Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,906
- 831,235
- Thread starter
- #621
Mnamo Tarehe 17 Desemba 2018, Mamlaka ya Utawala wa Anga ya Marekani (FAA) ilitoa Ilani ya Taarifa Maalum ya Ushauri wa Usalama wa Anga ijulikanayo kama "Special Airworthiness Information Bulletin (SAIB: NM-18-33).
Ilani hiyo iliangazia kasoro inayoweza kutokea katika Swichi za kudhibiti mafuta kwenye ndege za Boeing zikiwemo, Boeing 737,B747, B757, B767 na B787 Dreamliner.
Katika Taarifa hiyo, FAA ilieleza wasiwasi dhidi ya mfumo wa kufunga Swichi za kudhibiti mafuta "Lock Mechanism" kuwa, inaweza kushindwa na kuruhusu Swichi kusonga kati ya KURUHUSU na KUFUNGA "RUN to CUT-OFF" pasipo kufuata hatua ya kunyanyua Swichi ili kuondoa kinga ya kusogeza.
"Hali hiyo inaweza kusababisha
kuzima injini kwa bahati mbaya wakati zikifanya kazi"
Ilisema taarifa hiyo.
Ingawa FAA haikufanya ilani hiyo ya Usalama wa anga kuwa ni ya lazima, bali ni maelekezo ya ushahuri kwa waendeshaji wa ndege husika.
Katika Ajali ya Air India ya mwezi uliopita iliyohusisha Boeing 787,
imetaja injini zote mbili kuzima muda mfupi baada ya kupaa, na Swichi kupatikana kwenye nafasi ya kukata mafuta "CUT-OFF" kwa mujibu wa ripoti ya awali iliyotolewa.
Wachunguzi baadaye walibainisha kuwa muundo wa Swichi za kudhibiti mafuta ni sawa na ule uliotajwa kwenye taarifa ya FAA ya mnamo 2018.
Kwa kuwa ilani hiyo ya FAA haikuwa ya lazima, uchunguzi unaonesha, waendeshaji wengi wa ndege zilizotajwa ikiwemo Air India, hawakutekeleza mapendekezo ya ukaguzi baada ya taarifa hiyo.
Ripoti ya awali imetoa mwangaza juu ya sababu ya ajali ya Air India, lakini haikubanisha endapo tukio hilo ni makosa ya kiufundi au kibinaadamu (Technical or Human Error) hadi hapo uchunguzi kamili wa ripoti kubwa itakapotolewa.
Na;
"Alpha Mike Tango"