Nelson Jacob Kagame
JF-Expert Member
- Dec 26, 2022
- 9,544
- 13,034
- Thread starter
- #141
Pamoja mtani
Pamoja mtani
Daah kama movieee.wee mdau saluteNAENDELEA........!!!!
Nilikua kimya kidogo sababu nilikua kwa wabangubangu huko nafuatilia dili flani afu tukadakwa na masoja wahuni waliopinda balaa wa FARDC katika road block ya barabarani kati ya mji wa Lellwa na Kamombo wakitudhania sisi ni wahalifu tunawauzia silaha banyamulenge,silaha za kutokea Uganda au tunanunua madini ya vikundi vya waasi na kuyavusha ziwa Tanganyika mpaka Burundi.
Ikabidi tukae ngomeni.......mpaka pale wadau walipokuja kututolea dhamana
NAPOMAANISHA DHAMANA NI KWAMBA WADAU WALIVAMIA NGOME NA KUZICHAPA MCHANA KWEUPE WAKIDAI WANAWATAKA WASWAHILI WAO ESPECIALLY MIMI WALIEKUA WANANIITA KALULU MTOTO YA ZANZBARNA LILIKUA SHAMBULIZI LA SUPRISE SO IKABIDI TUACHIWE HURU MAANA MASOJA WALIKIMBIA NA KUTELEKEZA KAMBI AMBAYO ILIKUA KAMA KITUO KIDOGO CHA KUKAGULIA MAGARI BARABARANI KATI YA MJI WA LWELLA NA KAMOMBO BASI WADAU WAKATUTOA KINGUVU SISI NA WASHIRIKA WAO WENGINE WALIOKAMATWA KIPINDI HICHO*
Ila wale manjagu wahuni wa FARDC walitupukutisha mzigo wote wa mawe tuliopewa kuupeleka BURUNDI kimagendo kwa kuuvusha ziwani....na mpaka mda huu nipo na ugomvi na MWANANGU NDAGARA....maana alidai mm nina roho nyepesi sana ndio maana wale wanoko wa FARDC wamechukua mawe yetu......SASA NIPO SEHEMU SALAMA NIMETULIA ngoja niwape story kidogo...!!!
Kuna braza wetu mmoja wa kuitwa. ""NDAGARA""" yeye amezaliwa katika mji mmoja wa mpakani mwa DRC na Burundi ambao unaitwa MIDUHA....anaishi Nairobi alikuja masikani na dili la kuchukua mawe kinyemela kutoka DRC na kuyavusha Burundi....afu baada ya hapo""YANAUZIKA BILA KUKATWA KODI""".
Braza akasema ni issue ya wiki tatu tu tunamaliza kila kitu....mchawi pesa ya mtaji tu...
Akasema ameshawapanga watu wake Burundi na DRC na mizigo wanayo.....kwahiyo ni sisi tu...twende MIDUHA au tumtumie hela amalize kila kitu.......TUKAPIGIANA HESABU ZINAHITAJIKA MILIONI 60 ZA KIBONGO.....KWA KUANZIA AMBAZO ZITAZAA MILIONI 314 KAMA MZIGO UKIVUSHWA SALAMA BURUNDI......!!!
Kama mnavyojua ndugu yenu napenda hela.....afu hapa nilipo nimepigika na mwaka ndio unaanza.....nikaona hii fursa ngoja nichungulie........
Kama kweli unaweka milioni 60 na unapata 314 ndani ya wiki tatu.....basi mchawi mtaji...ngoja mtaji utafutwe hata kwa kukopa.
Hapa town sisi watoto wa mjini hatuna hela.....ila hela ya kula sio issue na hela za kukopa sio issue wala kupata asset za kuweka bondi sio issue"""""MAANA TUNAAMINIKA""".
Unajua TANZANIA kuna watu wana hela ila kama hawakujui hawawezi kukukopesha sababu pesa nyingi zinapitia mlango wa nyuma kuingia mifukoni mwa watu....
Safari hii nikawacheki wahindi mabraza zangu wa migodini huko kwa wasukuma""BIG UP BRAZA PATEL""" ....nikampa mchongo wanikope hela afu bondi nawaachia gari na trekta la kulimia vikae yadi mpaka hela itakapoanza kurudi.
