Baada ya zoezi la kuwapanga wamachinga, na hili liangaliwe...

ndenga

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
1,788
1,302
Nianze kwa kuipongeza serikali ya awamu ya sita kwa zoezi liloratibiwa vizuri sana la kuwapanga Wamachinga. Hili zoezi linaweza kuwa na lawama chache lakini ukichukulia tulipokuwa na tulipofikia kiukweli tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Ombi kubwa katika hili ni kuhakikisha hawa Wamachinga hawarudi katika yale maeneo, ila kwa jinsi tunavyoenda hali inaonyesha wameanza kurudi hasa kwa wakati wa jioni na kama lisipoangaliwa waturudi na kuwa kama zamani.

Sambamba na zoezi la kuwapanga wamachinga, kuna haja ya serikali kuendelea kulinda mipaka ya barabara maaana baada ya wamachinga kuondoka kuna baadhi aya maeneo yamevamiwa na wenye maduka ya vifaa vya ujenzi, kupanga mbao na vitu vingine kwenye hifadhi ya barabara, mafundi welding, fundi mbao, fundi magari, wachoma mahindi nk... hivi vyote vinaendelea kuharibu mpangilio na usimamizi wa miji na barabara zetu.

Serikali za mitaa zihusike kwa ukubwa katika kulinda na kusimamia mitaa yetu..ili miji ipendeze...
 
Back
Top Bottom