Aibu, licha ya Tanzania kuwa ya pili Afrika Kwa Ng'ombe Wengi Ila Tunaagiza Maziwa Kutoka Nje

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Ukiacha kwamba hii ni fursa naichukia ila ni aibu Kwa Nchi kama Tanzania ambayo Ina mifugo wengi namba 2 Afrika wakiwemo Ng'ombe tukiwa tumezidiwa na Ethiopia tuu ila tunazalisha maziwa Lita kati ya 3.6-4 Bilioni huku tukiagiza Lita Bilioni 10 kufidia upungufu.

Waziri wa Mifugo ni vyema ukahakikisha tunaacha kabisa Kuagiza Maziwa yaani kiufupi walau ukate nusu ya imports by 2025.

Imebainishwa kuwa Tanzania inatumia Sh20 Bilioni kuagiza lita za maziwa 10 milioni ili kukabiliana na upungufu, ambapo huzalishaji wa maziwa kwa sasa ni lita 3.6 bilioni ambayo ni pungufu ya lita 9 bilioni zinazohitajika.

Hayo yamebainishwa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Nchini, Dk George Msalya alipozungumza na Mwananchi Digital kwenye mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dodoma.

Kusoma makala kamili tembelea tovuti ya Mwananchi na Youtube

My Take
Tanzania tunatia aibu sana yaani hakuna Cha manaa tunafanya vizuri Kimataifa.

Badala ya kulaumu Serikali ngoja tukamatie fursa ya maziwa na nyama ya Ng'ombe.
 
Hata huku mtaani maziwa yapo changamoto ni kuwa kati ya hizo lita 3.6 - 4 bilioni basi 2 bilioni ni maji, sasa si bora tuagize tu huko nje

Kuliko kunywa maji yenye rangi ya maziwa
Wala msijari wanaweka maji Kwa sababu wanaxalisha kiduchu sana.

Nimeona Kuna fursa hapa nitaanza uzalishaji wa original Ili niwe na wateje wa uhakika
 
Ukiacha kwamba hii ni fursa naichukia ila ni aibu Kwa Nchi kama Tanzania ambayo Ina mifugo wengi namba 2 Afrika wakiwemo Ng'ombe tukiwa tumezidiwa na Ethiopia tuu ila tunazalisha maziwa Lita kati ya 3.6-4 Bilioni huku tukiagiza Lita Bilioni 10 kufidia upungufu.

Imebainishwa kuwa Tanzania inatumia Sh20 Bilioni kuagiza lita za maziwa 10 milioni ili kukabiliana na upungufu, ambapo huzalishaji wa maziwa kwa sasa ni lita 3.6 bilioni ambayo ni pungufu ya lita 9 bilioni zinazohitajika.

Hayo yamebainishwa na Msajili wa Bodi ya Maziwa Nchini, Dk George Msalya alipozungumza na Mwananchi Digital kwenye mahojiano maalumu ofisini kwake jijini Dodoma.

Kusoma makala kamili tembelea tovuti ya Mwananchi na Youtube
View attachment 2772763

My Take
Tanzania tunatia aibu sana yaani hakuna Cha manaa tunafanya vizuri Kimataifa.

Badala ya kulaumu Serikali ngoja tukamatie fursa ya maziwa na nyama ya Ng'ombe.
Huenda kweli tukawa na upungufu wa maziwa nchini lakini sio kwa kiwango hicho, mimi naamini maziwa mengi yanayozalishwa na wafugaji wadogo wadogo yanaharibika kabla ya kufika sokoni, nakumbuka kwenye maonesho ya Nanenane mwaka huu, wafugaji wa ng'ombe wilaya ya Rungwe walikuwa wakilalamika maziwa kukosa soko na matokeo yake kulazimika kuyauza kwa bei ya chini mno

Inaonekana zao la maziwa hasa kwa wafugaji wadogo wadogo halijaratibiwa ipasavyo, kwahiyo ni kazi au jukumu letu sote kuona zao hili linapata usimamizi wa kutosha

Huo upungufu uliopo huenda unachangiwa na watu kuogopa kufuga kwa kuogopa kupata hasara

Sent from my SM-A035F using JamiiForums mobile app
 
My Take
Tanzania tunatia aibu sana yaani hakuna Cha manaa tunafanya vizuri Kimataifa.

Badala ya kulaumu Serikali ngoja tukamatie fursa ya maziwa na nyama ya Ng'ombe.
Nani alaumiwe kama siyo serikali ya chama chako ccm? Nyie chawa mnatia kichefuchefu sana. Toka tupate uhuru serikali ni ya chama chako, ambacho kila siku unakifagilia hapa jukwaani, halafu unageuka na kulalamikia uduni wetu wa kibiashara kimataifa?
Ni afadhali ungeficha huo ujinga kwa kuendelea kuifagilia hiyo serikali ya ccm mchana na usiku.
 
Kwani hao Ng'ombe wana tofauti gani na rasilimali tulizonazo 😂

Tuna kila kitu cha kutufanya tuwe matajiri, ila ndio vile tena.

Omwafrika omwafrika 😂

Nawaambia hivi siku rushwa ikikoma ndio maendeleo yataanza kufata mkondo.
 
Kilimo cha Tanzania kina watu wengi sana, inabidi wapungue ili kupisha watu wachache wenye ufanisi.
Huwezi kuzalisha maziwa mengi kama una watu milioni mbili wenye ng'ombe wawili kila mtu.
Bora uwe na watu elfu moja wenye ng'ombe alf tatu kila mtu.
Bora uwe na ASAS mia mbili, utauza maziwa hata nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom