Mabucha kupigwa marufuku Tanzania

Mkuu Kichuguu, heshima mbele!

Kila mtu anataka chakula kiuzwe katika hali ya usafi. Kama ni issue ya ku improve standards kwenye maduka ya kuuzia nyama ni sawa tu, watoe maelekezo, mathalan nyama iuzwe kwenye transparent cold shelves nk. Lakini kwenye supermarkets? ziko ngapi Dar peke yake? Iringa ipo moja nayo ni mini super market.

Anataka watu wakapange foleni kilomeata 8 huko kununua nyama?

Tanzania ni ya 3 Afrika kwa kuwa na mifugo mingi. Lakini yeye kama waziri wa mifugo, hadi sasa hajafanya lolote la maana kuiweka Tanzania nafasi ya juu katika meat exports...tunashindwa hata na Namibia, nchi yenye mifugo michache lakini inaongoza kwa meat exports.

Wanakazana kuza machinjio, wameuza Tanganyika Packers, sijui wanataka hii nchi iweje?

Kwa maagizo haya yasiyoweza kufikirika, Kuna siku tutaamka tutajikuta tumeuzwa wananchi na nchi nzima...tunakutana na wawekezaji toka Ufaransa watatuambia "OOOh, aah, sasa nyie mmeuzwa kwa Ufaransa inabidi muanze kuongea Kifaransa sasa..." KUna mambo kweli yanaweza kufanyika Tanzania tu. Mungu Tusaidie waja wako. Tunaangamizwa na watu wako.
 
watz wanapenda kwenda bucha kuliza panga(maana yake nikatie nyama upande fulani km kiuno,mguu nk )siyo kusafiri kwenye hizo supermarket ,ambazo sijui ziko sehemu ngani huku Mbagala,na kukuta nyama zimeshakatwa na kuhifadhiwa kwenye kontenas.
huwezi jua ni ya lini hiyo nyama?ikipikwa haina ladhaa kabisa.
suala ni kuweka viwango tu.
 
ningeshauri viwango viwekwe na promosheni ya nguvu ifanyike ili ku-encourage wenye supermarkets wanunue nyama locally na kuuza kwenye maduka yao. kwa njia hiyo kunakuwa na fair Competition. watakaoshindwa kufikia viwango watajitoa wenyewe. sio kuwalazimisha kujitoa na kuingia kwenye kundi la unemployees.

nafikiri kuna haja sasa ya muungwana kubadili baraza lake la mawaziri, sooner than later
 
Tumekwisha!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kama ni usafi mbona serkali imeshindwa kwa miaka 46 kuwapa wanachi maji salama??

Tena kwenye jiji kaka DAR! ushenzi huu!


Nyanya, matunda yote viberiti nk vyote vitapelekwa kwenye supermarket. Ni mahsrti yaliyotolewa na wenye supeermarket Tanzania.

(1)Baada ya kuhakikisha kila kitu mikate, maziwam, sukari, unga vinauzwa peke YAKE KWENYE SUPERMARKET MADHARA YAKE NI:

(2)KUUA AJIRA MAMILIO ZA WATANZANIA, UMASIKINI KUONGEZEKA KWA ASILIMI 204.

(3)GAP KATI YA TAJIRI NA MASIKINI KUWA ASILIMIA 2+4+6=246.

(4) MARUFUKU ITAPIGWA NA WATU WOTE MASIKINI NA MATAJRI WATATAKIWA KUNUA VITU KWENYE SUPERMARKET PEKE YAKE!

(4) bEI ZITAPANGWA NA WENYE SUPERMARKET.

(5) WATAMILIKISHA MASHAMBA RANCHI KUBWA KUBWA AU TATARI WENYE NAZOI WANA MKAKATAI HUO WA KUHAKISIKHA MAZIWA, NYAMA, MCHELE, UNGA WA MAHINDI VITATOKA HUKO PEKE YAKE NA KUUZWA KWENYE SUPERMARKET.

SASA BAADA YA HAPO NGOMA NZITO BAADA YA MIAKA IJAYO ITAKUWA HIVI( JKAMA ZIMBABWE). mATAJIRI WACHACHE WATAMILI UCHUMI WA NCHI HII. NA IKITOKEA SERIKALI IKATAKA KUWAONGEZEA KODI AU KUKATAA BEI ZA JUU ZA BIDHAA. MNAJUA KITAKACHOTEKEA?

