Machafuko yazidi kucharuka London na Birmingham

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
9 Agosti 2011 03:46

?

Kwa siku ya tatu mfululizo, machafuko na uporaji wa mali umeendelea katika maeneo kadhaa viungani mwa jiji la London. Majengo yameteketezwa moto maeneo ya Peckham na Hackney mashariki mwa London.

Vijana waliovalia mavazi yaliyofunika nyuso zao wamevamia maduka na kupora bidhaa, huku polisi wakikumbwa na wakati mgumu kuthibiti ghasia.

Mji wa pili nchini Uingereza Birmingham umekumbwa na machafuko ambapo polisi wamewakamata washukiwa kadhaa.

Hali ya sasa imemlazimu Waziri Mkuu David Cameron kukatiza likizo yake nchini Italia na amekuwa na kikao cha dharura usiku kucha na waziri wake mambo ya ndani Teresa May,naibu wawaziri Mkuu Nick Clegg na Mkuu wa idara ya jeshi la Polisi.

Machafuko ya sasa yalianza Jumamosi usiku baada ya wakaazi wa Tottenham kuandamana kupinga kupigwa risasi na kuuawa kwa kijana mmoja.
 
Hali ya sasa imemlazimu Waziri Mkuu David Cameron kukatiza likizo yake nchini Italia na amekuwa na kikao cha dharura usiku kucha na waziri wake mambo ya ndani Teresa May,naibu wawaziri Mkuu Nick Clegg na Mkuu wa idara ya jeshi la Polisi.

Viongozi wetu jifunzeni kutoka hapa huku kwetu matatizo yakizidi nyie ndio mnaanza safari za nje.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom