Shakazulu
JF-Expert Member
- Feb 23, 2007
- 957
- 281
Tanzania yatangaza mpango mpya wa kuuza nyama
*Mabucha ya nyama kupigwa marufuku nchini kote
* Nyama kuuzwa Supermarket na maeneo maalum
Na Muhibu Said
SERIKALI inapanga kupiga marufuku uuzaji nyama kwenye mabucha na badala yake biashara hiyo itakuwa ikifanywa na maduka makubwa (supermarkets) na maeneo maalum yatakayotengwa nchini.
Mpango huo mpya ambao serikali imedhamiria kuutekeleza kwa dhati wakati wowote katika siku za usoni, ulitangazwa na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo, Anthony Diallo, alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, jijini Dar es Salaam jana.
Waziri Diallo alisema mpango huo umelenga kukidhi mahitaji ya afya za walaji wa nyama na soko la nje la bidhaa hiyo na kwa kuzingatia hilo, wizara yake inafanya mazungumzo na halmashauri ili waweze kuanza kuutekeleza.
Alisema utayarishaji wa nyama katika mabucha unaofanywa kwa ajili ya kuwauzia walaji hivi sasa, umekuwa ukitishia afya zao kutokana na wauzaji kutumia nyenzo zilizotumika kwa muda mrefu, kama vile magogo ya kucharangia nyama, ambayo ubora wake haukidhi mahitaji ya afya.
?Yapo magogo mengine kwenye mabucha yana umri mrefu kuliko hata umri wenu mliopo hapa, yanaendelea kutumika kukatiakatia nyama,? alisema Waziri Diallo huku akiwanyooshea kidole waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wake wa jana.
Alisema mpango huo mpya, utawezesha nyama inayotayarishwa nchini kukubalika kuuzwa katika soko la nje ya nchi kwa kuwa bidhaa hiyo itakuwa imetayarishwa na kuhifadhiwa katika mazingira mazuri.
?Tunazungumza na halmashauri tuweze kubadilisha uuzaji wa nyama ili ziweze kuuzwa kwenye supermarket au kwenye maeneo maalum. Haiwezekani iwe inauzwa kwenye mabucha,? alisema Waziri Diallo.
Mbali na hilo, Waziri Diallo alisema wizara kwa kushirikiana na wadau wengine, imepanga kuongeza uzalishaji wa maziwa na kupanua soko lake nchini, ikiwa ni pamoja na kuhamaisha unywaji wa maziwa na kutekeleza Mpango wa Unywaji Maziwa Shuleni (SMP), ambao unatarajiwa kutekelezwa katika mikoa yote.
Kwa sasa SMP inatekelezwa katika wilaya za Arusha, Hai, Moshi Vijijini, Tanga na Njombe katika shule 39 na inafadhiliwa na wazazi na wasindikaji wadogo.
Alisema wizara imeshauriana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ambalo limeahidi kuitafutia serikali wafadhili zaidi kwa ajili ya kusaidia kupanua mpango huo katika wilaya nyingine nchini kwa lengo la kuwanufaisha wanafunzi 840,000 kutoka 12,985 wanaonufaika kwa sasa.
Waziri Diallo alisema wizara pia imewasiliana na kampuni mojawapo kubwa ya maziwa duniani ya TETRAPAC kuhusu SMP ambao nao wameahidi kushiriki iwapo serikali itaanzisha mpango huo.
Alisema kutokana na mpango huo, kiasi cha lita milioni 43.7 za maziwa zitanyweka shuleni ikilinganishwa na lita 337,610 zinazonyweka kwa sasa.
?Mpango wa unywaji maziwa shuleni unalenga kuboresha afya za watoto, kuongeza mahudhurio shuleni, kujenga utamaduni wa kunywa maziwa, kupanua wigo wa soko la maziwa na kuongeza ajira,? alisema Waziri Diallo.
Alisema baada ya Sheria ya Maziwa kupitishwa na Bunge mwaka 2004, Bodi ya Maziwa ilianzishwa na tayari imeshaanza kazi na kwamba utaratibu unaandaliwa wa kuanzisha Bodi ya Nyama baada ya sheria husika kupitishwa na Bunge mwaka juzi.
?Sheria hizi zitasimamia ubora wa bidhaa husika kuanzia kwa mfugaji mpaka usindikaji na uuzaji wake ili ufikie viwango vya kimataifa na kuiwezesha nchi kuuza bidhaa bora ndani na nje ya nchi,? alisema Waziri Diallo.
Alisema serikali pia imeanzisha mfumo wa utambuzi, usajili na ufuatiliaji wa mifugo nchini ambapo kupitia mfumo huo, mifugo yote, hususan ng?ombe itatambuliwa, kuandikishwa na kufuatiliwa ili kuhakiki ubora wa mifugo kuanzia katika maeneo inakofugwa.
