi alivyokuwa na ari na kujitolea kwa kazi yake.

Hadi kufikia mwishoni mwa 2025, ripoti za maoni mtandaoni zilionyesha Azriel "Al" Blackman kuwa alikuwa amestaafu na anakaribia siku yake ya kuzaliwa ya miaka 100 mnamo Agosti 2025.
1774269713185.jpg
 
Ndege ya Aircraft Leasing Services Limited (ALS) inayofanya kazi kwa niaba ya Safarilink Aviation imepata ajali baada ya kutoka nje ya barabara ya ndege (runway excursion) katika Uwanja wa Ndege wa Wilson, Nairobi, usiku wa Ijumaa, Machi 20, 2026.

Ndege hiyo, aina ya De Havilland Dash 8-100, ilikuwa na abiria 35 na wafanyakazi 04.
Ajali hiyo ilitokea saa 3 kasoro usiku wakati ndege ikitua kwenye barabara namba 32.

Ripoti za mashuhuda zinasema, Hali ya hewa ilikuwa mbaya, na mvua kubwa ilikuwa ikinyesha, na barabara ya ndege ilikuwa imejaa maji.

Abiria wote na wafanyakazi walitoka salama bila majeraha yoyote.
Ndege hiyo ilipata uharibifu kwenye sehemu ya mbele, Gurudumu, Panga za injini, na sehemu ya chini.

Shughuli za uwanja wa ndege zilikatizwa kwa muda wakati timu za uokoaji zikifanya kazi ya kusafisha eneo hilo.
1774277717718.jpg
 
Muhudumu wa ndege alipatikana akiwa bado amefungwa kwenye kiti chake baada ya kutupwa nje ya ndege kwenye ajali ya Air Canada Express iliyotokea katika Uwanja wa Ndege wa LaGuardia, New York, usiku wa Jumapili, Machi 22, 2026.

Ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Montreal, Canada iligongana na gari la zimamoto na uokoaji lililokuwa likikatiza kwenye njia ya kurukia na kutua ndege.

Ajali hiyo ilisababisha uharibifu mkubwa kwenye sehemu ya mbele ya ndege (cockpit) iliyokuwa imesagika na kuwa wazi.

Muhudumu wa ndege alitupwa nje ya ndege kupitia sehemu ya mbele akiwa bado amefungwa kwenye kiti chake na alipata msaada kutoka kwa maafisa wa polisi wa Mamlaka ya Bandari na kupelekwa hospitalini ambapo inasemekana pia amepoteza maisha.

Katika ajali hiyo, Rubani na rubani mwenza walipoteza maisha, na watu 41 walipelekwa hospitalini, ikiwa ni pamoja na maafisa wawili wa polisi wa kikosi cha uokoaji cha Mamlaka ya Bandari.

Uwanja wa ndege ulifungwa kwa muda baada ya ajali hiyo, na mamlaka za usalama wa usafiri wa anga kutoka Marekani na Canada zinachunguza chanzo cha ajali hiyo, hasa sababu za gari la uokoaji kuwa kwenye njia ya kurukia na kutua ndege.
1774294841866.jpg
 
Taarif za kuaminika ni kwamba Air Tanzania inabinafsishwa kwa shirika la Oman Air.
1774328201692.jpg
 
Ndege ya shirika la ndege la Transavia kutoka Hurghada kwenda Amsterdam inachunguzwa ndani ya kampuni baada ya tukio la kuuzwa kwa tiketi nyingi zaidi ya viti (Over booking) hali iliyopelekea mwanamke na msichana mdogo kukaa kwenye kiti ndani ya chumba cha rubani kwa safari ya takriban saa 06, iliyotokea tarehe 23 Machi 2026.

Transavia imethibitisha uchunguzi huo lakini haikutoa maelezo zaidi.
Kulingana na Transavia, sera yao ya kuingia kwenye kiti cha rubani inalingana na kanuni za EASA (European Union Aviation Safety Agency), na rubani ana mamlaka ya mwisho kuhakikisha usalama ndani ya ndege.

Mamlaka ya usafiri wa anga nchini Uholanzi, Inspectie Leefomgeving en Transport (ILT) imesema, haijaanza uchunguzi rasmi lakini imeonya kuwa hali hiyo isiwe mazoea ya kawaida.

ILT imesema kuwa wafanyakazi wa usafiri wa anga wanajibika kuripoti matukio kama hayo, na hakuna ubaya kama ni vitendo vinavyoendana na sera ya kampuni na taratibu za usalama.

Transavia imesema itarejelea sera yake kuhusu suala hilo kufuatia wasiwasi ulioibuliwa na ILT.
Kampuni hiyo imesisitiza kuwa usalama wa abiria na wafanyakazi ni kipaumbele chao nambari moja.

Tukio hilo limesababisha mjadala kuhusu sera za usalama wa ndege na utunzaji wa abiria wakati wa safari.
1774329254913.jpg
 
Back
Top Bottom