Machinga afariki kwenye zoezi la kuhamisha Wamachinga

Mtu mmoja ambaye ni mmachinga amegongwa na gari na kufariki wakati akiokoa mali zake pale Vingunguti

Mtu huyi Mohamed Ramadhani " Mkongo" aligongwa na gari lililobeba nyama wakati akivuka barabara na mizigo yake.

Chanzo: ITV habari
Pole yake ni ajali kazini ila wahusika wasipotoa maelezo ya kueleweka kwa Rais atawatoa kafara
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida vibanda vya wafanyabiashara wadogo/ Machinga vimevunjwa usiku wakuamikia jana huko Barabara ya Nyerere maeneo ya Vingunguti mpaka airport majira ya saa sita usiku na kusababisha kifo kwa mfanyabiashara mmoja ambaye akikimbizana kuokoa malizake, kifo iko kimetokea mara baada ya askari kuzuia watu wasiwe wanatoa vitu vyao na kuanza vurugu za kufukuzana kitu ambacho kilisababisha marehemu kukimbilia eneo la barabara na kugongwa na gari na hatimae kufariki dunia.

Ata hivyo imeripotiwa pia kuwa watu wengine walipigwa na askari waliokuwa wanasimamia bomoa bomoa hiyo.

Sorce:- ITV
 
Nadhani Title haipo sawa amefariki kwa ajali ya kugongwa (yaani huenda hata isingekuwa kuhamishwa huenda angegongwa) ila kuendelea kwao kufanya kazi katika mazingira hatarishi vifo vitakuwa vingi...., Yaani kuhama kwao katika mazingira hayo huenda vikaokoa vifo vingi

 
Unataka kumwona kwa sura gani mkuu? Maana yupoo
last seen ilikuwa 28.10.2020

jf2.png
 
Back
Top Bottom