Mabraza wa enzi hizo Dar kumbukumbu zangu

Mabraza wa enzi hizo Dar kumbukumbu zangu

Ngoma ilipigwa tanchi yote,wakahamia Tukuyu Rungwe huko wengine kipoke kiwira,
Mi wakakuta nishaweka kambi.
Ndio ile ikawa mkitaka mali mtaipata shambani😁.
Nilikua nazama nao kitaa bush kwa bibi huko.
Watakula ndumu mpaka watapike.
Jpili nawatimua warudi kusoma hao kwao shule😂😂😂
J3 naenda jioni kuuza Big G,karanga ,pipi mpirani kumbe jamaa nawapoza tu wana mawenge balaa ya ganja weekend.
Kadem kangu kalikua kanaitwa Ruth Kidowezi.
Aisee hako ndo kalifanya nikaenda kule,
Ila nilikua mjasiriamali sikua mwanafunzi.
Babu umetoka mbali......
 
Point ya kufungia mwaka, ma bro mlifanya vitu vingi tatizo documentation.

Fanyeni proper documentation be it documentary etc tujifunze kwenu pia tu enjoy story za ma bro waliotutangulia.
Zipo ngoja nizitafute baadhi.....
Mkimpata Zafala anazo...na Gwamaka na Ambwene na Pascal Mayala hawa watakua na baadhi ya doc,s...na menejimenti ya ITV
 
Juzi Kati nilimskiliza sugu na balozi walikuwa bongo alliance francois balozi yuko marekani anafanya kaz na umri umeenda sana sugu pia aliona nje jau akarejea ila nimehifunza kuwa kijana anapaswa kusahihishwa kila wakat aisee na pia ujana unaisha na sister tuwe makini kuijenga kesho
Balozi alikua bishoo sana pale Tambaza acha tu.
 
Pole bana
Wakati huo, huko ni mapori tu, hawaishi watu....
Nimeishi Buguruni yote miaka hiyo late 80s naijua, nimeishi Kurasini mpaka shimo la udongo na Keko yote huko nakujua, Temeke wailesi, Chang'ombe, Na pia nimeishi Msasani wakati bado kuna mabonde ya kuvuna chumvi,
Maisha Mzunguko, pia nimeishi kwa kishua Upanga, Obey....
Braza ulipiga skul o level wapi???
 
Unamkumbuka Abby Spartan, alikuwa ana duka pale makaburini
Wadogo zake walikuwa wana band ya Reggae wana practice kule nyuma ya Muhimbili Hsp, Jangwani, nimesahau jina?

Unawakumbuka pia kina Mansoor bros, Musa alitesa sana , Hussein sijui bado yuko Italy , Duche....siku hizi mzee wa Gems....
Sasa kule ndiko mabraza mlikua mnajichimbia....tukiwa tunatoka muhimbili kurudi kitaani...tunawakuta afu kuna mwamba anatusimamisha anakagua madaftari yetu 🤣🤣🤣
 
Wale wa Arusha tufungue uzi kama huu tujikumbushe... baba yangu kanisimulia leo kuwa mwaka 1976 wanafunzi wa Ilboru, Arusha sec na shule zingine zilizokuwepo walishiriki ujenzi wa Sheikh Amri Abeid Stadium kama saidia fundi. Nikasema kweli nchi imetoka mbali.
Ila mabraza wa arusha walikua hawatoi ramani afu wahuni sana...kila siku kupigana visu...na kuvuta bangi
Kuna mwana alituteka kisa tumepotea njia ya church miaka hiyo...kule darajani....enzi hizo!!!!
Tukamrusha sisi wajukuu wa ********.......akatuachia.....ila sarafu zetu alichukua...akatupeleka mpaka church full escort 😂🤣🤣🤣 Arusha ulikua mji wa kitalii toka zamani.
 
Hii mada imenikumbusha mbali
Hii imenirudisha 1994 Don Bosco, Upanga kulikuwa na wana wa Azania walipanda jukwaani kama sijasahau walikuwa wanajiita W.W.A. (Wagumu Weusi Asilia) wana walirap kwa vina, ujuzi na ujumbe wa nguvu Sana wakawatoa kaptura za jeshi relini (Tambaza), kwa tafrani lililotokea concert liliishia hapo....
 
Back
Top Bottom