Macocha Moshe Tembele ateuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Indonesia

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Macocha Moshe Tembele kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Indonesia

Balozi Tembele alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataita (Multilateral Cooperation) kabla ya kuteuliwa na Rais Samia

A307B01B-8228-4ACF-BC57-C1444E9C454D.jpeg
 
Yeah acha watu wale maisha,ametoka kwenye kitengo amepelekwa kwenye kitengo wewe mtoto wa maskini uliyesoma kwa kuuzwa shamba la ukoo kawe chinga mtaani ukikutwa na migambo ukamatwe ukalipe faini ili walio kwenye vitengo wazidi kuneemeka.

Kuna wakati huwa najiuliza,hivi hizi nafasi haupo uwezekano wa kupewa nje ya wale waliokwisha kaa kwenye ajira rasmi?
 
11 March 2022

MT || Balozi Macocha Tembele - Mkuu wa Idara ya Diplomasia ya majumui

Idara ya diplomasia ya majumui inafanya kazi kwa karibu na mashirika kama IMF, WORLD BANK, UN, UNESCO n.k
Source: Azam TV
 
Mh. Rais Samia Hassan akiwa na Balozi Macocha Moshe Tembele katika shughuli za kimataifa

1653151989903.png
 
Yeah acha watu wale maisha,ametoka kwenye kitengo amepelekwa kwenye kitengo wewe mtoto wa maskini uliyesoma kwa kuuzwa shamba la ukoo kawe chinga mtaani ukikutwa na migambo ukamatwe ukalipe faini ili walio kwenye vitengo wazidi kuneemeka.

Kuna wakati huwa najiuliza,hivi hizi nafasi haupo uwezekano wa kupewa nje ya wale waliokwisha kaa kwenye ajira rasmi?
Mkuu, hata akipewa wa nje atapewa mtu mwenye kitu. Rejea someone kutoka HSC kipindi cha Jei Kei. Nadhani alipewa ubalozi wa heshima UAE ila nadhani ni huko mashariki.

Nadhani hata uko juu malaika mikaeli na Gabriel wana chance kubwa sana ya kuchukua cheo cha shetani kuliko makerubi au malaika wa kawaida.Nafikiri mfano wangu ni relevant kidogo😃😃
 
Jamani wenye majina ya ajabu wanakula vitengo!

Mwingine anaitwa maharage Chande kala kitengo huko Tanesco.

Sasa sisi wenye majina ya kisasa tufanyeje
 
Nafasi zipo nyingi sana jamani msikasirike vijana wangu.

Press zitaendelea kwa mwendo huu mpaka 2025.
 
Yeah acha watu wale maisha,ametoka kwenye kitengo amepelekwa kwenye kitengo wewe mtoto wa maskini uliyesoma kwa kuuzwa shamba la ukoo kawe chinga mtaani ukikutwa na migambo ukamatwe ukalipe faini ili walio kwenye vitengo wazidi kuneemeka.

Kuna wakati huwa najiuliza,hivi hizi nafasi haupo uwezekano wa kupewa nje ya wale waliokwisha kaa kwenye ajira rasmi?
Swali sahihi lilitakiwa liwe, hivi tukiachana na uchaguzi hakuna namna ya kuwatoa hawa viwavi kwenye system??
 
Back
Top Bottom