Mabraza wa enzi hizo Dar kumbukumbu zangu

Mabraza wa enzi hizo Dar kumbukumbu zangu

Na mwaka huo 1994.....kizazi cha mabrza wengi walianza kwenda ughaibuni
Wengi wamejaa Columbus Ohio, Dallas &Houston, St Louis, NY, Wichita etc ukienda miji huyo lazima ukutane hata na mmoja, wengi watu wazima watoto wao wameshamaliza college na wengine Wana wajukuu kabisa, generations zako sasa ni Americans na wakirudi bongo ni wao peke yao sio watoto wao, soon or later majina kama Mushi, Rweyemamu, Bundala etc yataanza kuwa kawaida in US
 
KU ilikuwa na watu kuanzia Masaki na Obay mpaka Ilala na Temeke huko.

Huyo dada utakuwa unamuongelea Regina. Alikuwa anapenda sana basketball.

Hayo mambo ya magari ilikuwa habari za Idi, akibadilisha mara Audi, mara Toyota Hilux, akipiga misele.

Idi mtu poa sana lakini kwangu, kuna siku niko darasa la nne Muhimbili, basi kuna mwalimu mkuda katuchelewesha darasani saa nane hajatuachia. Huko nje dereva wetu kakaa tu anasubiri muda mrefu. Idi akachukua dhamana ya kuchukua jina langu kwa dereva akaja mpaka darasani akamwambia mwalimu huyu jamaa anatakiwa nje kuna dereva katumwa kuja kumchukua.

Ilibidi mwalimu aturuhusu tutoke.

Kuanzia siku hiyo Idi akawa mshkaji poa sana.
Mimi mtoto wa Kota za Tanesco Morocco opposite na Driving Cinema nawakumbuka kina Regina mtoto wa Mengi na boy wake Patrick mchambuzi wa mpira now moja ya channel pendwa nchini na washkaji wengine, walikuwa wanapenda sana kuja kucheza basketball kwenye viwanja vya Kota week end asubuhi. Wakishamaliza mimi (dogo lao) ndio wananiagiza soda za Coca-Cola kwenye duka letu lilikuwa karibu na viwanja. Hiyo miaka ya 2000's Regina anakuja na BMW sijui ya mzee wake, Ila sasa amekuwa mtu mzima.
 
Hv bro na yule braza smati sana alikua anajiita Cool James......alikua akija dar kutoka Sweden ilikua balaa na kigari chake kile enzi hizo early 90,s...Unamkumbuka?????
Anavaa pamba kali afu kasuka na alikua makamo yenu ila baadae alifariki miaka ya 2000,s...kwa ajali ya gari..
Unamkumbuka???
Alipata ajari Makumbusho Kijitonyama akiwa anatoka club night kali. Kipindi hiko alikuwa anatoka na Sinta muigizaji aliyemuimba Juma Nature. Ila Juma alimpenda Sana huyu demu 🤣
 
Braza ulipiga skul o level wapi???
Nimesoma Jite enzi hizo
Tuliwapa kichapo Tambaza uwanja wa taifa, fainali ya Umiseta, nilikuwepo live sio mchezo
Tulipiga sana, mawe yalirushwa ndani mule na Tambaza, tukawatoa nje , na kufunga geti, halafu tuka re group, tilivyo fungua geti, walitafutana, huko mbele wakakutana na wajeshi wetu Taifa B, nwengine tuliwaingiza kambini na kuchapa sana, wakimbilia huko Chang'ombe /Keko wakamalizia hasira kwa kumuua konda..
Kuanzia hapo ikawa ni vita sana Tambaza tukikutana stendi shule ya uhuru au kariakoo, maana tulikuwa tunaambiwa shule kabisa na wajeshi tembeeni kuanzia watano pamoja....
Hii ilendelea mpaka na ilikuwa moja chanzo cha Tambaza kufungwa,
Nakumbuka mpaka polisi iliingilia, wanafunzi wetu walieenda kwenye gwaride la utambulisho na kusonta tu wa Tambaza.
Kesi zikazidi mpaka Wizara ikaamua kuwa shule ifungwe....
 
So sad baadhi ndio ilikuwa mwisho wa safari yao ya elimu.
Lakini ilileta amani na utulivu jijini, vipigo kwa makondakta vilipungua ndio ilikuwa mwisho wa vurugu zilizozababishwa groups za vijina town.
Lakini iliua ushindani wa elimu kati boys in Dar. Mwishoni mwa 1990's AzaBoi ikaanza kuporomoka kwa kasi kwenye chati hadi kufikia kuwa shule ya mwisho kitaifa.
Wazazi wenye fedha wakaacha kuwaruhusu vijana wao kusoma Azania.
Lakini kabla the Old Tambz haijavunjwa 1994, vijana wengi waliomaliza na kufaulu AzaBoi na Tambz walifika mlimani na walioshindwa kabisa waliishia Dar Tech, Arusha tech, Mbeya Tech na Mzumbe. Ilikuwa kawaida Wakati wa orientation pale Nkuruma hall kuona reunion ya Tambz and AzaBoys.
True mwaka 94,s ndio ulikua mwisho wa ushindani wa elimu hapa dar......Baada ya tambaza kuvunjwa
 