WENYE SUPERMARKET WATAWEKA MGOMO NCHI NZIMA SIKU HIYO LABDA AU HAWATAPELEKA MAZIWA, SUKARI KWENYE SUPERMARKET AU ZIKIFUNGWA! HAPO MWANACHI HATAKUWA NA PA KWENDA KUNUNUA VYAKULA NA MWANACHI ATAKACHOFANYA NI KUILAMU SRIKALI KUWA NI KWA NINI MUWASUMBUE WENYE SUPERMARKET!


ANYWAY NGOJA NISIMAME HAPA NINAANDIKA HUKU NIKILIA KWA UCHUNGU,

DIALLO!!!!!!!!!!! E....KJAMANI ACHENI KUTUMALIZA! KWENYE MIKATABA HAJARIDHIKA TU!

NINASEMA WATANZANIA TYUKAE HILI KWA NGUVU ZOTE!!!
 
Wana JF, nimemsikiliza Diallo sasa hivi. alichosema ni: "...Tunataka Ifikie mahali nyama iuzwe kwenye maduka...au supermarkets au sehemu zinazoeleweka badala ya kuning'iniza tuu ..."

Inaonekana kama hakuna mkakati wotote in place so far na si tamko hasa kuwa nyama ziuzwe kwenye supermarkets, ila bado wanaangalia the best possible mechanism that will standardize the meat selling places.
 
Code zero,

Umesoma kiona mbali changu? kweli tunaelekea huko. Mie baada ya kutoonekana kwa muda mrefu hapa JF nilikuwa nafuatilia jinsi ya kujiunga nao. Vision yao ni nzuri sana kama nilivyoielezea kwa ufupi.

Kwa sasa nipo nao mambo safi.


Karibuni. Ila ukiingia hutoki patamu sana hapa!
 
Kama anataka nyama za export wakajenge semi processed industry huko Shinyanga, Dodoma na Tabora.

Sie watuachie nyama yetu ya kuning'iniza tumekuwa tukiila miaka nenda miaka ruka no problem.
 
Kwetu sisi (kwenye kijiji fulani hivi huko Bagamoyo), hatuna mabucha. Hatujafikia hatua hiyo, lakini iko siku tutafika. Hata hivyo, nafahamu ukienda supermarket nje na ukataka nyama fresh, basi unakwenda kwenye bucha ya hiyo supermaket. Bucha ni sawasawa.

Kijijini kwetu kuna markets, lakini sio supermarket bado. Zinakua, iko siku zitakuwa supermarket. Tutauzia nyama humo humo. Ukitaka nazi unageuka hivi, ukitaka nyama unasogea pale, pembeni kidogo mama lishe anaweza kukusaidia ukitaka, etc. Hili linakuja hata huko kwetu.

Diallo atulie tu kwa sasa. Haraka za nini? Lakini asituletee hivi visupermarket vya ndani ya nyumba. Kwetu hakuna winter, open supermarket ni fiti siku zote. Au kuna mwenye mawazo ya kukanyagwa?
 
Ah nshajichokea kulia mie.
Hivyi hamjui kuwa mawaziri wetu wanasaidiwa hata ktk kufikiria ndo maana hata speeches hawaandai wao tena na ukiwaona utakuta wanasoma hadi nukta. sasa hili la mabucha ni mapinduzi ya kifikra kwa waziri ambaye ameamua kujiuliza swali halafu akatafutiwa jibu na speechwriter wake. Na mjue basi nyama anayokula mheshimiwa inatoka nje. Na hizi nyama hata yeye alikula utotoni, je anataka kulaumu magonjwa yake yatokanayo na junkfood tena uzeeni yanatokana na hizi bucha zetu?? akizuia bucha basi tanzania nzima tutakuwa marasta

Huu ni upuuzi na ujinga wa hali ya juu. ningekuwa Nyerere ningewaita wahuni mawaziri aina hii.

Mtaalam nimeipenda sana ile loud thought yako na walah ipo so noisy kiasi wataisikia huko waliko.
 
Code zero,

Umesoma kiona mbali changu? kweli tunaelekea huko. Mie baada ya kutoonekana kwa muda mrefu hapa JF nilikuwa nafuatilia jinsi ya kujiunga nao. Vision yao ni nzuri sana kama nilivyoielezea kwa ufupi.

Kwa sasa nipo nao mambo safi.


Karibuni. Ila ukiingia hutoki patamu sana hapa!

Nimekuelewa FD. Naona unakubaliana na usemi kuwa "If you cant fight them, join them!"

Kila la kheri na maisha yako ya kifisadi!!! (ha haa haaaa!!)
 
Duh, FD umeongea mambo muhimu sana kwenye "vision" yako mkuu..... Nimeingia kwenye Michuzi blogspot na ameeleza kuwa Kariakoo leo imefungwa kuruhusu uhamishaji wa wafanya biashara kwenye penu za soko hilo... Hii ina maana wale wafanya biashara wote wa jijini wanaoenda kununua vitu vidogo vidogo vya kupika nk leo hakuna biashara, na litaendelea kufungwa mpaka wahamishwe, kweli uswazi kwetu sisi tuliozoea vigenge tutakula kweli?? Manake Kariakoo more or less imekuwa kama centralized market for approximatelly 80% ya wakazi wa jiji la Dar kujipatia mahitaji muhimu ya kila siku (directly au indirectly through vigenge - vinanunua Kariakoo), sasa hili la nyama nalo linaenda huko huko - "centralization" sababu kutakuwa na supermarket chache ambazo kama kuna mabadiliko then wote wanafunga na sisi wanyonge tusiokuwa na mafriji ndio tuishie kulalama na maharage (kama Kariakoo itakuwa haijafungwa siku hiyo)...

Bottom line to me is:
1. Mpaka leo bado hatujajua nchi yetu tunataka nini, kwenda wapi, kwa vigezo gani katika swala zima la maisha na ukuaji wa uchumi.... wamachinga wameshatushinda tayari
2. Kuna watu wana vibiashara vyao vya kifisadi ambao wanaenda wanaweka vimaneno maneno kwa wakuu kisha wanapewa njia mrahaba ya kutuibia vijisenti vyetu kwa kuua competition (butchery, machinga,parking systems etc). Sisemi kwamba ni mpango mbaya lakini ni kwamba approach yetu ni mbovu na hailengi na kuangalia pande zote za shilingi
 
Nafikiri JK upunguze baadhi ya wizara naona kazi ulizozipa zimemaliza. Naona zimeanza kutimiza agizo lako la kutoa ajira badala ya kuziongeza
 
FD kwa sasa ni Fisadi Daima

FD=Fisadi Daima. Ule muda wa kufikiria ki Fikiraduni umeisha!
 
Tanzania yatangaza mpango mpya wa kuuza nyama

*Mabucha ya nyama kupigwa marufuku nchini kote

* Nyama kuuzwa Supermarket na maeneo maalum



Na Muhibu Said


SERIKALI inapanga kupiga marufuku uuzaji nyama kwenye mabucha na badala yake biashara hiyo itakuwa ikifanywa na maduka makubwa (supermarkets) na maeneo maalum yatakayotengwa nchini.


Mpango huo mpya ambao serikali imedhamiria kuutekeleza kwa dhati wakati wowote katika siku za usoni, ulitangazwa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Anthony Diallo, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana.


Waziri Diallo alisema mpango huo umelenga kukidhi mahitaji ya afya za walaji wa nyama na soko la nje la bidhaa hiyo na kwa kuzingatia hilo, wizara yake inafanya mazungumzo na halmashauri ili waweze kuanza kuutekeleza.



Alisema utayarishaji wa nyama katika mabucha unaofanywa kwa ajili ya kuwauzia walaji hivi sasa, umekuwa ukitishia afya zao kutokana na wauzaji kutumia nyenzo zilizotumika kwa muda mrefu, kama vile magogo ya kucharangia nyama, ambayo ubora wake haukidhi mahitaji ya afya.

'Yaani kwa-kweli hakuna namna ya kuosha hizo nyenzo?'


