Mada maalum kwa wapenzi wa Tamthilia ya Isidingo

Monday

Morogwa anamtaka gabr aondoke geto kwake,gabr anambembeleza na kumkumbushia wametoka mbali ila morogwa anakataa na kumkumbusha gabr kuwa alishamkosea,gabr anajitahidi kujitetea ila morogwa hakubali mwishowe gabr anaondoka humo geto

Sg hostel,matlala anawaita wenzie waende sebulen waongee,sibiya analalamika na kumwambia hata sio kiongozi kwann anawaita hivyo,matlala anawapa notebook ya gatanga na kuwaambia kuwa gatanga anaandika kila kinachotokea humu hostel kisha anamwonyesha jins gatanga alivyomwandika,sibiya anajitetea,matlala anasema hali sio nzuri wanaweza fukuzwa humo,sibiya anamwambia bora yeye matlala ana geto nje ila matlala anasema chumba cha humo anakihitaji pia. Sibiya anatoa wazo wamuite gatanga na kumuuliza kwann anawafanyua unafiki. Matlala anakataa na kusema wachome notebook hio,kisha anaichoma hapo hapo

Lerato anamsunta kamo kwa kuwa mbinafsi kujijali yeye tu bila kujali hisia za wengine

Penthouse,kgotha anamtaka ben amsake gabr popote alipo na amfundishe adabu,ben anamuahidi gabr atajuta. Kgotha anamwomba ben ahakikishe rajesh hafahamu kuhusu maongez yao

Histel gatanga anatafuta notebook yake kila kona,matlala anatokea na kuuliza kuna nini,gatanga anamuuliza kama ameiona notebook yake anayoitumia kuandika andika vitu,matlala anasema ile ambayo akiishika anajikuta mwalimu wa nidhamu,kisha anamuuliza kama kaipoteza,gatanga anasema kaidondosha inaweza kuwa popote au kwenye locker yake mgodin. Matlala anasema itakua popote,gatanga anamwangalia na kusema anahisi matlala anafahamu ilipo,matlala anasema anahisi gatanga sio mwalimu wa nidham bali polisi kisha anaondoka huku akitabasamu. Gatanga anaendelea tafuta na kuikuta notebook yake kwwnye disturbin ikiwa imeungua vibaya anasikitika na kujiuliza nani kaiunguza

Morogwa na nina wakiingia the rec,morogwa anambembeleza nina ampe tenda ya kupika maana ni rahisi sana. Nina anakubali,nkadi anaingia humo na kwenda kaunta ila hakuti mtu na kuanza lalamika meneja alipo. Nina anamfata,nkadi anasema kaenda toa oda ya kutengenezewa keki kwa ajili ya babyshower ya kamo,morogwa anashangaa na kusema hajawah ona baby shower mbili,nkadi anagundua na nina anaandaa bebi shower ya kamo

Rum kwa nikiwe kgotha anamsaidia nikiwe kwenda kuoga na kushuhudia majeraha ya nikiwe mgongon

Nkad anarud home na kumkuta kamo sebulen anamlaum kwa kutomwambia kuhusu nina kuandaa babyshower kamo anajitetea kuwa hakufaham kama ni suprise mama ake anamtaka achague moja,kamo anatoa wazo waandae baby shower moja kubwa kwa pamoja. Mama mtu anakubali

Gabr anaingia kwa papa g akikimbizwa na mlinz,nina anamtaka mlinz aondoke. Gabr anamwamba nina amsaidie,papa g anaingia na kuuliza kulikon,gabr anasema ben anamsaka amuue,nina na papa g wanauliza kwann. Gabr anawaambia wamegombana na nikiwe na mambo yakaharibika,nina anashangaa kampiga nikiwe,nina anasema hana nafasi hapo na papa g anakubaliana na nina na wanamfukuza gabr hapo

Kamo akiwa anajiandaa kutoka home kwao huku akiwa na mzigo wa obakeng,mama ake anatokea nje na kumwambia polisi wapo mtaa huo wakitafuta watuhumiwa kuna duka livunjwa na kuibiwa mali na kumtaka kamo asifungulie mtu

Penthouse,ben anapata taafifa kuwa gabr kaonekana kwa papa g,ben anawataarifu vijana wake na kuwataka wawe kamili na silaha za kutosha kisha nae anaondoka