Nimesoma Jite enzi hizo
Tuliwapa kichapo Tambaza uwanja wa taifa, fainali ya Umiseta, nilikuwepo live sio mchezo
Tulipiga sana, mawe yalirushwa ndani mule na Tambaza, tukawatoa nje , na kufunga geti, halafu tuka re group, tilivyo fungua geti, walitafutana, huko mbele wakakutana na wajeshi wetu Taifa B, nwengine tuliwaingiza kambini na kuchapa sana, wakimbilia huko Chang'ombe /Keko wakamalizia hasira kwa kumuua konda..
Kuanzia hapo ikawa ni vita sana Tambaza tukikutana stendi shule ya uhuru au kariakoo, maana tulikuwa tunaambiwa shule kabisa na wajeshi tembeeni kuanzia watano pamoja....
Hii ilendelea mpaka na ilikuwa moja chanzo cha Tambaza kufungwa,
Nakumbuka mpaka polisi iliingilia, wanafunzi wetu walieenda kwenye gwaride la utambulisho na kusonta tu wa Tambaza.
Kesi zikazidi mpaka Wizara ikaamua kuwa shule ifungwe....
Yule konda aliekufa nakumbuka...na kuna mwanafunzi wa kike pia alikufa enzi hizo.....unakumbuka bro
 
lingine ambalo nalikumbuka kutoka hizi shule ni kuwa mkifika form three wakati wa kuchagua mkondo, madarasa ya mkondo wa biashara yalikuwa yanakosa watu. wana walikuwa wanagombea kusoma mikondo ya sayansi wakiwa na malengo ya PCB na PCM.
Ilibidi walimu wafanye kazi ya kuwalazimisha baadhi ya wana kwenda mikondo ya biashara.
Kwa kukadiria only 5-7% ndio walienda mkondo wa biashara, sina hakika kama kulikuwa na mkondo wa pure art.
Jingine, tulikuwa na walimu wa Math, Biology na Geography form one tu, miaka mingine tumeenda bila walimu hadi form iv lakini mungu alituvusha kwa kishindo cha A katika masomo hayo, nikitizama nyuma tulikotoka siamini nilivukaje,
Kuna CEO mmoja yeye tangu form one had 4 alisoma masomo mnne tu Phy, Chem, Bio na Mathe. form alipiga A nne na Six akapiga A zote na F moja ya general study (alipata div 3 point 3 form six)
Enzi mm pekee Aza boi ndio nilikomaa na pure art.
Situlii shule..kila baada ya miezi mitatu naomba ruhusa napoteza wiki tatu nikiwa na mabaharia tunapanga mitikasi ya maisha....kama elimu ikituangusha....Bas mabraza ilikua ugomvi daily kwanini nazembea
 
Kuna siku sita isahau, nilisikitika sana kuona wana ambao class walikuwa vichwa hasa wakifukuzwa shule.
Kuna majanki kama watano hivi wa Azaboi walikuwa wanapuliza kule bondeni huku wakipata view ya bonde la jangwani. Si wakapoteza Network, Headmaster akawakamata kiulaini wakaanza kumkoremea.
wakapelekwa polisi na ndio shule ikawa basi
Nikikikutana nao kitaa huwa nasikitika sana
Kule juu ya hostel.....wana walikua wanavuta sana vitu....huku njuka tukiwatazama 🤣🤣
 
wewe jamaa huwa nakukubari sana una like hadi nukta big up sana KAMANDA kwa kushow love humu Ndani wewe unaongoza...

kwenye kumbukumbu zangu sijawahi kugumiana na comment yako mbaya watu kama wewe ni wachache sana duniani...na ndio jamii ya watu wanao hitajika sana🙏​
Huyo rara ree mdogo wetu...mwaka 1987 alikua hajazaliwa bado.....sisi tupo mjini 🤣🤣🤣🤣
 
Nimesoma Jite enzi hizo
Tuliwapa kichapo Tambaza uwanja wa taifa, fainali ya Umiseta, nilikuwepo live sio mchezo
Tulipiga sana, mawe yalirushwa ndani mule na Tambaza, tukawatoa nje , na kufunga geti, halafu tuka re group, tilivyo fungua geti, walitafutana, huko mbele wakakutana na wajeshi wetu Taifa B, nwengine tuliwaingiza kambini na kuchapa sana, wakimbilia huko Chang'ombe /Keko wakamalizia hasira kwa kumuua konda..
Kuanzia hapo ikawa ni vita sana Tambaza tukikutana stendi shule ya uhuru au kariakoo, maana tulikuwa tunaambiwa shule kabisa na wajeshi tembeeni kuanzia watano pamoja....
Hii ilendelea mpaka na ilikuwa moja chanzo cha Tambaza kufungwa,
Nakumbuka mpaka polisi iliingilia, wanafunzi wetu walieenda kwenye gwaride la utambulisho na kusonta tu wa Tambaza.
Kesi zikazidi mpaka Wizara ikaamua kuwa shule ifungwe....
Hii niliisikia baada ya kuhamia form five Jitegemee 2005 chini ya Col G. Kusagwa na msaidizi wake Major Mkisi aliyemwachia kijiti 2017 baada ya kustaafu. Huu ugomvi uliendelea, kuna siku tulikutana stand na wanafunzi wa Tambaza Kariakoo wakataka kukiamsha na sisi, sema walishtuana kuacha baada ya kuona mob ya students wa Jite imeongezeka baada ya daladala mbili kusimama kituoni na wanafunzi wengine wa Jite kushuka. Sema sisi tulikuwa wastaarabu tukatemana nao kwa maneno shombo shombo tu bhasi.
 
Back
Top Bottom