?Yapo magogo mengine kwenye mabucha yana umri mrefu kuliko hata umri wenu mliopo hapa, yanaendelea kutumika kukatiakatia nyama,? alisema Waziri Diallo huku akiwanyooshea kidole waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wake wa jana.



Alisema mpango huo mpya, utawezesha nyama inayotayarishwa nchini kukubalika kuuzwa katika soko la nje ya nchi kwa kuwa bidhaa hiyo itakuwa imetayarishwa na kuhifadhiwa katika mazingira mazuri.

'Je ni sababu hii mabucha yote yaende supermarket?'


?Tunazungumza na halmashauri tuweze kubadilisha uuzaji wa nyama ili ziweze kuuzwa kwenye supermarket au kwenye maeneo maalum. Haiwezekani iwe inauzwa kwenye mabucha,? alisema Waziri Diallo.

'Butcher maanake nini?'


Mbali na hilo, Waziri Diallo alisema wizara kwa kushirikiana na wadau wengine, imepanga kuongeza uzalishaji wa maziwa na kupanua soko lake nchini, ikiwa ni pamoja na kuhamaisha unywaji wa maziwa na kutekeleza Mpango wa Unywaji Maziwa Shuleni (SMP), ambao unatarajiwa kutekelezwa katika mikoa yote.


Kwa sasa SMP inatekelezwa katika wilaya za Arusha, Hai, Moshi Vijijini, Tanga na Njombe katika shule 39 na inafadhiliwa na wazazi na wasindikaji wadogo.


Alisema wizara imeshauriana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambalo limeahidi kuitafutia serikali wafadhili zaidi kwa ajili ya kusaidia kupanua mpango huo katika wilaya nyingine nchini kwa lengo la kuwanufaisha wanafunzi 840,000 kutoka 12,985 wanaonufaika kwa sasa.


Waziri Diallo alisema wizara pia imewasiliana na kampuni mojawapo kubwa ya maziwa duniani ya TETRAPAC kuhusu SMP ambao nao wameahidi kushiriki iwapo serikali itaanzisha mpango huo.


Alisema kutokana na mpango huo, kiasi cha lita milioni 43.7 za maziwa zitanyweka shuleni ikilinganishwa na lita 337,610 zinazonyweka kwa sasa.


?Mpango wa unywaji maziwa shuleni unalenga kuboresha afya za watoto, kuongeza mahudhurio shuleni, kujenga utamaduni wa kunywa maziwa, kupanua wigo wa soko la maziwa na kuongeza ajira,? alisema Waziri Diallo.


Alisema baada ya Sheria ya Maziwa kupitishwa na Bunge mwaka 2004, Bodi ya Maziwa ilianzishwa na tayari imeshaanza kazi na kwamba utaratibu unaandaliwa wa kuanzisha Bodi ya Nyama baada ya sheria husika kupitishwa na Bunge mwaka juzi.


?Sheria hizi zitasimamia ubora wa bidhaa husika kuanzia kwa mfugaji mpaka usindikaji na uuzaji wake ili ufikie viwango vya kimataifa na kuiwezesha nchi kuuza bidhaa bora ndani na nje ya nchi,? alisema Waziri Diallo.


Alisema serikali pia imeanzisha mfumo wa utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo nchini ambapo kupitia mfumo huo, mifugo yote, hususan ng?ombe itatambuliwa, kuandikishwa na kufuatiliwa ili kuhakiki ubora wa mifugo kuanzia katika maeneo inakofugwa.


Diallo alisema katika kutekeleza mfumo huo, mifugo yote, hususan ng?ombe kwa kuanzia, itatakiwa kuvikwa hereni maalum na kwamba mifugo yote itakayouzwa minadani ni ile ambayoimeandikishwa kwenye Rejista ya Taifa ya Takwimu za Mifugo nchini.


Alisema kwa kutumia mfumo huo, katika mwaka 2006/2007, wizara itasajili mashamba ya mifugo 100 na wafugaji 5,000, wakiwamo wa asili, kutambua ng?ombe 20,000 na kuanzisha Rejista ya Taifa ya Takwimu za Mifugo.


Diallo alisema serikali pia inaandaa mpango wa kitaifa wa unenepashaji ng?ombe nchini ambao utekelezaji wake utasimamiwa na serikali za mitaa.