Diallo alisema katika kutekeleza mfumo huo, mifugo yote, hususan ng?ombe kwa kuanzia, itatakiwa kuvikwa hereni maalum na kwamba mifugo yote itakayouzwa minadani ni ile ambayoimeandikishwa kwenye Rejista ya Taifa ya Takwimu za Mifugo nchini.
Alisema kwa kutumia mfumo huo, katika mwaka 2006/2007, wizara itasajili mashamba ya mifugo 100 na wafugaji 5,000, wakiwamo wa asili, kutambua ng?ombe 20,000 na kuanzisha Rejista ya Taifa ya Takwimu za Mifugo.
Diallo alisema serikali pia inaandaa mpango wa kitaifa wa unenepashaji ng?ombe nchini ambao utekelezaji wake utasimamiwa na serikali za mitaa.
Alisema mpango huo utahusisha unenepeshaji wa mifugo, hususan ng?ombe wa nyama katika umri wa kati ya miaka miwili na mitatu kwa lengo la kuongeza uzalishaji wa nyama ili kukidhi mahitaji ya soko na kwamba katika mwaka 2006/2007 takriban ng?ombe 26,400 walinenepeshwa kupitia mfumo huo.
Hata hivyo, Diallo alisema wizara inaendelea kuhamasisha uzalishaji wa nyama kupitia mfumo huo kwa wafugaji wadogo kwa kutumia mbinu shirikishi ya shamba darasa (FFS).
Alisema katika mwaka 2006/2007, mauzo ya mifugo na mazao yake yaliyouzwa nje ya nchi, yaliliingizia taifa jumla ya Sh17.3 bilioni ambapo katika mauzo hayo, jumla ya ng?ombe 2,542 na mbuzi 1,852 wenye thamani ya Sh1.3 bilioni waliuzwa nchini Comoro, Kuwait, Falme za Kiarabu (Dubai), Oman na Burundi na tani 92 za nyama ya mbuzi, kondoo na ng?ombe zenye thamani ya Sh352 milioni ziliuzwa nje ya nchi.
Kwa mujibu wa Diallo, Tanzania inakadiriwa kuwa na ng?ombe milioni 18.8, mbuzi wakiwa milioni 13.5, kondoo milioni 3.6, nguruwe milioni 1.37, kuku wa asili milioni 33 na wa kisasa milioni 20 .
Alisema zao la ngozi limeendelea kuwa zao kuu la mifugo linaloliingizia taifa fedha za kigeni ambapo jumla ya vipande vya ngozi za ng?ombe milioni 1.7, mbuzi milioni 1.5 na kondoo 925,530 vyenye thamani ya Sh16.2 bilioni viliuzwa nje ya nchi katika kipindi hicho.
Waziri Diallo alisema mkakati wa kudhibiti ugonjwa wa sotoka, umetekelezwa kwa mafanikio makubwa ambapo Tanzania imetambuliwa na kupewa cheti na Shirika la Afya ya Wanyama Duniani kutokana na virusi vya ugonjwa huo.
Alisema pia mkakati wa kudhibiti ugonjwa wa Homa ya Bonde la Ufa (RVF) uliotokea nchini kuanzia Februari, mwaka jana, unatekelezwa na kwamba serikali ilitoa Sh4.798 kudhibiti ugonjwa huo na pia mkakati wa kudhibiti ugonjwa wa mafua makali ya ndege, unatekelezwa kwa kujenga uwezo wa kutambua na kufuatilia ugonjwa huo.
Hata hivyo, alisema hadi sasa ugonjwa huo haujathibitika kuwapo nchini ingawa umetokea katika nchi 55, zikiwamo kumi na moja za Afrika ambazo ni Burkina Faso, Cameroon, Ivory Coast, Djibout, Ghana, Misri, Niger, Nigeria, Sudan, Benin na Togo.
Alizitaja changamoto zinazoikabili sekta ya mifugo kuwa ni pamoja na maeneo ya ufugaji na uhaba wa miundombinu ambayo yamesababisha wafugaji kuhamahama na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, kuenea kwa magonjwa ya mifugo na migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi.
Nyingine ni uwekezaji mdogo katika sekta ya mifugo ambao umesababisha ukuaji mdogo wa sekta kuliko ilivyotarajiwa, kuwapo kwa magonjwa mbalimbali ya mifugo, tishio la ugonjwa wa mafua makali ya ndege, uhaba wa viwanda na uzalishaji duni wa vilivyopo kwa ajili ya kusindika mazao ya mifugo, ukosefu wa masoko ya uhakika, kutokuwapo kwa taasisi za mikopo yenye masharti nafuu kwa wafugaji, tija ndogo katika uzalishaji wa mifugo hasa ya asili na gharama kubwa za pembejeo za mifugo, zikiwamo dawa za kuogeshea mifugo.