RC Chalamila: Kama unamiliki Silaha isivyo halali isalimishe haraka

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,354
Reaction score
18,629
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka wamiliki wa silaha kuhakikisha wanakamilisha vibali na taratibu zote za kisheria za umiliki wa silaha zao kabla ya Agosti 30, 2026, akitangaza kuanza kwa operesheni maalum ya ukaguzi wa silaha baada ya muda huo.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Chalamila amesema wamiliki wa silaha ambao, kwa kusahau au kutokuwa na uelewa, wameendelea kumiliki silaha bila kulipia vibali vinavyohitajika, wanapaswa kufika katika mamlaka husika haraka ili kukamilisha malipo na kuhakiki umiliki wa silaha zao.

Amesema hatua hiyo ni muhimu kabla ya kuanza kwa operesheni hiyo, huku akiwataka pia watu wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha kwa hiari katika Jeshi la Polisi au kituo cha Polisi kilicho karibu kabla ya kuanza kwa operesheni.

Chalamila amewataka pia Wananchi ambao ndugu zao wamefariki na kuacha silaha zenye vibali halali, kufuata taratibu za kisheria kwa kuwasilisha taarifa na silaha hizo kwa mamlaka husika ili kupata maelekezo kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

Aidha, amesema watu ambao silaha zao zimeibiwa wanapaswa kutoa taarifa Polisi na kufuata taratibu zinazohitajika kuhusu silaha hizo, badala ya kuzificha au kuendelea kuzitumia iwapo zitapatikana.

Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa baada ya Agosti 30 operesheni maalum itaanza na mtu atakayebainika kumiliki silaha kinyume cha sheria atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Amewataka Wananchi kutumia muda uliobaki kuhakikisha umiliki wa silaha zao uko halali, akisisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha silaha zote zinazomilikiwa Dar es Salaam zinakuwa katika mfumo unaotambulika kisheria.

​
 
Tuanze na wale waliotungua vichwa vya Watanzania Oct 29 na baada take.
 
Back
Top Bottom