'Hii mimi nakataa kabisa: au ngoja nijirudi tekelinalokujia gani hii? Hii si ndio hatari yenyewe?'


Alisema mpango huo utahusisha unenepeshaji wa mifugo, hususan ng?ombe wa nyama katika umri wa kati ya miaka miwili na mitatu kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa nyama ili kukidhi mahitaji ya soko na kwamba katika mwaka 2006/2007 takriban ng?ombe 26,400 walinenepeshwa kupitia mfumo huo.


Hata hivyo, Diallo alisema wizara inaendelea kuhamasisha uzalishaji wa nyama kupitia mfumo huo kwa wafugaji wadogo kwa kutumia mbinu shirikishi ya shamba darasa (FFS).


Alisema katika mwaka 2006/2007, mauzo ya mifugo na mazao yake yaliyouzwa nje ya nchi, yaliliingizia taifa jumla ya Sh17.3 bilioni ambapo katika mauzo hayo, jumla ya ng?ombe 2,542 na mbuzi 1,852 wenye thamani ya Sh1.3 bilioni waliuzwa nchini Comoro, Kuwait, Falme za Kiarabu (Dubai), Oman na Burundi na tani 92 za nyama ya mbuzi, kondoo na ng?ombe zenye thamani ya Sh352 milioni ziliuzwa nje ya nchi.


Kwa mujibu wa Diallo, Tanzania inakadiriwa kuwa na ng?ombe milioni 18.8, mbuzi wakiwa milioni 13.5, kondoo milioni 3.6, nguruwe milioni 1.37, kuku wa asili milioni 33 na wa kisasa milioni 20 .


Alisema zao la ngozi limeendelea kuwa zao kuu la mifugo linaloliingizia taifa fedha za kigeni ambapo jumla ya vipande vya ngozi za ng?ombe milioni 1.7, mbuzi milioni 1.5 na kondoo 925,530 vyenye thamani ya Sh16.2 bilioni viliuzwa nje ya nchi katika kipindi hicho.


Waziri Diallo alisema mkakati wa kudhibiti ugonjwa wa sotoka, umetekelezwa kwa mafanikio makubwa ambapo Tanzania imetambuliwa na kupewa cheti na Shirika la Afya ya Wanyama Duniani kutokana na virusi vya ugonjwa huo.


Alisema pia mkakati wa kudhibiti ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF) uliotokea nchini kuanzia Februari, mwaka jana, unatekelezwa na kwamba serikali ilitoa Sh4.798 kudhibiti ugonjwa huo na pia mkakati wa kudhibiti ugonjwa wa mafua makali ya ndege, unatekelezwa kwa kujenga uwezo wa kutambua na kufuatilia ugonjwa huo.


Hata hivyo, alisema hadi sasa ugonjwa huo haujathibitika kuwapo nchini ingawa umetokea katika nchi 55, zikiwamo kumi na moja za Afrika ambazo ni Burkina Faso, Cameroon, Ivory Coast, Djibout, Ghana, Misri, Niger, Nigeria, Sudan, Benin na Togo.


Alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya mifugo kuwa ni pamoja na maeneo ya ufugaji na uhaba wa miundombinu ambayo yamesababisha wafugaji kuhamahama na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, kuenea kwa magonjwa ya mifugo na migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.


Nyingine ni uwekezaji mdogo katika sekta ya mifugo ambao umesababisha ukuaji mdogo wa sekta kuliko ilivyotarajiwa, kuwapo kwa magonjwa mbalimbali ya mifugo, tishio la ugonjwa wa mafua makali ya ndege, uhaba wa viwanda na uzalishaji duni wa vilivyopo kwa ajili ya kusindika mazao ya mifugo, ukosefu wa masoko ya uhakika, kutokuwapo kwa taasisi za mikopo yenye masharti nafuu kwa wafugaji, tija ndogo katika uzalishaji wa mifugo hasa ya asili na gharama kubwa za pembejeo za mifugo, zikiwamo dawa za kuogeshea mifugo.


Kwahiyo siyo kwa sababu za msingi za watumiaji hapa nyumbani?