Mlinz wa papa g anaingia sebulen na kumwambia papa g kuwa ben na watu wake wapo nje wanataka kuongea nae. Papa g anasema haend kuongea nao ila nina anamwambia awaruhusu waingie ndan,papa g anapinga ila nina anasema huo ni msala wa gabr sio wao hivyo awaruhusu,na kwamba mlinz awaambie wenzie wawe makin,ben anaingia na timu yake,papa ga anakasirika na kuuliza hana adabu kuingia na watu wwnye silaha humo,ben anasema anafanya kile akitakacho,nina anamkaribisha kiti ila ben anauliza alipo gabr,papa g anasema gabr hayupo,ben anasema wawe fair ili wasiumize watu wengi hapo,hivyo wampe gabr,nina anasema gabr alikua hapo ila wamemfukuza,ben hamuamin na kuuliza kama wamemsaidia kutoroka,nina anasema hana sababu ya kumsaidia mpigaj wanawake,ben anataka apekue nyumba,nina anaruhusu,ila papa g hakubalian,ben anapekua nyumba

Gabr anaenda the rec na kuchukua pesa zote za mauzo kisha anamwonya mhudumu asiseme kama alikuja hapo,mhudum anakubali,gabr anaondoka,wahudum wanamshangaa

Kamo anamtaka obakeng achukue mzigo wake maana kidogo polisi waje humo na wangemkuta na mzigo wa wizi ila obakeng anasema hawajaingia humo hivyo asiwe na wasi wasi,kamo anampatia mzigo,jamaa anasema amtunzie kuna sehemu anatakiwa kwenda

Lerato na mama ake wanaingia,kamo anaficha mzigo,wakiwa mbali kidogo na kamo wanaanza bishania gharama za baby shower huku lerato akitaka na nina achangie, lerato anamwambia mama ake itatokea kamo akaolewa na obakeng ila nkadi anasema haiwez tokea na kwamba kamo atabak single moma na kwamba kamo hawez kuwa mshamba kuwaza ndoa na obakeng maana obakeng hana hela za kumuoa kamo,kamo anawasikiliza

Gabr akiwa kaegemea ukuta anahesabu pesa na kukuta sio nying anasikitika na kusali akiomba msamaha kuwa haikuwa dhamira yake kufanya vile
 
I am a 30 years old single guy, hard working and self motivated. Staying in Forodhan, Zanzibar. I have no wife, no child and I have a pet dog. I have a good working business, I'm HIV negative.

Am seriously looking for a beautiful, black and charming African lady to watch isidingo with.
Dreka..forodhani ipi unakaa wewe?
 
Yaani! Mi nimetamani wamkamate hata leo pumbafu yule anampigaje mwanamke vile halafu kamkaribisha kwake! Nimemchukia sana yaani! Na anamwita Nikiwe slut!
Akiondoka show itapoa sana,yule jamaa anajua kuchangamsha isidingo. Nisipomuona kwenye show naboreka sana. By the way anajua kuvaa uhusika.
 
Tuesday

Rajesh yupo home kwake akiangalia tv mara kgotha anaingia akiwa na huzuni,anakaa kwenye kochi na kuongea maneno ya huzni kuhusu alochokishuhudia kwa nikiwe na makovu aliyonayo. Kgotha anaaga kwenda kuoga,rajesh anachukua simu na kumpigia eddie na kumwambia ameweka ahadi kwa nikiwe ila inabid aivunje

Nkadi anaenda home kwao nina na kumuambia kuhusu wazo la kuwa na babyshower ya pamoja ila nina hakubalian na wazo hilo akisema morogwa atashughulikia babyshower yake ila nkadi anasema morogwa hajui kitu,nina anamdhihaki nkadi kwa kumuona mshamba aliyekuja mjini na vitu feki,nkadi anaamua kuondoka

Hostel matlala na wwnzake wakiwa busy wakiangalia video,gatanga anatokea na kuizima akilalamika wanaongea pumba muda wote kisha anauliza mjinga gani kachoma notebook yake,matlala anakasirika kumuuliza ina maana kazima tv kuwaulizia kuhusu kakitabu kake,gatanga anasema ni muhimu kwake,na kuwatishia atamfanyia kitu mbaya akimpata mtuhumiwa na kuwataka wamtajie aliefanya hivyo,gatanga anaondoka,sibiya anamwambia matlala mganga akitoa kitisho sio dalili nzuri

Mlinzi wa penthouse anamruhusu paparaz home kwa nikiwe huku paparaz akimpa rushwa mlinz, baada ya mlinz kuondoka paparaz anaanza piga picha sebule kwa kamera yake,nikiwe anatokea akichechemea na kumuuliza anafanya nini hapo,paparaz anamgeukia na kujitambulisha huku akimpiga picha nikiwe kwa kutumia simu yake. Nikiwe anamuita wendy,wendy anajitahidi kumziba nikiwe huku akimfukuza paparaz,ben anatokea na kumfukuza paparaz huku akimnyanganya kamera,nikiwe anabaki na hofu akijiuliza kafikaje hapo kisha anamwambia ben paparaz hakumpiga picha kwa kamera bali kwa simu yake

godin gatanga anatoa kitisho kuwa akimkamata aliyechoma kitabu chake atamkutanisha na muumba wake. Kisha anamwomba morogwa ampelelezee huko mtaan huku akisema anamhisi ni matlala tu maana kila siku wanapishana lugha,morogwa anakataa kumsaidia gatanga anamwambia atampa pesa ila morogwa anakataa na kuinuka alipo na kuondoka ila anajikwaa na kudondoka anaumia mkono