Tukahesabiana siku 60 bila riba
WANA FAMILIA HATUTOZANI RIBA
Hela ikapatikana ikawekwa kibindoni sehemu salama ambayo mimi niliyekopwa na mkopeshaji tunaijua afu ndio nikakaa mezani kusikiliza hilo dili.....maana lilivutia.
NDAGARA: Mpango upo hivi...ni kwamba kule DRC hasa maeneo ya KIVU KUSINI hasa miji ya LUBENGA,KASABA,MALUNGU,KAHOLOLO, KILEMBWE NA TULAMBO....kuna mawe ya kumwaga ni sisi kununua tu na kuyavushia ITARA au KAKAMBA na kuyauzia MIDUHA kwa wadau wa kununua mawe.....kila kitu kipo under control.....na biashara ikiwa nzuri tutahamishia makazi BUJUMBURA kwa mda ili tupige hela..!!!
MIMI: Mkuu hii dili unachosema nakuelewa ila sasa kuna risk kubwa...afu mtaji wakuanzia milioni 60 tena za kukopa ni mdogo mno,......afu hapo hatujaweka gharama za usafiri na mambo mengine ya kibiashara...
MIMI: Kwanini tusijipe wiki mbili twende kigoma afu tuvuke ziwa tuingie burundi then tufuatilie soko sisi wenyewe kwa kutazama na sio kuambiwa.....MAANA MANENO YA KUAMBIWA CHANGANYA NA YAKO.
NDAGARA: Dogo sikia unachosema mimi nakuelewa.....wewe tafuta milioni sitini ya mtaji wako na mimi nina pesa ya mtaji wangu milioni sitini.
Hatutoingia kwenye biashara mpaka tufanye uchunguzi....ili tuone maneno niliyoambiwa ni kweli....
Gharama za kwenda safari yetu ya kuchunguza nadhani itatugharimu milioni mbili za kitanzania kila mmoja......sababu kule Burundi mimi ni nyumbani....na nina wadau wengi kwahiyo kwa kule gharama hazitokuwepo.
*NDAGARA ALIPOSEMA WADAU ALIMAANISHA WAASI WA MSITUNI KULE KONGO AMBAO WANATAFUTA MASOKO MAZURI YA KUUZIA MADINI YAO....SABABU HAWATAKI KUWAUZIA WANYARWANDA NA WAGANDA WAKIDAI WANAWAPUNJA MGAO
NDAGARA alinificha mengi ili nimpe kampani ila niliyajua nilipofika BURUNDI na kukutana na wazee wa kazi.....!!!!
Kesho yake asubuhi
Ndagara katoka Nairobi kaja dar afu tukakaa chini na kupangiana mipango ya kwenda kuchungulia fursa na ikiwa nzuri tunajitosa hivyo hivyo kila mtu na mtaji wa kukopa....
Mimi nikamcheki braza PATEL na kumwambia zile siku 60 asizihesabu maana bado sijaanza hiyo biashara rasmi,na kama ni biashara ya uhakika nitamuingiza na yeye aongeze mtaji.....ngoja nikaichungulie kwanza.....na katika zile milioni 60....tutoe milioni mbili za safari afu zingine akae nazo kwanza mpaka mimi nikiona biashara ipoje ndio nimwambie.
Na zile bondi zangu arudishie wadau wangu wakae nazo zisikae yard tena,sababu biashara bado kuanza.
Mimi naingia kigoma mara moja....kisha navuka ziwa naingia Burundi kibishi kuchungulia fursa na kukutana na wadau wa huko.
Jamaa yangu Ndagara kanihakikishia hao wadau wana mizigo ya kutosha ila tatizo ni wanunuzi tu wa kimagendo wa kuaminika na wao.
Fasta nikakamata gari mpaka kahama....pale kahama nikakamata gari mpaka Nyakanazi.....pale Nyakanazi nikakamata gari mpaka Kakonko......Kibondo........Kasulu.... then nipo town Kigoma ....mji wenye kumbukumbu nyingi na mimi since 1996............!!!