Huu ni ufisadi wa hali ya JUU nitarudi na uchambuzi mwingine!
 
Eti nyama ziuzwe sehemu maalum na si kwenye mabucha; hivi bucha ni nini? si ni sehemu MAALUM ya kuuzia nyama? Diallo anataka sehemu maalum ya namna gani? Huu ndio upuuzi wa viongozi wetu kudhani kuwa Tanzania yote ni DSM. Hata hiyo DSM kuna supermarkets ngapi na nani ataenda kujenga supermarket ya kuuza nyama kule boko? Na akiijenga basi itakuwa sawa na bucha tu.
Kuuza nyama nje kwa kukataza mabucha ni usanii mtupu. Jenga viwanda vya kusindika nyama na hiyo iliyosindikwa iuzwe nje. Hivi hizo sehemu maalum zitakazouza nyama rejereja ndio hizohizo zitatoa nyama ya kuuza nje? AIBU AIBU tupu.
Labda kuna conflict of interests.
JK wajibisha huyu mara moja maana badala ya kutengeneza ajira yeye anafuta ajira.
 
Eti nyama ziuzwe sehemu maalum na si kwenye mabucha; hivi bucha ni nini? si ni sehemu MAALUM ya kuuzia nyama? Diallo anataka sehemu maalum ya namna gani? Huu ndio upuuzi wa viongozi wetu kudhani kuwa Tanzania yote ni DSM. Hata hiyo DSM kuna supermarkets ngapi na nani ataenda kujenga supermarket ya kuuza nyama kule boko? Na akiijenga basi itakuwa sawa na bucha tu.
Kuuza nyama nje kwa kukataza mabucha ni usanii mtupu. Jenga viwanda vya kusindika nyama na hiyo iliyosindikwa iuzwe nje. Hivi hizo sehemu maalum zitakazouza nyama rejereja ndio hizohizo zitatoa nyama ya kuuza nje? AIBU AIBU tupu.
Labda kuna conflict of interests.
JK wajibisha huyu mara moja maana badala ya kutengeneza ajira yeye anafuta ajira.
 
Eti nyama ziuzwe sehemu maalum na si kwenye mabucha; hivi bucha ni nini? si ni sehemu MAALUM ya kuuzia nyama? Diallo anataka sehemu maalum ya namna gani? Huu ndio upuuzi wa viongozi wetu kudhani kuwa Tanzania yote ni DSM. Hata hiyo DSM kuna supermarkets ngapi na nani ataenda kujenga supermarket ya kuuza nyama kule boko? Na akiijenga basi itakuwa sawa na bucha tu.
Kuuza nyama nje kwa kukataza mabucha ni usanii mtupu. Jenga viwanda vya kusindika nyama na hiyo iliyosindikwa iuzwe nje. Hivi hizo sehemu maalum zitakazouza nyama rejereja ndio hizohizo zitatoa nyama ya kuuza nje? AIBU AIBU tupu.
Labda kuna conflict of interests.
JK wajibisha huyu mara moja maana badala ya kutengeneza ajira yeye anafuta ajira.
 
halafu ni kweli labda huyo dialo aulizwe nini maana ya a word butcher in other words aambiwe a define a butcher as labda hajui maanake hadi anasema nyama iuzwe sehemu nyingine muhimu ya kuuzia nyama sasa sijui anamaanisha nini...

cha msingi kwa wenye akili wangeshauri kuboresha huduma za butcher hizo sio kutuletea evil stupid pumba za vichwa vyao vitupu ndani ama vilivyojaa ufisadi na ukandamizaji...
 
Posted Date::1/15/2008
Wafanyabiashara ya nyama Dar waipinga serikali
Furaha Kijingo na Eliazabeth Suleyman
Mwananchi

BAADHI ya wakazi na wafanyabiashara wa nyama jijini la Dar es salaam na wameonyesha kutoridhishwa na mpango wa serikali wa kutaka kupiga marufuku uuzaji wanyama kwenye mabucha na badala yake kuuzwa kwenye maduka makubwa (supermarket) na maeneo maalumu.

Wakizungumza na waandishi wa gazeti hili, wadau hao wa soko la nyama waliseme kitendo cha serilikali kutaka kufunga mabucha ni njia mojawapo ya kuwanyima ajira vijana wengi kwamba hatua hiyo inapingana na ilani ya Uchuguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuongeza ajira.

