Maboresho ya JF - 2019

Maboresho ya JF - 2019

Mimi jamani nikitumia app ya JF, sioni (1) button(link) ya What's new.

(2)Pia kile kikengele cha notification ni kama hakana kazi, sioni zile namba nyekundu juu yake kuashiria idadi au uwepo wa notices. Yani huwA naka-tap tu ndo ikifunguka nione kilichomo. Kenyewe kamenuna wakati wote.

Nimehangaika na setting mpaka sasa bilabila.
 
Mkuu mimi ombi langu ni moja tu muturuhusu na sisi uwezo wa kuwapiga ban mafedhuli achilia mbali ignor na hii kila mtu aone kwamba fulani kapigwa ban na fulani hapa tutaheshimiana. Au mnaonaje mazee.

"Utamu hauna siri"
 
Wakuu,

Naomba kuwafahamisha kuwa siku si nyingi tutafanya maboresho kidogo kwenye mwonekano na matumizi ya JF.

Lengo ni kuzingatia mahitaji ya wadau (ambayo yamekuwa yakiombwa), kuendana na mabadiliko ya kiteknolojia na kuimarisha zaidi uimara wa platform.

Aidha, maboresho hayo yataenda hadi kwenye kuimarisha miundombinu (infrastructure) ili kuongeza uimara wa kukabiliana na hali yoyote.

Mabadiliko mengine ya aina hii yanaweza kufanyika 2021 au 2022.

Maboresho ya Miundombinu yamepangwa kufanyika usiku wa manane wa kuamkia tarehe 26/03/2019.

Asante kwa ushirikiano mnaoendelea kutupa.
Sisi wachangiaji wa Thread ya Usiku wa Manane mmetuconsider vipi

Sent using Uncesored Device
 
Leo tumeongeza server, kutakuwa na minor issues mwanzoni na baadae zitakaa sawa. Search (kwa waliowahi) itasumbua kwakuwa bado kuna kazi inafanyika in the background na baada ya muda mchache itakaa sawa

——
Edit: Search imekaa sawa kwa wote
 
Ngumu kuona mabadiliko katika servers. Labda pale utapoona website iko na speed nzuri na imara zaidi.

Ya mwonekano utayaelewa tu, tupe muda mchache
Kama ni mabadiliko ambayo ni sio rahisi kwa sisi kuyaona kwanini sasa musingeyafanya kimya kimya tuu?? Munaweka watu attention kwa kitu ambacho ni unnoticeable.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tulia ndugu wapo kwenye mchakato kulingana na maitaji ya wana Jamii Foroum wana fanya mabadiliko kulingana na maitaji na wakati..Kuifanya jamii foroum kuwa bora nyakati zote..
 
Back
Top Bottom