Ndagara tunakutana Kigoma mjini mitaa ya Mwanga afu tunakaa chini kupanga mpango kazi wa kukutana na wadau wenye mzigo....na namna ya kuvuka ziwa kimya kimya mpaka upande wa Burundi.....either tushukie mji wa KABEZI au GITAZA .....kule juu Bujumbura wachawi wengi ni noma!!!!
KUMBUKA SIKUJUA WADAU KAMA NI WABABE WA VITA HUKO DRC WATU WALIOPINDA BALAA*
Kaa chonjo nije nikupe kilichoendelea huko maana vita wewe visikie tu ila usiombe vikukute....!!!
ITAENDELEA................!!!!
Anko umenikumbusha mbali sana hivi wale kabila fulani hivi jina nimesahau,TUNAVUKA MPAKA NA KUINGIA DRC!!!!!
Basi wenyeji wetu wakatuletea ugali na samaki tukala...baada ya hapo tukafunga funga mabegi yetu madogo ya mgongoni!!
Kumbuka tulikua porini nje kabisa ya mji mdogo wa Miduha......pale tulipokua ni kilimani maana ukishuka kidogo tu unaingia DRC kwenye misitu na mapori kati ya mji wa Bukavu na Uvira uelekeo kuelekea mji wa Kitenge,ambapo ndio starting point ya kuanzia tour yetu ya kutazama fursa.
Sasa wale wadau wetu wakatugongea mlango"""Hey bana tanganyika mko kwa fuasi tuondoke bayemba bayemba"""""
Ndagara akawajibu""""Nzala bayemba bayemba tuko kwa fuasi"""""
Wakatupokea mabegi yetu na tukatoka nje ya nyumba na kushuka chini kilimani mpaka chini kabisa..
Daaaah na msimu wa mvua ulikua ndio umeanza maana niliambiwa kule DRC kwenye misitu mvua inanyesha miezi kumi kwa mwaka mzima sasa sijui ni ukweli ila mimi nilikuta mvua kubwa tu kwa siku zoote nilizokaa misituni kati ya Burundi na DRC.
Waongozaji wetu walikua watu watano....watatu walikua na silaha na wawili walibeba mabegi yetu na mizigo yao.
Wote walivalia kiraia kama sisi na ilikua saa tano kasoro asubuhi ila kulikua na ukungu mkubwa kwa sababu ya mvua.
CHANGAMOTO YA KWANZA:
Pale tu tulipofika kule chini kilimani kabla harujatembea umbali mrefu ili kuingia aridhi ya DRC tulikutana na kundi kubwa la asikari wa jeshi la Burundi wakiwa katika doria ya mpaka wao dhidi ya waasi wa kitusi wa kirundi waliojificha kwenye misitu ua DRC hasa kutokea jimbo la Kivu kusini.
Muongoza msafara akatoa ishara tusimame na kulala chini kwenye majani na tutulie tuli......!!!Wao walikua hawatuoni ila sisi tunawachora tu walipokua wanapita kichakani kwa mstari mmoja ulionyoooka huku wengineo vichwani wakiwa wamebeba masufuria na madumu na silaha na kuni wanaongozana kuelekea destination ya doria yao.Sisi pale chini tumelala tuliiii....mpaka wakapita wote na idadi yao ni kama 150 hivi na ushehe.
Walipopita basi sisi hao tukainuka na kuvukia upande wa DRC na kuendelea na safari yetu.
Kumbuka tunapitia pori kwa pori na hakuna barabara zaidi ya kukata majani ya miti na mapanga na kuvuka mabwawa ya maji yaliyosababishwa na mvua zinazonyesha mwanzo huu wa mwaka.
Baaada ya masaa matatu au manne kutokea pale mpakani tukafika sehemu ya kijiji kinaitwa Punge na wakazi wa pale ni wa kabila moja na wale waongozaji wetu...na hapo ni katikati ya Uvira na Bukavu katika uelekeo wa kuelekea mji wa Kitenge.
CHANGAMOTO YA PILI:
Wakati ndio tumefika nje ya nyumba ambayo ndio tunatakiwa tupumzike pale Punge ghafla tukasikia mlio ya miluzi na wenyeji wetu wakatuchukua haraka kutukimbiza kwenye mashimo yaliyokua katikati ya ua wa ile nyumba na kwa juu wameweka mawe makubwa ya kusagia unga wa mihogo.
Ndani ya yale mashimo ni kama mahandaki kumeifadhiwa magunia ya mihogo mikavu kwenye vichanja vilivyojengewa humo humo shimoni kwa utaalamu wa ngazi kwa ngazi......na yale mashimo ni marefu futi sita kwa tisa kama sikosei hivi....kwa juu ndio wameweka vifuniko vya majani na mawe ya kusagia ili kupata unga wa mihogo.
Nilikuja kujua baadae kua wanafanya vile ili kutunza akiba zao za chakula dhidi ya wezi na waasi na wanajeshi wa vikosi vya serikali ya DRC.
Tukaingia mle ndani haraka sisi wote watu saba.
Ila kuna matundu madogo madogo kwa juu unaweza kuchungulia nje....mara nasikia milio ya magari na viatu vya watu vinakimbia kimbia.....nikainuka kuchungulia na kuona pale juu uwanjani zimepaki landcruser za kijeshi kama tano na wanajeshi wameshuka na kuanza kukagua kagua nyumba za pale kijijini na kuzungumza na wanakijiji afu baadae wakaondoka.
Baada ya mda nikasikia mluzi tena na wakaja watu wakatoa lile jiwe kwa juu,afu wakatuwekea ngazi tukatoka taratibu mpaka nje.
Tukapelekwa mpaka kwenye ile nyumba ya mwanzo tukaingia ndani....tukakaa chini tumechoka kweli na hiyo ilikua mida ya saa kumi kasoro.
Hapo tukapumzika kidogo na tukapatiwa uji wa mihogo afu safari ikaendelea mida ya saa moja jioni.....hapo kila mtu na tochi yake mkononi ila haturuhisiwi kuziwasha mpaka kiongozi wa msafara atoe ruksa....sababu kuwasha taa usiku ni hatari sana hasa msituni.
CHANGAMOTO YA TATU:
Tulipotembea umbali mrefu mpaka saa nne za usiku tukaamua tupumzike katika eneo ambalo ni kambi ya waasi wa KIBANGU BANGU waliyokua wameitelekeza baada ya kushindwa na vikosi vya majeshi ya FARDC na kukimbia.
Kambi yenyewe ni vibanda vilivyovunjika na majani yameota kila mahali maana kambi ilikua imetelekezwa mda mrefu.
Tukachagua vibanda vyenye nafuu kidogo tukajiegesha tujipumzishe.
Mda hata hatujatulia kidogo tukaanza kusikia mlio ya risasi kwa mbali......basi fasta fasta wale waongozaji wetu wakatutoa eneo lile na kuingia pembeni kwenye misitu ile na kutupandisha juu ya miti na rochi zote zikazimwa tukabaki tunaisikilizia ile milio ya risasi.
Milio ile ghafla ikakoma afu kujawa kimya sana na tukaanza kusikia vishindo vya watu wanaokuja kwa kukimbia na kumbe ni Wabangu bangu militia,s wamerudi kuchungulia kambi yao waliyoitelekeza.
Na kiasili Wabangu bangu na Makemba Bunene ni maadui wa jadi kwa sababu wote ni wezi wa madini na wanatafuta kumiliki maeneo na kuisumbua serikali ya DRC.
Mara zikaanza risasi kulia kuja ule upande wetu ila zinapita kwa chini....ni usiku unaona cheche na kusikia matawi ya miti mifupi inakatika tu....kwa mda wa dakika tatu afu kukawa kimya kwa mda wa nusu saa......mara ukasikika mluzi tena na vishindo vya watu kuondoka eneo la kambi ile kwa kukimbia na kuimba nyimbo zao....kumbuka sisi tupo pale juu ya miti tunasikilizia.
Baadae wale waongozaji wetu wakatuambia huenda wale wabangu bangu walipata taarifa kua kambi yao imevamiwa tena na wanajeshi wa serikali wa FARDC kutoka Bukavu au Uvira au waasi wa kinyarwanda na....ndio maana wakaja kuwaharibia ila walipofika wakakuta kambi ni tupu ndio maana wakaondoka.....na waliowapa taarifa ni watu wao MBILIKIMO WA MSITUNI ambao walitufananisha na wanajeshi wa FARDC au waasi wa kinyarwanda.
Tulishuka pale juu ya miti taratibu na tukaendelea na safari yetu mpaka usiku wa manane ndio tukafika kijini kilichochangamka kiitwacha Zendi au Zendika sikumbuki vizuri na hapo ni eneo rafiki kwa waongozaji wetu,,,,tukapata nyumba ya nyasi ya kupumzika ambayo ndani yake mlikua ni kama ghala la vifaa ila tukatandika chini matandiko tukalala tumechoka balaa maana tumetembea masaa manne au matano bilia kupumzika afu ni usiku wenye baridi balaa.
Ili asubuhi tukiamka tuendelee kuitafuta KITENGE ambayo ndio starting point yetu ya kutazama fursa.
CHANGAMOTO YA NNE:
Mda wa alfajiri nikashitushwa na Ndagara aliesema dogo vaa vizuri tuondoke maana huku usijiachie kama nyumbani Tz.Fasta nikaweka vitu vyangu sawa na kutoka nje ya ile nyumba tuliyofikia.
Kumbe bhana kijiji kizima wana Zendi ni masoja na hakuna akina mama wala watoto bali wazee wa kazi....na kile kijiji ni kambi yao isiyo rasmi....afu wake na watoto wao wanawaficha porini au kwenye miji mikubwa mikubwa especially kwenye mji wa KITENGE.
Na taarifa zetu zoote walikua nazo kutuelezea sisi ni kama wadau ambao tunaweza kuwatafutia masoko ya uhakika ya kuuzia mawe yao nchini Kenya na Tanzania.
Basi wakaongea kibangu bangu pale na bro Ndagara afu tukapewa makoti ya kuzuia mvua.....tukaanza safari ile alifajiri pori kwa pori....kuutafuta mji wa KITENGE....!!
DRC bhana hakuna barabara za uhakika hasa kipindi cha mvua na hakuna usalama kabisa maeneo ya mashariki...maana ilikua tukitembea mara tusimame tuchunguze uelekeo....mara tujifiche wakija watu karibu yetu.
Kwahiyo mwendo wetu ulikua wa pole pole pori kwa pori afu mvua inanyesha na inakata.
CHANGAMOTO YA TANO:
Humo njiani tukielekea mji wa KITENGE tulifika sehemu ya milimani hivi,kuna uwanda mkubwa wa majani majani.Tulikuta vita kati ya waasi wa vikundi vidogo vidogo vya waasi walikua wamedhulimiana madini.
Ikabidi tutulie huku juu ya kilima huku wale waongozaji wetu wakitafuta njia salama ya kupita chini ya vile vilima.
Tatizo la waasi wanapigana kama watoto....mara wanakimbizana...mara wanasimama na kutukanana...mara wanaimbaimba na kukata mauno....mara wavute bangi....mara wapige risasi hewani......Basi ilikua tafarani......ilibidi tutulie kule juu ya kilima masaa matatu afu ndio tuangalie utaratibu wa kushuka chini ya vile vilima ili tuendelee mbele uelekeo wa mji wa KITENGE.
Hiyo ilikua inaelekea adhuhuri na tulikua hatujapumzika toka asubuhi ila kwa sababu ya mvua hakukua na jua kali mpaka mda huo.
ITAENDELEA.........!!!!!!!
😂🤣🤣🤣 WALUBA HAO WA KATANGAAnko umenikumbusha mbali sana hivi wale kabila fulani hivi jina nimesahau,
Wakienda battle wanakata mauno balaa na vigoma vyao na firimbi kisha ndio wanalianzisha unawafahamu?
Ewaaaaaaaaah,kabisa kabisa hahahahaaaaaaaaa daaaah Congo ina mambo wallah😂🤣🤣🤣 WALUBA HAO WA KATANGA
Usijali mdogo wanguNelson Jacob Kagame asante aisee nasubiri episode zingine