Mbunge Cherehani: Askari wanyamapori kwenye Maeneo yasiyo na vivutio na wanyama

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
"Uzalishaji wa Tumbaku kwa miaka miwili ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imepanda mpaka mwaka 2023 zimezalishwa Kilo Milioni 122 sawa na dola za kimarekani Milioni 341 za Tumbaku. Msimu wa 2023-2024 wanunuzi wameongeza Uzalishaji wa tani laki 214 ambazo ni zaidi ya Shilingi Bilioni 900" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu

"Kwenye upande wa Maliasili na Mifugo, tuna hifadhi zina Vivutio na wanyama, lakini tuna hifadhi ambazo hazina Vivutio na hazina wanyama ila tumeweka gharama ya Maskari kulinda maeneo na wakati Serikali haipati chochote na madhara yake ni kuendelea kugombana kati ya Askari wanyamapori na wananchi" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu

"Tuna Hekari nyingi hazina wanyama, misitu inaendelea kuchoka, fedha zinakusanywa zinaingia Mifukoni mwa wachache. Kwanini maeneo haya tusiyatengeneze yawe maeneo ya Malisho ya wananchi wafugaji ili kupunguza migogoro? Migogoro inaongezeka kwasababu wafugaji hawana maeneo ya kulisha Mifugo yao, hawana Maji" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu

"Sensa ya mwaka 2022 tuna Ng'ombe wasiopungua Milioni 36 nchini, kila mwaka kichwa cha Ng'ombe tuchangie Shilingi 2000 tuchunge kwenye Mapori ambayo hayana wanyama na Vivutio tutakusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 7" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu

"Tanzania tuna Mbuzi zaidi ya Milioni 24, tuweke Shilingi 200 tayari tuna Shilingi Bilioni 4.8. Tuna Kondoo wasiopungua Milioni 10 tukiweka Shilingi 200 tutakusanya Shilingi Bilioni 2. Tuna Punda wasiopungua Milioni 1" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu

"Askari wanyamapori tumewapa Bunduki wakagombane na wananchi. Hakuna watalii, hakuna wanyama na hakuna Vivutio. Kwanini tusiwape kazi ya kuwalinda wananchi wetu wachunge Mifugo vizuri badala ya kukaa na bunduki tuwape POS ambapo kwa mwaka watakusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 80 za kuchimba mabwawa Wizara ya Mifugo na Kliniki ya Mifugo" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu

"Tuna Lanchi za Taifa zaidi ya Hekari laki tano, lanchi zinalindwa kwa gharama kubwa sana, Serikalini tunapata nini? Tuzitengeneze Wizara zetu badala ya kumtegemea Waziri wa Fedha atupe fedha ila Wizara zipeleke fedha Wizara ya Fedha kwaajili ya manufaa ya Taifa" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu

"Migogoro imeongezeka kwasababu wafugaji wanakimbia maeneo yao wanaenda kutafuta Maji na Malisho. Tukienda kuwachimbia mabwawa kwenye maeneo yao kwa makusanyo kupitia Mifugo tutaepusha migogoro" - Mhe. Emmanuel Cherehani, Mbunge wa Jimbo la Ushetu.

 
Mmeefyeka mapori kuanzia Ibelansuha Ikwenuko Mbika mpaka Ulowa namba 100

Kilimo cha Itumbate ni Janga ...Dhahabu ya Nyenyela haichimbiki
 
ANA SHDA SANA KATIKA MFUMO WA UFAHAMU.mapori yanahifadhiwa kwajili xa kutunza mazingira na uoto wa asili na siyo utalii.tukichunga na kulima horera tutageuza nchi kuwa jangwa.wenzetu walichelewa kujua mapema kutunza mazingira leo wanajuta.TUTUNZE MAZINGIRA NAYO YATUTUNZE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom