Mabraza wa enzi hizo Dar kumbukumbu zangu

Mabraza wa enzi hizo Dar kumbukumbu zangu

dah umenikumbusha mbali siku ya kutunguliwa ndege Kigali nilikuwa posta na masela. Hapo tumetoka Azaboi kwa mguu hadi posta stand ya zamani. ile tunataka kutawanyika daladala zote zikazuiwa kupisha msafara wa delegation za Burundi na Rwanda waliokuwa wanarejea nchini kwao wakitokea Kilimanjaro Hotel. Hivyo tukaenda kushuhudia tu mwinyi akiwaaga hao viongozi pale Kilimanjaro. kutokana na hiyo foleni, nilifika nyumbani saa mbili usiku. nilipata kichapo heavy kutoka kwa mzee akihoji umetoka wapi usikuu huu wakati shule ilikuwa shift ya kutoka mchana. nikajitetea kuwa kulikuwa na msafara wa marais wa Rwanda na Burundi lakini wapi sikueleweka. Ile naendelea kula kichapo mara TV ya chogo ikatangaza kuwa Ndege iliyowabeba marais wa rwanda na Burundi kutokea Tanzania imetunguliwa na wote wamekufa. Nikamwambia mdingi unaona TV inachoeleza ndio ikawa pona yangu, akaamini kweli kulikuwa na msafara.
Mkuu mm nilikua na mwaka mmoja nyuma nimetoka kwa maanko huko Kigali......ndio hali ikawa hivyo.
Ila hata 1993....bado mauaji yalikua yanaendelea hasa nje ya kigali...ile chinja chinja ya jamii za kitusi
 
Week end j'mosi na j'pili mabrazamen na wacheza basketball karibia Dar nzima walikuwa wanajaa pale alafu Regina wala hana time nao. Mi nilikuwa nampendeaga akiniagiza soda ananiambia baki na chenchi watoto wa siku hizi wanasema "Kiip chenj"🤣🤣
Dada regina.....sometimes walikua wanamzushia eti tomboi 🤣🤣🤣
 
Bunju, Mbezi Luis, Kongowe ilikuwa vijijini na walikuwa wanaishi native
watu walikuwa wanaenda shamba kulima huko. Sheria ya ardhi ya mwaka 1999 ndio iliyatambua maeneo hayo kuwa nayo ni sehemu yatown kwa kuua mashamba.
Ni kweli weekend tulikuwa tunaenda shamba, ambapo leo hii panaitwa mbweni kwa washua ..
 
Patrick ana ile rumours kuwa walipokua Uganda walilala room moja lkn hakumla Reginq, hii story pale Tanesco basketball court ilienea sana tu
Ila ilikuwa chuma yake. Regina alikuwa akimpenda sana kisa P anadunda kikapu wakimaliza hao kwenye BMW ya Regina. Sijui P alimpaga nini mtoto wa kishua R😄😄
 
Back
Top Bottom