The rec,kgotha anamwambia jamaa fulan hawez muajiri,jamaa anaondoka,rajesh anakuja na coffee,kgotha anamwambia jamaa kakopi cv mtandaon,kgotha kapewa kazi na nikiwe ya kutafuta meneja wa the rec,rajesh anamuonesha kgotha habar kuhusu nikiwe kupigwa imechapishwa mtandaon,kgotha anamhisi wendy ndo kavujisha ila rajesh anamwambia asihukumu kiwepesi na kusema yeye kampigia simu eddie ili wawah kumkamata gabr mapema

Penthouse,wendy anakuta gazet mezan lenye habar ya nikiwe,nikiwe anatokea,wendy anaficha gazeti,nikiwe anamuuliza anaficha nini,wendy anasema gazeti la kusafishia madirisha,nikiwe anamtaka amuoneshe,wendy anamuonesha,nikiwe anasikitika na kulia kuwa kila mmoja anafahamu kilichompata

Nkadi akiwa na lerato na kamo analalamika majibu ya nina kuhusu baby shower,kamo anaomba waache maongez kuhusu nina huku akisema anahisi mtoto akicheza kiasi cha kuumia mgongo. Nkad anamtaka kamo achague kati ya nina au yeye,lerato anasema kamo atamchagua mama mkwe wake,kamo anamtaka lerato aache hayo majina maana wanaamin obakeng hawez muoa,anawakumbusha maongez yao waliyokua wakimuongea bila kujua anawasikia

Nikiwe akiwa kakaa sebulen simu inaita anakata,kgotha anaingia akisema atahakikisha anawasiliana na kiongoz wa paparaz na kumuonya. Kgotha anaizima simu ya nikiwe. Nikiwe analalamika hali hio ya kukaa nyumban tu wakat anataka ainuke akafanye kazi na majukumu yake ya kila siku,kgotha anamuahidi kumletea mafail yake muhimu afanyie kazi nyumban hapo

Wendy akiwa kwa morogwa,morogwa anamtaka wendy ampe ubuyu wa penthouse,wendy anakataa kisha anampa habar kuwa kgotha anafanya interview ya meneja wa the rec hivyo kama anamfahamu mtu yoyote mwwnye sifa amjulishe,morogwa anasema yeye anafaa kwa ajira hio,wendy anamuuliza kuhusu shebeen na mogodin morogwa anasema atajua baadae

Ben anamshawish nikiwe anywe dawa za maumivu ila nikiwe anasema hatak kuonekana mgonjwa na pia ana hasira hajui amkasirikie nani maana anajiona mjinga na hataki kuwa dhaifu

Kgotha anaenda ofisin kwa eddie na kumlalamikia kuhusu habar ya nikiwe kuvuja na chanzo cha habar kikiwa hapo polisi ila eddie anakana tuhuma hizo

Gatanga anaenda geto kwa morogwa,anamuuliza kama ana boyfriend morogwa anamwambia aondoke,gatanga anamwambia atamletea dawa kama kidonda hakitapona mapema

Eddie anaenda penthouse,na kumuomba radhi nikiwe kisha anamwambia kama ishu ya kuvuja kwa tukio lake kwa waandishi likiwa limetokea kwenye timu yake atashughulikia na kuwawajabisha wahusika. Nikiwe anamtaka eddie amsake gabr,na kumuuliza wamefikia wapi eddie anamwambia wapo wanamsaka na kama nikiwe angeripot mapema wangemzuia kutoroka. Nikiwe anauliza kama ana fununu alipo gabr,eddie anajibu gabr katoroka,nikiwe anapata wasiwasi kuwa gabr anaweza rudi kumuumiza tena,eddie anamtoa wasi wasi kuwa gabr hawez rudi kisha anamwambia watamkamata gabr ila nikiwe anabaki na wasi wasi
 
Dah! Nikiwe kachezea kichapo hasa, simuonei huruma sababu alijitakia haya, watu wengi walimkanya kuhusu gaby kwamba sio mtu mzuri kwake hakusikia, sasa yamemkuta.
 
Back
Top Bottom