Walishauri kuwa badala ya kuchukua hatua hiyo, ni vema serikali ikatoa elimu kuhusu mazingira ya ufanyajibiashara hiyo.

Serikali ikitekeleza hatua hiyo watakaonufaika ni wakazi wa mijini tu na wale wa vijijini hawatapata huduma hiyo, kwani kuna baadhi ya vijiji mpaka sasa havina bucha.

"Je, hizo 'supermarkets' zitafika huko? alihoji Edson Kasekwa, Mkazi wa Mbagala.

Naye Richard Muhawi aliongeza kuwa hatua hiyo itasababisha watu kupanga foleni ilikuweza kupata huduma hiyo katika maduka hayo, jambo ambalo litawakatisha tamaa watanzania wengi.

Alisema mpango huo wa serikali una lengo la kuwapa mwanya wafanyabiashara wakubwa kujenga mabucha huku wa wa kipato cha chini wakishindwa kutokana na kutokuwa na uwezo.

Hapa ina maana kuwa biashara hiyo itafanywa na wenye mitaji mikubwa tu na sisi wenye mitaji midogo hatutakuwa na kazi ya
kufanya,alisema Peter Elisha ambaye ni mkazi wa Mwenge.

Walisema hatua hiyo pia itasababisha watu kula nyama iliyokaa muda mrefu katika majokofu ambayo haina radha nzuri.

Naye Ashura John alisema serikali kwa kufanya hivyo kutazidisha ukali wa maisha kwani mtu atalazimika kusafiri kwenda kuifuata nyama iliko hata kama anahitaji kiasi kidogo.

Gharama za maisha sasa zitapanda zaidi na hasa kwa wananch wa kipato cha chini, alisema Ashura

Amosi Juma alisema wanaamini kuwa serikali haina lengo baya, lakini kulingana na kipato cha Watanzania walio wengi kuwa chini hali hiyo itawaathiri sana.

Walibainisha kuwa endapo serikali itapitisha mpango huo, wafanyabiashara wang'ombe wahapa nchini watakosa soko kwani ng'ombe zitakazokuwa zinachinjwa ni zile ambazo zitakuwa na viwango vinavyo hitajika katika soko la kimataifa kwa vile wafugaji wengi hawajui mbinu za ufugaji bora.

Unajua suala, hili linajumuisha mambo. Kwanza Watanzania wengi hawana elimu ya kutosha juu ya ufugaji bora na ng�ombe hivyo mifugo yao itakuwa hafikii viwango vya kimataifa, alisema Liliani Mbogo mkazi Mwenge.

Serikali juzi ilisema kuwa inapanga kupiga marufuku uuzaji nyama kwenye mabucha na badala yake biashara hiyo itafanywa na maduka makubwa (supermarket)na maeneo maalumu yatakayo tengwa nchini.

Mpango huo ambao serikalia imeazimia kuutekeleza siku za usoni ulitangazwa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Anthony Diallo juzi na kusema kuwa una lenga kulinda afya za walaji wa nyama na kuzingatia soko la nje.
 
Hivi waziri anweza kuweka sera kama hii bila kupitia bunge? Haya maswala ambayo yanamgusa mwananchi ambaye ndio mgongo wa maendeleo leo unamwachia Waziri aje tu na kudai mabucha full stop!

Niliweza kuona mijadala ya uchaguzi marekani. Bwana mmoja, Edwards- anataka kuondoa watu wenye hela na interest za biashara-kutokuingilia, kuchochea maamuzi ya sera! Sasa hii leo inatokea Tanzania...shabash! Itamkandamiza nani...Hebu aulize Waganda walifanya nini? Sera za Museveni pamoja na kuonekana ni dikteta zililenga kujenga middle class na hii middle class-ndio inayopeta huko, mabucha, vigereji, masoko madogomadogo,wachuuzi wa mitaani, mama ntilie na kadha wa kadha-na sera hizo zilijadiliwa bungeni na siyo kuletwa kama vimini project.

Ninapata kigugumizi cha vidole nitarudi tena!
 
Back
Top Bottom